Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,621
- 46,266
Naelewa vizuri sana na nakubaliana na mantiki ya kuchukua wanafunzi wa kike wenye ufaulu chini kidogo ya wale wa kiume kuwapeleka kidato cha sita na vyuo vikuu. Naona hilo ni jambo lenye mashiko.
Linapokuja suala la ubunge wa viti maalumu ndio huwa nashindwa kuelewa mantiki hasa ni nini. Wabunge wengi wanawake wanaopewa ubunge wa viti maalum ni watu wanaojiweza na wanaoweza kugombea ubunge sawa kabisa na wanaume na hata ikibidi kusaidiwa na vyama vyao kisha wapiga kura wenyewe wakaamua wanamtaka nani.
Wabunge wengi wanawake huwa wa viti maalum huwa hata hawajikiti katika mambo yanayowahusu wanawake tu katika maeneo yao bali wanazungumzia mambo yale yale ambayo yanazungumziwa na wabunge wanaume, sasa uwepo wao bungeni unasaidiaje mahususi maslahi ya wanawake wa nchi kwa ujumla?!
Na je serikali ina mpango mkakati wowote wa muda maalum wa kuhakikisha huo usawa unaotafutwa katika bunge unafikiwa na kwamba hiyo sera ya viti maalum kuna wakati itafika ukomo wake au hili ni jambo litaendelea kuwepo tu daima?