Alichokijenga Bashiru sasa kinambomoa

niah

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
6,898
8,847

Alichokijenga Dk Bashiru sasa kinambomoa​

Alhamisi, Novemba 24, 2022
bashiru-pic.png

Wana JF nimepakua hii habari ili kwa wale wasioingia kwenye magazeti muisome
By Luqman Maloto

Novemba 22, 1963 Rais wa 35 wa Marekani, John Kennedy “JFK”, alipigwa risasi na kuuawa. Mshituko ulikuwa mkubwa kuanzia eneo la tukio, Dealey Plaza, Dallas, Texas mpaka Marekani yote.

Ilikuwa Ijumaa. Saa 6:30 adhuhuri kwa Marekani. Mwanaharakati Malcolm X alikuwa msikitini kwa sala ya Ijumaa. Habari za Kennedy kuuawa zilisambaa haraka, kuanzia nyumba za ibada mpaka kumbi za starehe zilizokuwa kwenye pilika zake

Siku hiyo, baada ya kutoka msikitini, Malcom X alipofuatwa na waandishi wa habari ili aeleze mapokeo yake juu ya kifo cha JFK, alijibu: “Being an old farm boy myself, chickens coming home to roost never did make me sad, they always made me glad.”

Tafsiri ya Kiswahili: Kuwa kijana wa shamba wa zamani, binafsi kuona kuku wakirejea kwenye banda kamwe haijawahi kunifanya niwe na majonzi, daima hunipa furaha.

“Chicken come home to roost” ni methali ya Kiingereza ambayo imekuwa ikitumika kwa zaidi ya karne saba sasa. Maana yake ni kuwa ubaya ukishatendwa hurejea kwa aliyeutenda.

Ubaya unafanishwa na kuku wanapotoka bandani, huzunguka kuchakura wakisaka chakula. Hata hivyo, mwisho wa siku, kuku hurejea bandani kulala. Hiyo ni kanuni wa ufugaji wa kuku wa kienyeji.

X alimaanisha kuwa Wazungu wa Marekani walikuwa chanzo cha ubaya duniani, kutesa watu weusi na Wahindi wekundu. Kuvamia mataifa mengine na kusababisha maafa, ulemavu na kadhia nyingine. Hawakujali.

Sasa, ubaya wa Wazungu wa Marekani ulirejea nyumbani, Rais Mzungu, katika taifa ambalo Wazungu wanawakandamiza weusi na Wahindi wekundu, aliuawa. X akasema yeye kama kijana wa shamba wa zamani hakuchukia kuona kuku wakirejea bandani. Maana, ndiyo kawaida.

Bashiru Ally
Unaweza kujitenga na maneno ya X kuwa hakuumizwa na kifo cha JFK, nakushauri uchukue tafsiri ya kuku kurejea bandani, kisha tummulike aliyekuwa Katibu Mkuu CCM, Dk Bashiru Ally. Bashiru pia alipata kuishika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, kwa muda mfupi mno.

Hivi karibuni, video inayomwonesha Bashiru akihutubia jumuiya ya wakulima wadogo (Mviwata), ilisambaa kwa kasi. Bashiru alikuwa akiwaeleza wakulima umuhimu wao kwa mustakabali wa nchi.

Utaona kuwa hoja ya Bashiru ilikuwa nzuri mpaka pale alipoanza kutoa matamshi ya kukwazwa na sifa anazopewa Rais Samia Suluhu Hassan. Kwamba kuna mawakala humdanganya kwamba anaupiga mwingi.

Bashiru hakutaja jina la Samia. Hata hivyo, maneno “anaupiga mwingi”, yalipata umaarufu mno pale watu walipokuwa wakiuelezea utendaji wa Rais Samia, kwamba anafanya kazi nzuri. Wakitumia lugha ya soka kuwa anaupiga mwingi.

Katika hoja yake, Bashiru aliitaka jumuiya ya wakulima wadogo kutopenda kutoa shukurani kwa Serikali na kumsifu Rais Samia kwamba anaupiga mwingi. Kwamba wakifanya hivyo, watapoteza maana.

Mpaka hapo ukichukua maneno peke yake, huoni kama Bashiru alizungumza vibaya. Aliwakumbusha wakulima umuhimu wao, vilevile haki na wajibu ambao wanapaswa kuujenga mbele ya watu aliowaita wanyonyaji na watawala.

