Je Katiba ni mali ya Serikali? Kama sivyo, kwa nini mpaka Rais ndo aruhusu mchakato?

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Rais anavunja katiba wazi wazi kwa kuzuia mchakato wa Katiba Mpya. Anaposema wananchi hawana ufahamu kuhusu Katiba, yeye ni malaika? Aliikuta Katiba na wananchi tunataka Katiba Mpya ili tuweze kurekebisha makosa ambayo watawala wanayafanya wakiamini uongozi ndiyo umiliki wa nchi

Rais anapaswa kufahamu kwamba nchi hii haimilikiwi na vyombo vya ulinzi na usalama bali wananchi kwa ujumla wao.

Mchakato wa Katiba Mpya siyo zawadi bali ni TAKWA la wananchi.

SIsi siyo wajinga
 
kwahiyo wewe ndio una haki zaidi uskizwe? yeye kwa vile ni raisi,sio mwananchi....

kwan wewe na yeye si wananchi 🐒

na kwani ni lazima muwe na mahitaji, nia na mitazamo sawa juu ya katiba 🐒

kuna ubaya gani kukubaliana kutofautiana 🐒
 
Simply
Umepanic
haya sawa,
hata na hivyo pendekezo lako ni after general election, meaning ni 2026 ndipo serikali itaona kama kuna umhuhimu ama haja ya kulifanyia kazi kadiri itakavyoonekana inafaa....

kwasasa just relax,
Jiandae kuchagua viongozi wa serikali za mitaa mweshoni mwa mwaka huu2024 na mwaka ujao 2025 uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais waJMT...
 
haya sawa,
hata na hivyo pendekezo lako ni after general election, meaning ni 2026 ndipo serikali itaona kama kuna umhuhimu ama haja ya kulifanyia kazi kadiri itakavyoonekana inafaa....
Umeona hata hujui unachangia nini.

Safi sana kwa kujibu kwa.sehemu kwamba Katiba ni mali ya serikali
 
Kuna mambo tunayadai kwa haki ila njia inayotumika hupelekea uvunjifu wa uhutaji.

Raisi ni mamlaka kamili ambayo imepewa mamlaka na wananchi ndiyo maana analindwa na kusimamia katiba. Hayupo juu ya katiba bali anaisimamia.

Uwepo wa Serikali unaanza nyuma sana mpaka tunapata mtu mmoja aongoze wengi… Msome Thoma Hobbes utaelewa State of Nature ilikuaje.

Azimio la Serikali si Katiba tu lina vitu vingi vya msingi na ndiyo maana hakuna mtu anaizungumzia. Huenda wanaona hii katiba imejitosheleza.

Kipindi cha Kikwete palikua na Mchakato wa Katiba mpya, na ukaishia njiani.

Sasa unaposema Rais ni nani kwenye katiba unakua unakosea kwa sababu yeye ndo anaratify katiba, analipw watu wanaofuatilia mchakato wa katiba, ana mamlaka kamili ya kukubali au kukataa wazo la katiba. Si kila wazo analokuwa nalo mtu lazima liwe na makubaliano bande zote, ni muhimu pawe na ukinzani ili kuweka uhai wa hilo suala. Ukiona kila hoja unayoleta inapita na huwa haikosolewi baai jua tu hapo pana uozo sana.

Rais ndiye mwenye mamlaka na kila kitu. Soma katiba Kuanzia Ibara ya 33 utaelewa Rais ni nani na Mamlaka yake yapoje.
 
kwahiyo wewe ndio una haki zaidi uskizwe? yeye kwa vile ni raisi,sio mwananchi....

kwan wewe na yeye si wananchi

na kwani ni lazima muwe na mahitaji, nia na mitazamo sawa juu ya katiba

kuna ubaya gani kukubaliana kutofautiana
Wewe ni mental Simple.
 
ni mali yako pekeyako

sijua halafu nimejibu
Dalili za ubongo uliochanganyika na haja kubwa hizo.
JamiiForums663665719.jpg
 
Rais anavunja katiba wazi wazi kwa kuzuia mchakato wa Katiba Mpya.
Kiukweli elimu ya katiba inahitajika sana!, hakuna uvunjifu wowote wa katiba kwa kuzuia mchakato wa katiba mpya kwasababu kwenye katiba iliyopo hakuna takwa la Katiba mpya!. Ili katiba ivunjwe, lazima katiba iwe na takwa hilo!.
Anaposema wananchi hawana ufahamu kuhusu Katiba, yeye ni malaika?
Haihitaji malaika kujua Watanzania hawaijui katiba, sheria wala haki zao!. Msikilize hapa kwa makini
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=bmY2lAbL7vLKSaTM
Aliikuta Katiba na wananchi tunataka Katiba Mpya ili tuweze kurekebisha makosa ambayo watawala wanayafanya wakiamini uongozi ndiyo umiliki wa nchi
Naunga mkono hoja
Rais anapaswa kufahamu kwamba nchi hii haimilikiwi na vyombo vya ulinzi na usalama bali wananchi kwa ujumla wao.
Naunga mkono hoja
Mchakato wa Katiba Mpya siyo zawadi bali ni TAKWA la wananchi.
Mchakato wa katiba mpya ni hisani
SIsi siyo wajinga
P
 
Kiukweli elimu ya katiba inahitajika sana!, hakuna uvunjifu wowote wa katiba kwa kuzuia mchakato wa katiba mpya kwasababu kwenye katiba iliyopo hakuna takwa la Katiba mpya!. Ili katiba ivunjwe, lazima katiba iwe na takwa hilo!.
Mkuu Paskali,
Neno mazingara au kwa lugha yenu wataalam circumstantial hupelekea uelewa ama ufafanuzi wa jambo fulani lionekanike ama lieleweke kwa mizania ya anayeliishi muda huo. Nitarejea kwenye hili soonest (nitakutag)
Haihitaji malaika kujua Watanzania hawaijui katiba, sheria wala haki zao!. Msikilize hapa kwa makini
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=bmY2lAbL7vLKSaTM

Sample uliyoitumia haijustify kuwa Watanzania hawaielewi ama kuijua Katiba. Naweza kusema uwezekano wa kuokoteza vipande kujustify hoja ndiyo nimeliona hapa
Mchakato wa katiba mpya ni hisani

P
Nini maana ya Katiba?
Nini chimbuko la Katiba?
Katiba ni kitu gani?
Nani anamiliki Katiba?

Hayo maswali ni muhimu kuyaelewa kabla ya kuinuka na kuyajibu.

Narejea kusema Katiba siyo Hisani
 
haya sawa,
hata na hivyo pendekezo lako ni after general election, meaning ni 2026 ndipo serikali itaona kama kuna umhuhimu ama haja ya kulifanyia kazi kadiri itakavyoonekana inafaa....

kwasasa just relax,
Jiandae kuchagua viongozi wa serikali za mitaa mweshoni mwa mwaka huu2024 na mwaka ujao 2025 uchaguzi Mkuu wa madiwani, wabunge na Rais waJMT...
Kama hawataki nguvu itumike kuwaondoa. Nguvu gani? Hapo ndio sijui maana sina ushauri wowote, yaweza kuwa nguvu ya umma au vinginevyo

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom