MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,009
- 2,173
Haya mambo sasa tuseme yanafanyika kiushabiki na pia kiukabila. Nimeona mitandaoni eti UDOM wanaanzisha kampasi mpya mkoa wa Njombe. Hii ni uharibifu wa pesa ya umma unaoongozwa na ukabila.
Ni uharibifu kwa sababu Kampasi kuu ya UDOM pale Dodoma mjini haijafikia kiwango chake cha udahili kama ilivyopangwa, wanafunzi 40,000. Kinakadiriwa kuwa na wanafunzi 25,000 tu. Ina maana miundombinu iliyopo, bado inatumiwa chini ya kiwango. Kwa nini chuo cha aina hiyo kianzishe kampasi nyingine mkoani Njombe?
Njombe ni mkoa mdogo sana ulio karibu na Iringa, na Mbeya na tayari Iringa kuna tawi la Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Mbeya kuna chuo kikuu cha MUST! Huu uamuzi ulio na ukabila ndani yake.
VC wa UDOM anatoka mkoa wa Njombe. Ukiilinganisha na mikoa mikongwe isiyokuwa na matawi ya vyuo vikuu vya serikali huu siyo uamuzi wenye sababu. Kwa upande wa bara njombe ndo mkoa wenye idadi ndogo kabisa ya watu, kiasi cha laki 9 tu! Je, kwa idadi hiyo na ukiwa karibu na tawi la UDSM na MUST ya Mbeya, kuna dsababu ya kuwa na tawi la chuo ambacho hakijatimiza malengo ya kampasi kuu yake?
Maoni yangu tawi hilo lingepelekwa Mkoani Lindi au Mtwara ili kupunguza usafiri wa wanafunzi watakaopenda kubaki mikoa ya Kusini. Au lipelekwe KIgoma. Tuache ukabila wa kiasi hiki!