Dhambi ya Bashiru
Tukope maneno yaliyotamkwa Siku ya 74 ya kalenda ya Roma (Ides of March). Mwaka ulikuwa wa 44 Kabla ya Kristo (BC). Siku hiyo alikuwa anauawa mtawala wa zamani wa Roma, Julius Caesar.

Caesar hakutegemea kama kijana wake, Marcus Brutus, aliyepata kumsaliti kisha akamsamehe, angeweza kumgeuka tena kuwa mstari wa mbele katika mpango wa kukatisha uhai wake. Caesar alipomwona Brutus, alimuuliza kwa Kilatini: “Et tu, Brutus?” – “Hata wewe, Brutus?”

Nakopa maneno hayo ya Caesar “Hata wewe, Brutus?” kisha nayageuza kidogo kumwelekea Bashiru: “Hata wewe, Bashiru?” Swali kwa Bashiru si kwa tafsiri ya usaliti wa kuua kama Brutus kwa Caesar, bali kwa kusahau haraka. Wote wasahau, hata Bashiru jamani?

Miaka imepita ila kumbukumbu za matukio zinafanya ionekane kama juzi tu. Bashiru akiwa Katibu Mkuu CCM. Likaibuka kundi la watu walioamua kumsifia aliyekuwa Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli.

Wabunge wa upinzani walihama vyama vyao na kuisababishia nchi hasara ya kurudia uchaguzi. Waliohama walisema “wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli”, naye Bashiru aliwapokea. Akawakumbatia.

Watu walewale waliojiuzulu ubunge na kuhama vyama, Bashiru akiwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya CCM, alihakikisha hakuna mchakato wa ndani ili wasishindane na wana-CCM wengine katika kupata tiketi ya kugombea ubunge jimbo lililokuwa wazi.

Waliohamia CCM walisimamishwa kugombea ubunge kwenye majimbo waliyojiuzulu na kushinda tena. Yapo maeneo nguvu iliyotumika ilikuwa kubwa mpaka damu ilimwagika. Aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini, alipigwa risasi katika vurugu za uchaguzi wa marudio Kinondoni.

Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia, alijiuzulu kwa usemi kuwa “aliunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuleta maendeleo”. Bashiru alikuwa hajawa Katibu Mkuu, aliona. Kisha akakubali uteuzi.

Baada ya Bashiru kuwa Katibu Mkuu, kasi ya wabunge na madiwani wapinzani kuachia viti vyao na kuiiunga CCM ilikuwa kubwa. Bashiru alisimamia michakato yote na alikwenda kuwafanyia kampeni waliohamia CCM.

Ni kipindi ambacho kumsifia Dk Magufuli kwa mapambio ya kila aina ilionekana ndio ‘fasheni’ na Bashiru hakukerwa. Kuna kipindi mapambio ya Magufuli yalivuka kiwango cha sifa za kawaida za binadamu, lakini Bashiru hakuchukizwa.

Yaliibuka magazeti yenye kushambulia watu na kuwapa uhusika mbaya, vilevile yakawa yanamsifu Magufuli. Magazeti yalikosa weledi na kuchafua hadhi ya taaluma ya habari. Bashiru hakuwahi kukasirishwa.

Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba, aliibuka kinara wa kumsifu Magufuli na kushambulia watu aliodai wanataka kumhujumu Rais huyo wa tano wa Tanzania.

Waliotajwa na Musiba walipata mitikisiko mikubwa. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe alipitishwa kwenye bomba la moto mpaka akafukuzwa uanachama.

Aliyekuwa Katibu Mkuu CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana alifungiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi. Yusuf Makamba ambaye naye alishakalia kiti cha Katibu Mkuu CCM, ilibidi aombe radhi yaishe.

Kisa, walitajwa na Musiba kuwa walikuwa wanamhujumu Magufuli. Bashiru hakuwahi hata kutoa tamko la kumwonya Musiba, au kumwita na kuketi pamoja na aliowatuhumu ili kupata mwafaka au kujua kiini na ukweli.

Leo Bashiru anachukia watu kusema “Rais Samia anaupiga mwingi”, kipindi cha Magufuli, wabunge walitia fora. Angesimama mbunge na kutumia zaidi ya nusu ya muda aliopewa kuchangia bungeni, kumsifu Magufuli.

