Tuwe wakweli: Ubunge umekuwa rahisi na usiotisha tena. Kuna wa kulaumiwa au kupongezwa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Mimi si mtu mzima sana ingawa nami najongea miaka ya kuweza kugombea Urais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba yetu ya sasa(miaka 40). Hatahivyo, nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa siasa na mambo ya kinchi tangu nikiwa mdogo. Leo, nitalizungumzia Bunge kama Mhimili mmojawapo wa dola. Mingine, wengi mnajua, ni Serikali na Mahakama. Nimeanza kulifuatilia Bunge lililokuwa likiongozwa na Hayati Chief Adam Sapi Mkwawa.

Bunge hili chini ya Hayati Mkwawa lilikuwa la chama kimoja: CCM. Lakini, Wabunge walipambana kwa hoja na kulipuana kwa shahidi mbalimbali. Mbunge alipokuwa akisimama kuchangia hoja au kutoa hoja, kiti cha Spika na Wabunge wenzake walitega sikio vya kutosha kusikia 'madini' ya Mbunge husika. Ilikuwa ni hoja juu ya hoja, vijembe, kebehi na matusi havikuwepo. Kama ni 'upinzani' basi ilikuwa ni kutofautiana kwa mawazo na hoja.

Likafuata Bunge la Spika Pius Msekwa. Lilifanana pakubwa na lile la Chifu Mkwawa ingawa hili lilikuwa na Wabunge kadhaa wa upinzani kama wa CHADEMA na NCCR-Mageuzi. Hatahivyo, hoja kinzani zilitolewa hata na Wabunge wa CCM. Katika Bunge hili, kashfa za kifisadi ziliibuliwa na wapinzani na hata Wabunge wa CCM. Ndipo paliposhamiri hoja nzito za Mzee Mzindakaya na wengineo (mfano kumhusu Waziri Mbilinyi na Waziri Simba).

Likaja Bunge la Hayati Samwel Sitta. Bunge la Viwango na Ubora. Likajionyesha na kujisimamia hivyo. Hoja, kutoka CCM na wapinzani zikawa motomoto na za uhakika. Bunge hili lilimuweka kwenye chati Balozi Slaa, kwa kumtaja mmoja. Baadaye likaja Bunge la Mama Makinda. Ufanano mkubwa wa Mabunge haya ya Hayati Sitta na Mama Makinda ni 'uhuru' wa Wabunge kutoa hoja zao na kutumia tafiti kujenga hoja zao. CCM na wapinzani walifanana katika hilo.

Baadaye, hivipunde, likaja Bunge la Spika Ndugai. Hakika, Bunge hili lilianza vyema katika kufuata nyendo za watangulizi wake. Halafu, mambo yakabadilika. Bunge likawa sehemu ya 'mapambio', 'kejeli', 'vijembe', matumizi makubwa ya maneno ya kuudhi na kutweza na kadhalika. Katika hali hiyo, Wabunge wengi wa upinzani wakajikuta kwenye wakati mgumu wa kukumbana na adhabu za mara kwa mara. Si kwamba wa CCM hawakuwa wakitenda makosa, ila wingi wao na kiti cha Spika viliwabeba.

Bunge la Ndugai limeonyesha taswira la Bunge lijalo. Limeonyesha uzito au urahisi wa Ubunge na kuwafanya maelfu ya watanzania kutamani kuwa Wabunge. Kiukweli, kama ni wa CCM wanaamini kuwa wakiwa Wabunge hali itakuwa ile ile. Wanajiamini na kuona kuwa hakuna haja ya 'hard work' katika Ubunge wao. Kwa wapinzani, wao wanatamani na kuamini kwenda kuendelea kupambana na kiti cha Spika. Hoja zinawekwa kando. Labda yaonekana hoja si ajenda tena ya Bunge lijalo. Mambo yamekuwa rahisi na kila mtanzania anaweza kuwa Mbunge.

