NYOTA YAKO LEO ALHAMIS JULAI 31/2025:
UKIWA NA SHIDA YOYOTE YA KINYOTA NA TIBA, NIPO MOROGORO MJINI NAPATIKANA KILA SIKU OFISINI KWANGU FOREST KILEKA KUANZIA SAA 12 ASUBUHI MPAKA SAA 12 JIONI.
MAALIM ANAPATIKANA MUDA WOTE.
★SIMBA LEO 🦁 (Julai 23– Agosti 22)
usiwaze wala usiwe na wasi wasi maana inaonekana mawazo wakati mwingine yanakujia gafla lakini utabiri wako unaonyesha kila utakacho kifanya utafanikiwa ni vyema kuitumia fursa ulioipata vizuri kwa kutimiza malengo yako.
•Utasikitishwa na mahusiano yako leo yatakukosesha furaha vumilia yatakuwa sawa lakini marafiki sio wazuri kwenye mahusiano yako kuwa na tahadhari hiyo.
★MASHUKE– VIRGO ♍ (Agosti 23– September 23)
Kazi zako Leo zina khasara ongeza umakini na ikiwa kazi binafsi basi zidisha ustaarabu Leo ukali kidogo utapoteza vyote Leo na kuna mtu atahitaji mgombane basi jizuie na hasira zako na ikiwezekana jishushe kupitiliza Leo kwakuwa kuna hali ya kudhalilishana au kufedheheshana kati yako na huyo adui yako.
•Alhamisi hii ni nzuri kwako ingawa kuna jambo linakushuhulisha sana muda mrefu lakini niwakati wakuwa na subra utaona muelejeo mzuri katika mambo yako.
★MIZANI– LIBRA ⚖️ (September 24– Oktoba 23)
Mapenzi kwako Alhamisi hii yapo kati kati mwenza wako anaweza kukupa taarifa ambazo zinaweza kukuchanganya unashauriwa kukaa kimya na kuweza kufanya uhakiki wa hizo taarifa kabla ya maamuzi.
•Kazi zako au biashara zako zinaonekana zitaenda vizuri na utanufaika.
★NG'E– SCORPION 🦂 (Oktoba 24– November 21)
jikaze kufanya kazi jitume sana huenda ukawa na mafanikio makubwa katika kipindi hiki lakini inawezekana pia ukatafuta mtu akakuondolea vifungo ulivyo navyo.
•Punguza zarau kwa mwenza wako ulie nae kitambo usiijigambe sana kwake na ukasahu aliko kutowa ingawa una mahusiano sehemu nyingine isiwe ni sababu ya kumkejeli na kumdharau mpenzi wako wa zamana kwani inawezekana ukauwa mapenzi yenu na siku moja utamkumbuka.
★MSHALE– SAGITTARIUS 🏹 (November 22– December 21)
inawezekana Alhamisi hii ukapata jambo la ghafla ambalo linaweza kukushituwa au unaweza kupata taarifa ambazo hujazitegemea ni vyema ukawa mpole maana jambo lenyewe linaweza likawa sababu ya wewe kufaulu mtihani ulio nao.
•Utapata matumaini mazuri mno Leo na ishara ni njema zaidi kwenye maswala yako inaonekana nuru tu leo.
★MBUZI– CAPRICORN 🐐 (December 22– January 20)
inaonyesha Alhamisi hii kuna uwezekano mkubwa wakupata mtu atakae kutatulia shida yako maana unakabiliwa na matatizo mengi ni vyema ukawa na subra na kuzidi kuomba mungu mambo yako yatakaa sawa.
•Mahusiano yako yapo vizuri na mtu wako wa karibu atakufurahisha au atakufariji Leo na kuna habari njema atakuja nayo Leo au atakupatia.
★NDOO– AQUARIUS 🏺 (January 21– February 19)
Alhamisi hii kuwa makini maana utakutana huenda ukakutana na adui yako ambae hamuelewani ni vyema ukawa mpole na kukubali kujishusha maana inawezekana ikawa ndo chanzo cha wewe mambo yako kuharibika.
•Utapata msaada mkubwa kwenye mambo yako na bahati zako kubwa zitafunguka kwa kasi zaidi tegemea mazuri na chochote nafsi yako inakusukuma ufanye kifanye usijali gharama wala muda ila kila kitu chako kinaonekana kipo vizuri na haja zako zitatimia .
★SAMAKI– PISCES 🐟 (February 20– March 20)
Inawezekana kuna jambo unalotaka au unafikiria kufanya juu ya mapenzi yako huenda ukafanikiwa lakini unashauriwa upunguze tamaa unapenda huyu na yule huwezi kukamilisha malengo yako ya kimapenzi endapo utaendelea na tabia yako hiyo.
•Pia kuna kitu chako kizuri kitaharibika au utakiharibu mwenyewe tegemea kupoteza kitu muhimu.
★PUNDA– ARIES 🐏 (March 21– Aprili 20)
Alhamisi hii unatakiwa kujipanga pia kupata utulivu wa kuweza kukamilisha majukumu yako ulio nayo maana una majukumu mengi kiasi kwamba unahisi yatakulemea ila kwakuwa wewe ni punda ujasiri wako na kujiamini kwako ndio kutakufanya uweze kufanikiwa kutimiza majukumu yako yote.
•Mahusiano yako yatakuwa na vurugu za hapa na pale ila yanapita pia safari zako ni nzito leo panga siku nyingine.
★NG'OMBE– TAURUS 🐂 (Aprili 21– May 20)
Alhamis hii utapata fedha au utapata Ahadi ya kupata kiasi Fulani cha fedha lakini pia unashauriwa ulipe au uwanze kupunguza madeni ulio nayo maana yanaweza kukuletea Shida na ukose furaha na amani.
•Mahusiano yako yapo vizuri na ikiwa una mgonjwa atakuwa sawa
Safari zako ni nzuri.
★MAPACHA– GEMINI ♊ (May 21– Juni 20)
usiwe mtu uliekosa maamuzi fanya dua nyingi Alhamis hii kuna pesa utapata ambayo hukutegemea lakini uwe muaminifu na mkweli kwani inawezekana ukapata fursa nzuri na ukafanikiwa kutimiza malengo yako ulio nayo.
•Utapata matumaini makubwa na mazuri kwenye mipango yako haja zako kwa ujumla zitaenda vizuri au zitatimia bila shaka yoyote.
★KAA– CANCER 🦀 (Juni 21– Julai 22)
Alhamisi hii ni nzuri kwako kiasi ingawa nyota yako inaonekana kutawaliwa na vifungo vya mufilisi yani kuna uwezekano mkubwa ukapata hasara katika biashara zako au cheo chako kikashuka lakini ukitumia akili ya kupata ushauri kwa watu wenye elimu ya nyota utafamikiwa kueka mambo yako sawa.
•Waheshimu walio juu yako au waliokuzidi umri ili kuruhusu bahati kuvwa zaidi kuwa na wewe pia safari zako ni nzuri sana.
★★★★★★★★★★★★★★★
Kwa ushauri na mengineyo wasiliana na maalim,niwatakie siku njema na mafanikio mema
MAALIM DOGOLI KINYAMKELA 💀 ☠️ MTABIRI WA NYOTA NA MTAALAM WA MAMBO MBALI MBALI YANAYO HUSIANA NA NYOTA ZENU.