Aliitwa “Chuma”, “Jembe”, “Rais wa Wanyonge”, “Kiboko ya Wapinzani”, “Kiboko ya Mabeberu”, “Kiongozi wa Malaika”, na majina mengi ya mapambio, hakuna mahali Bashiru alichukia.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, alipata kusema (na video zipo), kwamba kwa kazi nzuri aliyoifanya, watu wa Tabora watamwambia Mungu amshukuru Magufuli. Bashiru hakuogopa hata hii kauli kuwa Muumba ndiye ampe shukurani muumbwa, Magufuli.

Kuku wanarudi bandani
Kuitendea haki kauli ya Bashiru lazima kuigawa katika pande nne. La kwanza ni kuwa tabia ya kusifu sana viongozi sio nzuri. Inalemaza. Huwapa viongozi u-Mungu mtu. Ndivyo akina Bashiru walimtengeneza Magufuli.

Alichokisema Bashiru ni sahihi, lakini katika kinywa ambacho hakina usahihi. Tunahitaji kuona nchi ina viongozi wanaowajibika ipasavyo kwa wananchi na sio kubeba tafsiri kuwa wanachokifanya ni msaada. Bashiru ni sehemu ya walioleta hayo mazingira ya kubadili utumishi wa viongozi kuwa msaada.

Pili, ni ukumbusho kwa viongozi walio kwenye nafasi leo. Wasiwe chawa wa mabosi wao, bali waitende kazi inavyotakiwa. Wanapaswa kumshauri jinsi ya kupokea sifa na kutenda. Kiongozi lazima awe mnyenyekevu kwa wananchi.

Bashiru hakuifanya kazi yake vizuri kipindi cha Magufuli, kumshauri namna bora ya kuishi kama Rais na kutolemazwa na sifa mfululizo. Alifurahia cheo kutoka Katibu Mkuu CCM mpaka Katibu Mkuu Kiongozi.

Hivi sasa yupo nje ya cheo ndio anakumbuka kuwa sifa nyingi kwa viongozi sio sawa. Hii ina maana iwasaidie na walio kwenye mfumo leo, si sawa sana kumsifu Rais Samia mpaka kupitiliza. Wamshauri na wampongeze anapostahili. Sio sifa kedekede mpaka zimlemaze.

Viongozi wote ni binadamu. Hawana sifa ya malaika. Wanapatia na wanakosea. Sifa zikiwa nyingi, kiongozi anaweza kudhani kila kitu kipo sawa. Haya ni madhara makubwa.

Tatu, Bashiru ni mbunge wa kuteuliwa. Anayo nafasi ya kuwasaidia wakulima kwa kujenga hoja bungeni, ama kwa maneno au maandishi. Mbunge hupaswa kubeba shida za wananchi na kwenda kuzisemea.

Haipaswi mbunge kwenda kuwachochea wananchi dhidi ya Serikali, wakati yeye ndiye mwakilishi wao. Haya Bashiru anayajua. Ni mwanzuoni, anajua jinsi mhimili wa uwakilishi (Bunge), unavyopaswa kufanya kazi na Serikali. Ni kwa sababu hiyo ndio maana Bashiru anachukuliwa ana nongwa na sifa za Rais Samia.

Nne, tangu Bashiru alipotoa maoni yake, chama chake kinamshughulikia kwelikweli. Vijana hawakumbuki kama alipata kuwa Katibu Mkuu wao. Haya ndio matokeo halisi ya kuku kurejea bandani.

Bashiru alipokuwa Katibu Mkuu CCM, vijana wa chama hawakuwa na adabu kwa wastaafu. Musiba, Ally Hapi, Livingstone Lusinde, Hussein Bashe, hawakuwa na adabu kwa akina Makamba na Kinana. Wazee walishughulikiwa, naye alinyamaza.

Ona leo, Lusinde anamshughulikia Bashiru. Katibu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Kenani Kihongosi, anampa maneno makavu bila staha kuwa alikuwa kiongozi wao mwandamizi. Ni malipo. Kuku ambao Bashiru aliwafuga, wanarejea bandani.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
33,874
60,228
That was my basic argument in one of my threads!

Umeeleza vema kabisa. That was the tenet of my argument in one of my threads!
 
