Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
Tamko la waislamu: Waislamu wapinga mfumo wa serikali wanao uita mfumo kristo
Ingawa ukisikiliza vizuri wanaonyesha adui mkubwa ni WAKATOLIKI
 
Hizi hoja zakijinga zakidini nadhani sasa zimeanza kuchosha. Jukwaa la siasa limekuwa kama mwembechai ama St. Peters sijui azania. Tumechoka na hizi dini zenu.
 
Mtu anayeupinga Uislam au Ukristo anakuwa na lengo gani? Faida anayoipata ni ipi? Unataka nchi igawanywe ili iweje? Maendeleo ndio yatakuja kwa kasi zaidi? Ni nchi ngapi zina wakristo wengi lakini bado kuna masikini wa kutupwa? Ni nchi ngapi za kiislamu lakini bado zina masikini wa kutupwa? Zanzibar imewahi kuongozwa na mkristo? Ni wakristo wangapi wako Zanzibar? Je hakuna watu masikini Zanzibar? Ni nani anawaonea waislamu wa Zanzibar?

Mtu anayechangia kwa jazba hana nia njema ya kuleta suluhu. Kama radio Imaan na chombo kingine chochote cha kiislamu kinachochea udini lazima kiambiwe na kisipobadilika kifungiwe.

Kama radio tumaini na chombo kingine chochote cha kikristo kinachochea udini ni lazima kiambiwe na kisipobadilika kifungiwe.

Hakuna anayetakiwa kuogopwa, mkristo au muislamu. Ukiona vyombo hivyo vinaendelea na propaganda za kidini ujue kuna upungufu wa kiuongozi. Huwezi kukemea rushwa kama ndio imekuingiza madarakani hivyo hivyo huwezi kukemea udini kama ndio umekuacha madarakani!!
 
Inasikitisha sana wapi nchi yetu tunakoelekea, hakika , hata vugu vugu la vyama vingi lilianza hivi hivi na sasa limeshamiri kwa hali ya juu, kwa mtindo huu wa mashekhe na maaskofu kulumbana kwa eti kisa UDINI, tutakaoathirika ni sisi wananchi walala hoi na familia maskini. wenye zao watahamisha makazi yao uhamishoni...Waislam wameanza kuibua masuala ya udini kwenye utawala namna hii, wanatuandalia nini? suala la kujigawa linakujaje? kweli wanaoanzisha udini ni viongozi wetu waliopewa mamlaka ya juu, wanatuharibia sana ustaarabu na utu huku chini.. HEBU VIONGOZI WA DINI JARIBUNI KUSOMA HISTORIA YA MAUAJI YA RWANDA NA BURUDI CHANZO CHAKE NI NINI? WAPI TUTAKIMBILIA JAMANI.. NINGEPEWA NAFASI, YA KUTOA MCHANGO WANGU..
 
Nadhani tatizo lako ni kudhani kuwa ukiwa Muislamu utakubaliana na yote hata kama ni uharo. Hili la Radio Imaan in propaganda za Kijihad ambazo ni sawa kabisa na UGHAIDI. Chonde waislam, ujinga wenu ndio utatupeleka pabaya. Ona Nigeria (JOS State) kila mara waislam wandhani wao ni bora sana kuliko wenzao. Huu ni uzandiki, hauwezi kuvumiliwa. Kibaya zaidi JK ndiye tatizo, kwa historia ya karibuni tu, Mchungaji Mtikila alikuwa sahihi kumuita Ghaidi, kweli Uislam ni Ughaidi.

Of ALL THE PEOPLE! HATA WEWE MAGID UNATHUBUTU KULAUMU RADIO IIMAAN NA WAISLAMU. You are too young ndugu yangu lakini fanya tafiti nzuuuri ndio baadae uje na hadithi yako hii. Mbaya zaidi umeirusha kwenye internet!!! hii itaendelea kubaki... na ukisha maliza home work yako utarudi any day kwenye media yoyote na utoe the other side of the story.

