Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,893
- 3,200
Baada ya kudodosa dodosa mikataba ya makampuni ambayo yamejikita katika uwekezaji wa Bandari, nimeona na nimejiridhisha kabisa kwamba, masharti ya Wachina kwa Bandari ya Bagamoyo, yalikuwa nafuu kuliko hawa jamaa wa DP World.
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zilizonifanya nifikie maamuzi haya:
1. Mkataba wa Wachina wa Bagamoyo ulikuwa na ukomo wa miaka 99, huu wa DP World hauna ukomo (ni wa milele na milele)
2. Wachina wa Bagamoyo hawakutaka kutupoka bandari zetu Tanzania Bara, hawa jamaa wa DP World wana "njaa kali" wanataka bandari zote za Tanzania bara (Tanganyika) isipokuwa Zanzibar. Tena DP World wanataka bandari hadi za kwenye mito na mabwawa, achilia mbali bahari na maziwa makuu tuliyo nayo.
3. Wachina wa Bagamoyo walitaka kuja kujenga na kuendeleza bandari ya Bagamoyo, hawa Waarabu wanakuja tu na tu-mitambo twao ambatwo hata hatuna uhakika kama wanatwo hutwo tu mitambo au la! Bandari ya Dar Es Salaam ni Bandari kongwe ambayo ipo tayari na serikali imekuwa ikitumia mabilioni ya fedha kuiboresha. Leo hii eti tu kwa sababu waarabu wana mitambo tuwapatie tena kwa masharti ya kijinga kijinga.
Zingine, wana jamvi mtaendelea kuziweka.
Asalaam Aleykum..