Walker Water

Member
Aug 23, 2022
60
60
Yaani mnaenda mbele na kurudi nyuma lakini hamtoki hapo mlipo!,Mi nadhani swali hili la msingi sana analouliza Bw,Paschal Mayala mara kwa mara siku likijibiwa tutasonga mbele,swali,"ccm imeshachokwa na wananchi,lakini nani(mpinzani) anaweza kuwa mbadala wa kupewa nchi!??"
 
Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
12,894
18,606
Kwa kweli Bashiru anavuna kile alichopanda.
Walealiowawekea kifua-hata wapinzani- ndio kwanza wanampiga kikumbo!
Basiru ana PhD ya usomi, lakini kisiasa ameonyesha kuwa yuko chekechea.
Maneno ya kisiasa yana wakati wake muafaka, wakati unaotawaliwa na mazingira yanayokuzunguka.
PhD haijamsaidia kuyaelewa mazingira hayo.
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
12,628
9,536
Kwa hiyo mnapanga kumnyofoa uhai wake?

Nilishasema juzi hapa CCM haioni hasara kutoa uhai wa watu ili kuondoa tishio la kuondoleea madarakani

Muueni tu maana Watanzania wengi wapo na wanajua sasa nini mlimfanya Kolimba
 
niah

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
6,898
8,847
Kwa hiyo mnapanga kumnyofoa uhai wake?

Nilishasema juzi hapa CCM haioni hasara kutoa uhai wa watu ili kuondoa tishio la kuondoleea madarakani

Muueni tu maana Watanzania wengi wapo na wanajua sasa nini mlimfanya Kolimba
Ndugu yangu mimi nimekopi na kupaste na aliyeandika siyo mwanasiasa nadhani. Mimi na siasa wapi na wapi ila ninapenda uhai na maendeleo ya nchi yangu ndo maana niliona hii habari nikaona tujuzane. Iwe CCM au nini watajijua mimi nahitaji maendeleo katika kata yangu, wilaya yangu bahati mbaya anatokea huko Bashiru mdini aliyemkatalia mpendekezwa wa kata mtu aliyefeli miaka 15 bila maendeleo ya kata mtu wa dini na uswaiba wake lakini nguvu ya wanannchi ilikataa akapita mtu ambaye hakutegemewa ACT wazalendo. Hiyo ndo nguvu ya UMMA.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
50,040
86,316
Yaani mnaenda mbele na kurudi nyuma lakini hamtoki hapo mlipo!,Mi nadhani swali hili la msingi sana analouliza Bw,Paschal Mayala mara kwa mara siku likijibiwa tutasonga mbele,swali,"ccm imeshachokwa na wananchi,lakini nani(mpinzani) anaweza kuwa mbadala wa kupewa nchi!??"

Kama CCM wameweza kuongoza nchi muda mrefu bila ufanisi, unadhani ni chama gani kitashindwa?
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,404
7,090
Kwenye siasa na hasa za ccm hakuna fariki au adui wa kudumu.
Ni kama ukoo wa mafisi.wenzao akizubaa analiwa chap!
Huyo Bashiru aliwaingiza wengi bungeni lakini leo wanamchuna ngozi.
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
12,628
9,536
Ndugu yangu mimi nimekopi na kupaste na aliyeandika siyo mwanasiasa nadhani. Mimi na siasa wapi na wapi ila ninapenda uhai na maendeleo ya nchi yangu ndo maana niliona hii habari nikaona tujuzane. Iwe CCM au nini watajijua mimi nahitaji maendeleo katika kata yangu, wilaya yangu bahati mbaya anatokea huko Bashiru mdini aliyemkatalia mpendekezwa wa kata mtu aliyefeli miaka 15 bila maendeleo ya kata mtu wa dini na uswaiba wake lakini nguvu ya wanannchi ilikataa akapita mtu ambaye hakutegemewa ACT wazalendo. Hiyo ndo nguvu ya UMMA.
Wewe na siasa wapi na wqpi?

Sasa hizi harakati humu jukwaa la.mbavu nene unafanyaje?

Enwwei. Umeshasema na tumekusikia na sisi tunatoa maoni yetu
 
Walker Water

Member
Aug 23, 2022
60
60
Kama CCM wameweza kuongoza nchi muda mrefu bila ufanisi, unadhani ni chama gani kitashindwa?
Chama chochote kitaweza ndiyo,lakini kitakuwa na kazi kubwa ya kufanya zaidi ya ccm maana kipimo chao kitakuwa ccm iliyoondoka,ccm wamekaa muda mrefu maana hakijapimwa na chama kingine na hivyo inakuwa ngumu kujua ufanisi wao ni wa kiwango gani.
 
