TWAWEZA: Katika Watanzania watatu, Wawili wanataka Katiba Mpya

Watanzania wawapi hao? Wamehoji vijana wa CHADEMA wachache ndo wanakuja na matope haya.
 
Ifikapo 2025 msiwakatae hao TWAWEZA na utafiti wa Rais atakayeshinda kwa kishindo!
🤣🤣🤣siasa za Tanzania 🇹🇿 huwa hawa wenye mavyama yao sisiemu na come kupenda kusikia matamu tamu tu yanayokuwa kwenye maono yao tu.....tofauti na hapo ni mitusi tu, wakati hapo hapo utasikia wanasema friiidomu ofu eksipresheni
 
Elezea faida za katiba mpya hapa kwa mtanzania wa kawaida ambaye kila siku bado anahangaika kuweka chakula mezani. Low mind ni mtu asiyefafanua au kuelimisha jambo ila anategemea kutumia nguvu au lugha ya dharau kujaribu kunyamazishi wengine. Katiba zinasimamishwa au kubadilishwa wakati wowote ule hasa katika nchi zetu za Africa. Pesa kidogo tuliyonayo itumike -kupatia maji kwa kila mwananchi, afya bora , elimu kwa kila mtoto wa kitanzania , ajira kwa vijana na madawa hospitalini.
Si kweli. Katiba ni sheria kuu hueleza watu waishije. Kuna shda nyngi kama haki, uhuru, nk. Bila hizi watu huteseka na huishi kwa shida. Katiba huweka sawa kila kitu watu wakiifuata. Katiba nzuri ni maisha mazuri ni maendelep

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Umeeleweka vizuri. Kwa sasa Tanzania ina katiba ambayo imekuwa ikitumika tangu uhuru na kufanyiwa maboresho kila ilipohitajika. Kiuchumi serikali ina kiasi fulani cha pesa, je hii pesa tuipangie kwenye maendeleo ya kupunguza matatizo ya mwananchi wa kawaida au kwenye mchakato wa katiba mpya. Kama ulifuatilia ule mchakato wa katiba - unajua kitu kilichokwamisha - miundo ya serikali. Mchakato hauwezi kusogea - pesa zitatumika na mchakato hauta songa mbele. Jambo zuri ni kufuata ahadi ya Rais alivyoshauri - kazi ziendelee, katiba mpya baadae- waswahili wanasema ahadi ni deni. Hizi kelele za katiba mpya zinaweza kuwa mbinu za watu wachache kupunguza kasi ya Rais katika kutimiza ndoto ya kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi. Uchaguzi ukifika wati wale wale waliopiga kelele za katiba mpya watasimama majukwani na kudai - hakuna maendeleo yoyote kwa wananchi, watasahau kwamba walitumia pesa nyingi kwenye mchakato wa katiba mpya. Kupanga ni kuchagua.
 
20 Oktoba 2017

Wawili kati ya Watanzania watatu wanadhani kwamba ni wakati taifa hilo linafaa kuwa na katiba mpya, kulingana na matokeo ya utafiti uliofanywa na Twaweza.

Utafiti huo kwa jina ''Unfinished Business'' unaangazia mkwamo wa mkakati wa katiba mpya kutokana na data ya sauti za wananchi.

Matokeo hayo yanatokana na data iliokusanywa kutoka kwa raia 1,745 nchini Tanzania bara kati ya mwezi Juni na Julai.

Matokeo hayo yanaonyesha kwamba nusu ya waliohojiwa ama asilimia 56 wanafikiria kwamba rasimu ya mwisho ya katiba inafaa kupigiwa kura ya maoni.

Hatahivyo utafiti huo unaonyesha kuwa nusu ya raia ambayo ni asilimia 48 wanaamini kwamba mkakati wa kuandika katiba mpya hautafanyika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Raia wanataka katiba itakayosisitiza uwajibikaji.

Watu wanane kati ya kumi wanataka nyadhfa za mawaziri kuthibitishwa na bunge ambayo ni asilimia 79 huku watu sita kati ya kumi wakitaka kupewa uwezo wa kuwaondoa wabunge katikati ya uchaguzi.

Afisa mkuu wa Twaweza Aidan Eyakuze alisema kuwa raia wanataka katiba mpya.

Wengi wanataka kuwepo kwa tume mpya ili kuwa na mwanzo mpya.
Lakini wengine wako tayari kuendelea na rasimu ya awali kutoka kwa tume iliopita, alisema.

Kulingana na utafiti huo, raia wamegawanyika katika hatua nyengine za uwajibikaji kama vile kuzuia akaunti za kigeni miongoni mwa viongozi na wanaharakati kama miongoni mwa maadili ya kitaifa.
 
Kumbe walifanya 2017 sahivi itakuwa imeongezeka mara dufu
 
Wafuasi wa Mbowe mmekuwa kama vichaa🤣🤣🤣

Hata kama mnalipwa lakini duh hali tete
 
Back
Top Bottom