Tusiukubali mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu zozote zile. Utakuwa ni mtego utakaotunasa kama nchi

Sasa iyo nguvu unayotumia tukatae huo mkataba basi ielekeze ili tuweze kuuona huo mkataba.

Unakataaje kitu ambacho hukifahamu? Embu jaribu kutafakari na wewe.

Nikukumbushe tu kuwa, hao hao wachina unaowaona na kusema wametaka bandar sijui wapi, ndio waliomsaidia Nyerere kuongoza nchi kwa kipindi chote alichokuwa madarakani.

Kuanzia ndege za jeshi, silaha za kijeshi, mifumo ya utawala n.k
Sawasawa kabisa ila ukumbuke ile ilikuwa china ya kijamaa na hii tunayo izungumzia niyakibepari
 
kachungulieni ZAMBIA nchi jirani....kuna maDC wachina.......tujifunzie hapo...ilikuwaje.....MALAWI napo na chokochoko ya ziwa NYASA.....chinese wako wanawapumulia......mikopo ya KIFEDHULI......hatukatai maendeleo....miyo MIKATABA IWEKWE HADHARANI.........wasomi wanazuoni wa SHERIA mko wapi.....wote mmemezwa na siasa za MATUMBO.......TANZANIA hakuna "MNYONGE" ila tuna wasomi DHAIFU.......SHENZI KABISA...
 
Tuna sababu moja kubwa ya kuukata Mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo nayo ni historia mbaya ya China kona mbalimbali za dunia walipotekeleza miradi ya aina hii au walipozikopesha nchi mikopo mikubwa ya miondombinu. Wamechukua bandari Sri Lanka, Pakistan, Australia na Djibouti kupitia mikataba ambayo haieleweki ni yenye utata sana.

Kama huko wameweza kufanya hivyo sisi hatutaweza kuwadhibiti na kuibakiza bandari ya Bagamoyo kuwa bado mali yetu endapo tukiwakubalia wajenge bandari hapo.
Tusijidanganye, sote tunafahamu jinsi gani mikataba midogo tu ya madini imekuwa changamoto kubwa kwa taifa hili, huu ukizingatia na usiri wa mikataba utakuwa funga kazi, tutauzwa mchana kweupe kama enzi za Mangungo wa Msovero.

Tukubali tu kwamba wao ni wajanja na kutekeleza kwa miradi ya aina hii duniani kumewapa ujanja zaidi. Tusikubali bandari zetu kujengwa na kuendelezwa na wageni kwa sababu yoyote ile. Kama tunafikiri ni muhimu sana na tunatakiwa kuwa na Bandari Bagamoyo tukope pesa tujenge wenyewe, vinginevyo tutaiuza nchi yetu nzuri.
Itakuwa white elephant kama tazara iliyojengwa kunufaisha jirani ambaye ana reli yake Zambia Railways.

Bandari tunazo Dar, Tanga, Mtwara zinatosha. Bagamoyo bila wadau zaidi ya TZ na China kama DRC, BURUNDI, RWANDA na taasisi za kimataifa tutaishia kugharamia pekeyetu halafu mjirani ndio watafaidika na bandari hiyo. Mfano ni barabara zetu za lami. Bidhaa kama petroli BURUNDI bei ndogo kuliko TZ ambapo zinapita Dar Port na kusafirishwa kwenye barabara zetu!

Bila data na physibility studies za miradi hii kuonyesha umuhimu wake sasa na baadae ni kukurupuka.
 
Kwani ripoti y CAG inasemaje? Hii ndio itakata mizizi yote ya fitina
Marehemu hata achukue miaka 10 kutooza halitaondoa ukweli kuwa hafufuki tena
Ripoti ipi mkuu? Kuna swali liliulizwa humu kuwa, je, ripoti aliyoisoma Kichere hivi karibuni kwa raisi Samia ndio ambayo angeisoma mbele ya raisi Magufuli kama angekuwa hai?

Kuna mtu amesema alinyimwa nyaraka za ununuzi wa ndege hivyo ikamzuia kutimiz wajibu wake. Hii ni baada ya Magufuli kufariki, kwa maoni yangu ni kumaanisha kuwa nyaraka hizo zilizuiliwa na Magu. Kichere alipata wapi na kwa muda gani, baada ya jamaa kufa? Kwamba Samia akaruhusu zitoke na kabla ya siku 21 ukaguzi na taratibu zote zikakamilika? je, ni rahisi kiasi gani kukagua na kukamilisha taratibu zote za ukaguzi na uandishi wa ripoti hizo?

Tumuombe CAG atupatie taarifa za shirika mojawapo la serikali linalojiendesha kwa faida au lililojiendesha kwa faida kwa miaka 10 mfululizo bila kutegemea ruzuku.

TANESCO ni moja ya mashirika yanayopaswa kujiendesha kwa faida bila kupepesa macho kwakuwa wanazalisha na kuuza bidhaa inayotafutwa na kila raia, nini kinalikwamisha shirika? Serikali za awamu zilizopita hazikununua mitambo mikubwa kwa gharama maradufu? Usije sema unanufaika na umeme, sema uwezo wako wa kujiunga kwenye gridi na kununua units ndo zinazokufanya u-justify hilo.

Biashara ya mawasiliano, jinsi gani makampuni ya wawekezaji yanavuna pesa, TTCL kunani? Kwanini iwe ATCL tu?

Mamlaka za maji za miji yote, zinajiendesha kwa faida?

RADAR iliyonunuliwa kwa bei ya cha juu, inazalisha faida kiasi gani kwa taifa? Ulinzi ni kisingizio.

Ukitaka kutafuta makosa kwa mwanadamu aliyepata kuishi kuzidi utoto wa kutojitambua, hutakosa. Ukomavu ni kuanzia pale alipoishia mwingine na kwenda mbele kwa tahadhari zote bila kujali aliyetangulia alifanya mabaya mangapi.

Tukianza kula nyama za binadamu, hatutaacha. Inasemekana kuwa wewe unalijua hili vizuri zaidi.
 
Ripoti ipi mkuu? Kuna swali liliulizwa humu kuwa, je, ripoti aliyoisoma Kichere hivi karibuni kwa raisi Samia ndio ambayo angeisoma mbele ya raisi Magufuli kama angekuwa hai?

Kuna mtu amesema alinyimwa nyaraka za ununuzi wa ndege hivyo ikamzuia kutimiz wajibu wake. Hii ni baada ya Magufuli kufariki, kwa maoni yangu ni kumaanisha kuwa nyaraka hizo zilizuiliwa na Magu. Kichere alipata wapi na kwa muda gani, baada ya jamaa kufa? Kwamba Samia akaruhusu zitoke na kabla ya siku 21 ukaguzi na taratibu zote zikakamilika? je, ni rahisi kiasi gani kukagua na kukamilisha taratibu zote za ukaguzi na uandishi wa ripoti hizo?

Tumuombe CAG atupatie taarifa za shirika mojawapo la serikali linalojiendesha kwa faida au lililojiendesha kwa faida kwa miaka 10 mfululizo bila kutegemea ruzuku.

TANESCO ni moja ya mashirika yanayopaswa kujiendesha kwa faida bila kupepesa macho kwakuwa wanazalisha na kuuza bidhaa inayotafutwa na kila raia, nini kinalikwamisha shirika? Serikali za awamu zilizopita hazikununua mitambo mikubwa kwa gharama maradufu? Usije sema unanufaika na umeme, sema uwezo wako wa kujiunga kwenye gridi na kununua units ndo zinazokufanya u-justify hilo.

Biashara ya mawasiliano, jinsi gani makampuni ya wawekezaji yanavuna pesa, TTCL kunani? Kwanini iwe ATCL tu?

Mamlaza za maji za miji yote, zinajiendesha kwa faida?

RADAR iliyonunuliwa kwa bei ya cha juu, inazalisha faida kiasi gani kwa taifa? Ulinzi ni kisingizio.