Pole sana Maggid ngoma uichezayo hujui mpigaji ni nani?
Ma'ssalaam.
Shkh Yahya.
 
radio imaan wamesema walichosema,katka yote cwaung mkono kwenye kuigawa nch,lakin kuna madai ambayo yapo kwenye tamko,naweza sema ni sensitive sana,MAZNGRA 2NAYOISH WANANCH HAKUNA UDINI,lakini kwenye taasi mbalimbli kuna udini+ukabila,nina mfano hai,pale udsm kuna mhadhir aliwapa wakristo majib ya ue kanisani,kwa bahat ukaribu na yule mkristo ulisaidia kuipata nyanga,jaman haya masuala had leo wadau wanayazungumza ujue kuna jambo,MJENGWA UMENIPATA
 
Nadhani tatizo lako ni kudhani kuwa ukiwa Muislamu utakubaliana na yote hata kama ni uharo. Hili la Radio Imaan in propaganda za Kijihad ambazo ni sawa kabisa na UGHAIDI. Chonde waislam, ujinga wenu ndio utatupeleka pabaya. Ona Nigeria (JOS State) kila mara waislam wandhani wao ni bora sana kuliko wenzao. Huu ni uzandiki, hauwezi kuvumiliwa. Kibaya zaidi JK ndiye tatizo, kwa historia ya karibuni tu, Mchungaji Mtikila alikuwa sahihi kumuita Ghaidi, kweli Uislam ni Ughaidi.

That is too harsh, my brother. Mbona sasa na wewe unakashifu dini ya watu? Na tena unamkashifu kiongozi wa nchi? Hata kama hatumpendi, bado kikatiba, ni kiongozi wetu.

Nakushauri kuwa si lazima kila unapotukanwa basi nawewe utukane. Hapo ndipo tutatofautisha wenye busara na wasio nazo.

Muhimu ni kuwa mamlaka zinazohusika zichukue hatua zinazostahili kwa vyombo vya dini vinavyokashifu dini zingine au vinavyotugawa watanzania. Vyombo hivi vinatakiwa kueneza mema ya dini zao na si mabaya ya dini zingine.
 
Mimi la kufelishwa makusudi nalikataa. Nilisoma Mtwara Technical na Dadi Yusuf Namtumba, aliongoza mchepuo wa "Mechanical" tangu siku ya kwanza hadi tunamaliza. Alipewa haki yake ya kuendelea na masomo Arusha Technical College. Katika familia yangu, babu mkubwa (kaka wa babu yangu) alifanya kazi ya jeshi huko Burma (leo Mynmar). Aliporudi kijijini, yeye na familia yake wakuwa waislam, ingawa wengine walikuwa bado wahehe (siyo waislam, sio wakristo; ukristo ukikuwepo ila ulikuwa bado mpya). Wakatoliki wakaanzisha shule (elimu dunia) na kuwasajili watoto wa wafuasi wa imani yao. Baba yangu akamshawishi babu mkubwa alimbadilisha jina baba mdogo (mtoto wa baba mkubwa) kutoka Ahmed kuwa Wailes ili asome shule ya wakatoliki (shule pekee kijijini wakati wetu ambayo ilisomesha watu wa imani yao). Kazi ilikuwa kubwa, kwani baba aliona hiyo ilkuwa ndiyo njia pekee ya kumsadia mdogo wake apate elimu, wakati babu aliona ni namna ya kumbadilisha mwanae imani. Baba akamwambia mdogo wake kuwa ukifika mbele huko utakuwa na uhuru wa kuabudu na elimu utakuwa nayo, Mungu akikupa uzima. Baada ya kuhitimu std 8, aliendelea na masomo Mkwawa High School (wakati huo). Alipokuwa anaingia A'Level alirudia jina lake la Ahmed. Matokeo ya mitihani yake (PCB) alitolewa hihalali, akapata scholarship kwenda kusoma udakitari; na hadi leo ni dakitari. Ingawa baba hakuwa Mkristo wala Mwislam, alijua faida ya elimu. Hata palipo na shida, vikwazo; tufikirie namna ya fanikiwa sio visingizio na kuchafuana. Tunaweza kuwaadhibu wale tunaohisi wanatusababishia matatizo, lakini tukashindwa kujiendeleza wenyewe wakati wale wamekwisha wamaliza.
 
Kwa taarifa RADIO IMAAN inasikika nchi nzima kwa sasa, hivyo inawasikilizaji wengi. Pia wewe u-mtu wa ajabu, maaskofu wakisema, wakitukanä wakichochea ni sawa LAKINI MASHEHE WAKISEMA NI KOSA. Nami nasema maaskofu mnatupeleka kubaya. Msichanganye siasa na dini.

inaelekea wewe ndio ulikuwa muongoza kipindi, mi hiyo redio cjawai kuisikia wala watu kuizungumzia. dar es salaam inapatikana katika frequence ipi?
 
Narudia kusema tena kuwa ni muhimu nchi kuwa na RAIS. Tungekuwa na RAIS angeshaikemea hali hii kwa mamlaka na hali ingekuwa shwari. Hii siyo mara ya kwanza hoja za udini kuibuka. tofauti ni kuwa hizi hoja huko nyuma zilikemewa kila zilipoibuka maana RAIS alikuwepo. Kwa sasa TZ ni kama nyumba ambayo baba amesafiri na kila mtoto anajitawala kivyake. Wa kurudi amelewa haya, wakuleta wasichana kwenye geto lake haya, wa kulala kwenye disko haya na hakuna wa kukemea maana wazazi hawapo. Tunahitaji kuwa na RAIS
 
Kwa kweli sijui tufanyeje, maana sasa wenzetu waislam wamebadili kabisa muelekeo wao. Mimi ni mkristo na mtafiti katika imani za dini. Tangu zamani nimekuwa nikisikiliza mawaidha yao tangu enzi za RTD. Mawaidha yalikuwa mazuri yenye kujenga jamii, mathalan kipindi walikuwa wakiwaelimisha waislamu wasifanye zinaa. Nakumbuka kuna siku katika mawaidha walikuwa wakifundisha kuwa kama wewe ni kijana una gheto lako halafu kijana mwenzio akaja kukuomba gheto lako ili wapate faragha na mwanamke ambaye si mke wake basi wote (yaani yule kijana mwenye gheto, aliyekuja na mwanamke na mwanamke mwenyewe) wamemkosea Allah. Mawaidha ya namna hiyo yalikuwa yanafaida sana kwa waislam na jamii yote.

Lakini sasa hali ni tofauti, wameacha kutoa mawaidha ambayo yatamfanya mja au binadamu awe na uhusiano bora na Allah. Hawaongei tena kuhusu maadili, kana kwamba waislam hawana au hawafanyi dhambi tena. Muda wote wanaongea kuhusu ukombozi, kana kwamba wako utumwani, wakati ukweli ni kwamba sisi tumefungwa na utumwa wa dhambi na si dini fulani. Kwa uelewa wangu wa dini zote, mtu hatakubaliwa au kupata kibali cha Muumba kwa kushambulia imani fulani au dini fulani. Ndugu zangu waislam ni uadilifu tu katika mambo yote ndiyo tiketi ya kuurithi ufalme wa mbinguni na si kulumbana au kuanzisha kadhi au kuifanya nchi iwe ya kiislamu.
 
I think, we just need to ignore those few who call themselves elite and hardliners on religious world. We need to be "kiasi" for us to live in our planet earth safely! Nadhani anayetugawa kwa udini akimaliza atatugawa kiukooo, ile ile ya Somali dhambi ambayo malipo yake ni makubwa mno. Nawapenda wote bila kujali dini wala tabaka wala kabila wala ukoo!!!! That is me and help me so God.
 
Majjid,
Kama system ya nchi inabaguwa na imeweka misingi (ya siri na dhahiri) ya kuwabaguwa waislamu, kufuta mchango wao wa historia ya ukombozi ya nchi hii, kuuwa jumuiya zao za kimaendeleo (by Nyerere) na kuwawekea jumuiya pandikizi (Bakwata) na chungu tele ya vizingiti visivyokuwa na sababu, mnataka wanyamaze kimya kwa kisingizio cha kulinda umoja ambao tokea hapo haupo?

Waislamu wameshauliwa nchi hii, weshafanywa vilema, weshafungwa magerezani bila ya sababu ya msingi hakuna aliyewajibika kwa madhila yao, mnataka bado wanyamaze?
Hebu twambieni Mkiristo gani alipigwa bomu la machozi kwasabu ya ukiristo wake?
Mkiristo gani aliuwawa kwa risasi kwa sababau ya ukiristo wake?
Mkiristo gani alifungwa jela kwasababu ya Ukiristo wake?
Hayo yote waislamu wa Tanzania wameshafanyiwa tena kwa jeuri na hakuna yeyote aliechukuliwa hatua kuwajibishwa, kwanini wao wasipaze sauti zao kusema na kujilinda wenyewe?

Au hatujawahi kuambiwa kuwa tusichanganye dini na siasa linapokuja suala la waislamu lakini wakiristo hata waraka na maazimio ya kisiasa wanatowa kwenye majukwaa ya kidini, kwanini isiwe " wao na sisi" wakati " usisi" haupo tokea hapo?
Majjid naona kuna mambo unayatizama kwa jicho pembe, hujuwi kuwa waislamu wa Tanzania ni binaadamu kama wengine? wanahisia, vipi leo wakae waseme tu haki zao zilindwe kikatiba kama zilivyo kwa makundi mengine ya kidini, wewe uone ni tatizo, kwani hujuwi kuwa mtumzima akilia kuna jambo?

Ulichoshituka wewe Majjid si uliyoyasikia bali kutoamini ulichokisikia kuwa waislamu wa Tanzania wanadai wanachoona haki yao ya kutobaguliwa nchi hii ambayo tokea kuasisiwa kwa Taifa hili imekuwa ni jambo la kawaida kwa tawala zote za CCM ambazo "mfumo kristo" alioushupalia Nyerere ndiyo itikadi ya kuiongoza nchi hii tokea wakati huo mpaka leo.
 
Wadau, jana katika kubadilisha station ya radio yangu nilikutana na mjadala uliokuwa ukiendeshwa redio imani, hii ni redio ya kiislamu iliyoko mjini Morogoro. Ingawa si kawaida yangu kuisikiliza lakini nilishawishika kuwasikiliza kutokana na uzito wa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Mjadala ulihusu tamko walilotoa kuhusu maaskofu, walivilaumu vyombo vya habari – magazeti particularly mwananchi na magazeti mengine kama nipashe, Tz Daima etc kwamba yamepotosha tamko lao pamoja na kuwa waliwapa tamko hilo kimaandishi. Nilijiuliza inakuwaje magazeti yote yanakosea kitu kilekile.
Kilichonisikitisha katika mjadala huo ni uchochezi na upotoshaji wanaoueneza hawa masheikh kwa sababu wanazojua wao. Kwa mfano walisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kikiristu toka enzi za Nyerere, moja ya madai yao ni kwamba waislaumu walikuwa wakifelishwa makusudi shuleni ili wasisome, bila shaka haya ni madai makubwa sana.
Mambo mengine ni kwamba ili kudhibitisha kwamba nchi inaendeshwa kikristo ni kwa nini wakristo wana university na hospitali nyingi kuliko serikali, madai mengine ni kwamba kwa nini hospitali za kikristo zilizotaifishwa na serikali zilirudishwa , bila shaka katika hili ni kwamba serikali ilishindwa kuziendesha, lakini kwa sababu wanazojua wao waliishia kulaumu mfumo wa utawala wa kikristo. Katika hili wao walikiri kwamba hakurudishiwa kitu kwa kuwa hawakunyanganywa kitu!
Baada ya kumaliza majadiliano waliruhusu wasikilizaji kutuma sms na kupiga simu studio, wengi wa wachangiaji waliwashukuru masheikh kwa hatua yao lakini pia kuna waliosema watajichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu waandishi, na wengine walitaka itangazwe jihad dhidi yao.
Nilivyoona mimi hakuna shabaha nyingine zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa dini jambo ambalo si kawaida yetu watz.

Ingawa najua kwamba redio hii haina wasikilizaji wengi lakini mijadala ya uchochezi namna ile haitakiwi kupita bila kukemewa. Katika mauaji ya Rwanda redio zilitumika sana kuchochea chuki baina ya watu, hatutakiwi kufika huko, nadhani ni wakati muafaka kwa “intelijensia” ya polisi kufanya kazi sasa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokana na uchochezi wa redio imani

Wana JF naomba kuwakilisha

jamani watu hawa wanafadhiliwa na Ikulu unafikiri wataongea nini?jambo moja tu aliyeanzisha swala la udini litamtafuna yeye kabla ya wengine.
 
Salaam bro Maggidi.
Ndg yangu mimi mwenyewe nimeshangazwa sana hii redio yetu ya kiroho kufanya mambo ya ajabu kiasi hiki, sisi waislam wengine tunabaki kushangaa, hivi adui wetu mkubwa ni wakristo na Maaskofu au ni shetani?

nilitarajia redio yetu na magazeti yetu ya dini yahusike zaidi kutujenga kiimani na kuishi maisha mema kama alivyotufunza mtume na maswahaba walivyoishi. Sasa wamegeuka kuwa wachochezi na wafuatiliaji wa siasa za kipumbavu za kidini nchini.
Nimesoma hata gazeti letu la An-Nuur, ni madudu matupu ya siasa ndio yanaandikwa badala ya mafunzo ya imani.

ndg zangu waislam, lazima tukubali kushinda mambo kwa hoja na sio kuchocheana kwa mambo ya ajabu kama yale ya pale Daimond J. Na vilele watatucheka watu baadae kwamba hatukuwa makini,
 
hali ya Hewa sio nzuri dalili za uchokozi kazianzisha Mkuu wetu ikiwa itatokea mambo yakawa mabaya, wa kulaumiwa ni Mkuu, lakini tukiyakemea yataisha mbona mauaji ya albino yameisha, mbona kenya wamemaliza kikisi cha Mungiki, serikali inashindwa nini? kila mskiti au Kanisa huwa kuna UWT kusikiliza maubili ina maana UWT aina maan sasa kama mambo yote haya yanatokea badala ya kuyadhibiti inachochea
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom