Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
hayo yameanza muda mrefu sana, hapa dar kuna radio kheri, kule moro kuna radio imaan, pia kuna radio kuran pale magomeni, na magazeti kibao wanayoyatumia kuwahamasisha waislam..cha ajabu ni kwamba, watajikuta wamejigawa wao wenyewe away from christians , watasoma shule za kwao, wataenda hospitali za kwao kwa kina shehe yahya kule mwembe chai, na wataishia kubuya bwimbwi tu badala ya kula ugali halisi. the more they incite hatred, the more wanavyojiaibisha na kujianika na kuiabisha dini yao, na mwisho wa yote, tutavuna kondoo wengi waje kwa Bwana kwasababu huko kwao wataona ukweli waziwazi ipi njia sahihi, njia ya ugaidi au njia ya amani na uponyaji katika Yesu Kristo.
 
Ndugu Zangu,
JANA usiku katika pekuapekua zangu za idhaa za redioni, nikakutana, kwa mara ya kwanza, na Redio Imaan FM. Inatangaza kutoka Morogoro. Nilichosikiliza kilikuwa kipindi maalum cha marudio kutoka Jumapili iliyopita. Niseme neon moja tu na kwa msisitizo: NILISHTUKA.

Hakika, kilichokuwa kikirushwa hewani ni matangazo ya uchochezi. Kuchochea uhasama baina ya Watanzania Waislam na Watanzania wenzao Wakristo. Nilijiuliza, kama taifa tunakwenda wapi? Na maswali yakawa mengi. Je, Tume ya Utangazaji inafahamu kinachoendelea au imelala usingizi? Je, watu wetu wa Intelijensia hawana taarifa za Kiintelijensia juu ya kinachooendelea?

Naam. uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.

Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.

Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Mwezi Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia Watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.

Bi Mukanyange alisema: ” Naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994,” alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.

Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, na hasa wanasiasa, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.

Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.

Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.

Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya Watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.
Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda.

Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa.

Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu wasio na nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.

Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.

Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.

Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya Tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa Wahindi, Walutheli, Waprotestanti, Wasabato, Wakatoliki, Washia, Wasunni, Waismailia, wenye kuamini jadi, Wazaramo, Wagogo au Wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.

Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si Wakristo peke yao, si Waislamu peke yao, si Wapagani peke yao, si Wamachinga peke yao na si Wazaramo peke yao.

Wahenga walisema ”kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Mungu Ibariki Tanzania.

Maggid
 
Bi Mukanyange alisema: " Naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994," alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.

Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, na hasa wanasiasa, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.

Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.

Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.

Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya Watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.
Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda.

Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa.

Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu wasio na nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.

Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.

Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.

Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya Tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa Wahindi, Walutheli, Waprotestanti, Wasabato, Wakatoliki, Washia, Wasunni, Waismailia, wenye kuamini jadi, Wazaramo, Wagogo au Wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.

Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si Wakristo peke yao, si Waislamu peke yao, si Wapagani peke yao, si Wamachinga peke yao na si Wazaramo peke yao.

Wahenga walisema "kamba hukatikia pabovu". Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Mungu Ibariki Tanzania.

Maggid

haya yote sababu ya JK kuleta UDINI UDINI UDINI

Mimi la kufelishwa makusudi nalikataa. Nilisoma Mtwara Technical na Dadi Yusuf Namtumba, aliongoza mchepuo wa "Mechanical" tangu siku ya kwanza hadi tunamaliza. Alipewa haki yake ya kuendelea na masomo Arusha Technical College. Katika familia yangu, babu mkubwa (kaka wa babu yangu) alifanya kazi ya jeshi huko Burma (leo Mynmar). Aliporudi kijijini, yeye na familia yake wakuwa waislam, ingawa wengine walikuwa bado wahehe (siyo waislam, sio wakristo; ukristo ukikuwepo ila ulikuwa bado mpya). Wakatoliki wakaanzisha shule (elimu dunia) na kuwasajili watoto wa wafuasi wa imani yao. Baba yangu akamshawishi babu mkubwa alimbadilisha jina baba mdogo (mtoto wa baba mkubwa) kutoka Ahmed kuwa Wailes ili asome shule ya wakatoliki (shule pekee kijijini wakati wetu ambayo ilisomesha watu wa imani yao). Kazi ilikuwa kubwa, kwani baba aliona hiyo ilkuwa ndiyo njia pekee ya kumsadia mdogo wake apate elimu, wakati babu aliona ni namna ya kumbadilisha mwanae imani. Baba akamwambia mdogo wake kuwa ukifika mbele huko utakuwa na uhuru wa kuabudu na elimu utakuwa nayo, Mungu akikupa uzima. Baada ya kuhitimu std 8, aliendelea na masomo Mkwawa High School (wakati huo). Alipokuwa anaingia A'Level alirudia jina lake la Ahmed. Matokeo ya mitihani yake (PCB) alitolewa hihalali, akapata scholarship kwenda kusoma udakitari; na hadi leo ni dakitari. Ingawa baba hakuwa Mkristo wala Mwislam, alijua faida ya elimu. Hata palipo na shida, vikwazo; tufikirie namna ya fanikiwa sio visingizio na kuchafuana. Tunaweza kuwaadhibu wale tunaohisi wanatusababishia matatizo, lakini tukashindwa kujiendeleza wenyewe wakati wale wamekwisha wamaliza.

Sijui unakataa nini unakubali nini! unasema alibadili jina ndo akasoma halafu unasema la kufelishwa unalikataa.sasa angefelishwa vipi wakati ana jina la kikristu? Kwa taarifa yako baadhi ya waislamu waliopenya ktk elimu walitumia ama majina ya kikristu au ya kimila.mfano Jakya Mrisho Kikwete,Ukiwaona Ditopile Mzuzuri,Makwaiya Wakuhenga,Kigoma Malima nk.Hata hivyo tatizo lilikuwa sana kutoka primari kwenda sekondari,mtu aliyekuwa anafanikiwa kuvuka hapo alikuwa anaendelea bila ubaguzi.Wabaguzi hata hivyo walikuwa wanauma na kupuliza walikuwa wanaachia namba ndogo sana ya Waislam ili wasije wakashtuka mapema
 
Maggid sijui dini yake lakini nahisi ndo walewale akina Rashid Kawawa waliotumika kukandamiza waislamu nchini.Wakti akina kawawa wanajenga nchi wezao akina Nyerere wanajenga ukristu,ndio maana unaona sasa Nyeyrer anatngazwa mwneye heri si ujiulize kulikoni kiongozi wa nchi kutangazwa mwenye heri na dini yake.Mbona hajatangazwa Kadinali Rugamwba mwafrika wa kwanza kuwa Kadinali anatangazwa Nyerere.What is the secret behind?Akina Maggid and his type wakishasifiwa kidogo kuwa wao ndo wamesoma na wako civilsed basi tembo wanalitia maji.
Ushauri wabure kwako Mggid,kuna waislam waliotumika bila kujijua baadae walijutia,unacheza ngoma usiojua bora ukakaa kimya waache wenyewe wacheze
 
Tutafika tu wanako taka tufike,maana matusi sasa yamedhidi kuanzia jumatatu hadi hivi leo ukipita maeneo ya manzese(barekhesa)kuna mdahalo mkubwa sana unaendelea pale,japo sijawai kuhudhuria na wala sitarajihii hata siku moja kuudhuria,lakina ukiwa napita na gari kikubwa kinacho jadiliwa ni bibilia(bible)na kuwatukana wakristo,sasa sijui tunaelekea wapi,yaani watu baada ya kufanya kazi wanaadhisha vitu vya ajabu na kuongea ujinga.angalizo:Tufanye kazi watanzania tuache kuhubiri dini kwa kutukana watu na kutoa maneno ya uchochezi.hii nchi yetu sote na hizi habari za udini hazita tupa maendeleo bali maumivu tu.mungu ibariki tanzania.
 
Ndugu yangu Kivia je unataka kutuambia hoja ya kwamba wao walikua wanafelishwa makusudi ni ya kweli? Historia waijua vizuri wewe? Hoja zao zoote hazina vigezo vyovyote vya kuthibitisha waliyoyasema. Msitafute wachawi wenu kwingine bali ndani mwenu
 
Tutafika tu wanako taka tufike,maana matusi sasa yamedhidi kuanzia jumatatu hadi hivi leo ukipita maeneo ya manzese(barekhesa)kuna mdahalo mkubwa sana unaendelea pale,japo sijawai kuhudhuria na wala sitarajihii hata siku moja kuudhuria,lakina ukiwa napita na gari kikubwa kinacho jadiliwa ni bibilia(bible)na kuwatukana wakristo,sasa sijui tunaelekea wapi,yaani watu baada ya kufanya kazi wanaadhisha vitu vya ajabu na kuongea ujinga.angalizo:Tufanye kazi watanzania tuache kuhubiri dini kwa kutukana watu na kutoa maneno ya uchochezi.hii nchi yetu sote na hizi habari za udini hazita tupa maendeleo bali maumivu tu.mungu ibariki tanzania.