Ukitaka kutafuta makosa kwa mwanadamu aliyepata kuishi kuzidi utoto wa kutojitambua, hutakosa. Ukomavu ni kuanzia pale alipoishia mwingine na kwenda mbele kwa tahadhari zote bila kujali aliyetangulia.

Tukianza kula nyama za binadamu, hatutaacha. Inasemekana kuwa wewe unalijua hili vizuri zaidi.
Tukianza kula nyama za binadamu, hatutaacha. Inasemekana kuwa wewe unalijua hili vizuri zaidi.
 
Darasani kwa Dr
Yahya Msangi

Notice: jifanye yako ule block fasta

BANDARI YA BAGAMOYO HAIFAI HATA IKITIWA TUI LA NAZI NA KINA "MADE IN CHINA"

Awali ya yote nimshukuru Allah kwa kuniponya maradhi na kuniwezesha kufunga mwezi mtukufu. Niwashukuru wote mlioniombea.
Wakati nikiwa naumwa nilijitahidi kupitia hoja mitandaoni kila nilipoweza. Haswa za kuhusu report ya CAG na Bandari ya Bagamoyo. Léo nitajikita kwenye bandari kwa kuwa ni suala linaonyesha ni jinsi gani baadhi ya viongozi wetu walivyo wanafiki kwa kuwa wamepigwa mhuri mgongoni wa "MADE IN CHINA"!

Kabla ya kueleza ni kwa nini bandari ya Bagamoyo haifai hata ikipuliziwa pafyumu na kina Lusinde na wenzake waliosimama kumtetea spika eti watu "hawakumuelewa" nianze kwa kuwakumbusha (mnaosahau haraka) mauzauza ya hii bandari.

Uzauza namba 1:
Ndugai alitoa taarifa bungeni mara tu alipofanya ziara na ujumbe wake (ingefaa muwajue waliokuwa msafara wa Ndugai Kabla hamjawasifu). Katika taarifa île pale bungeni (Kabla Magufuli hajaeleza masharti ya hovyo ndani ya mkataba) Ndugai alitamka kuwa walikutana kwa bahati mbaya na viongozi wa China...! Fikiria mwenyewe hivi: Spika wetu na ujumbe wake walikutana kwa 'bahati mbaya' na viongozi wa taasisi iliyotupa masharti ya kihayawani? Spika alidai ilikuwa bahati mbaya kwa kuwa safari yao ilihusu mkutano wa kuanzisha utaratibu wa kidijitali (digitalization of parliament aka BUNGE DIGITAL).

Hivi inawezekanaje spika na ujumbe wake wakutane kwa 'bahati mbaya' na waliotoa masharti ya kuhujumu nchi? Spika alidai walifanyiwa presentation "nzuri mno"! Hivi hiyo presentation "nzuri mno" nayo iliandaliwa kwa bahati mbaya? Haikueleza masharti ya kuhujumu nchi? Spika na ujumbe wake hawakupewa nakala ya mkataba? Pale bungeni spika alisherehesha hoja yake kwa kudai katika kampuni inayotaka kutujengea bandari wamebaki wazee wachache mno wanaoipenda Tanzania! Éti tukubali haraka mradi kabla hawajafa au kustaafu! Spika akaendelea kusherehesha hoja yake kwa kudai wachina wanatucheka sana na wanaweza kwenda kuwekeza kwingine! Hakika ukishapigwa muhuri kama ng'ombe mnadani unaweza kutetea hoja yako kipumbavu mno!

