Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
Kwa taarifa RADIO IMAAN inasikika nchi nzima kwa sasa, hivyo inawasikilizaji wengi. Pia wewe u-mtu wa ajabu, maaskofu wakisema, wakitukanä wakichochea ni sawa LAKINI MASHEHE WAKISEMA NI KOSA. Nami nasema maaskofu mnatupeleka kubaya. Msichanganye siasa na dini.

Kauli za maaskofu (hasa Wanglikani, Walutheri na Wakatoliki) huwa hazina uchochezi wowote wa kidini bali zinahusu maendeleo au matatizo ya Watanzania wote. Kauli za masheikh mara nyingi zinapiga vita Ukristo na hasa Kanisa Katoliki na kuchochea vurugu! Ni mara chache sana masheikh wanatoa kauli kuhusu uboreshaji wa huduma za kijamii au kuchangia katika kuboresha huduma fulani.
 
Mdau, binafsi nakupongeza kwa kuliona hilo na kuona kwamba ipo haja ya kutoa angalizo kwa kile ulichokisikia kupitia redio hiyo inayomilikiwa na taasisi ya dini ya Kiislam.

Kwangu mimi, cha msingi ninachokiona kwenye mada yako ni kuhusu uchochezi wa kidini unaofanywa na Redio hiyo na maafa yanayoweza kulikumba taifa letu kama hatua za haraka hazitachuliwa kudhibiti hali hiyo. Mimi binafsi sina tatizo na hoja yako. Kimsingi ni angalizo linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda amani. Hata hviyo, ninachotaka kuongeza hapa ni kwamba, hali ya mustakabali wa kidini katika Tanzania kwa sasa ni tete. Na hili halina ubishi hata kidogo, labda iwe kwa mtu mwenye hulka ya kubishia kila jambo ndiye pekee anayeweza kupingana na ukweli huu.

Hali tuliyo nayo sasa hapa nchini haishirii dalili njema hata kidogo mbele ya safari. Zinahitajika hatua za maksudi kabisa katika kukabiliana na hali hii kabla bomu halijalipuka. Ni vema watanzania tukatambua kwamba machafuko yenye sura kama hizi za kidini mahali popote yalipopata kutokea duniani, hayakuja kama mvua au kwa bahati mbaya, la hasha!. Machafuko yalianza kama masihala kwa njia kama hizi hizi za chochoko, malumbano,na uchochezi wa chini kwa chni kama tunavyoanzashudia hapa kwetu Tanzania.

Binafsi sipendi kuhukumu kwamba ni dini gani hasa ndio inayoonesha dalili za kutaka kutupeleka kwenye machafuko ya kidini ambayo ni machafuko mabaya kupita machafuko mengine yoyote katika dunia hii. Nasita kufanya hivyo kwa sababu imani yangu inanizuia kukuhukumu na kusisitiza zaidi kuchunguza boriti ndani ya jicho langu kabla ya kutoa kibanzi katika mboni ya jicho la mwenzangu. Hata hivyo, natambua dhahiri shahri kwamba mustakabli wa hali ya kidini hapa nchini imekuwa tete tangu mchakato wa uchaguzi Mkuu wa mwaka jana. Hivyo basi, ni wajibu wa kila mtanzania mwenye dini na asiye na dini kuliona hilo na kuchukua hatua kwa nafasi yake ili kuzuia dalili mbaya zinajitokeza katika taifa letu.

Na mwisho ninapendekeza kwamba, kama ilivyo hitaji la watanzania kuwa na Katiba Mpya, basi halikadhilika iwe hivyo hivyo katika jambo la kidini. Sio vibaya tukawa na mjadala wa kitaifa kuhusu hatma ya mivutano ya kidini iliyoanza kujitokeza hapa nchini. Na kwa njia hiyo pekee ndipo tutaweza kutoa fursa kwa kila upande utoe dukuduku lake na kisha kufikia muafaka wa pamoja. Lakini, tukiendelea kupuuza, kukejeliana,kutukanana na kushutumiana bila kuchukua hatua zozote haitatusaidia. Tukumbuke kwamba panapofuka moshi lazima pana moto!!

Mungu ibariki Tanzania na watu wake!!!

Redio hii, na watu wachache wanaojiita waislamu, hawawezi kufanikiwa kupandikiza chuki. Waislamu safi hawapendi haya mambo ya hovyo hovyo. Hiyo redio ipo na wanaotakiwa kuishughulikia ni Waislamu wa kweli. Mimi nina ndugu kabisa waislamu na tunapendana, nina marafiki wengi sana waislamu, kulikoni.:disapointed:
 
Kwa mwislam ambaye amesoma na kuelewa sidhaani kama anaweza kukubaliana na huo mjadala, manake ni uongo mtupu na uchochezi.

