Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Baada ya kauli ya aliyekuwa waziri wa Katiba, Dkt Ndumbalo kusema kuwa watatoa elimu ya Katiba Kwa miaka 3, nilidhani kuwa huo ulikuwa ni mtazamo wake na siyo wa chama chake.
Hata kuondolewa kwake kwenye wizara hiyo na kupelekwa kwenye wizara ya michezo, niliamini kuwa ilitokana na kauli yake ya kutaka kufanya "delaying tactics" katika suala nyeti kama Hilo.
Hata hivyo baada ya kumsikia Rais Samia Suluhu Hassan, naye akikilipigilia msumari kuwa ni LAZIMA, watanzania wapewe elimu ya Katiba kwanza, kabla hatujatunga Katiba mpya, ndipo nimetambua kuwa, kumbe huo ndiyo msimamo wa chama chao Cha CCM!
Najaribu tena kujiuliza, hivi kumbe Hawa watu wa CCM, ni watu wanaotumia ulaghai katika shughuli zao za kisiasa?
Nani atakuwa amesahau, wakati Halmashauri Kuu ya CCM, ilipotoka na kauli kuwa hata wao CCM, wanaitaka Katiba mpya haraka iwezekanavyo?
Ninajua vile vile kuwa, kutopatikana Kwa Katiba mpya, kunatokana na wenyewe watawala wa CCM, kutokubali kuwepo Kwa Katiba mpya, ili tuendelee kutumia hii Katiba ya mwaka 1977, wakati huo tukiwa bado kwenye mfumo wa chama kimoja.
Hivi watawala wetu wanadhani kuwa wananchi watakubaliana nao, kuendelea kutumia Katiba hii ya mwaka 1977 ya mfumo wa chama kimoja??
Kwani Tume ya Jaji Warioba ilifanya kazi Gani, kama siyo kutoa elimu na kukusanya maoni ya Katiba mpya??
Hivi Hawa watawala wetu, wanataka kutuambia kuwa hii Katiba tuliyonayo hivi sasa, ndiyo utashi wa wananchi walio wengi??
Hebu tujikumbushe, hata kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi, hao hao CCM, walitaka kutumia mbinu hii hii, wanayotaka kutumia hivi sasa, ya kwenda Kwa wananchi na kupokea maoni yao.
Mnakumbuka kilichotokea?
Pamoja na hayo maoni ya wananchi, ambao walikuwa asilimia 80, kudai kuwa bado wanapendelea kuendelea na mfumo wa chama kimoja, lakini Mwalimu Nyerere, ndiye aliyewalazimisha CCM, kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi.
Mwalimu alitoa sababu Kuu ya kukubaliana na asilimia Ile 20 iliyotaka mfumo wa vyama vingi, kuwa kutokana na dunia ilivyokuwa ikienda Kwa wakati huo, wanalazimika watawala wa CCM wa wakati huo, waingie kwenye mfumo wa vyama vingi, watake au wasitake!
Ninaamini pia kama Mwalimu Nyerere angekuwa hai hivi Leo, angelazimisha chama chake Cha CCM kikubaliane na kuleta Katiba mpya, Kwa kuwa inabidi nchi iende katika mfumo wa vyama vingi kiukweli, badala ya huu ulaghai unaoendelea.
Ukitafakari Kwa makini, utagundua kuwa hawa CCM, hawapendi nchi hii iwe na Katiba mpya, Kwa kuwa wanajua Katiba iliyopo sasa ndiyo inayoendelea kuwaweka madarakani!
Hivi unaweza kuwa na Katiba ya nchi yenye mfumo wa vyama vingi, Huku ukimrundikia madaraka makubwa mno, Rais aliyeko madarakani, ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama chake Cha CCM??
Nieleze kifupi tu Rais aliyepo madarakani, ambaye na yeye ni mgombea wa uchaguzi wa vyama vingi, ndiye anayewachagua wakurugenzi wa wilaya zote, ambao hao ndiyo pia wasimamizi wa uchaguzi zote, zinazotokea kwenye maeneo yao.
Bila kusahau kuwa yeye Rais aliyeko madarakani ndiye pia anamchagua Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na makamishna wake wote!
Hata hili suala la kumfananisha na Mungu, Kwa Rais aliyeko madarakani, kutoshitakiwa katika mahakama yoyote nchini, Kwa makosa yoyote aliyoyafanya, alipokuwa madarakani na hata pale anapotoka madarakani!
Kwa hiyo kutokana na kunogewa na madaraka makubwa mno aliyopewa Rais, ndiko kunakomfanya Rais yeyote anayeingia madarakani, achukie nchi kuandika Katiba mpya!
KATIBA MPYA NI SASA