Mudawote

JF-Expert Member
Jul 10, 2013
9,559
11,461
Nilichoelewa tu hapa ni kuwa viongozi wote wa ngazi za juu walioshabikia kifo cha Dkt Magufuli watakufa vifo vya ajabu ajabu kama Malcom X alivyouawa na kama alivyo shangilia kifo cha risasi cha JF Kennedy.
 
voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
3,629
6,370
Mleta hoja umeongea Mengi mazuri...

Lakini pia umeshindwa kuuficha upande wako wewe binafsi!

Naomba ukiweza unijibu hili swali lifuatalo...

Je!
Majambazi wakivamia eneo ulipo wewe, na kisha wakati uvamizi ukiendelea...

Ikatokea Jambazi mmoja akujuaye binafsi ambae kumbe ni jirani yako kule mtaani kwako.Ila bahati mbaya mmekutana akiwa kazini ila asiyetaka wewe jirani yake udhurike au kuuwawa!
Na akakupigia kelele ulale chini ili kuepa Risasi ya mwenzake aliyeko nyuma yako,aliyekulenga kutaka kukupiga Risasi wewe!

Utaacha kutii tahadhari ilebkutoka kwa jirani yako jambazi ili kujiokoa na kutulia ukisimama wima ili Risasi ikupate bila kulala chini.?
Eti Kisa tu anayekutahadharisha ni Jambazi mwenzao?

La hasha!
Tahadhari imetoka Moyoni kwa mtoa tahadhari!
Haitoki mdomoni bali imepitia hapo mdomoni ili kumfikia mtahadharishwa!

Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.

Pia hata wasio na nguvu au mamlaka,lakini wanao uwezo wa kuyaona na kuyajadili yanayokuwa yakitendwa na wanasiasa walioko kwenye siasa za moja kwa moja kiutendaji.

Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.

Hivyo basi huwezi ukamzuia Bashiru kuyasema yale ambayo ametasema,kulingana na upeo wake yeye kwa wakati husika,tofauti na upeo aliokuwa nao wakati ule.

Huwezi iharamisha tahadhari sahihi kwa wannchi...eti kwa sababu imetoka kwenye kinywa kisicho Sahihi?

Pia watu wengi walikuwa wakimsifia Magufuli (R.I.P),sio kwa ukatili wake,bali walimsifia kwa utendaji na mtindo wake wa Utoaji Maamuzi.
Ambao kutokana na hali ya wakati husika ilivyokuwa imefikia,alionekana kama Muarobaini wa magonjwa ya wakati ule!
Ambayo tayari yalikuwa Sugu.

Na huko tuendako sasa,ni kama vile atahitajika Magufuli mwingine tena,ili kuyatibu yale tunayougua kwa sasa!

Alamsikhi.
 
niah

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
6,898
8,847
Chama chochote kitaweza ndiyo,lakini kitakuwa na kazi kubwa ya kufanya zaidi ya ccm maana kipimo chao kitakuwa ccm iliyoondoka,ccm wamekaa muda mrefu maana hakijapimwa na chama kingine na hivyo inakuwa ngumu kujua ufanisi wao ni wa kiwango gani.
Hilo ndo tatizo hapa nchini. Tangu vianze vyama vingi hapa nchini, kumekuwa na kubadilika kwa viongozi au kuhama toka chama hiki kwenda kingine hivyo hakujawa na ustawi wa vyama vya upinzani.
Kazi ni kubwa kuiondoa CCM madarakani sababu karibia na uchaguzi kunakuwa na hotuba za kutisha watu hasa wa vijijini ambao hawaoni mbali na wala hawana uelewa mzuri wa dunia ya sasa. Tishio la vita na vurugu ndo huwa fimbo ya kupigia upinzani. Saa nyingine vurugu na mauaji ya viongozi wa vyama vya upinzani hutisha watu. CCM inabidi ijitafakari mbinu inazozitumia kuongoza watu hasa wale wenye uelewa mdogo wa dunia ya sasa au tuseme Exposure.
 
Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
3,027
4,426

Alichokijenga Dk Bashiru sasa kinambomoa​

Alhamisi, Novemba 24, 2022
bashiru-pic.png

Wana JF nimepakua hii habari ili kwa wale wasioingia kwenye magazeti muisome
By Luqman Maloto

Novemba 22, 1963 Rais wa 35 wa Marekani, John Kennedy “JFK”, alipigwa risasi na kuuawa. Mshituko ulikuwa mkubwa kuanzia eneo la tukio, Dealey Plaza, Dallas, Texas mpaka Marekani yote.

Ilikuwa Ijumaa. Saa 6:30 adhuhuri kwa Marekani. Mwanaharakati Malcolm X alikuwa msikitini kwa sala ya Ijumaa. Habari za Kennedy kuuawa zilisambaa haraka, kuanzia nyumba za ibada mpaka kumbi za starehe zilizokuwa kwenye pilika zake

Siku hiyo, baada ya kutoka msikitini, Malcom X alipofuatwa na waandishi wa habari ili aeleze mapokeo yake juu ya kifo cha JFK, alijibu: “Being an old farm boy myself, chickens coming home to roost never did make me sad, they always made me glad.”

Tafsiri ya Kiswahili: Kuwa kijana wa shamba wa zamani, binafsi kuona kuku wakirejea kwenye banda kamwe haijawahi kunifanya niwe na majonzi, daima hunipa furaha.

“Chicken come home to roost” ni methali ya Kiingereza ambayo imekuwa ikitumika kwa zaidi ya karne saba sasa. Maana yake ni kuwa ubaya ukishatendwa hurejea kwa aliyeutenda.

Ubaya unafanishwa na kuku wanapotoka bandani, huzunguka kuchakura wakisaka chakula. Hata hivyo, mwisho wa siku, kuku hurejea bandani kulala. Hiyo ni kanuni wa ufugaji wa kuku wa kienyeji.

X alimaanisha kuwa Wazungu wa Marekani walikuwa chanzo cha ubaya duniani, kutesa watu weusi na Wahindi wekundu. Kuvamia mataifa mengine na kusababisha maafa, ulemavu na kadhia nyingine. Hawakujali.

Sasa, ubaya wa Wazungu wa Marekani ulirejea nyumbani, Rais Mzungu, katika taifa ambalo Wazungu wanawakandamiza weusi na Wahindi wekundu, aliuawa. X akasema yeye kama kijana wa shamba wa zamani hakuchukia kuona kuku wakirejea bandani. Maana, ndiyo kawaida.

Bashiru Ally
Unaweza kujitenga na maneno ya X kuwa hakuumizwa na kifo cha JFK, nakushauri uchukue tafsiri ya kuku kurejea bandani, kisha tummulike aliyekuwa Katibu Mkuu CCM, Dk Bashiru Ally. Bashiru pia alipata kuishika ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, kwa muda mfupi mno.

Hivi karibuni, video inayomwonesha Bashiru akihutubia jumuiya ya wakulima wadogo (Mviwata), ilisambaa kwa kasi. Bashiru alikuwa akiwaeleza wakulima umuhimu wao kwa mustakabali wa nchi.

Utaona kuwa hoja ya Bashiru ilikuwa nzuri mpaka pale alipoanza kutoa matamshi ya kukwazwa na sifa anazopewa Rais Samia Suluhu Hassan. Kwamba kuna mawakala humdanganya kwamba anaupiga mwingi.

Bashiru hakutaja jina la Samia. Hata hivyo, maneno “anaupiga mwingi”, yalipata umaarufu mno pale watu walipokuwa wakiuelezea utendaji wa Rais Samia, kwamba anafanya kazi nzuri. Wakitumia lugha ya soka kuwa anaupiga mwingi.

Katika hoja yake, Bashiru aliitaka jumuiya ya wakulima wadogo kutopenda kutoa shukurani kwa Serikali na kumsifu Rais Samia kwamba anaupiga mwingi. Kwamba wakifanya hivyo, watapoteza maana.

Mpaka hapo ukichukua maneno peke yake, huoni kama Bashiru alizungumza vibaya. Aliwakumbusha wakulima umuhimu wao, vilevile haki na wajibu ambao wanapaswa kuujenga mbele ya watu aliowaita wanyonyaji na watawala.

Dhambi ya Bashiru
Tukope maneno yaliyotamkwa Siku ya 74 ya kalenda ya Roma (Ides of March). Mwaka ulikuwa wa 44 Kabla ya Kristo (BC). Siku hiyo alikuwa anauawa mtawala wa zamani wa Roma, Julius Caesar.

