Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,597
- 46,224
Tuna sababu moja kubwa ya kuukata Mradi wa Wachina wa Bandari ya Bagamoyo nayo ni historia mbaya ya China kona mbalimbali za dunia walipotekeleza miradi ya aina hii au walipozikopesha nchi mikopo mikubwa ya miondombinu. Wamechukua bandari Sri Lanka, Pakistan, Australia na Djibouti kupitia mikataba ambayo haieleweki ni yenye utata sana.
Kama huko wameweza kufanya hivyo sisi hatutaweza kuwadhibiti na kuibakiza bandari ya Bagamoyo kuwa bado mali yetu endapo tukiwakubalia wajenge bandari hapo.
Tusijidanganye, sote tunafahamu jinsi gani mikataba midogo tu ya madini imekuwa changamoto kubwa kwa taifa hili, huu ukizingatia na usiri wa mikataba utakuwa funga kazi, tutauzwa mchana kweupe kama enzi za Mangungo wa Msovero.
Tukubali tu kwamba wao ni wajanja na kutekeleza kwa miradi ya aina hii duniani kumewapa ujanja zaidi. Tusikubali bandari zetu kujengwa na kuendelezwa na wageni kwa sababu yoyote ile. Kama tunafikiri ni muhimu sana na tunatakiwa kuwa na Bandari Bagamoyo tukope pesa tujenge wenyewe, vinginevyo tutaiuza nchi yetu nzuri.