Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania: Uwezekano wa kupata Corona Dar ni mkubwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,861
Ubalozi wa Marekani umesema Dar es Salaam ni mkoa ambao hatari ya kupata #CoronaVirus ni kubwa. Wamedai japo serikali haitoi takwimu kuhusu hilo ushahidi wa kimazingira unaonyesha wagonjwa wanaongezeka kwa kasi ndani ya Dar.

Wamedai hospitali nyingi zinahofu kutokana na ukosefu wa vifaa tiba kwa ajili ya kupambana na #COVID19. Serikali ya Tanzania imezuia safari zote za abiria tangu Aprili 11, hivyo ubalozi umewataka raia wake kubaki ndani ili kujikinga na #CoronaVirus

1589358110708.png
 
Kesho 14-05-2020 kuna ndege ya kukodi EMIRATES inakuja kukomboa wamarekani waliokuwa wamebaki, wanajua idadi ni kubwa ya kutisha, wameamua kukimbia na kuacha kila kitu chao , bora kufia hospitali marekani kuliko mapokezi mwananyamala, maana hapo unaona wanasema hata wagonjwa hawapokelewi, unaachwa ujifie tu na tena wanakwambie kanywe pilipili kichaa na mirungi ndio daawa
 
Wakati mwingine ukimya nalo ni jibu ..vyema tukakaa kimya tuu

It is never too late to begin. Start now

Thank you. Watu wanabeza kana kwamba hawajui tatizo letu hapa ni kubwa sanaaa kuliko huko wanakokufa sana! Kwani sisi tunakufa kidogo? Sasa hivi hata ugonjwa wa kawaida wa kulazwa unakimbiwa na madaktari na manesi, mazishi kwa wingi kila siku; majirani wanatufungia mipaka, SADC wametuweka pembeni; AU wamepinga mambo yetu ya ovyo eti maabara sijui wataalum wana matatizo, kumbe matatizo ni yao wapima mapapai na oil (aibu!); WHO wametufungia milango, wanasema watafanya kazi na Zanzibar, sisi vichwa maji visivyo na akili! bado tu hatushtuki, na mbaya zaidi, bado kuna watu wanaimba mapambio kwa raisi wao "mwenye akili na ujuzi tele"! Shame on us!
 
Hamia huko kwa hao mabwana zako USA
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom