Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by emalau, Jan 17, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. e

  emalau JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wadau, jana katika kubadilisha station ya radio yangu nilikutana na mjadala uliokuwa ukiendeshwa redio imani, hii ni redio ya kiislamu iliyoko mjini Morogoro. Ingawa si kawaida yangu kuisikiliza lakini nilishawishika kuwasikiliza kutokana na uzito wa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

  Mjadala ulihusu tamko walilotoa kuhusu maaskofu, walivilaumu vyombo vya habari – magazeti particularly mwananchi na magazeti mengine kama nipashe, Tz Daima etc kwamba yamepotosha tamko lao pamoja na kuwa waliwapa tamko hilo kimaandishi. Nilijiuliza inakuwaje magazeti yote yanakosea kitu kilekile.

  Kilichonisikitisha katika mjadala huo ni uchochezi na upotoshaji wanaoueneza hawa masheikh kwa sababu wanazojua wao. Kwa mfano walisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kikiristu toka enzi za Nyerere, moja ya madai yao ni kwamba waislaumu walikuwa wakifelishwa makusudi shuleni ili wasisome, bila shaka haya ni madai makubwa sana.

  Mambo mengine ni kwamba ili kudhibitisha kwamba nchi inaendeshwa kikristo ni kwa nini wakristo wana university na hospitali nyingi kuliko serikali, madai mengine ni kwamba kwa nini hospitali za kikristo zilizotaifishwa na serikali zilirudishwa, bila shaka katika hili ni kwamba serikali ilishindwa kuziendesha, lakini kwa sababu wanazojua wao waliishia kulaumu mfumo wa utawala wa kikristo. Katika hili wao walikiri kwamba hakurudishiwa kitu kwa kuwa hawakunyanganywa kitu!

  Baada ya kumaliza majadiliano waliruhusu wasikilizaji kutuma sms na kupiga simu studio, wengi wa wachangiaji waliwashukuru masheikh kwa hatua yao lakini pia kuna waliosema watajichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu waandishi, na wengine walitaka itangazwe jihad dhidi yao.
  Nilivyoona mimi hakuna shabaha nyingine zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa dini jambo ambalo si kawaida yetu watz.

  Ingawa najua kwamba redio hii haina wasikilizaji wengi lakini mijadala ya uchochezi namna ile haitakiwi kupita bila kukemewa. Katika mauaji ya Rwanda redio zilitumika sana kuchochea chuki baina ya watu, hatutakiwi kufika huko, nadhani ni wakati muafaka kwa "intelijensia" ya polisi kufanya kazi sasa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokana na uchochezi wa redio imani

  Wana JF naomba kuwakilisha
   
 2. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao ni masheikh uchwara wackupe taabu,cc waislaum tulioelimika hatuwezi kudanganywa na hao wapuuzi
   
 3. l

  libaba PM Senior Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Waislamu ndugu zangu, mbona tunamatatizo mengi kijamii yanayohitaji utatuzi wetu wala sio kulialia kwa wakristo, mbona tunatafuta huruma katika maswala ambayo tunaweza kutatua wenyewe ? ni ujinga kwakweli
   
 4. Antonov 225

  Antonov 225 JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mungu atusaidie maana yeye pekee ndiye mtetezi wa haki na kweli. Tuwe makini na hulka na hisia za watu ambao wanapenda kukusanya wafuasi kwa nia ya kuleta machafuko na kutimiza malengo yao.
   
 5. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Unataka Kikwete a-justify namna gani kwamba kuna udini Tanzania? bila kuwatuma hao mashehe mbumbumbu kwenye redio na kufanya mihadhara isiyokuwa na tija?

  Wametumwa hao kuna wakati kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka jana pia nishawahi kusikiliza hiyo redio ikimcritisizi Dr.Slaa kwamba ni mtu anayependa udini sana so kwa hili pia sishangai kabisaaaa..... wako kazini wametumwa nashindwa kuelewa hao wanaojiita kupokea taarifa za kiinterejensia kwa nini wasizitumia kuzuia vitu kama hivi ....full nonsense issues wanaziweka ili kuwahadaa wale wenzangu na mimi wasioweza kuchakatua jambo/mambo na waamini kwamba udini ni kweli upo ..
   
 6. K

  Kivia JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa taarifa RADIO IMAAN inasikika nchi nzima kwa sasa, hivyo inawasikilizaji wengi. Pia wewe u-mtu wa ajabu, maaskofu wakisema, wakitukanä wakichochea ni sawa LAKINI MASHEHE WAKISEMA NI KOSA. Nami nasema maaskofu mnatupeleka kubaya. Msichanganye siasa na dini.
   