Hata ukifuatilia wanachosema si kweli maana wao ndo wachawi wa maendeleo yao, fanya tu utafiti mdogo wa shule za sekondari za kiislam kuhusu maendeleo yao utahisi kichefuchefu, manake viongozi ambao hawana elimu dunia wanang'anga'nia kuzisimamia hatimaye kuzipeleka ambako siko.

tatizo waislamu wengi hawajasoma..hivyo wengi watakuwa wamekubaliana na huo mjadala..no wonder wengi wakawa wapiga simu na kutaka itangazwe jihad..hiko kituo muhimu kikafungiwa. hao masheikh uwezo wao wa kifikra mdogo sana..hawajui yaliyotokea RWANDA kwa kupitia uchochezi wa radio..
 
Binafsi nimeona influence ya redio imani, jamaa yangu mmoja tena msomi tu alikuja na hoja nilizozisikia redio Imani. Eti serekali ya Nyerere ilitaifisha shule zote za wakristu na waislam baadae ikarudisha shule zote za wakristu lakini za waislam hazikurudishwa. Hakujua shule niliyosoma ya serikali ilikuwa seminari zamani na hadi leo iko chini ya serekali!
 
Wanadhani wakifanikiwa kuchochea vurugu watabaki salama wakila kuku kwa mrija, thubutu! wawaulize wenzao huko Rwanda wakati wa mauaji ya kimbari, wamiliki wa radio chochezi wote wana nyea debe maisha yao yote. Hayo ndiyo yatakayowakuta. Dunia inaona na watu wanarekodi ushahidi.
 
Wadau, jana katika kubadilisha station ya radio yangu nilikutana na mjadala uliokuwa ukiendeshwa redio imani, hii ni redio ya kiislamu iliyoko mjini Morogoro. Ingawa si kawaida yangu kuisikiliza lakini nilishawishika kuwasikiliza kutokana na uzito wa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Mjadala ulihusu tamko walilotoa kuhusu maaskofu, walivilaumu vyombo vya habari – magazeti particularly mwananchi na magazeti mengine kama nipashe, Tz Daima etc kwamba yamepotosha tamko lao pamoja na kuwa waliwapa tamko hilo kimaandishi. Nilijiuliza inakuwaje magazeti yote yanakosea kitu kilekile.

Kilichonisikitisha katika mjadala huo ni uchochezi na upotoshaji wanaoueneza hawa masheikh kwa sababu wanazojua wao. Kwa mfano walisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kikiristu toka enzi za Nyerere, moja ya madai yao ni kwamba waislaumu walikuwa wakifelishwa makusudi shuleni ili wasisome, bila shaka haya ni madai makubwa sana.

Mambo mengine ni kwamba ili kudhibitisha kwamba nchi inaendeshwa kikristo ni kwa nini wakristo wana university na hospitali nyingi kuliko serikali, madai mengine ni kwamba kwa nini hospitali za kikristo zilizotaifishwa na serikali zilirudishwa, bila shaka katika hili ni kwamba serikali ilishindwa kuziendesha, lakini kwa sababu wanazojua wao waliishia kulaumu mfumo wa utawala wa kikristo. Katika hili wao walikiri kwamba hakurudishiwa kitu kwa kuwa hawakunyanganywa kitu!

Baada ya kumaliza majadiliano waliruhusu wasikilizaji kutuma sms na kupiga simu studio, wengi wa wachangiaji waliwashukuru masheikh kwa hatua yao lakini pia kuna waliosema watajichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu waandishi, na wengine walitaka itangazwe jihad dhidi yao.
Nilivyoona mimi hakuna shabaha nyingine zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa dini jambo ambalo si kawaida yetu watz.

Ingawa najua kwamba redio hii haina wasikilizaji wengi lakini mijadala ya uchochezi namna ile haitakiwi kupita bila kukemewa. Katika mauaji ya Rwanda redio zilitumika sana kuchochea chuki baina ya watu, hatutakiwi kufika huko, nadhani ni wakati muafaka kwa “intelijensia” ya polisi kufanya kazi sasa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokana na uchochezi wa redio imani

Wana JF naomba kuwakilisha
Tuwaache Mashekh na Maaskofu waendelee, sisi wafuasi wao tupambane na nchi yetu, huwa sichangii kwenye haya yanaturudisha nyuma, watanzania tuna desturi ya kupendana sana with regardless ya dini zetu na makabila yetu.
 
mkuu kwanza asante kwa taarifa yako! Kwa maoni yangu ingawa hukupendezwa na kituo hicho cha radio kuweka taarifa hii hapa kumewasaidia kuzidi kufikisha ujumbe na dhamira yao. Hivyo kuwapa nguvu hawa ndugu zetu wanaoeneza siasa za udini.
 
