Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 987
Sasa ni wazi kwamba pamoja na sarakasi zote za kukamata wapinzani wanaoendekeza mijadala juu ya katiba mpya, lengo liko wazi ni kuzima Mjadala ili kuepusha kuiamsha jamii ili isipige kelele juu ya mchakato wake. Sasa ni wazi kua hii siyo CCM tu bado ni mfumo mzima hautaki katiba mpya huenda wana yao tusiyoyajua na wala siyo kuyumba kwa uchumi.
Watawala wetu wanashindwa kuelewa kuwa hakuna mgogoro mbaya duniani kama wa kudai katiba mpya, wamefumba macho hawakuelewa hili,mjadala wa katiba ni mgumu sana kuuzima kuliko kudai haki yeyote ile. Tunakoelekea kila kosa litakalofanyika wananchi watasema ni kwa sababu ya katiba mbovu. Itafika wakati wataona kua hawana haki katika taifa lake na wanufaika ni kikundi cha watu wachache wanaozuia mchakato wa katiba mpya. Hapa ndio watu watachoka na itapatikana kwa kupenda ima kwa kutopenda.
Ni askari gani atakayeweza kukukamata watu kwa sababu ya kuandamana kudai katiba mpya? Ataenda kuwafungulia kesi gani wakati wanachodai ni haki yao? Zaidi zitakua ni kesi za uhujumu uchumi na ugaidi ili kuwanyima dhamana wanaoongoza vuguvugu hili ili wasitoke ambapo nako hakuna ushahidi utakaoweza kumtia mtu hatiani . Huwezi kuondoa uhai wa mtu kwa sababu anaidai haki yake, katika hili itajikuta uko matatani.
Kwahiyo hakuna mwenye uwezo wa kuuzima mjadala wa katiba mpya huu ukishaanza umeanza, hua ni ngumu kuuzima zaidi ya kusikiliza wanaoidai. Kumfunga Mbowe haitakua njia ya kuuzima mjadala huu kwa sababu ni wa kitaifa, zaidi ni kutengeneza mijadala mipya ya wafungwa wa kisiasa.
Walioshauri kuuzima mjadala wa katiba mpya kuna siku watatajana wao wenyewe na watakumbuka maamuzi yao.