Kuna wa kulaumiwa au kupongezwa kwa kufikisha hali hii ya Bunge na Ubunge kwa ujumla?
 
toka lissu atoke hakuna bunge tena wenye hoja wamesajiliwa kama wachezaji kwenye vilabu vya mpira na wamekua kimnya au wakata mauno, na uchaguzi ujao ndio unaonekana utakua na wakata mauno wengi, tuombe Mungu wakatwe maana litakua sio bunge dhaifu tena Bali litakua mfu!
 
Kitendo cha watu wengi kujitokeza kutia nia na kuchukua fomu za kuwania ubunge ni dhihaka na dharau kubwa kwa kazi ya ubunge. Ukilichukulia jambo hili kwa akili za juujuu bila kufikiri kwa undani, unaweza kudhani kitendo hiki kinaashiria kukomaa kwa demokrasia kumbe sivyo. Jambo hili nalitazama kwa dhana kuu mbili:

Mosi, baada ya wabunge wengi vilaza (wanajulikana) kufanikiwa kuingia mjengoni mwaka 2015, wananchi wameanza kuichukulia kazi hii ya uwakilishi wa wananchi kwa wepesi usiokuwa wa kawaida. Kwa kuwa sifa za kuwa mbunge zimerahisishwa mno, ilmradi tu mtu anajua kusoma na kuandika (kwa Kiswahili) hata kama uwezo wake unaishia kusoma mstari mmoja tu wa maandishi, na pasipo kuzingatia kama ana uwezo wa kuchambua hayo maandiko kwa uyakinifu, kumewafanya watanzania wengi wasiokuwa na ajira rasmi kuona kuwa kimbilio rahisi kabisa ni mjengoni.

Katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia vilaza wengi wakiingia bungeni kwa sababu tu ya ushabiki wa kisiasa na ‘njaa za wananchi’. Watanganyika wengi wanauchukulia ushabiki wa kisiasa kama ushabiki wa Yanga na Simba. Hawajui jinsi ushabiki holela wa siasa unavyoathiri maisha yao. Juzi nilikuwa naongea na mwananchi mmoja ambaye alidai tangu azaliwe hadi sasa anapokaribia umri wa miongo 5, hajawahi kupiga kura kwa sababu haoni faida na umuhimu wa kumchagua kiongozi yeyote (kuanzia ngazi ya mtaa hadi Urais!). Watu wa kaliba hii wapo wengi hapa nchini Tanganyika na ni rahisi sana kuwanunua wakati wa uchaguzi.

Kwamba wapigakura mara nyingi hawaangalii sura au uwezo wa mwakilishi wao ghairi ya ushabiki uchwara wa kisiasa, sio suala geni katika nchi hii. Tumeshuhudia wananchi wengi wakilaghaiwa kwa T-shirts, kofia na pombe za kienyeji kila uchaguzi mkuu unapowadia. Na kwa sababu watu ni masikini na wana njaa kali, hujikuta wametumbukia kwenye mtego huu wa panya, hivyo kupelekea kuwachagua vilaza wa kutupwa kuingia mjengoni huku wao wakiendelea kuzama kwenye lindi la umaskini, maradhi na ujinga mamboleo.

Katika uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, uchukuaji fomu kwa vilaza umeongezeka maradufu. Ikiwa vilaza wengi watafanikiwa kupenya kwenye chekekeche la vyama na hatimaye kushinda viti vya ubunge, rais ajaye atakuwa na kazi ngumu sana kuteua mawaziri zaidi ya ilivyokuwa miaka 5 iliyopita tuliposhuhudia wabunge wote wa kuteuliwa wakipewa uwaziri baada ya waliochaguliwa na wananchi kutokidhi vigezo.

