Tuwe wakweli: Ubunge umekuwa rahisi na usiotisha tena. Kuna wa kulaumiwa au kupongezwa?

Kiukweli nimeshangaa. MC Pilipili ndani, Mwijaku ndani, Steve Nyerere ndani, Zamaradi Mketema ndani...

Ila Tz hatuna ajira. Na hii ni ajira ambayo ukiimaliza tu baada ya miaka 5 kiinua mgongo unalipwa ndani ya siku ambacho ni zaidi ya 200M. Mshahara zaidi ya 10M kwa mwezi, seating allowance zaidi ya 200K.

Now kwanini tusifanye mtu alipwe kulingana na elimu yake? Kwamba sawa wewe Msukuma umechaguliwa kua mbunge hii ndiyo ajira yako ila kwa elimu yako mshahara ni 300K.

Sidhani kama watapinga. Si wamechagua kutumikia wananchi au?
 
JPM anapaswa kulaumiwa sana kwa kuleta mambo ya kienyeji, ubabe, udikteta, uonevu, kuua upinzani kwa kununua wapinzani, kuua demokrasia na kuruhusu siasa za kuabudu mtu mmoja. Tumepoteza muelekeo kabisa kama Tanzania. Hivi sasa hatuongozi tena kama kinara wa demokrasia Afrika, bali tumekuwa taifa lenye kutizamwa kwa jicho kali na jumuiya ya kimataifa kwa uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria.

Tumefika mhali pa hata kuwa "blacklisted" na nchi kama Marekani na hata baadhi ya viongozi kuzuiliwa kuingia nchini humo. JPM ameleta siasa za kibinafsi (populism). Amekuwa dikteta na amejenga misingi ya viongozi wengine kuwa madikteta na kuona ni sawa tu. Tafadhali tuondokane na uongozi huu la sivyo miaka mingine mitano mambo yatakuwa mabaya zaidi!
 
Ndiyo. Kupokea, kuchambua na kuwasilisha shida za wananchi wa Jimbo Bungeni si jambo dogo. Ni jambo linalohitaji kufanyiwa kazi kubwa ya kiakili na kimwili. Ubunge si lelemama!

Hata kama kazi ya kuwakilisha wananchi si ndogo, hiyo haina maana kazi hiyo ndo iwe ngumu na ya kutisha!

Kwa nini iwe ngumu? Ugumu wake ni nini hasa?

Zaidi, kwa nini itishe?

Uchaguzi wako wa maneno umekosa umakini [pengine kuliko hata hao uliolenga kuwakosoa].

Kuwakilisha wananchi siyo sayansi ya maroketi ya kwenda angani wala si upasuaji wa ubongo.
 
Taarifa kutoka kwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa zinadokeza kwamba kujitokeza kwa watia nia wengi kwenye majimbo ya uchaguzi kunatokana na ugumu mkubwa wa maisha ambao haujawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru wake 1961, uliosababishwa na ukosefu wa ajira na kuanguka kwa biashara nchini, ikiwemo kukosekana kwa wanunuzi hata wa mazao ya chakula , Mpunga wa Kyela unawadodea wakulima baada ya kukosekana kwa wateja kutokana na wafanyabiashara kufirisika.

Ikumbukwe kwamba kwa miaka mitano sasa nchi hii haijawahi kuajiri yeyote zaidi ya vibarua wabeba zege na mataruma ya reli kwenye ujenzi wa SGR unaoendelea, jambo lililofanya wasomi wote waliograduate katika kipindi hicho kukimbilia kwenye biashara duni za kimachinga na bodaboda ambazo hazikidhi matarajio yao.