Caesar hakutegemea kama kijana wake, Marcus Brutus, aliyepata kumsaliti kisha akamsamehe, angeweza kumgeuka tena kuwa mstari wa mbele katika mpango wa kukatisha uhai wake. Caesar alipomwona Brutus, alimuuliza kwa Kilatini: “Et tu, Brutus?” – “Hata wewe, Brutus?”

Nakopa maneno hayo ya Caesar “Hata wewe, Brutus?” kisha nayageuza kidogo kumwelekea Bashiru: “Hata wewe, Bashiru?” Swali kwa Bashiru si kwa tafsiri ya usaliti wa kuua kama Brutus kwa Caesar, bali kwa kusahau haraka. Wote wasahau, hata Bashiru jamani?

Miaka imepita ila kumbukumbu za matukio zinafanya ionekane kama juzi tu. Bashiru akiwa Katibu Mkuu CCM. Likaibuka kundi la watu walioamua kumsifia aliyekuwa Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli.

Wabunge wa upinzani walihama vyama vyao na kuisababishia nchi hasara ya kurudia uchaguzi. Waliohama walisema “wanaunga mkono juhudi za Rais Magufuli”, naye Bashiru aliwapokea. Akawakumbatia.

Watu walewale waliojiuzulu ubunge na kuhama vyama, Bashiru akiwa Mwenyekiti wa Sekretarieti ya CCM, alihakikisha hakuna mchakato wa ndani ili wasishindane na wana-CCM wengine katika kupata tiketi ya kugombea ubunge jimbo lililokuwa wazi.

Waliohamia CCM walisimamishwa kugombea ubunge kwenye majimbo waliyojiuzulu na kushinda tena. Yapo maeneo nguvu iliyotumika ilikuwa kubwa mpaka damu ilimwagika. Aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini, alipigwa risasi katika vurugu za uchaguzi wa marudio Kinondoni.

Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maulid Mtulia, alijiuzulu kwa usemi kuwa “aliunga mkono juhudi za Rais Magufuli kuleta maendeleo”. Bashiru alikuwa hajawa Katibu Mkuu, aliona. Kisha akakubali uteuzi.

Baada ya Bashiru kuwa Katibu Mkuu, kasi ya wabunge na madiwani wapinzani kuachia viti vyao na kuiiunga CCM ilikuwa kubwa. Bashiru alisimamia michakato yote na alikwenda kuwafanyia kampeni waliohamia CCM.

Ni kipindi ambacho kumsifia Dk Magufuli kwa mapambio ya kila aina ilionekana ndio ‘fasheni’ na Bashiru hakukerwa. Kuna kipindi mapambio ya Magufuli yalivuka kiwango cha sifa za kawaida za binadamu, lakini Bashiru hakuchukizwa.

Yaliibuka magazeti yenye kushambulia watu na kuwapa uhusika mbaya, vilevile yakawa yanamsifu Magufuli. Magazeti yalikosa weledi na kuchafua hadhi ya taaluma ya habari. Bashiru hakuwahi kukasirishwa.

Mwandishi wa habari, Cyprian Musiba, aliibuka kinara wa kumsifu Magufuli na kushambulia watu aliodai wanataka kumhujumu Rais huyo wa tano wa Tanzania.

Waliotajwa na Musiba walipata mitikisiko mikubwa. Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe alipitishwa kwenye bomba la moto mpaka akafukuzwa uanachama.

Aliyekuwa Katibu Mkuu CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana alifungiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi. Yusuf Makamba ambaye naye alishakalia kiti cha Katibu Mkuu CCM, ilibidi aombe radhi yaishe.

Kisa, walitajwa na Musiba kuwa walikuwa wanamhujumu Magufuli. Bashiru hakuwahi hata kutoa tamko la kumwonya Musiba, au kumwita na kuketi pamoja na aliowatuhumu ili kupata mwafaka au kujua kiini na ukweli.

Leo Bashiru anachukia watu kusema “Rais Samia anaupiga mwingi”, kipindi cha Magufuli, wabunge walitia fora. Angesimama mbunge na kutumia zaidi ya nusu ya muda aliopewa kuchangia bungeni, kumsifu Magufuli.