Uzauza Namba 2:
Katika kujieleza na kupigia chapuo mradi wa wachina Spika hakujua anatupa habari nyingine ya kusikitisha na kustua. Kwa kuwa watanzania wengi sio wachambuzi hakuna aliyeona hatari iliyopo! Wachina ndio walijenga ukumbi wa Umoja wa Afrika (AU) na ndio walifunga vifaa vya digital pale Addis Ababa. Siku moja kwa bahati mbaya usiku wa manane mtaalam mmoja mzalendo akahisi kuna mawasiliano yanaendelea ! Katika kuchunguza akakuta ni mawasiliano kati ya wataalamu wa kichina na wenzao walioko China! Ndipo uchunguzi ulipofanyika ikagundulika wachina walikuwa wananasa mawasiliano na taarifa zoote ya AU! Ikumbukwe mawasiliano mengine ni siri n'a yanahusisha wakuu wa Nchi! Kashfa hii inafahamika vizuri na nchi zote na hâta Tanzania ! Sasa Spika WETU alienda China kuonyesha digitalization ya bunge letu! Kuna kinachozungumzwa au kujadiliwa bungeni kwetu mchina asijue?Je hawa wanaotetea mradi wa mchina sio kwamba wanajua aliyewapiga mhuri mgongoni anawasikiliza?

Uzauza namba 3:
Nilimsikiliza Spika akirejea hoja yake baada ya kifo cha Magufuli. Spika hakusema chochote kuhusu kurekebisha masharti! Hawa kina Kibajaji wanaodai watu hawakumuelewa Spika sio miongoni mwa waliopigwa mhuri mgongoni kwa bahati mbaya kule China? Au tu unafiki wao? Maana Magufuli alipoeleza ubaya wa masharti hatukumsikia Kibajaji na wenzie wakimwambia masharti yarekebishwe! Kibajaji ni mmoja wa aliyesifu hatua thabiti ya Magufuli kupinga bandari! Léo mnapataje Akili ya kumsifu msaliti sampuli hii? Kibajaji kacheza na akili za wasiofikiri! Kakemea kumdhalilisha Marehemu na hapohapo kamsaliti kwenye hoja ya bandari. Anayethamini kazi ya Magufuli hawezi kutetea bandari ya mchina! Hivi masharti aliyaweka Kibajaji au Spika? Sio wachina? Utasemaje yaondolewe wakati hukuyaweka wewe na tukikutizama una mhuri wa made in China mgongoni? Pindi Serikali itakapofungua majadiliano mapya na mchina uwezekano za kina MADE IN CHINA kuwasaidia wachina utakuwepo! Tutajikuta hatujadiliani na wachina peke yao! Nyuma yao kina MADE IN CHINA watakuwepo! Tutafungua kitu kwa kiingereza inaitwa "Pandora's Box"! Litatoka jini kwenye box! Serikali ikatae katakata kuanza majadiliano mapya. Hao wachina waende watakapo! Acha watucheke kwa kukataa wasituibie!

Uzauza Namba 4:
Mradi huu awali ulikuwa ufadhiliwe na hao wachina na Serikali ya Oman. Lakini kina MADE IN CHINA wetu hawatuambii ni kwa nini na lini Serikali ya Oman ilijitoa? Je Oman waliona huu utapeli? Waliondolewa? Watanzania wanapaswa kujua Oman ilijiondoa au iliondolewa? Kisa? Au humo ndani bado Oman Fund wamo?

Uzauza Namba 5:
Toka tupate uhuru sikuwahi kuona Spika sampuli hii! Spika ambaye ameonyesha waziwazi kuhalalisha marupurupu ya wanaompigia kura. Spika huyu ukimsikiliza wakati bunge linavunjwa au uchaguzi wa spika unafanyika utasikia akiwakumbusha wabunge namna anavyoboreshaga maslahi yao! Ni spika ambaye ANATAFUTA uspika kwa "kuwahonga" wapiga kura kwa ahadi za kuwaongezea maslahi. Huyu ni spika ambaye hachelei kutafuta fursa. Mfano ni juzi akitetea upya hoja ya Bandari. Alimaliza kwa kudai eti Serikali ijenge miundombinu halafu usafirishaji waachiwe hâta wabunge wawekeze! Akatolea mfano wa barabara. Serikali inajenga watu binafsi ndio wanafanya biashara. Hivi kwa nini asidai na serikali ijenge viwanja vya ndege, magereza, mashule, mabwawa, mahospitali n.k. halafu iwaache wabunge au raia wafanyie biashara? Kwa nini achague SGR? Tuna spika mwekezaji? Hivi bunge letu likawa ni la wawekezaji watupu tutasalimika? Hivi kwa tamaa anayoonyesha spika huyu mwaka 2025 au hâta 2030 hawezi kutia nia? Na kwa kuwa anaboresha maslahi ya wabunge wengi wakiwa wajumbe wa vikao hawezi kupita? Bandari haitajengwa? Nadhani ni wakati sasa wa kumtizama spika huyu kwa jicho kali!

Sasa baada ya haya mauzauza tujiulize hivi ni kweli tunahitaji bandari mpya? Kina MADE IN CHINA hawatuelezi kama tunahitaji bandari! Walau Magufuli alisema hatuihitaji kwa kuwa itaua bandari aliyoanzisha baba wa taifa. Hivi hili kina Lusinde hawakulisikia?

Ukweli ni kwamba hatuihitaji bandari mpya! Tizama wenye bandari eneo letu: Kenya, Msumbiji, South Africa na Namibia. Wana bandari ngapi? Walau Tanzania inazo Dar, Tanga na Mtwara. Zinatosha mnoo! Bahari ya Hindi sio njia kuu ya meli za mizigo au abiria. Kina Ndugai wanakosea kufananisha Singapore na Tanzania. Singapore iko eneo lenye njia kuu za Meli. Na hâta hivyo ina bandari moja yenye terminals kama 5 hivi! Ndugai ama haijui Singapore au anasherehesha hoja yake ya MADE IN CHINA!

Hakuna comparative advantage na majirani zetu wa Indian Ocean kwa kujenga bandari mpya. Tanzania inatakiwa iboreshe tu Bandari zake haswa kwa kujenga miundombinu kama alichofanya Magufuli. Ijenge SGR, barabara, bandari za Nchi kavu, iikarabati TAZARA, iongeze terminals n'a container handling equipment, n.k.

Bandari mpya tuwaachie kina MADE IN CHINA wabwabwaje wao na wachina wao. Kina Lusinde wajue watanzania sio wapumbavu. Wamemwelewa Spika na wamewaelewa mnaomtetea! Wamewaelewa wasaliti hâta wanaojifanya kumsifu marehemu!
 
Hilo nalo neno
 
Tuna sababu moja kubwa ya kuukata Mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo nayo ni historia mbaya ya China kona mbalimbali za dunia walipotekeleza miradi ya aina hii au walipozikopesha nchi mikopo mikubwa ya miondombinu. Wamechukua bandari Sri Lanka, Pakistan, Australia na Djibouti kupitia mikataba ambayo haieleweki ni yenye utata sana.

Kama huko wameweza kufanya hivyo sisi hatutaweza kuwadhibiti na kuibakiza bandari ya Bagamoyo kuwa bado mali yetu endapo tukiwakubalia wajenge bandari hapo.

Tusijidanganye, sote tunafahamu jinsi gani mikataba midogo tu ya madini imekuwa changamoto kubwa kwa taifa hili, huu ukizingatia na usiri wa mikataba utakuwa funga kazi, tutauzwa mchana kweupe kama enzi za Mangungo wa Msovero.

Tukubali tu kwamba wao ni wajanja na kutekeleza kwa miradi ya aina hii duniani kumewapa ujanja zaidi. Tusikubali bandari zetu kujengwa na kuendelezwa na wageni kwa sababu yoyote ile. Kama tunafikiri ni muhimu sana na tunatakiwa kuwa na Bandari Bagamoyo tukope pesa tujenge wenyewe, vinginevyo tutaiuza nchi yetu nzuri.
 
Attachments

  • VID-20211118-WA0107.mp4
    11.2 MB
  • VID-20211118-WA0045.mp4
    5.9 MB
So sad,

vijizi vifupi vinaenda kupewa na kumilikishwa ufuke wetu wa bagamoyo kwa ajili ya bandari

Baada ya hapo tujiandae kisaikolojoa kishuhudia anguko la bandari yetu pendwa ya Dar es salaam
 
Back
Top Bottom