Uchaguzi Urais, USA - 2020: Anavyopigwa Donald Trump (R) katika Ballot Box, ndivyo ambavyo alikuwa anapigwa John P. Magufuli (CCM)..

Hayo yote ulosema si ya kweli na hawa watu wawili hawafanani hata kidogo.

Donald Trump anashindwa kutetea kiti chake cha uraisi kwa sababu mbili kubwa.

1. Ameigawa Marekani na kuifanya iwe na watu wenye chuki baina ya wao kwa wao.

Hiyo ni kwa kutoa kauliza mara kwa mara za kuwaunga mkono wazungu wenye msimamo mkali wa KKK.

2. Amezembea katika kuchukua hatua kupambana na ugonjwa wa COVID-19 ambao umeua raia 235,000 wengi wao wakiwa wadengereko wenzetu.

Hawa ni wale walokuwa wakiokotwa mabarabarani na kuzikwa kama mizoga ya wanyama.

Wakati mwingine tukitoa maoni yetu tuondoe hisia kali tuegemee zaidi uhalisia.
Point namba moja..ni similar to Magufuli alipoigawa Tanzania na kuleta chuki na taharuki. rejea matamko yake ya kutopeleka maendeleo sehemu walizochaguliwa wapinzani kikatiba.

Kuhusu corona, tushukuru tu Mungu jiografia yetu imetubeba pia population ya Tanzania si sawa na Marekani, Hivyo kama coronà ingetukamata vizuri, Magufuli will be a big looser.!
 
Trump bado ana fursa ya kwenda mahakamani kupinga matokeo hiyo ndio tofauti ya demokrasia na udikteta.

Hapa unapigwa na kudhulumiwa kisha unalazimishwa uunge mkono juhudi au uletewe wasiojulikana.

Ndio maana nchi kama hizi ni laana tupu hata tufanyeje maendeleo ni ndoto tu kwa sababu dhuluma ndio sera kuu ya serikali, haki ni mwiko.
 
Hujielewi kabisa, hiyo sababu ya kwanza pekee ndio inamfunga kabisa huyo "role model" wako.

Hukuwahi kumsikia anavyoropoka akiwa Mwanza; "hawa walinichagua msiwafukuze barabarani" au "hawa walinichagua msiwavunjie nyumba zao" hata kama wamejenga kwenye hifadhi ya uwanja wa ndege.

Hiyo Corona nayo mmeamua tu kujitoa akili, huku kwetu haikuwa na madhara makubwa kama ilivyokuwa kwa nchi za wazungu, tuliishia kunawa mikono kwa maji tiririka na kuvaa mask, unadhani wazungu hawakujua kutumia njia hizo? na kama mlikuwa mnaziamini hizo njia kwanini mkakimbilia Chato zaidi ya mwezi mzima!
Point namba moja..ni similar to Magufuli alipoigawa Tanzania na kuleta chuki na taharuki. rejea matamko yake ya kutopeleka maendeleo sehemu walizochaguliwa wapinzani kikatiba.

Kuhusu corona, tushukuru tu Mungu jiografia yetu imetubeba pia population ya Tanzania si sawa na Marekani, Hivyo kama coronà ingetukamata vizuri, Magufuli will be a big looser.!

Wakuu, uchaguzi imeisha tuungane tuwe dugu moja tujiletee maendeleo ya mtu mmojammoja.

Kama mmeamua kuendeleza kampeni bado mna nafasi cha msingi ni kujipanga.

Mi saa hizi naingia hapa mtaa wa Jamatini kupata chochote, nimetamani supu ya ulimi wa ng'ombe.

Kila la kheri wakuu.
 
Tuwe WA moja na jizi?
 
Mfanano wa chaguzi hizi mbili:

1. Wote, Donald Trump (Republican) na John Magufuli (CCM) ni incumbent presidents waliokuwa wanatetea nafasi zao..

2. Wote ni maRais wasema ovyo na wasiopenda kulaumiwa kwa makosa yao..

3. Wote ni wapenda sifa na wakati mwingine kutaka sana kupenda "kuabudiwa"..

4. Wote ni wapenda kusema uongo na kulazimisha watu waamini uongo wao...

Utofauti wao;

1. Rais Donald Trump anatawala chini ya mamlaka na taasisi zenye uhuru mkubwa wa kumdhibiti, hafurukuti hawezi kuzitumia kumpendelea. Magufuli Pombe, ndiye anayezitawala, kuzielekeza cha kufanya mamlaka na taasisi za udhibiti kama polisi, NEC nk. Anazilamisha kumpendelea yeye na kuwakandamiza wapinzani wake..

2. Rais Trump ndiye anahaha kutafuta haki mahakamani kwa kudhani kuwa kuna wizi wa kura dhidi yake. Kwa Magufuli, hilo halipo, halikuwepo.!!

Nini Kinaendelea sasa?

1. Rais Trump Donald anaelekea kupoteza Mamlaka ya Urais wake. Mpaka sasa mpinzani wake Joe Biden (D) anaongoza kwa kura (Electoral College) 264 huku counting ya kura kwenye baadhi ya majimbo ukiendelea, Joe Biden akiwa anaongoza ktk kura hizo zinazoendelea kuhesabiwa sasa..

2. Donald Trump haamini kinachoendelea. Haamini kuwa pamoja na "maendeleo ya vitu" aliyowaletea wamarekani, cha ajabu wanamkataa kwenye sanduku la kura. Hajui amewakosea nini...!!

Kwa nini hapa Tanzania, Magufuli (CCM) tumeambiwa "ameshinda?"

1. Kwa hakika, kama uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 ungefanyika ktk mazingira ya uwazi kama USA, Magufuli asingeshinda na angepigwa kama ambavyo mwenzake Trump ananyongwa mchana kweupe..!

2. Tanzania na Magufuli wa CCM ili kujipatia ushindi "wenye mashaka" makubwa, ilibidi afungulie "giza totoro" ili kuruhusu mifumo yake ya "kumshindisha" ifanye kazi..

3. Kufungwa kwa mtandao wa internet; kuzuia zaidi ya mawakala 57,000 wa vyama pinzani katika vituo vya kupigia zaidi ya 80,000 kuwakilisha wagombea wao ktk vituo vya kupigia kura; kukamata baadhi ya wagombea wa vyama pinzani na kuwaweka ndani (selo za polisi) kabla na siku ya uchaguzi yenyewe nk nk ni miongoni mwa mikakati ya kumpa ushindi "fake" Magufuli na CCM kwa ujumla...!
kijana umepewa uhuru wa kutoa maoni katu usiutumie vibaya kwa kumsema vibaya Rais wetu. Kama humpendi hama nchi nendaa nchi zingine hukoo
 
Point namba moja..ni similar to Magufuli alipoigawa Tanzania na kuleta chuki na taharuki. rejea matamko yake ya kutopeleka maendeleo sehemu walizochaguliwa wapinzani kikatiba.

Kuhusu corona, tushukuru tu Mungu jiografia yetu imetubeba pia population ya Tanzania si sawa na Marekani, Hivyo kama coronà ingetukamata vizuri, Magufuli will be a big looser.!
will be, would be
 
Mfanano wa chaguzi hizi mbili:

1. Wote, Donald Trump (Republican) na John Magufuli (CCM) ni incumbent presidents waliokuwa wanatetea nafasi zao..

2. Wote ni maRais wasema ovyo na wasiopenda kulaumiwa kwa makosa yao..

3. Wote ni wapenda sifa na wakati mwingine kutaka sana kupenda "kuabudiwa"..

4. Wote ni wapenda kusema uongo na kulazimisha watu waamini uongo wao...

Utofauti wao;

1. Rais Donald Trump anatawala chini ya mamlaka na taasisi zenye uhuru mkubwa wa kumdhibiti, hafurukuti hawezi kuzitumia kumpendelea. Magufuli Pombe, ndiye anayezitawala, kuzielekeza cha kufanya mamlaka na taasisi za udhibiti kama polisi, NEC nk. Anazilamisha kumpendelea yeye na kuwakandamiza wapinzani wake..

2. Rais Trump ndiye anahaha kutafuta haki mahakamani kwa kudhani kuwa kuna wizi wa kura dhidi yake. Kwa Magufuli, hilo halipo, halikuwepo.!!

Nini Kinaendelea sasa?

1. Rais Trump Donald anaelekea kupoteza Mamlaka ya Urais wake. Mpaka sasa mpinzani wake Joe Biden (D) anaongoza kwa kura (Electoral College) 264 huku counting ya kura kwenye baadhi ya majimbo ukiendelea, Joe Biden akiwa anaongoza ktk kura hizo zinazoendelea kuhesabiwa sasa..

2. Donald Trump haamini kinachoendelea. Haamini kuwa pamoja na "maendeleo ya vitu" aliyowaletea wamarekani, cha ajabu wanamkataa kwenye sanduku la kura. Hajui amewakosea nini...!!

Kwa nini hapa Tanzania, Magufuli (CCM) tumeambiwa "ameshinda?"

1. Kwa hakika, kama uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 ungefanyika ktk mazingira ya uwazi kama USA, Magufuli asingeshinda na angepigwa kama ambavyo mwenzake Trump ananyongwa mchana kweupe..!

2. Tanzania na Magufuli wa CCM ili kujipatia ushindi "wenye mashaka" makubwa, ilibidi afungulie "giza totoro" ili kuruhusu mifumo yake ya "kumshindisha" ifanye kazi..

3. Kufungwa kwa mtandao wa internet; kuzuia zaidi ya mawakala 57,000 wa vyama pinzani katika vituo vya kupigia zaidi ya 80,000 kuwakilisha wagombea wao ktk vituo vya kupigia kura; kukamata baadhi ya wagombea wa vyama pinzani na kuwaweka ndani (selo za polisi) kabla na siku ya uchaguzi yenyewe nk nk ni miongoni mwa mikakati ya kumpa ushindi "fake" Magufuli na CCM kwa ujumla...!
Mtoa mada MAGUFULI sio wa kushindwa na mtu mropokaji kama Tundu lissu ,hata MUNGU angekuja kusimamia uchaguz wa Tanzania bado MAGUFULI angeshinda kwa aslmia kwanzia 80,,,
 
..Donald Trump ni Amiri Jeshi dhaifu na bwege sijapata kuona.

..Inawezekana vipi Joe Biden afanye kampeni muda wote na hatujasikia hata mara moja amepigwa mabomu ya machozi, au kuswekwa mahabusu?

..Amiri Jeshi Mkuu gani asiyeweza kutumia DOLA kubaki madarakani?
kwani IGP wa kule ni Sirro ?
 
..Donald Trump ni Amiri Jeshi dhaifu na bwege sijapata kuona.

..Inawezekana vipi Joe Biden afanye kampeni muda wote na hatujasikia hata mara moja amepigwa mabomu ya machozi, au kuswekwa mahabusu?

..Amiri Jeshi Mkuu gani asiyeweza kutumia DOLA kubaki madarakani?
Mimi nawaoongeza Marekani kwa kuweka taasisi imara zinazosimamia haki na maoni ya wananchi kiasi kwamba Raisi akiwa madarakani hawezi kuingilia taasisi na kuziamurisha atakavyo na pia Raisi hawezi kuwa dictator na kuharibu tofauti na huku Africa, Raisi ni mungu mtu, anaingilia kila state organ, haheshimu katiba, Wala wataalamu, dah Mimi hapo ndio nawapomgeza wazungu walio establish taasisi imara
 
Tushauri sasa tufanyeje? Na walioshindwa huku waende mahakamani au waandamane?
Siandiki na kukuambia nini cha kufanya juu ya dhuluma..

Tunaandika haya ili watu waijue kweli ya nini kilichotokea na waamue wenyewe cha kufanya..

Mtu akiamua ku - connive na wezi wa haki za watu, afanye vile akijua na mtu anayekataa uhuni aukatae toka ndani ya nafsi yake...
 
Hayo yote ulosema si ya kweli na hawa watu wawili hawafanani hata kidogo.

Donald Trump anashindwa kutetea kiti chake cha uraisi kwa sababu mbili kubwa.

1. Ameigawa Marekani na kuifanya iwe na watu wenye chuki baina ya wao kwa wao.

Hiyo ni kwa kutoa kauliza mara kwa mara za kuwaunga mkono wazungu wenye msimamo mkali wa KKK.

2. Amezembea katika kuchukua hatua kupambana na ugonjwa wa COVID-19 ambao umeua raia 235,000 wengi wao wakiwa wadengereko wenzetu.

Hawa ni wale walokuwa wakiokotwa mabarabarani na kuzikwa kama mizoga ya wanyama.

Wakati mwingine tukitoa maoni yetu tuondoe hisia kali tuegemee zaidi uhalisia.

Nimeandika kwa muono wangu..

Wewe vipi, unasemaje? Kama hafanani naye, basi eleza anatofautiana naye kwa mambo gani?
 
Back
Top Bottom