TWAWEZA: Katika Watanzania watatu, Wawili wanataka Katiba Mpya

20 Oktoba 2017

Wawili kati ya Watanzania watatu wanadhani kwamba ni wakati taifa hilo linafaa kuwa na katiba mpya, kulingana na matokeo ya utafiti uliofanywa na Twaweza.

Utafiti huo kwa jina ''Unfinished Business'' unaangazia mkwamo wa mkakati wa katiba mpya kutokana na data ya sauti za wananchi.

Matokeo hayo yanatokana na data iliokusanywa kutoka kwa raia 1,745 nchini Tanzania bara kati ya mwezi Juni na Julai.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba nusu ya waliohojiwa ama asilimia 56 wanafikiria kwamba rasimu ya mwisho ya katiba inafaa kupigiwa kura ya maoni.

Hatahivyo utafiti huo unaonyesha kuwa nusu ya raia ambayo ni asilimia 48 wanaamini kwamba mkakati wa kuandika katiba mpya hautafanyika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Raia wanataka katiba itakayosisitiza uwajibikaji.

Watu wanane kati ya kumi wanataka nyadhfa za mawaziri kuthibitishwa na bunge ambayo ni asilimia 79 huku watu sita kati ya kumi wakitaka kupewa uwezo wa kuwaondoa wabunge katikati ya uchaguzi.

Afisa mkuu wa Twaweza Aidan Eyakuze alisema kuwa raia wanataka katiba mpya.

Wengi wanataka kuwepo kwa tume mpya ili kuwa na mwanzo mpya.
Lakini wengine wako tayari kuendelea na rasimu ya awali kutoka kwa tume iliopita, alisema.

Kulingana na utafiti huo, raia wamegawanyika katika hatua nyengine za uwajibikaji kama vile kuzuia akaunti za kigeni miongoni mwa viongozi na wanaharakati kama miongoni mwa maadili ya kitaifa.

Hii ni habari mbaya sana kwa wale chawa
 
Naamini utafiti mwingine ukifanyika sasa na hao Twaweza wakaacha uoga wa kulazimisha kumfurahisha bosi wao basi asilimia za wanaoitaka Katiba Mpya zitakuwa zimeongezeka.
Mimi hawajaniuliza ninataka Katiba mpya.
 
1648550640301.png


2878995_images_9.jpeg
 
Washaanza tafiti za mchongo maana waliosuka hiyo tafiti tunawajua sababu ilitakiwa iwe kila wapinzani watatu wawili wanataka katiba mpya.
 
Washaanza tafiti za mchongo maana waliosuka hiyo tafiti tunawajua sababu ilitakiwa iwe kila wapinzani watatu wawili wanataka katiba mpya.
Tuache mob psychology,katiba iliyopo we imekuathiri kitu gani ukiachana na hao wenye kutaka madaraka ili hiyo katiba mpya iwarahisishie.
 
Back
Top Bottom