Wadau, jana katika kubadilisha station ya radio yangu nilikutana na mjadala uliokuwa ukiendeshwa redio imani, hii ni redio ya kiislamu iliyoko mjini Morogoro. Ingawa si kawaida yangu kuisikiliza lakini nilishawishika kuwasikiliza kutokana na uzito wa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Mjadala ulihusu tamko walilotoa kuhusu maaskofu, walivilaumu vyombo vya habari – magazeti particularly mwananchi na magazeti mengine kama nipashe, Tz Daima etc kwamba yamepotosha tamko lao pamoja na kuwa waliwapa tamko hilo kimaandishi. Nilijiuliza inakuwaje magazeti yote yanakosea kitu kilekile.

Kilichonisikitisha katika mjadala huo ni uchochezi na upotoshaji wanaoueneza hawa masheikh kwa sababu wanazojua wao. Kwa mfano walisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kikiristu toka enzi za Nyerere, moja ya madai yao ni kwamba waislaumu walikuwa wakifelishwa makusudi shuleni ili wasisome, bila shaka haya ni madai makubwa sana.

Mambo mengine ni kwamba ili kudhibitisha kwamba nchi inaendeshwa kikristo ni kwa nini wakristo wana university na hospitali nyingi kuliko serikali, madai mengine ni kwamba kwa nini hospitali za kikristo zilizotaifishwa na serikali zilirudishwa, bila shaka katika hili ni kwamba serikali ilishindwa kuziendesha, lakini kwa sababu wanazojua wao waliishia kulaumu mfumo wa utawala wa kikristo. Katika hili wao walikiri kwamba hakurudishiwa kitu kwa kuwa hawakunyanganywa kitu!

Baada ya kumaliza majadiliano waliruhusu wasikilizaji kutuma sms na kupiga simu studio, wengi wa wachangiaji waliwashukuru masheikh kwa hatua yao lakini pia kuna waliosema watajichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu waandishi, na wengine walitaka itangazwe jihad dhidi yao.
Nilivyoona mimi hakuna shabaha nyingine zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa dini jambo ambalo si kawaida yetu watz.

Ingawa najua kwamba redio hii haina wasikilizaji wengi lakini mijadala ya uchochezi namna ile haitakiwi kupita bila kukemewa. Katika mauaji ya Rwanda redio zilitumika sana kuchochea chuki baina ya watu, hatutakiwi kufika huko, nadhani ni wakati muafaka kwa "intelijensia" ya polisi kufanya kazi sasa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokana na uchochezi wa redio imani

Wana JF naomba kuwakilisha

Ungelianza kuwakemea maaskofu wenu na magazeti yenu ya msemakweli ndipo uje kukemea Redio Imaan. Kama hujapendezwa na mjadala unaweza kubadilisha idhaa mkuu kila mtu yuko huru kutoa opinion yake in a democratic country....
 
Maskini Dini ya Mwenyezi Mungu imekamatwa na WAVIVU WA KUFIKIRI.
 
Kwa hiyo Uislam ulivyoingia Tanganyika na Zanzibar, kama sio East Africa uliingia kwa Upanga, kama unavyofikiria... Hivi unaijuwa historia ya nchi yako kweli.

Hivi Jihadi maana yake nini?

Kuna jamaa mmoja liuliza hili swali: Waarabu na wazungu waliendesha bishara ya utumwa hapa Afrika, Afrika Mashariki.
1. Tuna descendants was Africa huko Amerika na pengine kwingineko Ulaya.
2. Je, descentants kutoka Uarabuni wako wapi au baada ya hao watumwa kutumika walikula upanga?
 
Kwanza nikushukuru kwa angalizo lako maana naona wewe ni mkereketwa wa amani ya nchi yetu, na pia unatambua mambo yatakapoharibika hakuna atakayesalimika eti kwa sababu ya dini yake. Lakini pia nikukumbushe tu sisi wakirsto huwa tunatafakali kwanza kabla ya kuanza kufanya jambo lolote, mifano ipo mingi na hata kama nitamua kuitaja hapa itakuwa ni upotoshaji wa mada. Kwa hiyo jambo la msingi ni kutafakali na kisha kuchukua hatua, ninamanisha nini kwa kusema hivyo, ni kwamba hayo yaliyosemwa katika redio imaan ni propaganda za watu ambao uelewa wao upo chini saana, na kwa sababu wameanzisha redio lakini bila kuwa na wataalam wenye uwezo wa kuwasaidia katika kuandaa mada ambazo ni za msingi na zenye kugusa maisha ya watu kama hizo basi ni jukumu lako wewe unayesikiliza kuona yote yaliyosemwa ni "off point" kisha achana nao. Katika utandawazi kama huu huwezi kufukili kuwa watu wataishia kuamini wanayoskia peke yake, lazima watajaribu kutafuta msaada na kupima waliyosikia na kisha kuchukua hatua. Tafadhali usikate tamaa kwani tayali ukweli unaujua
 
ninashawishika kwamba wewe ni mtu makini sana na uwezo wako wa kutafakari ni mkubwa
 