Enzi za Nyerere wakristu walikuwa wanagawa biblia bure kwa kila mtu bila kujali dini yake.Waislam wakazisoma na kuzielewa wakagundua kuna mapungufu mengi kwenye imani ya ukristu ndo wkaanza kuwaelimisha lakini huwa hawtukani. hivi mtu akikwambia kuwa 1+1+1=1 unaweza ukakubali? Sasa waislamu baada ya kusoma hizo biblia na kukuta hiyo fomula haikuwaingia akilini ndio maana wanajribu kuifafanua vizuri.Hii mihadhara ilianza hata baba wa kanisa Nyerere akiwa bado hai,walipomwendea kumuomba aingilie kati yeye akawaambia kuwa nanyie someni Qurani muwachalenji
 
wanatengeneza magaidi wa kujilipua, watajilipua, watatuachia nchi sisi tutaendelea kuishi kwasababu hatuamini kupigana au kufanya vita...wakati mambo yanachangamka kwenye mihadhara yao, nawashauri wakristo na waislam wale wasiopenda fujo wajikite zaidi kupiga shule na kutafuta maisha....wao watakula mihadhara hiyohiyo.....

ukweli ni kwamba, hata ufanye nini, ukimweka mkristo na mwislam pamoja wafanye kitu, mwislam hawezi kwenda pamoja na mkristo...chukua mfano shule....mimi mtoto wangu nampeleka chekechea anaanza kupiga shule, mwislam anampeleka madrassa kusoma dini, wakianza wote lakwanza wangu atakuwa na background nzuri hivyo ataongoza darasani, atakuwa na moyo huo matokeo yake anaishia university.

uislam unafanya kazi nchi zenye mafuta sehemu ambao watu hawatumii sana elimu/akili, bali wanachota tu mafuta na kuishi....dunia nzima tembea utakuwa waislam wanaishia kuuza vijiduka vidogo tu na si investment za akili......Nigeria nayo ni tz? mbona Nigeria maeneo yale ya kusini kwa wakristo ndo kuna maendeleo ukienda kule kaskazini kwenye sharia, umasikini wa kutupwa...tz nayo hawa watu wa pwani wanatandika mkeka tu na kusubiri majini yakachume ulete...nafikiri kama kuna kitu cha kuwasaidia hawa wenzetu ni kuwapa elimu..itawakomboa sana.

wake wanaoa wengi, wanashindwa kusomesha watoto, matokeo yake wanalalamika wanaonewa, wakati sisi wakristo watoto wetu ni wa bajeti hivyo tunawasomesha wote...wake wengi wanawamaliza, madrassa zinamaliza watoto wenu....kalagabaho.
 
hayo yameanza muda mrefu sana, hapa dar kuna radio kheri, kule moro kuna radio imaan, pia kuna radio kuran pale magomeni, na magazeti kibao wanayoyatumia kuwahamasisha waislam..cha ajabu ni kwamba, watajikuta wamejigawa wao wenyewe away from christians , watasoma shule za kwao, wataenda hospitali za kwao kwa kina shehe yahya kule mwembe chai, na wataishia kubuya bwimbwi tu badala ya kula ugali halisi. the more they incite hatred, the more wanavyojiaibisha na kujianika na kuiabisha dini yao, na mwisho wa yote, tutavuna kondoo wengi waje kwa Bwana kwasababu huko kwao wataona ukweli waziwazi ipi njia sahihi, njia ya ugaidi au njia ya amani na uponyaji katika Yesu Kristo.
Umenikumbusha kitabu cha Padri John Sivalon 'SIASA ZA TZ NA KANISA KATOLIKI'. Anaeleza kuwa Nyerere aliahidi kulipa kanisa a better chance(Upendeleo maalum) pia alisema kuwa ilikuwa ni vigumu ktk utawala wa Nyerere kutofautisha ni lipi la kanisa na ni lipi la serikali. Sasa unaposema kuwa waislam watasoma shule zao na kutibiwa hospitali zao una maana taasis za serikali zitakuwa wapi? au hizo taasisi za serikali ndo hizo hizo za kanisa? ndo matunda ya fumo kristu hayo uliojengwa na Nyerere.
Hata hivy usijali waislamu wanaweza wakatumia taasisis zao na wakaishi bila kutegemea za kanisa.
 
Ndugu Zangu,

JANA usiku katika pekuapekua zangu za idhaa za redioni, nikakutana, kwa mara ya kwanza, na Redio Imaan FM. Inatangaza kutoka Morogoro. Nilichosikiliza kilikuwa kipindi maalum cha marudio kutoka Jumapili iliyopita. Niseme neon moja tu na kwa msisitizo: NILISHTUKA.

Hakika, kilichokuwa kikirushwa hewani ni matangazo ya uchochezi. Kuchochea uhasama baina ya Watanzania Waislam na Watanzania wenzao Wakristo. Nilijiuliza, kama taifa tunakwenda wapi? Na maswali yakawa mengi. Je, Tume ya Utangazaji inafahamu kinachoendelea au imelala usingizi? Je, watu wetu wa Intelijensia hawana taarifa za Kiintelijensia juu ya kinachooendelea?

Naam. uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.

Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.

Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Mwezi Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia Watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.

Bi Mukanyange alisema: ” Naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994,” alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.

Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, na hasa wanasiasa, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.

Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.
Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.

Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya Watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.
Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda.

Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa.

Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu wasio na nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.

Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.

Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.
Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya Tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa Wahindi, Walutheli, Waprotestanti, Wasabato, Wakatoliki, Washia, Wasunni, Waismailia, wenye kuamini jadi, Wazaramo, Wagogo au Wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.
Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si Wakristo peke yao, si Waislamu peke yao, si Wapagani peke yao, si Wamachinga peke yao na si Wazaramo peke yao.

Wahenga walisema ”kamba hukatikia pabovu”. Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.

Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Mungu Ibariki Tanzania.
 
Katika moja ya hotuba za Nyerere ambazo hadi sasa huwa wanziweka anasema: "Ukitaka kumsaidia mtu maskini wasomeshe watoto wake". Baada ya uhura aliahidi angondoa kabisa gepu lililokuwepo baina ya waislam na wakristu katika elimu na yeye ndie alikuwa na jukumu la kuwasomesha wtz bila kujali dini zao lakini kwa makusudi akaamua kuwasomesha wakrsitu akijua kuwa hiyo ndo njia pekee ya kuwaondoa kwenye umaskini na unyonge akwaacha waislamu.
Akajifanya anataifisha shule za seminari lakini kumbe ilikuwa ni kiini macho,malengo ya shule hizo na viongozi walibaki ni walewale,yeye alizitaifisha ili serikali iweze kuziendesha vizuri maana wakati wa mkoloni zilikuwa zinaendeshaw na ruzuku ya serikali sasa baada ya uhuru ndo akatumia janja lakini kwekli waislamu tuliumia sana
 
Mahakama ya kadhi hamtaki kutupa, inawakera tupeni basi tusijitenge

Kujiunga OIC hamtaki, unawakera jiungeni basi tusijitenge

Tukitaka kuijitenga ili tuendeshe mambo yetu ikiwemo mahakama ya kadhi etc hamtaki

Ok here is a deal, nyinyi chukue mikoa yote tupeni 10 tu ambayo hamuitaki ili nasi tuwe huru na dini yetu

mbona wachoyo hivi nyie mkoje?
 
WaTZ tusiyumbishwe na watu wachache. Kilio cha waTZ ni ufisadi unaofanya maisha yetu kuwa magumu sana; raslimali za nchi zinanufaisha wachache kwa maksudi mazima; wanaweka mazingira ya mikataba mibovu inayoigharimu nchi nk.
Umeme ulipopanda wote tumeathirika - mwislamu, mkristo, na wasio na dini;
Nauli ikipanda wote tunaumia mwislamu, mkristo, na wasio na dini;
Tukipinga kwa maandamano na polisi wakatuua kwa risasi - wote tunakufa; waislamu na wakristo
Karo ya shule ikipanda, wote tunaathirika - mwislamu, mkristo, na wasio na dini nk.
Mafisadi ni wote wakristo na waislamu - Andrew Chenge, Rostam Aziz, Basil Mramba, JK, EL, Manji nk.
Tusikubali kutoka kwenye mada za msingi.
 
wanatengeneza magaidi wa kujilipua, watajilipua, watatuachia nchi sisi tutaendelea kuishi kwasababu hatuamini kupigana au kufanya vita...wakati mambo yanachangamka kwenye mihadhara yao, nawashauri wakristo na waislam wale wasiopenda fujo wajikite zaidi kupiga shule na kutafuta maisha....wao watakula mihadhara hiyohiyo.....

