Tumezoea kusikia machafuko ya wakulima na wafugaji. Haya ni machafuko rahisi kuyadhibiti wawili hao hupatanishwa. Tumezoea pia kusikia kwa watu wengine machafuko ya makundi ya kidini kama ilivyo huko Nigeria na sehemu zingine duniani.
Machafuko haya ya pili yaani machafuko ya kidini yaliachwa yachipue na kutoa matawi kama yanavyoonekana kuelekea kuwa hivyo hapa Tz, ni machafuko ya damu na mnyama tena kwa muda mrefu na kwa watu wengi wa aina mbalimbali.
Si muda mrefu tulisikia watu wanaandamana wanaona Baraza la Mithani linawafelisha Watoto wa kiislam. Ktk hili watu walipaswa kufungua kesi mahakamani na kutoa ushahidi usiokuwa na shaka. Bahati mbaya sana jambo hili pia likashughulikiwa kwa vitisho vya kidini!
Si muda mrefu tumetoka kushuhudia maandamano yaliyofunga barabara tena bila hata kibali cha polisi hadi makao makuu ya jeshi la polisi. Yakapokelewa. Asante polisi mlitumia uungwana Kamhanda akatuliza mzuka, risasi wala mabomu havikurindima wala kufumua matumbo yao.
Sasa tunasikia mtoto ati kakojolea Qorani. Hatujui mazingira yaliyokuwepo mlaka tendo hilo likafanyika. Inaweza kweli kwa utovu wa nidhamu mtoto huyo kafanya hivyo au pia by blassfemy wahusika wanatafuta mahali pa kupenyezea vitendo vya vurugu. Wamefanikwa, wamefanya vurugu kubwa. Vurugu ya jumla kwa kutafuta shari itoke ktk kuchoma makanisa na kituo cha polisi. Wanamtafuta huyo mtoto ati WAMUUE! Sijui kama huyo mtoto asingeweza kufunguliwa mashtaka. Au ushahidi haupo? Au kuua ndiyo maelekezo ya imani husika? Sijui.
Hapo ndipo ninaposema Rais wangu JK hili siyo la Hotuba ya Mwisho wa Mwezi linatakiwa kauli yako LEO ili Tz ipate kupona. Usipofanya hivyo, leo ama kesho ya Watz iko mashakani kwa sababu ya jazba za kidini.
Rais wangu Sema NENO kwa Taifa kama vile nami nilivyokusemesha NENO hili