Pili, suala hili la watu wengi ‘kukimbilia’ mjengoni limechochewa na ugumu wa maisha miongoni mwa watanganyika walio wengi (99.9%). Watu wamechungulia wakaona jinsi wabunge wanavyolipwa mishahara minene na marupurupu chekwa wameona kuwa wenzao wanafaidi mno keki ya taifa. Hivyo, nao wanatamani kuingia mjengoni wale maisha. Na ikiwa vyuma vitaendelea kukaza kama ilivyo sasa, mwaka 2025 tutarajie ‘mafuriko’ makubwa zaidi ya mwaka huu. Kitu kingine kinachowapa jeuri watia nia ni ushabiki holela wa kisiasa uliopo kwenye baadhi ya majimbo. Katika majimbo yenye ushabiki kintekinte, mtu akishapitishwa na chama chake tayari unakuwa ‘mbunge mteule’. Hii huwasukuma watia nia kutumia rasilimali nyingi kadri wawezavyo, hata ikibidi mtu kumuuza mkewe au mumewe, ilmradi tu apenye kwenye chekeche la chama. Na kwa kuwa wapigakura wana njaa, kazi inakuwa nyepesi kuliko kumsukuma mlevi.

Katika nchi zilizoendelea ni nadra sana watu wenye njaa kukimbilia mjengoni. Hawana nafasi hiyo. Kumchagua mwakilishi mwenye njaa ni sawa na kumchagua fisi kulinda bucha. Fisi atakula nyama zitaisha, atakula gogo na mashoka ya kukatia nyama, hadi mzani! Hata katika nchi jirani sifa kubwa ya mgombea lazima awe tajiri. Hii husaidia kudhibiti ‘njaa kali’ na wachumiatumbo kukimbilia mjengoni. Nchini Tanganyika, kinyume chake ndio ukweli. Sasa vilaza na watu waliokata tamaa ya maisha wanapigana vikumbo kuingia mjengoni.

Hasara za kuchagua wabunge vilaza zipo nyingi. Hivi unadhani mbunge kilaza anaweza kutunga sheria yenye kuleta mashiko kwa wananchi? Ndio maana tunashuhudia sheria zikirudishwa bungeni kufanyiwa marekebisho hata kabla hazijatungiwa kanuni na kuanza kutumika. Haya ni matokeo ya vilaza wa kutupwa waliorundikana mjengoni. Na uzuri wa siasa za Tanganyika mtu anayepayuka sana hata kama hana kitu kichwani ndiye anaoenekana mwanasiasa bora na wananchi humshangilia sana.

Tofauti na nchi jirani ambako kiwango cha chini cha elimu ya mbunge ni shahada ya uazmili, nchini Tanganyika vilaza wengi waliokimbia shule wakaenda kujifunzia mwituni *kusoma na kuandika* ndio wanapigana vikumbo kuingia mjengoni kuwawakilisha watu wenye akili kubwa. Inasikitisha kwamba wasomi wengi wameacha kuingia kwenye siasa, hivyo kuwapa mwanya vilaza kuchukua hatamu. Ifike wakati serikali ya Tanganyika itunge sheria ya kudhibiti vilaza kutumia matobo ya kisheria kupenya hadi mjengoni ili kurudisha heshima ya ubunge.
 
Kwny Bunge la 2020-2025 Spika anatoa tangazo:

" kikao chetu cha mchana khs Muswada wa kuruhusu matumizi ya Nishati ya Nuclear kuzalishia umeme ataanza Mh. Harmonizer kuchangia hoja then atafuatiwa na Mh. Steve Nyerere akitoka hapo Mh. Kingwendu nae anatoa hoja zake huku Mh. Musukuma akipewa dakika tano za kuongea na tutafunga kikao chetu kwa hoja za Mh. Babu tale.'

Hakika hili litakua bunge la kisayansi.
 
Si unaona wabunge km kina lusinde, msukuma huwa kazi yao kusema watu na kuchekesha huku wakilamba posho za maana kwa nn watu wote wasitake kua wabunge huku wabunge wa ccm kazi yao ni kusema ndio na kupiga makofi huku wengine wengi wakilala kwa nn isionekane ubunge ni kitu rahisi?????!!!!!

Tumefikishw ahapa na serikali hii ya kishetani
 
Back
Top Bottom