Uchambuzi wa nyota kila siku

Uchambuzi wa nyota kila siku

NYOTA YAKO LEO ALHAMIS AGOSTI 07/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Utapata matatizo ya kiafya na kiuchumi kuna lawama utakumbana nazo Kuwà makini na mali zako kutatokea upotevu au kuibiwa kitu cha thamani sana Omba msaada utapewa japo kidogo hii ni kwa majira ya asubuhi.

•Utapata maudhi maudhi leo na zitakufikia habari mbaya mbaya maadui zako wanakutafuta ila hawakupati endelea na ibada zako zaidi na usirudi nyuma.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Utajikita umefufua penzi lako liliokuwa vlimechuchuka siku ambayo utaelewana na kila mtu Utaingia makubaliano yà kushirikiana jambo habari za posa uchumba na ndoa zitatawala Uliyemuagiza akufanyie kitu amefanikisha kuwa makini na mahusiano mapya uliyoyaanzisha yatakuwa na kelele nyingi.

•Kazi zako zitaenda kwa wepesi mkubwa na utafanikiwa kila unalolifuatilia katika mambo yako ya kikazi au biashara.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Suala la mahusiamo sio zuri kumeingia dosari kuwa makini Kumetokea kuzorota kwa penzi taarifa zinazokufikia ni mbaya Kuna kupeana talaka na ndoa kuvunjika yale matarajio ya kupewa tenda uliyoiomba hutaipata Utalazinika kutumia hila au nguvu Utapokea taarifa za maziko.

•Mahusiano yako yatakuwa vizuri na watakosa nguvu wafitini wako.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Jiandae kwa mabadiriko yatakayo fanyika leo Kuna taarifa za safari au kuhamishwa Utapokea taarifa kutoka kwa mtu aliye mbali pia kuna mgeni ambaye anakufuata wewe Kuja kwake kutakuwa msaada mkubwa kwako.

•Utapata habari nzuri sana leo na haja zako zitatimia bila shaka yoyote.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Tarajia kupata mafanikio katika shughuli zako kazini utapewa jukumu la kusimamia jambo Ambalo litakuletea heshima na kukuinua ki uchumi tegemea kupata uhamisho wa kwenda kufanyia kazi eneo jingine.

•Safari zako sio nzuri leo tulia nyumbani kuna misukosuko katika safari zako.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Utapata nafasi ya kuwa msemaji kwenye mkutano utakaofanyika leo shirikiana na wanachama wenzio katika kuimarisha umoja wenu utapata wasaa wa kudhibiti hali inayo ikumba jamii yenu.

•Utafanikiwa kurudisha matumaini miongoni mwenu siku ya maelewano na kushirikiana na marafiki.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Kutajitokeza upinzani na kupingana pingana na watu wako wa karibu Uko kwenye wakati mgumu tarajia kupata safari ya ghafla Acha kubishana ovyo utajikuta umepata kesi ya kujibu habari za kufungwa kuibiwa na kupotea kwa kitu zitakuhusu.

•Safari zako sio nzuri utapata balaa au bahati mbaya.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Usipoteze muda kwa kufikiria cha kufanya huu ni muda muafaka kwako kufanya utakacho Shughulikia fursa mpya zinazojitokeza leo utakutana na mtu ambaye hamkuwahi kujuana nae tegemea kupata habari za kustusha zinazohusu mtoto na mimba.

•Utapata matumaini mazuri kwenye mambo yako na utulivu mkubwa utajidhihirisha katika maswala yako pia kazi zako zitaenda vizuri na biashara zako zitastawi zaidi.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Utapokea taarifa za kupatikana kwa kazi mpya ahadi uliyopewa itatimizwa.

•Siku nzuri kwako kupata ulicho kuwa unatafuta utapokea pesa leo kutoka kwa mtu uliye anzisha nae mahusiano hivi karibuni.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Hali ya uhitaji wa kazi na pesa itawakumba jamaa zako wape ushirikiano Njia nzuri ya kufanikisha malengo yako ni kuwa pamoja katika kila jambo Kazi za kijamii zitawamufaisha leo tembelea ndugu na jamaa zako na fanya mawasiliano nao.

•Mahusiano yako yataingia kiza na vurugu zitajaa ndani kwako au kutokuelewana na mwenzako.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Shughulikia masuala yako yanayo kutatiza kwa kukutana na viongozi wa ukoo Hujarogwa wala kufanyiwa fitna yoyote kuna jambo limesahaulika kwa kipindi kirefu Ni siku nzuri kwako kuwà karibu na wazee mambo yatakuwa shwari.

•Mahusiano yako yapo vizuri na hakuna tatizo kubwa kila kitu kitakuwa sawa.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Kuna kuombwa au kupokea misaada kutoka nyumbani usiwe mbali na watoto au watu uliowazidi umri.

•Shughulika ile habari ya mikopo iko kwenye muelekeo mzuri utapokea mualiko wa sherehe nenda lakini fuatana na mtu.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250629-WA0012(43).jpg
 
NYOTA YAKO LEO IJUMAA AGOSTI 08/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Tumia siku yako vizuri utajikuta ni mwenye kufurahia jambo Leo masuala ya ndoa uchumba na posa yatakuwa vizuri Utajikuta inakamilisha jambo muhimu na kukubaliana katika shughuli uliyoomba Tarajia kujikuta katikati ya penzi jipya.

•Licha ya kuwa ni siku miongoni mwa siku zako za bahati lakini leo utapata naudhi sana ikiwa utasafiri au kwenda popote mbali safari yako haitakuwa na kheri na utahuzunishwa.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Pamoja na kuwa ni siku nzuri lakini mambo yako yote yatakuwa na ucheleweshwaji Ili yaende uzuri uñashauriwa kupaza sauti na kutumia nguvu Sio siku ya kuacha mambo uajiendee tafuta msaada na utapata Taarifa utakazo pokea leo si nzuri.

•Kazi zako leo usitumie nguvu kubwa kwakuwa utakaokutana nao leo hawana utu wala huruma na wewe.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Utatembelewa na mpenzi ambaye anaishi mbali unatakiwa kufanya mabadiliko katika taratibu zako Shughuli uliyo iomba itahitaji makubaliano na leo utatakiwa kusafiri kwenda kukamilisha mkataba.

•Safari zako leo zina majuto panga siku nyingine.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Uko kwenye kipindi cha mafanikio utapanda daraja na kupata heshima kubwa Kile cheo ulichokuwa unakisubiri utafanikiwa kukipata ila ni kwa taabu saana Biashara zitakua nzuri na kukufanya uheshimiwe Utapewa jukumu vla kusimamia shughuli.

•Utapata matumaini mazuri na habari nzuri sana leo haja zako zitatimia na siku itakuwa ya faraja na baraka kwa kila jambo lako.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Acha kujitenga jumuika na jamaa zako leo una nafasi kubwa ya kuondokana na shida zilizokuwa zinakuandama.

•Hudhuria mualiko wa mkutano utakaofanyika leo kuwa karibu na rafiki zako Kuna taarifa utapokea kutoka jamaa mbali.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Matumaini yote yatapotea utajikutà ni mwenye kuhangaikia hali iliyojitokeza ya kukwama kwa shughuli zako Utaporomoka kibiashara na kiuchumi utapoteza nafasi iliyokuwa nayo Fitna na majungu zitakuandama tafuta suluhisho kabla hujapotea.

•Kazi zako ni nzuri usikatae wito wala maelekezo yoyote ya kheri.

★NDOO– AQUARIUS 🏺(January 21– February 19)

Jitathmimi upya na hali unayopitia achana na kundi kubwa la marafiki wasio na faida kwako Ni kipindi cha kuwa na watu wapya wenye tija kwako anza upya katika kila jambo Mafanikio hayako mbali kuna mtu ambaye hamkuwahi kujuana nae atakupa ushauri utakao kufaa.

•Mahusiano yako kwa leo hayana tatizo au maswala ya mapenzi hayana tatizo pia safari zakk ni nzuri.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Utafanikiwa kulipwa pesa ambayo umekuwa ukidai kwa muda sasa Mipango yako ya kazi inahitaji kuishughulikia utapata lakini ni baada ya kuondoa vikwàzo.