Aliitwa “Chuma”, “Jembe”, “Rais wa Wanyonge”, “Kiboko ya Wapinzani”, “Kiboko ya Mabeberu”, “Kiongozi wa Malaika”, na majina mengi ya mapambio, hakuna mahali Bashiru alichukia.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, alipata kusema (na video zipo), kwamba kwa kazi nzuri aliyoifanya, watu wa Tabora watamwambia Mungu amshukuru Magufuli. Bashiru hakuogopa hata hii kauli kuwa Muumba ndiye ampe shukurani muumbwa, Magufuli.

Kuku wanarudi bandani
Kuitendea haki kauli ya Bashiru lazima kuigawa katika pande nne. La kwanza ni kuwa tabia ya kusifu sana viongozi sio nzuri. Inalemaza. Huwapa viongozi u-Mungu mtu. Ndivyo akina Bashiru walimtengeneza Magufuli.

Alichokisema Bashiru ni sahihi, lakini katika kinywa ambacho hakina usahihi. Tunahitaji kuona nchi ina viongozi wanaowajibika ipasavyo kwa wananchi na sio kubeba tafsiri kuwa wanachokifanya ni msaada. Bashiru ni sehemu ya walioleta hayo mazingira ya kubadili utumishi wa viongozi kuwa msaada.

Pili, ni ukumbusho kwa viongozi walio kwenye nafasi leo. Wasiwe chawa wa mabosi wao, bali waitende kazi inavyotakiwa. Wanapaswa kumshauri jinsi ya kupokea sifa na kutenda. Kiongozi lazima awe mnyenyekevu kwa wananchi.

Bashiru hakuifanya kazi yake vizuri kipindi cha Magufuli, kumshauri namna bora ya kuishi kama Rais na kutolemazwa na sifa mfululizo. Alifurahia cheo kutoka Katibu Mkuu CCM mpaka Katibu Mkuu Kiongozi.

Hivi sasa yupo nje ya cheo ndio anakumbuka kuwa sifa nyingi kwa viongozi sio sawa. Hii ina maana iwasaidie na walio kwenye mfumo leo, si sawa sana kumsifu Rais Samia mpaka kupitiliza. Wamshauri na wampongeze anapostahili. Sio sifa kedekede mpaka zimlemaze.

Viongozi wote ni binadamu. Hawana sifa ya malaika. Wanapatia na wanakosea. Sifa zikiwa nyingi, kiongozi anaweza kudhani kila kitu kipo sawa. Haya ni madhara makubwa.

Tatu, Bashiru ni mbunge wa kuteuliwa. Anayo nafasi ya kuwasaidia wakulima kwa kujenga hoja bungeni, ama kwa maneno au maandishi. Mbunge hupaswa kubeba shida za wananchi na kwenda kuzisemea.

Haipaswi mbunge kwenda kuwachochea wananchi dhidi ya Serikali, wakati yeye ndiye mwakilishi wao. Haya Bashiru anayajua. Ni mwanzuoni, anajua jinsi mhimili wa uwakilishi (Bunge), unavyopaswa kufanya kazi na Serikali. Ni kwa sababu hiyo ndio maana Bashiru anachukuliwa ana nongwa na sifa za Rais Samia.

Nne, tangu Bashiru alipotoa maoni yake, chama chake kinamshughulikia kwelikweli. Vijana hawakumbuki kama alipata kuwa Katibu Mkuu wao. Haya ndio matokeo halisi ya kuku kurejea bandani.

Bashiru alipokuwa Katibu Mkuu CCM, vijana wa chama hawakuwa na adabu kwa wastaafu. Musiba, Ally Hapi, Livingstone Lusinde, Hussein Bashe, hawakuwa na adabu kwa akina Makamba na Kinana. Wazee walishughulikiwa, naye alinyamaza.

Ona leo, Lusinde anamshughulikia Bashiru. Katibu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM), Kenani Kihongosi, anampa maneno makavu bila staha kuwa alikuwa kiongozi wao mwandamizi. Ni malipo. Kuku ambao Bashiru aliwafuga, wanarejea bandani.
Alichokijenga Bashiru sicho kinachombomoa. Ingekuwa ni hivyo asingetoka kukemea.

Bashiru alipanda mbegu, alipoondoka, usiku wa mane adui naye akaja akapanda Magugu.

Mbegu zilipomea, akiyakuta Magugu lazima akasirike, usimzuie Kwa kisingizio Eti Yeye ndo mwenye shamba na ulimwona alipanda mbegu mchana.
 
9 Reactions
Reply
Top Bottom