 7. m

  mamakunda JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 371
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa mwislam ambaye amesoma na kuelewa sidhaani kama anaweza kukubaliana na huo mjadala, manake ni uongo mtupu na uchochezi.

  Hata ukifuatilia wanachosema si kweli maana wao ndo wachawi wa maendeleo yao, fanya tu utafiti mdogo wa shule za sekondari za kiislam kuhusu maendeleo yao utahisi kichefuchefu, manake viongozi ambao hawana elimu dunia wanang'anga'nia kuzisimamia hatimaye kuzipeleka ambako siko.
   
 8. M

  Mkwele JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hatugombani ng'ooooo kwani sisi wengine familia zetu zimechanganyika waislamu na wakristo tena wakatoliki na tunapendana kishenzi.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Malalamiko yao hayana ishu...Kama wakkristu wana hospitali na vyuo, je dawa ni kulalamika au kujenga ili nawe uonekane mjanja?..Na je kwani haospitali na vyuo hivyo vinabagua dini?
   
 10. U

  UMPUUTI Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mdau, binafsi nakupongeza kwa kuliona hilo na kuona kwamba ipo haja ya kutoa angalizo kwa kile ulichokisikia kupitia redio hiyo inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Kiislam.

  Kwangu mimi, cha msingi ninachokiona kwenye mada yako ni kuhusu uchochezi wa kidini unaofanywa na Redio hiyo na maafa yanayoweza kulikumba taifa letu kama hatua za haraka hazitachuliwa kudhibiti hali hiyo. Mimi binafsi sina tatizo na hoja yako. Kimsingi ni angalizo linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda amani. Hata hviyo, ninachotaka kuongeza hapa ni kwamba, hali ya mustakabali wa kidini katika Tanzania kwa sasa ni tete. Na hili halina ubishi hata kidogo, labda iwe kwa mtu mwenye hulka ya kubishia kila jambo ndiye pekee anayeweza kupingana na ukweli huu.

  Hali tuliyo nayo sasa hapa nchini haishirii dalili njema hata kidogo mbele ya safari. Zinahitajika hatua za maksudi kabisa katika kukabiliana na hali hii kabla bomu halijalipuka. Ni vema watanzania tukatambua kwamba machafuko yenye sura kama hizi za kidini mahali popote yalipopata kutokea duniani, hayakuja kama mvua au kwa bahati mbaya, la hasha!. Machafuko yalianza kama masihala kwa njia kama hizi hizi za chochoko, malumbano,na uchochezi wa chini kwa chni kama tunavyoanzashudia hapa kwetu Tanzania.

  Binafsi sipendi kuhukumu kwamba ni dini gani hasa ndio inayoonesha dalili za kutaka kutupeleka kwenye machafuko ya kidini ambayo ni machafuko mabaya kupita machafuko mengine yoyote katika dunia hii. Nasita kufanya hivyo kwa sababu imani yangu inanizuia kukuhukumu na kusisitiza zaidi kuchunguza boriti ndani ya jicho langu kabla ya kutoa kibanzi katika mboni ya jicho la mwenzangu. Hata hivyo, natambua dhahiri shahri kwamba mustakabli wa hali ya kidini hapa nchini imekuwa tete tangu mchakato wa uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Hivyo basi, ni wajibu wa kila mtanzania mwenye dini na asiye na dini kuliona hilo na kuchukua hatua kwa nafasi yake ili kuzuia dalili mbaya zinajitokeza katika taifa letu.

  Na mwisho ninapendekeza kwamba, kama ilivyo hitaji la watanzania kuwa na Katiba Mpya, basi halikadhilika iwe hivyo hivyo katika jambo la kidini. Sio vibaya tukawa na mjadala wa kitaifa kuhusu hatma ya mivutano ya kidini iliyoanza kujitokeza hapa nchini. Na kwa njia hiyo pekee ndipo tutaweza kutoa fursa kwa kila upande utoe dukuduku lake na kisha kufikia muafaka wa pamoja. Lakini, tukiendelea kupuuza, kukejeliana,kutukanana na kushutumiana bila kuchukua hatua zozote haitatusaidia. Tukumbuke kwamba panapofuka moshi lazima pana moto!!

  Mungu ibariki Tanzania na watu wake!!!
   
 11. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Sasa mbona nawe unaongeza tatizo hapa badala ya kulipunguza?

   
 12. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nami nilisikiliza hicho kipindi live yakiwemo maneno ya MAFIA MOB yakitajwa etc...
   
 13. REBEL

  REBEL Senior Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  yaani mimi nikitaka kuongeza kisukari uwa nasikiliza hiyo redio na nyingine iliyoko dar!full upuuzi,mashekhe wawe na degree kama mapadre labda IQ YAO ITAONGEZEKA!MTU UTAFELISHAJE WAKATI MITIHANI INAFANYA KWA NO?
   