ukweli ni kwamba, hata ufanye nini, ukimweka mkristo na mwislam pamoja wafanye kitu, mwislam hawezi kwenda pamoja na mkristo...chukua mfano shule....mimi mtoto wangu nampeleka chekechea anaanza kupiga shule, mwislam anampeleka madrassa kusoma dini, wakianza wote lakwanza wangu atakuwa na background nzuri hivyo ataongoza darasani, atakuwa na moyo huo matokeo yake anaishia university.

uislam unafanya kazi nchi zenye mafuta sehemu ambao watu hawatumii sana elimu/akili, bali wanachota tu mafuta na kuishi....dunia nzima tembea utakuwa waislam wanaishia kuuza vijiduka vidogo tu na si investment za akili......Nigeria nayo ni tz? mbona Nigeria maeneo yale ya kusini kwa wakristo ndo kuna maendeleo ukienda kule kaskazini kwenye sharia, umasikini wa kutupwa...tz nayo hawa watu wa pwani wanatandika mkeka tu na kusubiri majini yakachume ulete...nafikiri kama kuna kitu cha kuwasaidia hawa wenzetu ni kuwapa elimu..itawakomboa sana.

wake wanaoa wengi, wanashindwa kusomesha watoto, matokeo yake wanalalamika wanaonewa, wakati sisi wakristo watoto wetu ni wa bajeti hivyo tunawasomesha wote...wake wengi wanawamaliza, madrassa zinamaliza watoto wenu....kalagabaho.
We kweli ni mzushi.Elimu ya madrasa ni elimu kama elimu zingine,inalenga kupanua kichwa cha mtoto na wala sio kukidumaza kama unavyodhani.Mnajitahidi kuipiga vita lakini mmefeli kwa sababu kila msikiti sasa unakuta madrsa sambamba na chekechea.kwa hiyo mmeula wa chuya.
Waislam walipomfukuza mkoloni walikuwa wanaju umuhimu wa elimu lakini Nyerere aliwahujumu.Enzi za Nyerere shule za sekondari zilikuwa chache sana hata wale waliokuwa wanakwenda sekondari sio kwmaba walikuwa wanashinda bali walikuwa wanchaguliwa kwa upendeleo,enzi hizo kama mtoto hakuchaguliwa kwenda sekondari ndo mwisho wa elimu,hapakuwapo na sekondari za binafsi.Lkini sasa kwa sekondari za kata wewe toa muda tu ndo utagundua kwamba kumbe waislam nao wanzo bongo kali.
Waislm sio malofa kama unavyofikiria.Nenda barbara ya Pugu na Mandela hesabu vile viwanda na wamilki wake ndo uje utajua kuwa waislamu ni hodari wa kuwekeza na biashara.Hakuna mafuta hapa.Hata hiyo story ya Nijeria ni upotoshaji unaleta hoja za nguvu tu.Abuja mabo ndio mji wa kisasa zaidi Nijeria uko kaskazini kwa waislamu wengi.We achana na story za abunwasi.
 
Nimepata info kuwa Jambo Leo, Mtanzania, Uhuru na Habari Leo ni vyombo dhaifu vya mbele kuendeleza propaganda chafu za udini Tz. Ukiangalia vyote ni ndugu na ni vya CCM/Serikali.

Basi sio kosa kusema Serikali inachochea udini Tz!
 
adui ya muislamu siyo mkiristo ni ibilisi, na adui ya mkiristo siyo muislamu ni ibilisi
tukifahamu kwamba ibilisi ndiyo baba ya ufisadi, ubaguzi, uchoyo, dhulma, uwongouwongo basi sisi wana wa adamu tukaungana kwa pamoja kupambana na mambo haya bila shaka tutakuwa tunamdhoofisha ibilisi na hatimaye kusimika misingi ya amani ya kweli, fanaka na furaha.

Mwenyezi mungu ni mmoja na ni wetu sote, askofu akikemea maovu yatupasa kuwaunga mkono, mashehe wakikemea maovu yatupasa kuwaunga mkono.
Mwenyezi mungu anasema katika qur'an (nukuu isiyo rasmi) [" tuliandika katika zaburi kwamba hii ardhi itarithiwa na waja wetu watenda mema"],
na ukisoma zaburi ya 37 inasema (nukuu isiyo rasmi) ["the earth will be inherited by the humble"].

Sasa hii hali ya kuzodoana, kunyoosheana vidole ya nini?, kwa nini tusitafute kujenga kwa kutumia njia nzuri, za mazungumzo, za kuheshimiana?.

kwani ibilisi ni dini gani?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom