Wagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ambao wameshafariki

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Wafahamu Wagombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 ambao wameshafariki

Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha Civic United Front (CUF) alifariki Februari 17, 2021 akiwa na umri wa Miaka 77 baada ya kupata Maambukizi ya Ugonjwa wa Corona.

Dkt. John Joseph Pombe Magufuli (61) ambaye alitangazwa kuwa Mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015 na 2020 alifariki Machi 17, 2021 akiwa Madarakani (Muhula wa Pili) kwa Maradhi ya Moyo baada ya kulazwa katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es Salaam.

Anna Mghwira aliyegombea Urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo alifariki Julai 22, 2021 akiwa na umri wa Miaka 62 katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Jijini Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu ya Changamoto za Upumuaji. Kabla ya Kifo chake, Anna aliwahi kuteuliwa na Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Edward Lowassa ambaye alikuwa Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitokea CCM alikuwa mshindi wa pili kwenye Uchaguzi wa 2015 na alifariki Februari 10, 2024 akiwa anapatiwa matibabu ya Magonjwa ya Kujikunja Utumbo, Matatizo ya Mapafu na Shinikizo la Damu.

Kwa taarifa kama hizi na nyingine nyingi tembelea JamiiForums.com ambayo ina Majukwaa 38 yenye lengo la Kukuhabarisha, Kuburudisha na Kukuelimisha.
 
Back
Top Bottom