Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania: Uwezekano wa kupata Corona Dar ni mkubwa

Thank you. Watu wanabeza kana kwamba hawajui tatizo letu hapa ni kubwa sanaaa kuliko huko wanakokufa sana! Kwani sisi tunakufa kidogo? Sasa hivi hata ugonjwa wa kawaida wa kulazwa unakimbiwa na madaktari na manesi, mazishi kwa wingi kila siku; majirani wanatufungia mipaka, SADC wametuweka pembeni; AU wamepinga mambo yetu ya ovyo eti maabara sijui wataalum wana matatizo, kumbe matatizo ni yao wapima mapapai na oil (aibu!); WHO wametufungia milango, wanasema watafanya kazi na Zanzibar, sisi vichwa maji visivyo na akili! bado tu hatushtuki, na mbaya zaidi, bado kuna watu wanaimba mapambio kwa raisi wao "mwenye akili na ujuzi tele"! Shame on us!

Hama nchi hujafungwa.
 
Ni kweli marekani wanakufa lakini wanapambana, Vipi kuhusu wewe kila zinapokuja lawama unda-dil na hizo lawama tu bila ya kujitathmini wewe na hali yako, kuchukua hatua unabaki pale pale unaonaje hii hali inavyokwenda na matokeo yake baadae?

Toka tarehe 29 hakuna updates unaweza kupata hisia muko kawaida hakuna maambukizi ya Covid-19 nchini lakini jiulize swali dogo tu kwanini watoto hawaruhusiwi kurudi mashuleni na vyuoni? mnasema huu ugonjwa ni mdogo tu labda ut ashindwa kwa jina la yesu na kujifukiza majani ya miti na mumeagiza dawa toka madascar je akili yako inakupa hiyo dawa ya madagascar atakunywa nani aache nani box 13? lakini mpaka zifanyiwe utafiti.

Swali jengine je utafiti utachukua muda gani? vipi kuhusu kipindi hichi munatafiti dawa toka Madagascar ugonjwa umesismama hamna maambukizi?

Unafkiri kuvaa barakoa na kunawa maji tiririka kwa sabuni inatosha? China tayari wameanza kuruhusu kufungua miji yao lakini je wajuwa next wamefanya nini? utakuta watu wapo huru hivi kutembea na kufanya shughuli zao lakini nadhan tatizo kubwa hapa mumeshindwa kufahamu kwamba watu wapo kwenye mfumo (systeam) ikisaidiwa na vyombo vya usalama kama polisi kuwaelekeza watu lakini watu hupata ujumbe kupitia simu zao za mikononi kwamba hapo ulipo sasa mita 10 au mji ama mtaa huo kuna wagonjwa idadi hii labda fanya hivi na vile ama rudi ulikotoka na mfano wa hayo. Ndio mana hizi nchi wameondoa hizo tunazoita lock-down lakini kuna hatua nyengine wanachukua kila siku. Sasa jiulize huko kwenu hakuna lock-down hatua zinazochukuliwa ni zipi instead? jibu ni kunawa kwa maji tiririka kwa sabuni na kuvaa barakoa tu.

Jiulize kama madereva kadhaa wanaenda nchi jirani wamegundulika na corona vipi kuhusu huko mitaani na mijini?

Mtu anaumwa corona anapiga gia toka Dar hadi mipakani, sasa hiyo corona mnaiogopea nini?
 
si mwende kwenu ambako hakuna corona ???

unakumbuka hawa wapumbavu waliwahi kuwatahadharisha wananchi wake kuhusu hali ya usalama nchini ???
Hawa watoto wasio na Elimu wana I cost sana Nchi yetu. Ukiona Marekani wanaondoka ujue thamani ya pesa yenu itashuka tu muda siyo mrefu. Wanaondoka na dollars which means wana create more need for the this badly needed forex. Wajinga ninyi mnadhani ni rahisi kama kupost thread JF.
 
wanazengo hebu naomba ufafanuzi wa hili neno Global Level 4 Health Advisory for COVID-19

Zipo levels nne, yaani kuanzia level-1 hadi level-4, hiyo hapo level-4 ndio nyekundu na ya mwisho, hutolewa kwa nchi ambayo hali ni hovyoo kabisa, na ndio mliyowekewa. Hawajatoa level-4 kwa taifa lingine lolote duniani hata China kule kirusi kilianzia.
 
Wanatafuta kiki
Ubalozi wa Marekani umesema Dar es Salaam ni mkoa ambao hatari ya kupata #CoronaVirus ni kubwa. Wamedai japo serikali haitoi takwimu kuhusu hilo ushahidi wa kimazingira unaonyesha wagonjwa wanaongezeka kwa kasi ndani ya Dar.

Wamedai hospitali nyingi zinahofu kutokana na ukosefu wa vifaa tiba kwa ajili ya kupambana na #COVID19. Serikali ya Tanzania imezuia safari zote za abiria tangu Aprili 11, hivyo ubalozi umewataka raia wake kubaki ndani ili kujikinga na #CoronaVirus

View attachment 1448823

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Birashaka utakua chedema manaa chadema maneno yao yanajulikana ya kipropaganda ,hivi wewe ulitaka serikali ifanye nini ili uone imechukua hatua au ndo sababu hiyo lockdown ee ndio maana unalalamika cjui who wamefanyaje cjui , hivi nikuulize kwani lockdown ndio njia sahihi ya kupambana na korona ? Kama unayo akili jiulize maswali haya kwanini Nchi hizo za ulaya zinaondoa lockdown huku kukiwa bado maambukiz nmakubwa? Swali la pili: wewe Kama unajitegemea je ndani au benki una akiba ya sh ngapi? Kama unayo laki kadhaa ndizo zinazo kuzuzua jiulize hivi ingekua huu ugonjwa umefika kipindi unaakiba ya elfu 30 tu ungeishije? Maana ujue kipindi wewe unalilia lockdown wenzako hawana chochote ndani.ila Kama wewe kula kulala hautopata picha haric ya maswali haya hata ukijiuliza, punguzeni ushabiki ulalamike tumefungiwa mipaka kipindi hiki kwani huko ulaya munakoona Kuna watu wenye akili kilakitu wanafanya lazima nac tufanye wanafanya biashara? NB : ugonjwa wa corona haijulikani utaisha lini Sasa Kama unalilia lockdown useme kabisa unataka ya mwaka au miaka 2
Thank you. Watu wanabeza kana kwamba hawajui tatizo letu hapa ni kubwa sanaaa kuliko huko wanakokufa sana! Kwani sisi tunakufa kidogo? Sasa hivi hata ugonjwa wa kawaida wa kulazwa unakimbiwa na madaktari na manesi, mazishi kwa wingi kila siku; majirani wanatufungia mipaka, SADC wametuweka pembeni; AU wamepinga mambo yetu ya ovyo eti maabara sijui wataalum wana matatizo, kumbe matatizo ni yao wapima mapapai na oil (aibu!); WHO wametufungia milango, wanasema watafanya kazi na Zanzibar, sisi vichwa maji visivyo na akili! bado tu hatushtuki, na mbaya zaidi, bado kuna watu wanaimba mapambio kwa raisi wao "mwenye akili na ujuzi tele"! Shame on us!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani bado kuna wamarekani wapo bongo? Jana kariakoo nimemuona mzungu kavaa mask yuko busy tu anaingia huku anatokea kule nikashangaa huyu mzungu haogopi corona ya Dar alitakiwa ajifungie ndani au awe amekwishaondoka kwao.
 
Jamani huku watu wanamapovu wao wametoa alert kwa raia wao wanaishiwa Tz sio wa Tanzania .Sasa nyie mnakasirika nini.Ukitaka kujua kitu ni cha kweli ,angalia jinsi watu wanavyokua wakali.
 
View attachment 1449232
Hakuna anaefahamu idadi kamili ya maambukizi na vifo vya corona Tanzania. Hospital zimefurika na wahudumu wanapambana pamoja na vitendea kazi kuwa hana.

Ubalozi wa Marekani una tahadharisha kuwa ni rahisi sana kupata maambukizi ya corona Tanzania hasa Dar.

Wafanya kazi wa Ubalozi wameshauriwa kubaki majumbani mwao, watoke kwa shughuli muhimu kama kununua mahitaji ya ndani na chakula. Pia wawe makini kukaribisha wageni nyumbani.
Persona non grata! inakuja kesho
 
Tanzania inaenda kuwakomboa watanzania waliokwama India, bora kufia Mwananyamala kuliko Bangalore India.
Inategema na mtaa unaoishi, mimi nimesoma digrii ya pili NA KUISHI CHADRAKA, nikzuri kuliko Masaki, Sawa na mtanzania aliefika Nairobi akaenda kishi kibera ni tofauti na aliyeishi WESTLANDS
 
Persona non grata! inakuja kesho
LONDON (Reuters) - Prime Minister Boris Johnson said on Wednesday that increasing rates of infection in other countries which have relaxed some rules to tackle the coronavirus outbreak was a warning to Britain not to move too fast.

“We are watching intently what is happening in other countries and it is very notable that in some other countries where relaxations have been introduced there are signs of the R (reproduction number) going up again, and that is a very clear warning to us not to proceed too fast or too recklessly,” Johnson told parliament.

Boris ameamua hata uchumi udorore lakini maisha ya raia ni kipaumbele.
 
LONDON (Reuters) - Prime Minister Boris Johnson said on Wednesday that increasing rates of infection in other countries which have relaxed some rules to tackle the coronavirus outbreak was a warning to Britain not to move too fast.

“We are watching intently what is happening in other countries and it is very notable that in some other countries where relaxations have been introduced there are signs of the R (reproduction number) going up again, and that is a very clear warning to us not to proceed too fast or too recklessly,” Johnson told parliament.
thanks counsel, you are brilliant, not likr JIWE and kabudi
 
Ubalozi wa Marekani umesema Dar es Salaam ni mkoa ambao hatari ya kupata #CoronaVirus ni kubwa. Wamedai japo serikali haitoi takwimu kuhusu hilo ushahidi wa kimazingira unaonyesha wagonjwa wanaongezeka kwa kasi ndani ya Dar.

Wamedai hospitali nyingi zinahofu kutokana na ukosefu wa vifaa tiba kwa ajili ya kupambana na #COVID19. Serikali ya Tanzania imezuia safari zote za abiria tangu Aprili 11, hivyo ubalozi umewataka raia wake kubaki ndani ili kujikinga na #CoronaVirus

View attachment 1448823

Kwa yanayoonekana mipakani na dereva wa malori (wala si wa mabasi) ni ushahidi tosha kwa hali ya dar.
 
Back
Top Bottom