Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
Haina maana kwenda polisi wakati tuna vyombo vinavyotakiwa kufuatilia swala hili, hawa watu wanahatarisha usalama wa taifa, je hao watu wa kijitonyama a.k.a USALAMA WA TAIFA wanafanya nini? au kazi yao ni kuchakachua tu?

Hao watu wanaojiita wa Intelligence kwa bahati mbaya most of them are not intelligent. Kama wangekuwa na intelligence kidogo tu wangetambua kwamba nchi inapelekwa mrama na watu wachache sana kwa maslahi binafsi. Wangekuwa intelligent wangemuonya JK kuacha kuzungumzia suala la UDINI wa kusadikika wakati anaelewa fika kwamba watanzania hawana upuuzi huo wa UDINI. Nashangaa kuona kiongozi mkuu wa nchi anachochea UDINI, na sitashangaa kusikia kuwa anaunga mkono upuuzi wa hiyo radio na hata hawa waliojitokeza siku za karibuni na kujifanya kuwaonya maaskofu.
 

Asante mwanangu umelenga tusaidiane kupata ufumbuzi sina uhakika hata hili la mkutano wa katiba!
 


Hizi ni fikra za kijinga sana! Kuna ushahidi gani kwamba Wakristo walipendelewa katika elimu? Sio kwamba Waislamu waliamua kuwapeleka watoto wao Madrassa badala ya kuwapeleka shuleni kupata elimu sawa sawa? Nitakupa mfano wa tukio lililonikuta mimi mwenyewe (Mkristo). Miaka ya nyuma nilizaa na binti mmoja wa Kiislamu, na kisha nikaenda nje ya nchi kwa masomo ya juu. Niliporudi nilimtafuta yule mzazi mwenzangu kwa lengo la kumuona mwanangu, lakini nilipofika nikaambiwa mtoto hayupo ameenda Madrassa tangu asubuhi (ilikuwa saa saba mchana). Hatimaye aliporejea, niliongea naye kwa kirefu na kugundua kwamba hakuwa anajua chochote zaidi ya elimu ya dini na kuandika Kiarabu. Haraka sana nilimchukua mtoto na kumpeleka shule, na hivi sasa yupo chuo kikuu na anafanya vizuri sana. Nisingemchukua wakati ule na kumwacha kwenye mazingira yale ya Madrassa nina uhakika sasa hivi angekuwa miongoni mwa watu wanaolalamika kuwa hawakupewa fursa ya kusoma. Lakini ni nani anawanyima hiyo fursa? Inabidi kutafakari na kuchukua hatua.
 
Babu yangu (alikuwa mpagani) aliwahi kuniahadithia, kuwa zamani rafiki zake waliokuwa waislam walikuwa wanalalamika sana (hata kabla ya uhuru wa Tanganyika). Ikampa kujiuliza kwanini.

Mimi mjukuu nasikia bado wanaendelea kulalamika na kunung'unika leo hii. Kero za umasikini, ujinga, maradhi na ufisadi ni kero za kila raia mwema wa Tz. Hawawezi (mashehe) kuhalalisha hoja zao maana badala ya kuongoza matatizo wanapaswa kuwa sehemu ya jawabu.

Pia wajifunze kuwa wa wakweli. Mara nyingi wana-maanipulate population yao na kuwa-drive mad in the false hope vehicle
 
Mkuu, hiyo unasema wewe kwa kuwa unaelewa maana ya dini ya kweli. Bahati mbaya kwa waisilamu wanavyofundishana kule kwenye redio imaan FM, adui ya Muislamu siyo Ibilisi ni Mkiristo !
Ibilisi wa mtu ni mtu!!!
 
Maskini!!! Msiba mkubwa kabisa umeikabili nafsi yako na ubongo wako umedumaa!! (samahani lakini! nahisi unaishi dunia tofauti na hii na u mgeni kabisa!!) Sijui unaijua indonesia na malaysia ziko dunia gani au umeropokwa tu! je nako kuna mafuta kule? Hilo la Nigeria nadhani pia bado u ndotoni na si Nigeria pekee bali Afrika magharibi yote fuatilia upate majawabu halisi ili ububusa ukutoke. Wacha kutumia mdomo kufikiri tumia ubongo rafiki.
 