Wengi sasa wamestuka na kuamua kujaribu kwenye ubunge ama udiwani kwa chama cha CCM ili kutafuta kufahamika na hata kama hawatashinda lakini waweza kuonekana na kuteuliwa popote iwe utendaji wa vijiji , kata ama hata kwenye U DAS au hata U DC , taarifa zinadokeza kwamba watia nia wengi wakiwemo hata waliokula rambi rambi za misiba ya wenzao wanachokitafuta ni kutambulika na labda kukumbukwa huko mbele ikiwa kama Mgombea wa CCM atashinda ( jambo ambalo hata hivyo halitarajiwi sana kwenye uchaguzi huu)

FB_IMG_1549369100113.jpeg

Itaendelea .....
 
Si wanaona wao wanaambiwa wachape kazi na watu waliokuja kuomba kura, ambapo baadaye wakaonekana ndani ya magari ya kifahari na viyoyozi huku wao wanakula vumbi na kuvuja jasho! Halafu ukizingatia kazi kubwa ni kupiga meza na kusifu? Nani aache? Fungulia mbwa hii inaitwa🤣🤦🏾‍♂️

Tutaona na kusikia mengi sana mwaka huu!
 
Hasa hasa baada ya rais kutangazia umma kuwa wakurugenzi hawatakuja kutangaza wapinzani basi watu wote wanaona bora kutia nia tu akipitishwa lazima atashginda. Katibu mkuu naye aliapa kutumia dola kuendelea kubaki madarakani na tunaona dola inavojiapiza mbele ya umma kuilinda na kuitetea CCM.

CCM ni chama cha kigaidi na hii ni serikali ya kishetani
 
Una maono
Ukweli mtupu
Tumegeuka kituko
Taifa limekosa Mtetezi
Ni biashara au maslahi zaidi
I hope Mkuu atapindua meza ...hakuna malipo zaidi ya mshahara wa kawaida na kupanda usafiri wa jumuya kufika bungeni.. he's got nothing to loose
Tutaelewana
 
Taarifa kutoka kwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa zinadokeza kwamba kujitokeza kwa watia nia wengi kwenye majimbo ya uchaguzi kunatokana na ugumu mkubwa wa maisha ambao haujawahi kutokea tangu nchi hii ipate uhuru wake 1961, uliosababishwa na ukosefu wa ajira na kuanguka kwa biashara nchini, ikiwemo kukosekana kwa wanunuzi hata wa mazao ya chakula , Mpunga wa Kyela unawadodea wakulima baada ya kukosekana kwa wateja kutokana na wafanyabiashara kufirisika.

Ikumbukwe kwamba kwa miaka mitano sasa nchi hii haijawahi kuajiri yeyote zaidi ya vibarua wabeba zege na mataruma ya reli kwenye ujenzi wa SGR unaoendelea, jambo lililofanya wasomi wote waliograduate katika kipindi hicho kukimbilia kwenye biashara duni za kimachinga na bodaboda ambazo hazikidhi matarajio yao.

Wengi sasa wamestuka na kuamua kujaribu kwenye ubunge ama udiwani kwa chama cha CCM ili kutafuta kufahamika na hata kama hawatashinda lakini waweza kuonekana na kuteuliwa popote iwe utendaji wa vijiji , kata ama hata kwenye U DAS au hata U DC , taarifa zinadokeza kwamba watia nia wengi wakiwemo hata waliokula rambi rambi za misiba ya wenzao wanachokitafuta ni kutambulika na labda kukumbukwa huko mbele ikiwa kama Mgombea wa CCM atashinda ( jambo ambalo hata hivyo halitarajiwi sana kwenye uchaguzi huu)

Itaendelea .....
Huu ni uzushi usio na kichwa wala miguu. Walishakula hadi rambi rambi? Wapi huko? Kyela?
 
Una maono
Ukweli mtupu
Tumegeuka kituko
Taifa limekosa Mtetezi
Ni biashara au maslahi zaidi
I hope Mkuu atapindua meza ...hakuna malipo zaidi ya mshahara wa kawaida na kupanda usafiri wa jumuya kufika bungeni.. he's got nothing to loose
Tutaelewana
Nami natarajia something unpredictable to happen from 2020...
 
Back
Top Bottom