Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,491
- 40,999
Ifike wakati Watanzania tutoe amri kwa watawala kwamba kama hakuna katiba mpya, hakuna uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2024, wala uchaguzi mkuu mwaka 2025.
Nchi hii ni ya Watanzania. Watanzania ndio wanaotakiwa kuwa na maamuzi ya namna gani wanataka nchi yao ifanye kila kitu.
Katiba hii ambayo Baba wa Taifa alisema inamfanya Rais kuwa dikteta sasa ifike mwisho. Rais anatakiwa kupewa mwongozo tuliokubaliana namna anavyotakiwa kutuongoza, na siyo yeye kutupangia namna anavyotaka kututawala kama ilivyo sasa.
Leo hii kila kitu ni Rais, kama vile nchi ni ya Rais. Kodi ni ya mwananchi, lakini Rais ndiye anakuletea mkurugenzi kuja kusimamia matumizi ya pesa yako. Hata ukiona huyo mkurugenzi anaiba, wewe unayetoa pesa huna uamuzi, mpaka aliyemteua apende, asipopenda, mteule wake anaendelea kutafuta pesa ya wananchi na hamna uwezo wa kumfanya chochote.
Fikiria, mpaka pesa ya wananchi, siku hizi inatajwa kuwa ni pesa ya Rais, eti Rais emetoa bilioni kadhaa kwaajiki ya ujenzi wa kisima, zahanati, shule, n.k.
Hata huko kwenye mataifa yenye katiba nzuri, sheria nzuri na mifumo mizuri ya utawala, siyo kwamba watawala walikuwa malaika, bali pressure ya wananchi iliwalazimisha watawala kukubali matakwa ya wananchi.
Kwa kuwa Serikali inalegalega, na kupiga danadana nyingi kuhusiana na suala la katiba nzuri mpya, katiba ya wananchi, lazima nguvu ya wananchi ishike hatamu, na Serikali ilazimishwe kufuata matakwa ya wananchi.
Na kwenye hili wananchi tushikamane, tuache mambo ya uCHADEMA, uCCM, uCUF, uACT, au tofauti zile nyingine za kijinga eti huyu ni sukuma gang, yule ni msoga gang, nasema huo ni upuuzi, sote tuunganishwe na utaifa wetu.
Leo mmesikia kuwa TANESCO, inayoendeshwa kwa ruzuku ya Serikali ya bara (nishati siyo suala la muungano) imesamehe deni la zaidi ya shilingi bilioni 60 iliyokuwa ikiidai Zanzibar. Hizi ni pesa za wananchi walipa kodi. Msamaha huo umetolewa kwa namna gani? Ni utaratibu upi uliofuatwa? Ni nani aliyetoa uamuzi wa kusamehe hilo deni? Ana mamlaka hayo?
Mambo haya inawezekana yanafanywa ama kwa shinikizo ama kwa kujipendekeza kwa Rais kwa sababu ni mzanzibari. Hatupingi kusamehe deni, tena kwa sehemu mojawapo ya muungano au kutoa msaada inapolazimu, lakini ni utaratibu upi umefuatwa kwa shirika linaloendesha kwa pesa za walipa kodi kuweza kufuta deni? Mbona hatujawahi kusikia kuwa TANESCO imewafutia deni wadaiwa sugu wa huku bara?
Katiba mpya itayaweka haya mambo yote wazi, na kuweka taratibu zilizokubalika na ambazo kila mmoja, na hasa viongozi, watatakiwa kufuata.
Hii ya kila kitu Rais, haikubaliki kabisa kwa namna yoyote ile. Kwenye teuzi, Rais aishie kuwateua mawaziri tu ambao wataidhinishwa na wabunge. Wengine wote waajiriwe au wachaguliwe. Wakivurunda, mamlaka za uajiri ziwafukuze kiurahisi.
Katiba siyo ya akina Lisu na Mbowe, siyo ya Rais wala Mutungi, siyo ya Chongolo, bali ni ya Watanzania wote. Yeyote anayetaka kujimilikisha uandaaji wa katiba ni adui yetu sote. Yeyote anayetaka kutushirikisha sote kwenye kupata katiba tunayoitaka, ni mzalendo wa Taifa letu, ni mtu mwenye upendo kwa Watanzania wa leo na vizazi vijavyo, na huyo ndiye tuandamane naye.
Hatutaki katiba maslahi ya watawala au wanasiasa tu, bali katiba itakayompa mamlaka makubwa mwananchi.