Kagusa himaya nini? 🙂
 
Yes! Mimi pia nilisikia mjadala huo. Kweli nimeamini kuna viongozi wabaya. Laakini hapa hawa mashehe wameshindwa tena wameshalegea kabisa.

Mashehe dawa ya udini sio kuuendeleza hizi ni hulka mbaya. Mimi Ni Mkristo lakini naheshimu pande zote mbili. Mimi nina marafiki waislamu nawafamu, ni watu wazuri wenye upendo kwa hiyo ule ulikuwa msimamoiwa wale watu wachache wala sio wote. Tanzania haiwezi kugawanyika na kupewa sehemu yenu kama mchangiaji mmoja alivyodai.Hata uwe taka dini ili halitawezekana . Kama utaki kuishi bora ujiue wewe uliyechangia siku ile heti tukiendelea kuonewa bora nchi igawanywe. Haigawanyi NG'OOOO!!!!!. Tena nina mpango wakuwa Rais Wako.

Haya Ebu Mniambia Ubaya wa Nyerere ni nini? Waongo Wakubwa Nyie!!! Heti Nyerere aliwapa Elimu wakristo na kuwanyima waislamu. Mzee wa watu alijitahidi kuwanyang'anya wamisionari shule ili watanzania wasome. Mjue kuchukua shule za kidini na kuzifanya za serikali ni swala lisilo dogo. Leo tunaona nyingine zimerudishwa baada ya yeye kufariki (kama Mazengo). Na nyingine kama Kwiro niliyesoma mimi ndiyo zimechukuliwa moja kwa moja. Na haya maneno kwa nini mmeyaanza baada ya waasisi wa taifa hili lote kama wakina kawawa kufariki maana wasingiweza kuwasikia.

Tumeishi vizuri kwa kushirikiana na sasa tunapozeeka tusubiri kifo sio kuambukiza chuki kwa watoto. Nilikuwa naongea na mtu mmoja akaniambia heti JK alifanya ujanja wa kubadilisha jina ili liwe la kikristo ili aweze kusoma seminari. Nikamuuliza akaitwa nani? Jibu akasema sijui. una Uwakika?-Hapana. Ni vyema ukaacha kuzungumza vitu usivyokuwa na uwakika navyo. Vyuo vikuu dawa yake ni kuvijenga tu havitoki hewani nani kapewa chuo kikuu.
 
Haina maana kwenda polisi wakati tuna vyombo vinavyotakiwa kufuatilia swala hili, hawa watu wanahatarisha usalama wa taifa, je hao watu wa kijitonyama a.k.a USALAMA WA TAIFA wanafanya nini? au kazi yao ni kuchakachua tu?

Umeuliza vibaya ndg yangu! Uliza mkuu wa Idara ni nani kwanza!
 
Kwa jinsi ufa huu unavyozidi kupanuliwa,sidhani kama tutapona.Kila siku wenzetu kunung'unika tuuu....bah!acheni hizo banaa tupiganie maendeleo ya nchi yetu.Muhimu ni nyinyi wenyewe kuwekeza kwenye elimu dunia na sio madrasa...vinginevyo mtaendelea kulialia daima!
 
Radio imaan 104.4 FM kwa dar kipindi saafi kabisa
 
kinazungumzia nini?......isije ikawa wanakashfu iman za watu wengine halafu na ww unasifu kipindi kizuri.
 
anzisheni redio na vijarida wakati wenzenu wanafungua na kuanzisha vituo vya afya, hospitali za rufaa, shule za sekondari na vyuo vikuu .....
 
Punguzeni udini wadau,asilimia 90% ya watanzania koo zao zina mchanganyiko wa waislamu na wakristo so mnatupeleka wapi kwa maada za kidini?
 
huo udini utawafikisha pabaya na CCM yenu yenye kuuleta nchini! maacha kujadili mambo muhimu mnakalia udini?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…