•Utapata maudhi leo na siku itakuwa ya kero kero kwako na kelele na watu wako au unaoenda kukutana nao au kuonana nao mtapishana kauli au watakuudhi.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Kwa kupata unachokihitaji unashauriwa kutokukaa nyumbani toka kwa matembezi ya hapa na pale Huko utakutana na jamaa zako watakao kushauri nini ufanye Mawasiliano ni muhimu.

•Ikiwa kuna watu wanakudai basi walipe haki yao kwakuwa hiyo haki yao inaweza kukukwamisha kwenye mengi siku za mbele.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Masuala ya kazi na pesa yanahitaji majadiliano na viongozi wako umekuwa unasumbuka sana katika utafutaji wako Shirikiana nao katika kila hatua utakazo pitia hatimae utafanikiwa.

•Safari zako ni nzuri na kwa ujumla siku yako ni nzuri.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Leo utapata utakacho, kupitia kwa ndugu na jamaa zako tarajia kusaidiwa na watu wako wa karibu shughulikia masuala ya mkopo uliouomba Timiza nadhir zako kama ulivyo jiapiza utafanikiwa kununua ulichojipangia Siku nzuri kwako jipongeze kwa kujistarehesha.

•Kazi zako zitaenda kwa uzito asubuhi lakini mwisho wa siku mambo yataenda vyema pia safari zako ni nzuri zina kheri kwako.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Hali ya nyumbani inatia shaka taarifa za mgonjwa na kuugua kwa mtu muhimu tumia muda mwingi ukiwa umetulia nyumbani kuna mzozo utakao zuka baina yako na mtu mkubwa usijihusishe katika kubishana na watu usio lingana nao hasa walio kuzidi umri.

•Mahusiano yako hayana tatizo kwa leo ila usiwe mlipa visasi hii itakurudisha nyuma daima.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250629-WA0012(44).jpg
 
NYOTA YAKO LEO JUMAMOS AGOSTI 09/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Taarifa utakazopokea leo si nzuri ule msaada uliokuwa unauhitaji hutoupata Masuala ya watoto yatakuletea shida na shughuli zako nyingine hazitafanikiwa kuna kukwama kwama Leo tulia nyumbani usifanye safari zitakusababishia ajali au kukwama njiani kwa kipindi kirefu.

•Mahusiano yako na watu yatakuwa mazuri zaidi na utakuwa mwenye kufanikiwa kwenye kazi zako heshima yako itaongezeka na utasifiwa au kupongezwa.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Kuna habari za mgeni kutoka mbali kufika kwako na atakupa taarifa za kufanyia mabadiliko jambo fulani Kuna habari za safari na mpango wa kuhamishia biashara sehemu nyingine ukiomba msaada utapewa lakini kutoka mbali ya hapa au nje ya nchi.

•Mahusiano usiyape kipaumbele kwa sasa hayana nguvu yoyote ya kheri kwako pia safari zako ni nzuri sana.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Tarajia kufanya vizuri katika shughuli zako mahusiano uliyoyaanzisha yatakuletea mafanikio makubwa Utajikutà umepata heshima na nafasi ya kuongoza biashara zitanyooka na suala la uchumba posa na ndoa kitakwenda vizuri.

•Biashara zako na kazi zako zitazidi kustawi na kuzidi kukupa nguvu na bahati za wewe kufika mbali kwenye maisha yako.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Mambo yako yanaelekea kuwà mazuri na utafikia malengo uliyo jipangia Unatakiwa ufanye kazi na wenzio umshirikishe jamaa au rafiki yako wa karibu Leo usiwe pekee kuwa na marafiki au wanachama wenzio kikao mtakachofanya kuna jambo lenye manufaa kwako kutajitokeza.

•Utapata bahati nzuri sana Leo na faraja itakufika.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Kuna kukwama kwa safari ulivyotakiwa kwenda kuna mtu ambaye amekuwa akipingana na wewe kakuvurugia Kuna taarifa za upinzani mkubwa kutoka mbali zitakazo kufikia na kukufanya ubadili msimamo wako tafuta njia ya kujikwamua matumaini ya kusafiri siku zijazo yanaonekana bado yapo ila ni baada ya kutembelewa na mtu.

•Tumbo linaweza kukusumbua kwa muda litakuachia na utapata ugeni wenye kheri na wewe ukirimu utaneemeka baadaye.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Anza kufukuzia nafasi unayoitaka hiki ni kipindi ambacho kama utaweka mkazo kwenye shughuli yoyote ile itakwenda vizuri Mafanikio yapo karibu ila yanahitaji juhudi binafsi Kuna jambo au kitu kipya ambacho huenda utapata leo shughulilikia mambom kwa kujitangaza usifaye kimyakimya.

•Utapata kitu kizuri Leo au pesa tegemea mazuri zaidi pia Safari ni nzuri.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Utapokea taarifa za kazi na kupata pesa kwa ajili ya kazi iliyoahidiwa na jamaa yako Matumizi yako binafsi yataongezeka kuwa makini yasikuvurugie mipango yako Kuna kazi mpya utapata.

•Mahusiano yako yataimarika na migogoro itaisha.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo utajikuta unapingana na jamaa zako tafuta njia ya kuondoa hali hiyo Watembelee au fanya mawasiliano nao hii itakusaidia kupunguza shida zako.

•Utapata furaha leo na bahati nzuri zitakufikia haja zako zitatimia bila wasiwasi wowote.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Matatizo yako yatamalizwa na mtu ambaye amekuzidi umri mzazi au kiongozi yeyote ambaye ni mkubwa kuliko wewe Muelezee yote yanayo kukabili na atayashughulikia leo ni vizuri ukawa umetulia nyumbani Kuna taarifa zisizo rasmi zitakufikia kuhusiana na mimba au mtoto.

•Safari zako leo sio nzuri unaweza kupata mkosi au bahati mbaya bora kutulia nyumbani kwako na ikiwa lazima sana kutoka basi usikawie kurudi na usiwe wa kwanza kwenye mazungumzo kwakuwa mwisho mtagombana.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Utakuwa na maombi mengi ya watu kutaka kusaidiwa au kukopeshwa usihofu na wewe fuatilia maombi yako uliyotuma kwa kutaka mkopo na msaada Kutana na mwanao atakuwa na taarifa nzuri utapokea barua na mualiko.

•Kuwa makini sana Leo kwa kila kitu haswa ikiwa umeenda kazini usipingane na majukumu utakayopewa yatakuharibia kazi moja kwa moja na ikiwa nyumbani kwako basi hata ukiona mwanao kapigwa mchukue usijibizane kwakuwa vyote hivi vimetegeshwa ili wewe uingie kwenye hatari upepo mbaya unakunyemelea kupitia haya hivyo ukiuingia utakuwa matatizoni.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Chunga kauli zako kwa leo zitakuletea matatizo Utapata lawama na kujikuta katika ugomvi mkubwa sana na jamaa zako kuna kupotelewa au kuibiwa kitu cha thamani Kupata kitu chochote kile unalazimika kudai au kulalamika sana taarifa za kuuguliwa na habari za mgonjwa zitakufikia.

•Kazi yako kwa sasa inafitna sana za watu wanachonganisha huku na huku ili kuhakikisha unaharibikiwa lakini ni ngumu hilo kutokea jitahidi tu kuwadhibiti aidha kwa ibada dua maombi au sadaka na yasikutishe ni mapito.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Utakuwa na jukumu la kusuluhisha mgogoro wa muda mrefu sana leo itapokea taarifa za kukubaliwa ombi lako la kandarasi.

•Masuala ya mapenzi na ndoa yatakwenda vizuri utajikuta uko kwenye mahusiano mapya ambayo umeyaanzisha hivi karibuni hali ya nyumbani iko vizuri utafurahia kila jambo utakako lifanya leo.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250809-WA0044(1).jpg
 
NYOTA YAKO LEO JUMAPILI AGOSTI 10/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANG FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Kuna safari ya kwenda kuwatembelea watoto leo Utapokea mgeni au taarifa za kubadirishwa kwa ratiba yako Leo utakutana na mtu mliye poteza kwa muda mrefu suala la msaada na mikopo litasogezwa mbele.

