Bilioni 18.4 SUA Kujenga Chuo cha Kilimo Mkoa wa Katavi, Mpimbwe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,886
938

SHILINGI BILIONI 18.4 SUA KUJENGA CHUO CHA KILIMO KATAVI HALMASHAURI YA MPIMBWE

Katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi Mhe. Martha Festo Mariki ameuliza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Maswali yaliyojibiwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kuhusu mpango wa Serikali kujenga Vyuo Vikuu katika mikoa ambayo haina huduma ya elimu ya juu

"Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha matawi ya Vyuo Vikuu vya Umma katika Mkoa wa Katavi" - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Serikali ya Awamu ya Sita imelenga kupanua na kuboresha huduma za Jamii ikiwemo Elimu ya juu ili kufikia maeneo yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." - Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Serikali kupitia mradi wa Higher Education for Economics Transformation - HEET wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021-2026 inatarajia kujenga Kampasi mpya 14 za Vyuo Vikuu katika Mikoa ambayo haina taasisi ya Elimu ya juu ikiwemo Mkoa wa Katavi." - Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Kupitia mradi wa HEET Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimetengewa jumla ya Shilingi Bilioni 18.4 kwa ajili ya ujenzi wa Kampasi mpya katika Mkoa wa Katavi Wilaya ya Mlele Halmashauri ya Mpimbwe" - Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Kwa sasa kazi zinazoendelea katika Kampasi hiyo ni tathmini ya athari za Mazingira na Jamii (Environmental and Social Impact Assessments) na mchakato wa kumpata mshauri elekezi unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni 2023 na baadaye mkandarasi wa ujenzi" - Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia

"Kwa kuwa ni adhma ya Serikali kukuza Kilimo nchini, Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu wa kuwapa kipaumbele kwenye mikopo wanafunzi ambao wanachaguliwa kwenda kusomea masomo ya Kilimo hususani katika Kampasi zilizopo pembezoni mfano Kampasi ya Mizengo Pinda ambayo sasa ina zaidi ya miaka 3 ambayo imejikita zaidi katika kutoa elimu ya Nyuki? - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Kwa kuwa sasa katika Mkoa wa Katavi tuna Kampasi moja, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza Kampasi nyingine ili kupanua wigo wa Elimu katika Mkoa wa Katavi kwa kuongeza Kampasi kama Vyuo vya Afya pamoja na Vyuo vya Uhasibu"? - Mhe. Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Katavi

"Serikali imekuwa ikiongeza kiwango cha mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu. Mwaka 2021-2022 tulitenga na kupelekea jumla ya Shilingi Bilioni 570. Mwaka 2022-2023 tulipeleka Shilingi Bilioni 554 na Bilioni 3 kwa ajili ya Samia Scholarship. Katika bajeti ya 2023-2024 Vilevile tumetenga Shilingi Bilioni 738 kwa ajili ya mikopo mwaka ujao wa fedha. Pia, tuna kozi za kipaumbele za Sayansi, Uhandisi, Udaktari, Kilimo na Masuala ya Nyuki" - Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia
 

Attachments

  • Mariki.mp4
    98.4 MB
  • WhatsApp Image 2023-06-02 at 19.16.52.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-02 at 19.16.52.jpeg
    35.8 KB · Views: 13
Hao wahitimu wa SUA wameisaidiaje nchi hasa wakulima kuundoa umasikini?
Ningeshauri hio hela ingeanzishwa miradi ya kilimo ya kisasa kama ile ya Uyole kisha vijaba wajifunze kwa vitendo kwa kuchagua kilimo wanachokipenda.
Huko SUA waache kuandaa mabwana shamba waandae wajasiliamali wa kilimo.
Mabwana shamba watokane na wajasiliamali waliofanikiwa.
 
Hao wahitimu wa SUA wameisaidiaje nchi hasa wakulima kuundoa umasikini?
Ningeshauri hio hela ingeanzishwa miradi ya kilimo ya kisasa kama ile ya Uyole kisha vijaba wajifunze kwa vitendo kwa kuchagua kilimo wanachokipenda.
Huko SUA waache kuandaa mabwana shamba waandae wajasiliamali wa kilimo.
Mabwana shamba watokane na wajasiliamali waliofanikiwa.
Hebu kaa chini utafakari kwanza Vizuri.Hivi mtu akishafanikiwa anaweza kukubali kuwa Bwana Shamba,kwenda Mashambani kushauri Wakulima Badala ya kuboresha biashara yake?.Mjasiriamali akishafanikiwa hawezi tena kupoteza muda kuhudumia wakulima labda wawe wanamlipa gharama(consultation fee),kitu ambacho kwa nchi yetu ni ngumu.
 
Hebu kaa chini utafakari kwanza Vizuri.Hivi mtu akishafanikiwa anaweza kukubali kuwa Bwana Shamba,kwenda Mashambani kushauri Wakulima Badala ya kuboresha biashara yake?.Mjasiriamali akishafanikiwa hawezi tena kupoteza muda kuhudumia wakulima labda wawe wanamlipa gharama(consultation fee),kitu ambacho kwa nchi yetu ni ngumu.
Sawa basi waache habari za kuaanda bwanashamba Waandae watu wanaoenda kulima mashamba yao.
Mfumo wa kuanda mabwana shamba umepitwa na wakati maana wakulima wala hawawahitaji.
Wakulima wanajua njia zao za kulima.
 
Back
Top Bottom