 14. FuturePresident

  FuturePresident JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 321
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakubwa hili ni tatizo, lakini sio kwamba limeanza leo au jana au juzi la hasha......haya ni ya muda mrefu sanaaaa....kwa miaka hata kabla hawa mabwana hawajawa na chombo kama Radio!!!

  Mijadala mingi ya kuukashifu ukristo inaaachwa inaendelea tuuu kwa miaka mingi.. Lakini historia inatuonyesha kuwa uislaam ulienezwa kwa upanga tofauti na ukristo ulivyo huu ni ukweli usiopingika.....sasa cjui wapi tunaenda, kibaya zaidi hawa wanayofanya mambo haya upeo wa ni mdogo sanaaa kwa athari zitakazo tokana ni hili wanalolifanya huko serekali inawangalia tuuu sasa cjui. Mnakumbuka enzi za Mzee ruksa ile vita ya kuvunja mabucha ya nguruwe?

  Sasa fanya utafiti juu ya wale walioshiriki kwenye ile vita leo hii wengi wao waliofanya ule ujinga tena viongozi ni Wakristo!!!!
   
 15. D

  DOCTORMO Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii inanishangaza, chamuhimu nisisi kuwa mabalozi wa wenzetu kujaribu kuelimishana , ili kusiwe na mshiriki au supporter wa mambo haya. mimi naijua hii redoi tokea ninasoma SUA kwakweli inaudhi lakini nikujifanya mjinga tu kuwa husikii kitu.
   
 16. N

  Nsengimana Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bora wewe umeliona hili na kulileta hapa jamvin.Ipo haja kwa hiyo intelijensia kufuatilia mambo ya msingi kama haya na sio kuvunja maandamano ya aman.Radio Iman+gazet la Al nur ni vyombo vya habari vya kichochezi na visivyokuwa na maadili.Binafsi nimekuwa nikifuatilia habari zao hasa wakati wa kampeni,kwa kweli inasikitisha,sijui kwa nini yanazidi kukumbatiwa!
   
 17. e

  emalau JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 1,179
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Haina maana kwenda polisi wakati tuna vyombo vinavyotakiwa kufuatilia swala hili, hawa watu wanahatarisha usalama wa taifa, je hao watu wa kijitonyama a.k.a USALAMA WA TAIFA wanafanya nini? au kazi yao ni kuchakachua tu?
   
 18. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  wanaJF ukiwa na {jealous} wivu wa kijinga utabaki kuwa maskini au mjinga daima.

  Ukiona mwenzio kafanikiwa mwombe ushauri au mkomoe kwa kuwa na maendeleo zaidi yake, nawapongeza wachaga wanatabia ya kumsema mwenzio kama hajafanya maendeleo yoyote kule kwao mmoja akijisifu na biashara na nyumba za kupanga mwingine atajisifu na kikubwa zaidi yake.

  Ndugu zetu waamke wajiulize kwanini wako nyuma kimaendeleo na wapange mikakati ya kujikwamua na sii kulumbana ni kwanini wakristo wana mashule mengi na mahospitali wamesahau zimejengwa na wamisionari na ndio hao hao wamewatibu babu zao??????
   
 19. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Usipotoshe ukweli kwa dai lako la uongo kuwa Uislamu ulienezwa kwa upanga! haya nakuuliza, Uislamu ulipoingia huku kwetu miaka 1000 kabla ya ukristo kuja ni upanga gani huo uliotumika mpaka babu zetu wakasilimu?

  Maeneo ya Machame, Usangi, Ugweno, Moshi mjini, Bukoba, Musoma nk, kuna Waislamu pia sasa upanga uliotumika kuwasilimisha umeuhifadhi ktk MUSEUM yako?
  2) Indonesia ni nchi yenye idadi kubwa sana ya Waislamu duniani kote, sasa uislamu ulipoingia huko ni upanga upi huo uliotumika?
  India, Pakistani, Afganistani, Kosovo, Bosnia, mackedonia, Uzbekistan, Urusi, Chechenia, USA na nchi nyingi duniani wanakoishi waislamu ni upanga gani huo uliotumika?

  Labda Ukristo ndio ulioenezwa kwa mtutu wa bunduki ndio maana Wazee wetu akina KINJEKITILE walikataa kudanganywa na Wazungu waliokuja kama Wamisionari kumbe lengo lau ni kuwabatiza na kuwatala!

  Usituletee propaganda chafu zilizopitwa na wakati tafuta lingine la kuongea lakini sio *****!
   
 20. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama kuna watanzania wanaosikiliza hiyo redio basi hawazidi mia tano. Wengi wao wapo tandale, manzese, tandika, temeke, gongolamboto na mbagala.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...