•Kazi zako zitaenda vizuri na biashara zako zitafunguka na kukupa faraja zaidi pambana.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Utapata mafanikio makubwa katika shughuli zako usiwe na haraka haraka kati kuamua jambo Omba msaada katika tatizo likakalo jitokeza ghafla na utafanikiwa kupata japo kwa uchache na kusemwa semwa.

•Utapata bahati nzuri sana Leo na faraja itakufika pia Safari zako ni nzuri sana Kwa leo.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Maelewano na rafiki yako vyataimalika utajikuta umeingia mkataba nae Mtasuruhisha yaliyo wakwaza na kuanza upya kutaneni na mpange cha kufanya kwa ajili ya baadae.

•Biashara zako na kazi zako zitazidi kustawi na kuzidi kukupa nguvu na bahati za wewe kufika mbali kwenye maisha yako.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Jizatiti katika shughuli zako hali bado ina ugumu kidogo Na adui zako hawajachoka wanakufuatilia kwa chinichini Jiandae kuanzisha shughuli nyingine tafuta msaada na utaupata lakini ni baada ya kutokea ugomvi mkubwa.

•Mahusiano usiyape kipaumbele kwa sasa hayana nguvu yoyote ya kheri kwako.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Anza kufanya maandalizi ya safari ya ki maisha Unatakiwa kubadilisha biashara na shughuli unazozifanya na ikiwezeka hama hapo unapofanyia Tangaza shuguli zako kabla hujaanza kuzifanya lakini ziwe mpyaachana na mambo ya zamani.

•Ukikutana na mtu yupo mtupu kabisa Leo awe kichaa au mzima ni ishara mbaya kwako na unaweza kudhalilishwa au siri zako kuwekwa wazi na ukikutana na mtu ambaye hapendezi mara nyingi Leo kapendeza basi utafarijika mno Leo na siku itakuwa ya bahati kubwa kwako.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Utafanikiwa kupata utakacho kazi na pesa hazitakusumbua kwa leo Kazini utapata mabadiriko katika nafasi ya utendaji utaongezewa cheo kingine na kuwa kiongozi wa idara
Matumizi yako yalingagane na kipato chako utajikuta unaheshimiwa na kila mtu.

•Utapoteza kitu muhimu Leo na usilazimishe jambo lolote leo utapata bahati mbaya.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Jenga mazoea ya kuwatembelea jamaa zako katika kipindi hiki fanya mawasiliano nao mara kwa mara Mbali ya urafiki mnatakiwa na mshikamane kama ndugu Filikirieni kuanzisha shughuli ya pamoja itawapa mafanikio makubwa Uusipuuzie simu utakazopigiwa na ujumbe utakao tumiwa leo kwa ujumla leo ni siku nzuri kwako.

•Safari zako ni nzuri ila usiwe muwazi kwa kila mtu juu ya safari zako.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

JumapiliI ya leo itumie kuweka mambo sawa Kutana na mwanamke mtu mzima ambaye ni kiongozi wa katika ukoo atakusaidia kuliweka sawa jambo hili.

•Utapata rafiki mpya Leo na utasaidiwa mengi katika mambo yanayokunyima furaha kwa wazi na kwa siri.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Anza kushughulikia masuala ya watoto na masomo leo unatakiwa kutumia muda wako kifuatilia suala la mikopo na misaada Omba tena upya ndio utafanikiwa unashauriwa kutumia kama ulivyo jipangia.

•Mahusiano yako yataendelea kuwa na kelele za hapa na pale usitaabike nayo ni kawaida ya mahusiano yako kuwa na vurugu za namna hiyo.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo utapata wasiwasi au khofu kwenye mambo yako na hali inatokana na maneno maneno ya watu ambayo yatakuzalishia migogoro na hali ya kutokuelewana na watu fulani kutokana na wivu tu wakimaendeleo stahmili yote yanapita na utazidi kuinuka kimaisha hizi ni katika hatua zako za kusonga mbele.

•Safari zako ni nzuri kwa ujumla siku ni nzuri sana kwako.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Leo utajikuta katika dimbwi la furaha masuala ya mapenzi yako vizuri Utafanikiwa kuanzisha mahusiano mapya kuna maelewano makubwa kati yako na jamaa zako Utafanikiwa kupata kandarasi uliyoomba.

•Safari zako ni nzuri lakini jihadhari na ugomvi utakuletea shida kubwa.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Nyumbani hakuna maelewano hali ya uchumi sio nzuri kuna vikwazo nà kuzorota kwa mahusiano Kutazuka ugomvi na wazee tumia busara kulimaliza jambo hili Kuna taarifa mbaya utapokea.

•Ikiwa unaumwa umwa basi shida kubwa ipo tumboni nenda kapate utatuzi kwa wajuzi wa hayo maswala ya afya kwakuwa unaweza kulivumilia na likakuzalia makubwa zaidi.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250810-WA0062.jpg
 
NYOTA YAKO LEO JUMATATU AGOSTI 11/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.
MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.


★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Utafanikiwa kupata utakacho masuala ya kazi yapo vizuri utapata nafasi nyingine ya uongozi Biashara zitakua nzuri na zitakupa heshima kubwa itajikuta uko juu Shughulikia suala la mkopo na misaada kutoka kwa mtoto wasaidie watu wenye uhitaji timiza nadhir zako.

•Mahusiano yako ya Siri hayana kheri kwa sasa yatakuharibia kila mpango wako mkubwa unaoutegemea na itafika mahala utashindwa kuhimili yaliyopo utashindwa kujisaidia.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Leo utajikuta katika ugomvi na jamaa au rafiki yako ni kipindi ambacho unatakiwa kutoa maamuzi juu ya hatma ya mahusiano yenu Amekuwa hana misaada kwako kuna mtu atajitokeza na ataonyesha kubwa karibu nawe shirikiana nae.

•Mahusiano yako na watu wako yatakuwa mazuri zaidi na maadui zako watazidi kuporomoka na utawafahamu pia safari zako ni nzuri.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Kuvurugika kwa mahusiano kuna fitna na chuki zimepandikizwa Makubaliano yameshindikana na mipango ya kupata kandarasi haipo tena Tafuta msaada haraka kutoka kwa wataalamu kuna mambo ya kiswahili yanafanyika Uchumba posa na ndoa vimesogezwa mbele.

•Matumaini mazuri mno yatazidi kujidhihirisha kwako maradhi yanayosumbua mwanao au wewe mwenyewe basi yataisha na afya itaimarika zaidi.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Jipange upya katika kila jambo unalotaka kufanya ni kipindi ambacho unatakiwa kuachana na mambo ya zamani tangaza shuguli zako utapata mafanikio kama ilutaanzisha chochote kile Utapokea taarifa ambazo hukuzitegemea na ni mpya kwako.

•Tamaa zako ni nzuri na utafanikiwa kila unalolitamani litatimia kwa jitihada zako.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Mipango ya pesa na kazi iko vizuri utopkea pesa kutoka mbali au nje ya nchi na pengine kwenda kikazi Utaitwa na mtu ukachue pesa ya kuanzia kazi epuka matumizi makubwa yasiyo na lazima.

•Utapata maudhi makubwa leo na haja zako hazitatimia ila baada ya maudhi makubwa.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Utakuwa na wasiwasi kuhusiana namafanikio yako Jenga ukaribu na viongozi wako watakufikiria katika nafasi fulani Utapata mafanikio hivi karibuni na utaheshimika Kutana na wanachama wenzio mpange cha kuanza nacho.

•Mahusiano yako yapo vizuri na ugumvi wowote uliopo upuuze usiufuatilie sana hauna umuhimu kwa sasa kwako.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Kama utatulia nyumbani utakuwa wakati mzuri kukutana na wazee kutasaidia kutatua changamoto zinazo kukuta Washirikishe rafiki zako katika masuala yanayohusu malezi ya mtoto uliyezaa nae atakupa wakati mgumu.

•Safari zako leo zina mashaka mashaka lakini utafika salama.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo utapata misaada na kutakiwa na wewe utoe kwa wengine fanya hivyo kwa watoto na watu wenye uhitaji mkubwa Kutatokea vikwazo kidogo ila ni kwa muda si vibaya kama utajipongezea kwa hatua uliyoifikia.

•Kazi zako nyingi Leo zitakuwa za lawama na makelele hali ya kutokuelewana na mabosi zako vumilia Leo na ujizuie na kelele hizo kwakuwa zitaharibu biashara au kazi yako.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Siku si nzuri kwako usijichanganye na watu wasiofaa epuka kufanya mambo kwa haraka haraka Utaanza kupokea lawama kuhusu upotevu wa kitu hii itapelekea kutokea ugomvi mkubwa utakao kufikisha kwenye vyombo vya dola Utapokea taarifa za mgonjwa na kuharibika kwa kitu.

•Mahusiano yako yanaonekana yatakuwa pabaya na hakuna suluhu juu yake hivyo jitahidi umalize migogoro uliyonayo na mtu wako wa karibu kinyume na hapo hakuna kitakachoendelea kizuri kati yenu mtaishi maisha ya kinyama kila mtu na yake na hakuna kuulizana.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Kutakuwa na kuelewana katika masuala ya pesa na kazi utaingia makubaliano na mtu au taasisi Leo ni siku yako kwa yale uliyo yaanzisha utajikutà unafurahia mahusiano mapya Utapata ushindi kwenye kandarasi uliyoiomba.

•Safari zako ni nzito nzito leo na kuna ishara mbaya njiani pia unashauriwa usibishane na mtu leo au watu inaonekana utazomewa.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Utapokea taarifa za maziko ya ndugu au jamaa yako Mambo yako yataingia kwenye mkwamo na wewe kulazimika kutumia nguvu usipuuzie simu utakazo pigiwa na ujumbe utakao tumiwa hukumu ya kesi itatolewa lakini si nzuri kwa mshtakiwa Usifanye safari ya mbali.

•Utapata maudhi asubuhi ya Leo na mchana wake pia zitakufikia habari sio nzuri siku ya leo haswa kutoka mazingira ya ugenini au sehemu ngeni uliyopo.

★KAA– CANCER 🦀(Juni 21– Julai 22)

Unatakiwa kusafiri kwenda kukamilisha baadhi ya mambo yako nyumbani kazini kutatokea uhamisho Utalazinika kuhama hapo unapoishi kuna mgeni anakuja kwako mpe ushirikiano mambo mengi yatabadirika kubali ushauri wa wazee.

•Migogoro yako watu wako kwenda tofauti na makubaliano au migogo na wafanyakazi wenzako au wateja wako inatengenezwa na watu hivyo kuwa makini na kujiamini au kuwaamini sana wanakuharibia ilhali umewakumbatia.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250810-WA0062(1).jpg
 
VIJUE VITO NA MADINI YANAYOENDANA NA NYOTA YAKO.

SEHEMU YA PILI

Dr. DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️

Kwenye masomo yaliyopita, nilifafanua kwa kirefu kusema kwamba kila Nyota ina madini na Vito vyake maalum, vinavyoihusu.
Kwa wanaosoma masomo haya Kwa njia ya mtandao (Whatsapp) nilivielezea Vito vya thamani (mawe) almaarufu gemstones pamoja na madini ambayo yanaendana na kila Nyota.

Kwa wale tuliokwisha soma ile mada ya REINCARNATION mtakumbuka kwamba kila kiumbe kinahusiana na kiumbe kingine kwa namna moja au nyingine, yaani tumeunganishwa na uumbaji wote.

Sisi watu hatuwezi kuishi bila uwepo wa viumbe vingine.
Hatuwezi kuishi bila wanyama, ndege, wadudu, mimea, mawe, maji, hewa, Nyota, Sayari nk. nk. nk.

Tunategemeana.

Kuna nguvu za kiroho tunavuna kutoka kwa kila kiumbe.

Viumbe vinatusaidia kuvuna (absorbs) NISHATI CHANYA na kuondoa (emits) NISHATI HASI!!

Kumbuka maisha ya kila kitu ya yanaongozwa na NISHATI na kila kitu ni NISHATI.

Hata mimi na wewe ni NISHATI, unaweza kuita ROHO ukipenda!

Mfano unaweza kutumia kitunguu swaumu kuondoa uchawi unaotokana na kijicho (evil eye)
Unaweza kutumia mafuta au chochote kinachotokana na Ngekewa kuvuta bahati mbalimbali.

Unaweza kutumia maji ya chemichemi kuamsha nguvu zilizolala.

Unaweza kutumia chumvi ya mawe kuondoa mikosi, nuksi nk.

Hii ni kuonesha kwamba KIROHO tunavihitaji vitu vyote kutusaidia.

Ni Power of Nature.

Kuna watu wanafuga mbwa au paka ili kuwasaidia kutambua endapo wachawi watakaribia nyumba zao.
Kumbuka mnyama Paka amebeba nishati ya hali ya juu ya utambuzi wa nguvu za kiroho zilizo safi (positive or holy) na hata chafu (negative or evil)

Umewahi kuona namna ambavyo kila mtu anapotembelea nyumba yoyote alipo Paka, lazima Paka amkague!

Unajua anakuwa anakagua nini?

Anakagua kuona kama ni "mtu mzuri" au "mtu mbadi" (kama Mwaisa🤣🤣🤣)

Nimejaribu japo kwa kifupi kuwaelezea hayo ili mjue kuwa SISI NA UUMBAJI WOTE TU UMOJA, YAANI 'we are connected"

Tuendelee sasa na elimu ya mawe au vito pamoja na madini kwa kila Nyota . . .

Kwenye Kanuni ya Uumbaji, kila roho (consciousness) au kila mtu, tuseme 'binadamu' ameumbwa ili kutimiliza kusudi fulani, ndipo arejee kwenye asili yake (super cosmic being)

Mtu asipofanikiwa kutimiza kusudi lake uwa anapewa nafasi nyingine tena na maumbile; maana sheria ya maumbile inatoa nafasi au awamu karibu 9 (108 formula) za ku- reincarnate, yaani kurudi duniani kukamilisha kusudi ambalo hukulikamilisha huko nyuma.

Ukiona kwenye NATAL CHART yako kuna emptiness (nyumba tupu) ujue ulishakamilisha kusudi kwenye huo mlango/ nyumba.
Palipo na Malaika au Planets, panakuwepo na jukumu au majukumu ambayo hukuyakamilisha.

Sisi sote tulishaishi duniani maelfu ya miaka mingi iliyopita, tunakuja na kuondoka, tunakuja na kuondoka bila kukamilisha yote, bila kutimiliza yote ndio maana tumerudishwa tena, tupo hapa Mimi, wewe na yule for unfinished businesses!

Ndio maana nawasisitiza watu wote kuwa makini na pale ambapo una wajibu, ujikite hapo kwa bidii zote.

Endapo mtu atazaliwa tena na tena mpaka zile awamu zake zikaisha, basi ANASHUSHWA CHEO; kutoka kwenye HUMANOID KINGDOM (umbo la kibinadamu) kwenda kwenye ANIMAL KINGDOM na anapewa mwili wa mnyama fulani.
Wanyama hawana nafasi ya ku-reincarnate, wakifa bila kutimiza makusudi ya kuwepo kwao duniani, miili yao inaharibika, lakini roho zao zinaingia kwenye PLANT KINGDOM.

Mimea, miti na kila kinachoota ardhini na chenyewe kina wajibu duniani, lazima kiutimize; kisipofanya hivyo kinashushwa daraja na kuingia kwenye MINERAL KINGDOM!

Nilishafundisha hayo kwa marefu na mapana kwenye mada ya REINCARNATION, huko nyuma.

Mawe yote, madini, mchanga na vyote vilivyopo chini ya ardhi ni roho au consciousnesses ambazo zipo kwenye Mineral Kingdom!

Mamilioni ya miaka huko nyuma, hizo Consciousnesses ziliwahi kuwa kwenye maumbo ya binadamu (humanoid kingdom)

Kwa hiyo hizo ni Consciousnesses, ni roho.
Zinajua kila kitu ila ziko dormant.

Nguvu nyingi sana za kiroho zinapatikana kwenye ardhi na chini ya ardhi kwa sababu roho za wazee waliowahi kuishi thousands and thousands of years ZIMELALA PALE!

Ndio maana kinyota, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mtu wa nyota fulani na mawe/ Vito pamoja na madini aina fulani.

SOMO LITAENDELEA . . .


Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi

By Dr DOGOLI KINYAMKELA 💀☠️ , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
No reform no election
 
NYOTA YAKO LEO JUMANNE AGOSTI 12/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU MBANDE KIPONZA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

jumanne hii tegemea mambo mazuri kwako kwani utapata mtu atakusaidia kutokana na matatizo unayo yapata katika kipato chako huenda leo hii ukapata mtu akakuondolea madhila hayo.

•Leo ni siku ya kuchukua hatua Usipoteze muda kwa kusita kama kuna jambo limekuwa likikukwamisha leo utapata njia ya kulipenya fedha zinaweza kuja kupitia njia isiyotarajiwa usiku omba dua kwa jambo unalolitamani sana.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Jumanne hii ni nzuri kwako kuwa mkweli muaminifu unaweza kupata mtu atakae kusaidia matatizo yako ingawa una changa moto nyingi sana lakini usikate tamaa itakaa vizuri.

•Unae mpenda hana muda na wewe kutokana na mtafaruku katika mahusiano yenu endelea kunyenyekea bila kuchoka punguza kulalamika na kulia mambo yatakaa sawa.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

jumanne hii ni nzuri kwako epukana kuongozana na makundi makundi pia endelea kukaa karibu karibu na yule unae mtegemea atakukamilishia ahadi alio kupa kikubwa uwe mwenye subra na muelewa.

•Usimuache mpenzi ulie nae bilasababu kwani huyo ulie nae ni muongo nivyema ukae chini na mpenzi wako muweze kuyazungumza kwani usipo fanya hivyo unaweza kuikosa amani kwa muda mrefu.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

jumanne hii kipato chako kitaongezeka utapata pesa ya gafla ingawa una madeni lakini usife moyo utapata mbinu mpya za kuweza kupambana na madeni yako.

•Utulivu wako utakuwa silaha kubwa leo Hata hivyo unahitaji kuwa makini na watu wenye tamaa ya kutumia udhaifu wa wengine Nyumba na familia vitahitaji muda wako.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹(November 22– December 21)

jumanne hii ni njema kwako tegemea kukamilika kwa ahadi kwa mtu alue kuwahidi tegemea mipango mipya itakayo jiri kutoka na frdha kidogo utayo ipata.

•Epukana na marafiki wanao jaribu kukushawishi kuachana na mpenzi ulie nae kwani mtu ulie nae ni muhimu sana kwako hivyo kumkosa nisawa na kukosa kiungo muhimu katika mwili wako utateseka kwa muda mrefu.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Jumanne hii ni nzuri kwako sasa niwakati wa kutimiza malengo yako nakufanya kile unacho ona kinakufaa kwa maisha yako ya baadae nivyema kujiamini ukiwa unakamilisha majukumu yako.

•Jumanne hii ni nzuri kwako kimapenzi tegemea habari njema kutoka kwa mpenzi wako itakayo kupa furaha katika moyo wako zidi kuwa karibu na mpenzi wako ili furaha ulio nayo izidi kuendelea.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

jumanne hii sio mbaya sana kwako ingawa sio yote unayo yapanga yatakamilika ila endelea kupanga mipango yako mbali mbali kwani mbeleni matunda utayaona.

•Utakumbukwa na mpenzi wako wa zamani ingawa unae mpya wa sasa usipo kuwa makini unaweza kuiondowa amani ulio nayo kwasasa nivyema ukawa na msimamo uliokamilika.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

jumanne ilio isha ilikuwa nzuri kwako kipato chako kiliongezeka jumanne hii pia utapata kipato kikubwa usidharau simu ya mtu yoyote atakae kupigia kwani kuna simu leo hii utapigiwa na utapata habari za muhimu sana zitakazofanya kipato chako kiongezeke na utafanya vizuri popote kwa chochote unacho kifanya.

•Mawasiliano yako leo yana nguvu kubwa Unaweza kupata habari muhimu itakayokusaidia kuamua jambo kubwa Kwenye mapenzi kuwa makini na maneno yako yanaweza kuponya au kuumiza.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

jumanne hii sio nzuri kwako usipo kuwa makini utapoteza fedha katika biashara zako au utapoteza kitu cha thamani unashauriwa kufanya maombi au kufanyiwa dua na kadhalika nyota yako itakaa sawa.

•Unashauriwa upunguze kiburi na misimamo isio na maana kwani ukiendelea kufanya hivyo hutaweza kumaliza migogoro ya mapenzi ulio nayo leo hii mpe mwenzieo nafasi msikilize mambo yatakaa vizuri.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

jumanne hii unauwezo wa kukamilisha mipango yako ya kibiashara pia unashauriwa ukutani watu tafauti tafauti wenye fani kama ya kwako watakusogeza na kukupa mbinu mpya katika biasha yako au miradi yako ingawa kipindi hii nyota yako imetawaliwa na upepo mbya.

•Leo utahisi nguvu ya kiroho na hisia zako zitakuwa juu sana watu wa nyumbani wanaweza kukuona kama nguzo ya matumaini.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

jumanne hii utafanya vizuri utapata mawazo mapya na ushauri Mpya kutoka kwa marafiki zako ingawa bidii Yako ya kazi ilipunguwa siku zilizo pita lakini kwasasa tegemea mabadiliko mapya katika kazi zako jitume bila kuchoka kwani mbele yako kuna mengi yenye faida yatajiri kwako.

•Ni siku nzuri ya kufanya ibada au maombi ya shukrani. Fedha zinaweza kuongezeka kidogo kutokana na juhudi zako.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Jitahidi kuweka sawa tatizo linalo kusumbuwa kati yako wewe na mpenzi wako kuwa muwazi kwa kile unachotaka kumuambia kwani msipo fanya hivyo ugomvyi unaweza kuwa mkubwa zaidi mkaingia mashakani.

•Ni siku nzuri kwa kushirikiana na watu wa karibu katika mradi wa pamoja.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.1
IMG-20250810-WA0062(3).jpg
 
NYOTA YAKO LEO JUMATANO AGOSTI 13/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.



★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

jumatano hii utakutana na mtu atakusaidia mambo mengi sana kutokana na ukarimu wako ulio nao nivyema usidharau mtu kwani maisha yako sehemu kubwa unaishi kutokana na ukarimu wako nivyema pia ukawa makini ucije ukatapeliwa kwani kuna watu ambao wanataka kuchukuwa haki yako kwa njia ya utapeli.

•Ukikutana na mtu yupo mtupu kabisa Leo awe kichaa au mzima ni ishara mbaya kwako na unaweza kudhalilishwa au siri zako kuwekwa wazi na ukikutana na mtu ambaye hapendezi mara nyingi Leo kapendeza basi utafarijika mno Leo na siku itakuwa ya bahati kubwa kwako.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

jumatano hii tegemea mambo mazuri ahadi nzuri kutimia ingawa una madeni mengi lakini unashauriwa usiwakimbie wadeni wako kwani kuwa nao karibu inaweza kukusaidia wewe mwenyewe na huenda wakakupa muda zaidi wa kuweza kumalizia deni.

•Mahusiano usiyape kipaumbele kwa sasa hayana nguvu yoyote ya kheri kwako safari zako ni nzuri sana.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

jumatano hii unashauriwa uwende safari ambayo umekuwa ukiipanga kila Siku bila kutekeleza in vyema zaidi ukasafiri kwani safari hiyo inaonekana kuwa na faida kwako.

