Katiba mpya ni tishio kwa CCM, hawatakubali ipatikane kwa hiari labda walazimishwe

MGOGOHALISI

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
1,984
2,587
Huo ndio ukweli. survival ya Ccm inategemea katiba mbovu waliojifungia wenyewe wakaiandika. Leo wamekiri wenyewe kupitia mwenyekiti wao kuwa watu hatuijui katika ya sasa (japo twaijua).

CCM hawana uhakika katiba mpya itawasaidia vipi kuendelea kubaki madarakani, wana hofu, wamejawa na baridi ya simanzi.

CCM wanaona katiba mpya ndio mwisho wa wao kuwa miungu watu katika nchi hii. Ulaji wao unaporwa na katiba mpya. Ulaghai unamalizwa na katiba mpya.

Uelewa wa watu kuhusu katiba iliyo bora unawatisha CCM. Sio kweli kuwa watu hawajui katiba bali ni kinyume chake. Upepo wa katiba mpya hauibebi CCM kwa vyovyote vile. Wameshakaa na kutathimini, sasa ni mwendo wa visingizio tu.

Samia alifikiri wanaodai katiba ni watu wasiojua wanachokitaka. Akaingia mkenge kuahidi anaanzisha mchakato. Wenzake chumbani washampa makavu live, sasa hivi anayeongea sio yule Samia aliyesifiwa anaupiga mwingi. Anayeongea ndani ya Samia sasa hivi ni lile kundi la CCM, wasiokubali katiba mpya iwapoke tonge mdomoni. Samia ni kipaza sauti tu. Anyeongea ni CCM mpenda maslahi kuliko haki.

Katiba mpya itapatikana kwa CCM kulazimishwa. La sivyo hakuna katiba itapatikana.
 
Huo ndio ukweli. survival ya Ccm inategemea katiba mbovu waliojifungia wenyewe wakaiandika. Leo wamekiri wenyewe kupitia mwenyekiti wao kuwa watu hatuijui katika ya sasa (japo twaijua...
Huo ndo ukweli wenyewe. Hata hizo taarabu zote za leo shida ni Uraisi

Walikuwa wapi miaka yote kutoa elimu ya katiba.
 
Huo ndio ukweli. survival ya Ccm inategemea katiba mbovu waliojifungia wenyewe wakaiandika. Leo wamekiri wenyewe kupitia mwenyekiti wao kuwa watu hatuijui katika ya sasa (japo twaijua)...
Unataka katiba mpya utapata katiba mpya lakini useme unachokitaka ni kipi na kipi katika katiba mpya. Tuanzie hapo.

Au unasemaje?
 
Na huu ndio ukweli, kigezo cha itolewe elimu kwa miaka mitatu ni iwe msaada kwao wavuke uchaguzi mkuu wa 2025. Maana ukiwa huru na haki ni tanuru gumu sana kwao kuvuka
 
Back
Top Bottom