Taasisi ya IDS ya Chuo kikuu Cha Dar Es Salaam (UDSM), ninaomba kutumia jukwaa hili kuwaomba mbadilike hasa Kaimu Mkurugenzi wa Institute na Mratibu (Coordinator) wa Post-graduate Studies.
Nimeamua kuandika haya kutoka na ukweli kwamba mmekuwa mwiba mkali na kikwazo cha wanafunzi wa Masters na PhD kutomaliza kwa wakati. Usimamizi wenu umekuwa ni butu na usiokuwa na uungwana, wala kujali.
Baadhi ya changamoto ambazo ni kero ni pamoja na;
1. Mwanafunzi akisha-develop Mfano Research Proposal, na msimamizi wake (supervisor) akamruhusu akusanye, ikifika kwa coordinator na Mkurugenzi kwa ajili ya kuitwa kwenye presentation, lazima uchukue walau Miezi mitatu. Imagine Miezi mitatu, umekusanya research proposal mwezi Juni, unaitwa Kupresent October au November! Na siku hiyo kama supervisor wako hayupo, huwezi kufanya presentation hadi siku atakayokuwepo (hili ni utaratibu mpya).
2. Mwanafunzi akimaliza kuwasilisha Proposal, na baadae kukubaliana na msimamizi wake kukusanya kwa ajili ya kupata kibali Cha Utafiti (Research Clearence), hapo kasheshe ndo litakapoanza. Kibali hicho kwa sasa kinapatikana kwa mfumo (online).
Kasheshe lenyewe liko hivi;
(i). Mwanafunzi anaanzisha, akishaanzisha, anatuma proposal yake kwa supervisor, supervisor anatoa maoni yake, akishatoa maoni yake, hatua inayofuata ni kwa Coordinator, hapo kwa coordinator vumilia wiki 1 hadi 2 (kumbuka hapa ni kusema tu kama "sawa", au naridhia basi. Hayo maneno yanasubiri wiki.
Sasa kikitoka kwake kinaenda kwa Mkurugenzi wa Idara yaani Mkurugenzi wa Idara, hapo vumilia Miezi miwili au mitatu. Piga simu, tuma meseji jamaa wala haangaiki na wewe. Baada ya miezi miwili au mitatu ndo anaweza kukitoa.
Yaani mpaka ajisikie mwenyew, mwanafunzi atakula msoto akisubiri hisani ya le boss. Then, utasikia anasema master or PhD si mchezo unafikir Miezi 18 tu utakuwa umeimaliza?? Jamni, Sasa kwa nn mmeweka hiyo miezi, si iondoeni ijulikane tu kuwa muda haujulikani.
(ii). Mwanafunzi akitoka kukusanya data, akafanya analysis then Hadi mwisho akakubaliana na supervisor wake kukusanya, kimbembe kinaanza. Tarajia tena Miezi mitatu hadi minne ndo uitwe Kupresent findings. Yaani ni vurugu tupu.
Sasa utakuta mwanafunzi, labda ana ruhusa ya masomo, muda unaisha hata proposal hajapresent kisa tangu akamilishane na supervisor wake, bado kwenye idara hawajapanga tarehe ya kumuita muda unayoyoma mwisho wa siku muda unaisha mwanafunzi hajafanya chochote. Jambo ambalo si la uungwana!
KUHUSU ONLINE.
Ili mwanafunzi aweze kukusanya kazi yake mfano Proposal au Dissertation lazima iwe approved na supervisor, Coordinator na Director of institute. Na hawa unawapandia gari ili wakakusainie hizo nyaraka. Sasa mfumo ni online, niko huku Tandahimba, nipange superfeo kwenda Dsm kusainiwa hiyo form ya Approval afu sijui nirudi Tandahimba ndo niiscan na kuanza kutuma online! Online gani hiyo!
Hapo hapo, mwanafunzi akishasainiwa ndo anaiscan tena hiyo form na kuambatisha kwenye proposal au Dissertation ndo anaanza mchakato wa kuituma tena kwa Supervisor, huyo supervisor ambaye ameaprove manually anatumiwa tena ku-approve kwa kuweka comments, then atamfowadia Coordinator na Director, na kuendelea. Sasa sijui hii ni online gani hii jmn. Kwa nini mwanafunzi asipachike hiyo form, Wanafuata waweke scanned signature kwenye mfumo huko huko? Nini kinashindikana?
MALIPO YA EXTENSION
Hili ni kwa Chuo kizima. Watakuzungusha kote huko ikiwemo kukuharibia muda, lakini ile Miezi ikiisha wanakupa Miezi mitatu ya ziada, baada ya hiyo utatakiwa kulipa 25-50 elfu per month, hadi pale utakapohitimu. Wizi wa ajabu. Kama nyie ndo mmesababisha nalipaje extension?
Ushauri.
1. Coordinator na Director badilikeni. Ni vijana ambao mungeweza kuwa mfano wa kuigwa. Kama mnaona mna majukumu mengi hizo nafasi ziachieni. Waje ambao watajua kuwa hata jukumu la kushughulikia wanafunzi ni sehemu ya jukumu lao.
2. Kutengezwe ratiba ya presentation kwa mwezi walau na kwamba mwanafunzi akishakusanya kazi yake kwa ajili ya presentation au kibali basi isimalize mwezi na sehemu. Iwe ndani ya siku 30.
4. Online iwe kamili. Hizo taratibu za approval zifanyike online kweli. Mwanafunzi akishasaini yeye wengine wafanye online. Siyo mtu anaanza kutoka huko kote aliko kuja kukimbizana na wahadhiri wakti jambo lenyewe ni online. Haipendezi wasomi kuwa namna hii.
5. Majibu yenu yenye ukakasi na viburi hayajengi. Elewesheni watu kwa staha. Nafasi hizo ni mpito tu. Fanyeni kwa weledi na kuzingatia muda wa wenzenu (wanafunzi)pia.
Nawasilisha.