•Chaguwa kati ya wapenzi watatu ulio nao ubaki na mmoja kwani unashindwa kufanya maamuzi ya mapenzi kutokana na wapenzi wengi no vyema ubaki na moja kwani endapo utaendelea kubaki nao wote watakuja kukukimbia na utakosa msaada.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– Oktoba 23)

jumatano hii unashauriwa kusikiliza shida za wafanya kazi wako kwani wamekuwa wakisononeka juu ya shida zao kwakuwa umekuwa ukiwaahidi mafanikio in vyema kuwasikiliza na kuwatimizia Yale ulio wa ahidi ingawa hutoweza kutimiza yote lakini itakuwa nafuu kwako kwa Yale utakayo weza kutimiza.

•Mahusiano yako yataendelea kuwa na kelele za hapa na pale usitaabike nayo ni kawaida ya mahusiano yako kuwa na vurugu za namna hiyo.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Kuwa na msimamo kwani mpenzi ulie muacha anaweza kurejea tena kwako na ukakosa maisha ya furaha unayo ishi sasa kutokana na mpenzi mpya ulio nae no vyema uwe na muelekeo mpya kwani mpenzi wako wa zamani hana jipya zaidi ya usumbufu.

•Utulivu wako utakuwa silaha kubwa leo Hata hivyo unahitaji kuwa makini na watu wenye tamaa ya kutumia udhaifu wa wengine.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

jumatano hii unashauriwa ukae mbali na wabaya wako kwani wanaweza kukufanyia vurugu ikakufanya wingie police utakuwa na mafanikio mazuri katika kazi zako ingawa utapitia changa moto za hapa na pale.

•Mapenzi kwako yamekuwa shubiri kwani kila mpenzi unae mpata hana muelekeo mzuri wengi wamekuwa waongo chukuwa furusa hii ya yako kukutana na mtaalamu wa nyota ili aweze kukusaidia.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

jumatano hii ni nzuri kwako ukarimu wako na ucheshi wako ndio unao mfanya muajiri wako azidishe imani na were au wateja wako katika bishara kuzidisha mahaba na wewe ni vyema kuendelea hivyo ili kupata mafanikio zaidi.

•Mawasiliano yako leo yana nguvu kubwa Unaweza kupata habari muhimu itakayokusaidia kuamua jambo kubwa Kwenye mapenzi kuwa makini na maneno yako yanaweza kuponya au kuumiza.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

jumatano hii utapata taarifa ambazo zitakushituwa ila hutakiwi kuwa na khofu kwani taarifa hizo zinaweza kuwa nzuri kwako.

•Usimtegemee sana mpenzi ulie nae kwani jumatano hii itakuwa mgumu sana kutekeleza ahadi alizo kupa.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Jitahidi kuweka sawa tatizo linalo kusumbuwa kati yako wewe na mpenzi wako kuwa muwazi kwa kile unachotaka kumuambia kwani msipo fanya hivyo ugomvyi unaweza kuwa mkubwa zaidi mkaingia mashakani.

•Leo utahisi nguvu ya kiroho na hisia zako zitakuwa juu sana watu wa nyumbani wanaweza kukuona kama nguzo ya matumaini Ni siku nzuri ya kufanya ibada au maombi ya shukrani Fedha zinaweza kuongezeka kidogo kutokana na juhudi zako.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

jumatano hii unatakiwa utumie fursa ya kukamilisha malengo yako ya kusafiri kibiashara ama kuanzisha biashara au kwenda kuomba ajira
Ili kupata mafanikio katika masuala ya kipato.

•Katika mapenzi na maisha ni vyema uwache kufikiria mapenzi muda wote ingawa una wasi wasi na mpenzi wako kama huenda sio mkweli lakini vumilia na ukae kimya bila kuongea lolote juu yako kwani kufanya hivyo kutakufanya uwe makini katika mambo yako na penzi lako kukaa sawa kama mwanzo.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

jumatano hii unashauriwa utafute mtaalamu wa nyota aweze kukupa njia kwa maana kazi zako nyingi zinaonekana kutawaliwa na vifungo kila unalo lianzisha linaonekana kukwama ingawa una hangaika sana lakini leo hii kidogo inaonekana utapata mtu atakuondowa vifungo ulivyo navyo.

•Ujasiri wako leo unavutia Ni siku ya kuonyesha kipaji chako bila uwoga Hata hivyo epuka kujiingiza kwenye mashindano yasiyo na maana Usiku jaribu kutulia na kuipanga kesho yako.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

jumatano hii fuatilia ahadi ambazo uli ahidiwa na watu mbali mbali kwani inaonyesha muelekeo wa kufanikiwa ingawa umeshakata tamaa lakini ni vyema zaidi leo hii ukarudisha imani yako mambo yatakaa sawa.

•Punguza hasira usimfikirie mabaya mpenzi wako kwani unavyo mdhania siovyo ilivyo muonyesha tabasamu punguza kelele na ugomvyi jirekebishe wewe kwani ukifanya hivyo penzi lako litakuwa na muelekeo mzuri.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA PHD MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250810-WA0062(4).jpg
 
NYOTA YAKO LEO ALHAMIS AGOSTI 14/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.


★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Leo kuwa karibu na jamaa zako wape mawazo yako na waombe wakupe ushauri kutokana na changamoto zinazokukabili watakusaidia.

•Mahusiano yako yatakuwa mazuri hakuna shida juu ya hili na ulilolikusudia ndani yake endelea nalo halina tatizo.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Leo Hutaweza kuyatatua matatizo yako peke yako unahitaji msaada wa watu wengine bila msaada hakuna mafanikio.

•Utapata maudhi maudhi leo asubuhi na mchana wake haja zako hazitatimia ila baada ya kuudhiwa.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Leo yafanyie kazi mambo ambayo watu wanayasema jambo la muhimu kwako ni kuwa muangalifu Kuna bahati kubwa mbele yako inakuja.

•Ukikutana na msiba asubuhi ya leo ni msisitizo wa uzito wa siku yako leo hivyo zidisha umakini kwa kila kitu.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Leo itajikuta unakumbana na usumbufu wa hapa na pale katika utekelezaji wa majukumu yako hali hiyo isikutishe mwisho utafanikiwa.

•Tegemea kupokea taarifa mbaya ya msiba au mtu kuzidiwa maradhi yake usiogope ni maumbile yetu sote hayo.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)

Leo kuna mvurugano na kutokuelewana kutakaozuka kati ya wewe na wenzako au washirika wako dhamira yao ni kukudhulumu haki yako au kukutapeli lakini hawatofanikiwa.

•Safari zako leo sio nzuri zina uzito uzito maudhi mengi njiani.

★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Leo utajikuta umo katika hali nzuri na ya kufurahisha muda wa jioni baada ya kupata habari nzuri zitakazokufurahisha ungana na watu wako kufurahia habari hizo.

•Utapata bahati nzuri sana Leo na faraja itakufika.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Leo utapata Baraka nyingi na furaha tele jaribu kufanya mambo yako kwa ukamilifu wala usiwe na papara mambo yaende kwa mpangilio maalum.

•Biashara zako na kazi zako zitazidi kustawi na kuzidi kukupa nguvu na bahati za wewe kufika mbali kwenye maisha yako.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo tengeneza maisha yako yaweke pembeni mambo ambayo unayaona hayana maana maisha yako ni muhimu sana kwako kuliko jambo lolote.

•Utapoteza kitu muhimu Leo na usilazimishe jambo lolote leo utapata bahati mbaya.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Leo zungumza kwa kina mambo yaliyo moyoni kwako kwa watu unaowaamini ili upate suluhu hali hiyo itakuwa majawabu kwa matatizo yanayokukabili Kuwa muwazi na utafanikiwa.

•Safari zako ni nzuri ila usiwe muwazi kwa kila mtu juu ya safari zako.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo ni siku nzuri na yenye baraka sana kwako tumia siku ya leo kufanya mambo yako mwenyewe yale yote ambayo unayaona ni ya muhimu.

•Kazi zako zitaenda vizuri na biashara zako zitafunguka na kukupa faraja zaidi.

★MAPACHA– GEMINI ♊(May 21– Juni 20)

Leo jizuie kushiriki katika ubishani wowote Ni afadhali uonekane mjinga kuliko kushinda ukiwa hasira Kumbuka Hasira hasara.

•Utapata rafiki mpya Leo na utasaidiwa mengi katika mambo yanayokunyima furaha kwa wazi na kwa siri.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Alkhamisi ya leo Shirikiana na mtu yoyote unayemtaka unaweza kupata maarifa ya kufanikisha shughuli zako muhimu ulizonazo kwa sasa Hata hivyo kuwa makini.

•Safari zako ni nzuri kwa ujumla siku ni nzuri sana kwako.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
IMG-20250810-WA0062.jpg
 
NYOTA YAKO LEO IJUMAA AGOSTI 15/2025:

UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.

MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.


★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)

Leo siyo siku nzuri sana kwako na usiwe au usitoe ahadi zozote hasa mchana huu. Tumia siku ya leo kufanya mambo yako mwenyewe yale yote ambayo unayaona ni ya muhimu Jitahidi kujenga umoja wako na wa familia yako.

•Utapokea habari mbaya leo juu ya mtu kutoweka au kitu chako fulani kuharibika stahmili yote yanapita na ni kawaida tu usiwe na khofu.

★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)

Inaonekana utajihisi kuwa na hasira na utakasirika hovyo bila ya kuchokozwa na mtu yoyote Nyota zinakushauri jizuie kushiriki katika ubishani wowote.

★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)

Leo ni siku njema kwako fikiria kuhusu maisha yako weka pembeni mambo ambayo unayaona hayana maana kwa sababu maisha yako ni muhimu sana kwako kuliko jambo lolote jingine linalokukabili.

•Utapata habari njema sana leo na utajifunza kitu kizuri.

★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)

Leo fanya kila njia usiwe mpweke Kaa karibu na jamaa zako wape mawazo yako na waombe wakupe ushauri kutokana na changamoto zinazokukabili.

•Maswala yako ya kiuchumi yatafunguka na yataanza kustawi vizuri kwa namna usiyoitarajia.

★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 November 22– December 21)

Leo inaonekana Kuna mambo muhimu ya kwako na ya watu wengi ambayo unataka kuyafanya na yanahitaji pesa ambazo huna Hutaweza kuyatatua matatizo yako peke yako unahitaji msaada wa watu wengine.

•Kipindi hichi licha ya uzuri wake wote unashauriwa kuwa makini mno na siri zako za ndani kwakuwa zinaweza kugundulika kirahisi hivyo jitahidi uwe msiri zaidi.

★MBUZI– (CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)

Leo utakutana na rafiki ambaye atakuhitajia sana umsaidie katika jambo la faragha Usimnyime anachohitaji kwa sababu ameteseka sana Kumbuka huko nyuma ushawahi kujikuta ukiwa katika hali kama yake.

•Maswala ya kiroho yatakuinua yatakubeba kwenye mambo yako yote hivyo jitahidi kuyapa nafasi kubwa na kipaumbele dhidi ya yote.

★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)

Usijishughulishe na mambo ambayo watu wanayasema kwa sababu shida na matatizo waliyonayo hivi sasa ni kujitakiya wenyewe Kama walivyojitumbukiza katika dhiki ni juu yao kujisaidia jambo la muhimu kwako ni kuwa muangalifu.

•Mahusiano yako sio muhimu kuyazingatia sana ingawa katika msimu huu yatakuwa msaada mkubwa kwako.

★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)

Leo kaa na mtu wako wa karibu na mzungumze kwa kina mambo yaliyo moyoni kwako ili ipatikane suluhu Kwa kutumia njia hii utapata majawabu kwa matatizo yanayokukabili.

•Safari zako usighairi zina kheri na wewe haja zako zitatimia bila shaka yoyote.

★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)

Leo una uwezo wa kufikia kileleni kwa jambo lolote unalotaka kulifanya na hutopata pingamizi zozote Ni siku nzuri ya kujumuika na watu na kuwasaidia watakaohitaji msaada wako Kumbuka ukifanya wema kwao ni kama unajifanyia mwenyewe.

•Safari zako leo zina mashaka lakini utaenda salama na kurudi salama.

★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)

Leo itakuwa siku ya bahati kwa sababu mipango yako itakwenda kama unavyotarajia Siri kubwa ya wewe kupata na bahati hiyo ni kujikalia nyumbani na ikiwezekana kulala mapema na usijihangaishe.

•Safari zako ni nzuri mno na haja zako zitatimia bila shaka yoyote.

★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)

Leo jitahidi kutekeleza ahadi ulizowaahidi watu Jambo hili litakupa shida usipolifanyia kazi kiasi cha kuwapoteza marafiki zako Kama ikiwa ni vigumu kwako kutimiza ahadi basi waambie wasubiri lakini kamwe usighairi.

•Safari zako hazina uzuri wowote Leo na chochote cha kukufurahisha leo ni unafiki hakuna ukweli juu yake.

★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)

Leo shirikiana na mtu yoyote kwa sababu unaweza kupata maarifa ya kufanikisha shughuli zako muhimu ulizonazo kwa sasa Hata hivyo kuwa macho wadanganyifu ni wengi na hawalali wakifikiri namna ya kukudhuru.

•Haja zako nzuri hazitotimia leo ila mbaya tu ndo zinaweza kutimia Lakini Sio zile nzuri.

★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim niwatakie siku njema na mafanikio mema

MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.
downloadfile.jpg
 
MAMBO YANAYOCHAFUA NYOTA

Sehemu ya 2

(DOGOLI (Dr)


Sehemu ya kwanza nimefundisha kwa kirefu sana kuhusiana na nyota kwamba, mtu ni nyota na nyota ni mtu.
Kwa lugha nyingine nyepesi zaidi, Nyota ni mwili wa kiroho unaofunika mwili wa nyama. Tunaweza kuuita auric body (yaani mwili wa utukufu) wengine huita upako.
Mtu nyota yake ikiwa safi, imetakasika, inang'aa; watu wasiojua husema ana upako mwingi, ndio maana kila anachogusa kinafanikiwa.

Kama ambavyo mwili wa nyama huchafuka, kadhalika mwili wa kinyota huchafuka pia.

Kuna vitu ambavyo vikifanyika, lazima nguvu zako za kiroho zipungue na nguvu za kiroho zikipungua, yaani nguvu chanya, basi nguvu hasi uongezeka.
Huko kupungua kwa nguvu za kiroho ndio kuchafuka kwa nyota. Wengine wanasema utukufu au upako umepungua au umeondoka.

Ishara kwamba mtu ana negative vibes (nguvu hasi) nyingi au nyota yake ni chafu, ni pale ambapo mambo yake yanakuwa hayaendi kabisa, kila anachojaribu kufanyika kinagoma kabisa au kinaharibikia njiani.
Kila anachofanya kinakumbana na upinzani mkali.
Au eneo fulani la maisha linapata changamoto ambazo kila ukijaribu kuzitatua huoni matokeo mazuri.

Ndipo unasikia watu wengine wanasema fulani kalogwa, ana gundu (nuksi, mikosi), ana laana nk.
Kama ni magonjwa hayaishi, madeni, hasara kwenye biashara, kukosa kibali kazini, kukataliwa na watu, ndoa kushindikana, mahusiano kuvurugika nk.

Yote hayo na mengine mengi ni matokeo ya nguvu hasi nyingi mwilini.

Ni dalili kwamba mtu huyu ni mchafu kiroho, yaani nyota yake ni chafu!

Hizi nguvu hasi ninazozungumza ndio wengine huita nguvu za giza, mapepo, majini, mizimu, uchawi nk

Nguvu ni kama mizani.
Huku pakiongezeka, kule kunapungua.
Kama ukiwa na nguvu hasi nyingi, nguvu chanya zinakuwa kidogo na kama una nguvu chanya nyingi, basi nguvu hasi zinakuwa chache na ukiwa full positively charged, basi nguvu hasi zote hutoweka.
Ndio maana watu wengi sana duniani huangahika kutumia aina tofauti tofauti za vitakasaji kwa lengo la kuharibu nishati hasi kwenye miili yao ya kiroho (nyota zao)

Sisi maisha yetu ni mfano wa battery ya simu.
Kadiri unavyoitumia ndivyo nguvu (chaji) inavyozidi kupungua na usipochaji hatimaye simu itazimika.

Kadhalika, kwenye haya maisha kuna vitu tunakutana navyo, vinatupunguza nguvu (chaji) na tusipochaji nguvu zetu zinaisha, tunabaki makasha tu.

Namaanisha kuna vitu vinatuchafua iwe kwa kujua au hata bila kujua.


MAMBO YANAYOCHAFUA NYOTA ZETU NA HIVYO KUSHUSHA NGUVU ZETU KIROHO:

Ni hivi, kwenye haya maisha kila kitu ni nguvu, yaani ni energy (nishati)
Hakuna kitu kinachojiendesha, kila kitu kinaendeshwa na nguvu isiyoonekana.

Nguvu ikipungua kuna vitu vitagoma kabisa kusonga mbele.

Watu wanapokwenda kwenye maombi, wanakuwa wanatafuta nguvu.
Wanaokwenda kwa waganga wanatafuta nguvu.
Wanaotumia mitishamba ya kila namna, mafusho, mafuta, hirizi, vito, madini, kujichora tattoo, kukumbatia miti, kufanya matambiko na mengi mengineyo, wao pia wanakuwa wanatafuta nguvu.
Hakuna kitu kitaenda vizuri bila kuwa na nguvu ya kukiwezesha.

Kwa hiyo, kama unatafuta kufanikisha malengo yako uliyo nayo au mipango yako mikubwa uliyo nayo, unahitaji kuwa na nguvu na ukishakuwa nazo utalazimika kuzitunza kuliko chochote. Utazitumia kwa faida badala ya kuzivujisha bure.

Unapochafuka kiroho au kinyota, nguvu zako zinashuka/ zinapungua na hivyo unakuwa kwenye hatari ya kushindwa kufikia malengo yako.

Hapa chini nimeorodhesha kwa uchache sana mambo ambayo hushusha nguvu za kiroho au kuchafua nyota ya mtu.

1. CHA KWANZA KABISA NI TENDO LA KUJAMIIANA.

Tendo la kujamiiana au kwa kifupi S.E.X ni tendo ambalo kila linapofanyika, wahusika wanakuwa wanabadilishana nguvu zao za kiroho.
Ndio maana likaitwa Spiritual Energy Xchange (S.E.X)

Lazima mtu unayelala naye, uhakikishe ana nguvu chanya na muwe sawa kinyota, yaani muendane (muwe compatible)

Kwenye hili darasa tutakuja kusoma mada ya zodiac compatibility ambapo mtajifunza kwamba kila mtu ana mtu ambaye kinyota wanafaa kuoana (kufanya tendo la kujamiiana) na kuna mtu ambaye hafai kabisa hata kumsogelea!

Kuna mtu unaweza kukutana naye kimwili (mka-sex) na kuanzia hapo mambo yako yakaharibika kabisa kwa sababu kinyota hamuendani (au ni mchafu) na kuna mwingine mkikutana pamoja kimwili, mambo yako yanaanza kufunguka mpaka unaanza kushangaa, kumbe ni mambo ya kinyota!

Kila unapolala na mtu ambaye yupo chini kiroho au kinyota hamuendani, mtagawana nguvu, utampa zako (chanya) naye atakupa zake (hasi)

Sio kila anayekupa nguvu hasi hafai kwa kila mtu, kuna 'mtu wake' ambaye wanaendana/ wanafaana!

Kwa hiyo, kwa mtu ambaye ni mchafu kiroho na wewe ni msafi, kwake inakuwa heri, kwako ni loss kubwa sana.
Utanielewa yakishakukuta, kwa sasa unaweza usinielewe, lakini ndivyo ilivyo.

Na kama utalala na mtu ambaye kinyota hamuendani, basi atashusha nguvu zako za kiroho vile vile.

📌 Inashauriwa
watu wa air element watafute wale wa fire element au wakutane wao kwa wao.

📌 Wa earth element waoane na wa water element au wakikosa basi waoane wenyewe kwa wenyewe.

Summary iko hivi, kama mtu atapenda kutunza nguvu zake za kiroho:

Aries, Leo na Sagittarius; watafute Libra, Aquarius na Gemini au wahusiane wao kwa wao.

Taurus, Virgo na Capricorn watafute Scorpio, Pisces na Cancer au watafutane wenyewe kwa wenyewe.

Aidha, ikishindikana kote kote, basi mtu mwenye haja 'ya kujitakasa kinyota' (kiroho) amtafute mtu mwenye nyota ya Taurus au Leo, maana hizi nyota zina nguvu za 'kuchaji' nyota zingine!

Hata hivyo, kigezo cha 'usafi wa kiroho' kizingatiwe kwa makini, licha ya hizo compatibilities.

NB: SEX ni kinyonya nguvu cha kwanza, lazima iangaliwe kwa makini sana kwa watu wanaotaka kuamka na kukua kiroho.
Vigezo na masharti kama nilivyoeleza vizingatiwe, la sivyo kuacha kabisa kufanya sex ni muhimu zaidi.

MAMBO MENGINE YANAYOSHUSHA NGUVU ZA KIROHO AU KUCHAFUA NYOTA NI:

2. Matumizi ya pombe, kupita kiasi, kukesha kwenye night clubs nk.

3. Vyakula vyenye kemikali, vilivyosindikwa viwandani, nyama nyekundu nk.

4. Tabia za uongo, ugomvi, hasira, visasi, kujibizana na watu, kutokusamehe, chuki na yanayofanana na hayo.

5. Kushikana mikono na kukumbatiana na watu bila umakini.

Kwa sababu nishati au nguvu (energy) ni transferable, yaani zinaweza 'kumtoka mtu' kwenda kwa mwingine, unaweza kupeana mkono na mtu, baada ya hapo ukajisikia kuumwa ghafla, au ukaenda ofisini au kwenye biashara zako, siku yako ikawa mbaya; kisa umepeana mkono na mtu, au mmekumbatiana mkabadilisha nguvu!

Au mambo yakawa mazuri, kisa amekuambukiza nguvu chanya (amekuchaji)

Inategemea na alivyo kiroho!

Kuna kitu kinaitwa Spiritual whiffing and aroma ambapo watu wote mnaambukizana nguvu chanya.

Mnakutana mahali mnafanya meditation, mnafunga kisha mnashikana mikono au mnakumbatiana au mnakula pamoja kisha mkitawanyika mnakuwa mmepeana nguvu.
Wenye nguvu zaidi wanawagawia wenye nguvu kidogo, namna hiyo mnakuwa mmechajiana au kutakasana kinyota/ kiroho.
Watu wa kiroho wa zamani kila walipokuwa wakikutana kwa ajili ya mambo yao ya kiibada, walipenda sana kusalimiana kwa kukumbatiana, wenyewe waliita busu takatifu (holy kiss); lengo likiwa kuchajiana kiroho!

6. Kuongea ongea bila utaratibu au ubishi.
Kuongea sana na kubishana vinapunguza au kuathiri nguvu za kiroho.
Watu wengi wa kiroho sio waongeaji sana, ingawa pia hawazuiliwi kuongea, lakini huwezi kuwakuta kwenye mijadala isiyo na tija au mabishano yasiyofaa.

Sasa kwa hayo machache niliyoyaeleza kwa kifupi sana, ukifuatilia utagundua kuna namna nyingi sana tunapoteza nguvu zetu za kiroho, kwa namna moja au nyingine.

Hivyo ni muhimu 'kujichaji' namaanisha kujisafisha au kujitakasa mara kwa mara.

Huku kujichaji ndio tunaita cleansing, wengine wanaita kusafisha nyota.

Cleansing sio tukio la siku moja, ni tendo linalotakiwa kufanyika kila mara, walau mara moja kwa kila wiki.

Tukutane kwenye somo lijalo, lenye kichwa VITAKASA NYOTA: JINSI YA KUSAFISHA NA KUTAKASA NYOTA YAKO.


Kwa msaada wa tiba ya nyota, maisha, uchumi, mahusiano na magonjwa, wasiliana nasi
☎️📞
DOGOLI (Phd) , mtafiti na mkufunzi wa maswala ya kiroho
 
Leo ni LUCKDAY kwa watu wa nyota ya TAURUS na LIBLA Msisahu kuchoma ubani wa MUSTAKA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom