wagagagigi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2014
- 890
- 983
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi mzuri. Moja ya kitu kinatugharimu sana Tanzania ni woga wetu uliopitiliza mipaka, hasa kwa upande wa Tanzania Bara. itafika siku watu watachoka kutupigania na kutusemea!Mfanano wa chaguzi hizi mbili:
1. Wote, Donald Trump (Republican) na John Magufuli (CCM) ni incumbent presidents waliokuwa wanatetea nafasi zao..
2. Wote ni maRais wasema ovyo na wasiopenda kulaumiwa kwa makosa yao..
3. Wote ni wapenda sifa na wakati mwingine kutaka sana kupenda "kuabudiwa"..
4. Wote ni wapenda kusema uongo na kulazimisha watu waamini uongo wao...
Utofauti wao;
1. Rais Donald Trump anatawala chini ya mamlaka na taasisi zenye uhuru mkubwa wa kumdhibiti, hafurukuti hawezi kuzitumia kumpendelea. Magufuli Pombe, ndiye anayezitawala, kuzielekeza cha kufanya mamlaka na taasisi za udhibiti kama polisi, NEC nk. Anazilamisha kumpendelea yeye na kuwakandamiza wapinzani wake..
2. Rais Trump ndiye anahaha kutafuta haki mahakamani kwa kudhani kuwa kuna wizi wa kura dhidi yake. Kwa Magufuli, hilo halipo, halikuwepo.!!
Nini Kinaendelea sasa?
1. Rais Trump Donald anaelekea kupoteza Mamlaka ya Urais wake. Mpaka sasa mpinzani wake Joe Biden (D) anaongoza kwa kura (Electoral College) 264 huku counting ya kura kwenye baadhi ya majimbo ukiendelea, Joe Biden akiwa anaongoza ktk kura hizo zinazoendelea kuhesabiwa sasa..
2. Donald Trump haamini kinachoendelea. Haamini kuwa pamoja na "maendeleo ya vitu" aliyowaletea wamarekani, cha ajabu wanamkataa kwenye sanduku la kura. Hajui amewakosea nini...!!
Kwa nini hapa Tanzania, Magufuli (CCM) tumeambiwa "ameshinda?"
1. Kwa hakika, kama uchaguzi mkuu wa Tanzania 2020 ungefanyika ktk mazingira ya uwazi kama USA, Magufuli asingeshinda na angepigwa kama ambavyo mwenzake Trump ananyongwa mchana kweupe..!
2. Tanzania na Magufuli wa CCM ili kujipatia ushindi "wenye mashaka" makubwa, ilibidi afungulie "giza totoro" ili kuruhusu mifumo yake ya "kumshindisha" ifanye kazi..
3. Kufungwa kwa mtandao wa internet; kuzuia zaidi ya mawakala 57,000 wa vyama pinzani katika vituo vya kupigia zaidi ya 80,000 kuwakilisha wagombea wao ktk vituo vya kupigia kura; kukamata baadhi ya wagombea wa vyama pinzani na kuwaweka ndani (selo za polisi) kabla na siku ya uchaguzi yenyewe nk nk ni miongoni mwa mikakati ya kumpa ushindi "fake" Magufuli na CCM kwa ujumla...!
................................................
US - Updates Presidential Election results as at 21:00EAT
View attachment 1621656
Georgia State with 16 Electoral Colleges votes is under "votes recounting"..
Obviously, Joe Biden (D) atashinda...