Maskini!!! Msiba mkubwa kabisa umeikabili nafsi yako na ubongo wako umedumaa!! (samahani lakini! nahisi unaishi dunia tofauti na hii na u mgeni kabisa!!) Sijui unaijua indonesia na malaysia ziko dunia gani au umeropokwa tu! je nako kuna mafuta kule? Hilo la Nigeria nadhani pia bado u ndotoni na si Nigeria pekee bali Afrika magharibi yote fuatilia upate majawabu halisi ili ububusa ukutoke. Wacha kutumia mdomo kufikiri tumia ubongo rafiki.

Kama kweli upo wewe dunia ya sasa usingezungumzia upendeleo, kwakifupi ukanda wa pwani umelala na ndio ngome ya uislamu Tanzania, hata maeneo ya kati kama Tabora na Kondoa nako hakuna tofauti tatizo ni dini hailengi kumkwamua mwananchi bali kumdumaza kwa kumjengea maadui (wakristo) ambao ndio wenye rasilimali elimu (shule, vyuo nk) sasa unatarajia nini? Au hata zama hizi za utandawazi bado upendeleo upo? Maana shule binafsi zimeanzishwa nyingi lakini unajua wawekezaji wa kiislamu wangapi wamewekeza kwenye shule, tafiti utagundua mmelala sasa mnapaswa kuamka badala ya kulalama
 
Maskini!!! Msiba mkubwa kabisa umeikabili nafsi yako na ubongo wako umedumaa!! (samahani lakini! nahisi unaishi dunia tofauti na hii na u mgeni kabisa!!) Sijui unaijua indonesia na malaysia ziko dunia gani au umeropokwa tu! je nako kuna mafuta kule? Hilo la Nigeria nadhani pia bado u ndotoni na si Nigeria pekee bali Afrika magharibi yote fuatilia upate majawabu halisi ili ububusa ukutoke. Wacha kutumia mdomo kufikiri tumia ubongo rafiki.

Ama kweli msiba unao wewe ndugu yangu, hivi unataka kusema hata fursa za kibiashara zilitolewa kwa upendeleo wa udini au? Mbona pwani kuna umaskini wa kutupa unaoandamana na uvivu wa kupindukia sasa huo uvivu ni serikali imepanga muwe hivyo au? Nenda kilimanjaro utagundua wengi wamesoma kwa wazazi kujitoa kwa bidii maana wengi wamesoma shule binafsi nyie bado mpo kwenye zama za kusaidiwa, wakati fulani miaka ya mwl. ilibidi kubadili majina nakutumia majina ya pwani na kwingineko ili kupata nafasi na tulisonga mbele kwa hali hiyo hatukupoteza muda kwa malalamiko! Ndugu yangu amka hizo nchi unazosema hazijaendekeza udini, wameweka kazi mbele
 
Mchawi wa ndugu zetu waislam ni wao wenyewe, kuanzia walioleta dini ya Kiislam hapa Nchini. Waarabu walithamini sana elimu ya dini (kitu ambacho ni kizuri) bila kuthamini elimu dunia (huyu ndo mchawi wao). Tazama hawakujenga shule, hospitali, vyuo kwa wingi kama walivyofanya wajerumani na waingereza.Hali hii iliwafaidisha sana watu walioamua kufuata ukristu, kwani waliweza kufaidika na mafundisho ya dini pamoja na huduma za elimu na afya. Jamani MUNGU amlaze pema peponi Nyerere wetu. Inasikitisha kusikia ndugu zetu waislamu mnamlaani mtu huyu; aliyetaifisha shule, vyuo,na hospitali za dini ya kikristu kuwa public..ili hata ndugu zetu waislamu nao wapate.MUNGU awasamehe huenda hamjui mlitendalo.Namshukuru mtoa mada...kwani ananikumbusha siku Ben Mkapa, Rais wetu mpendwa wa awamu ya tatu alipokuwa anazindua Chuo Kikuu Cha Waislamu Cha Morogoro (itakumbukwa kwamba yale majengo yaliyotolewa kwa ajili ya chuo hiki yalikuwa ni mali ya umma, na lazima tujue kwamba umma ni pamoja na wakristu); maneno kama yaliyotolewa na Radio Imaan, mimi niliyasikia kwa watu waliokuwa karibu yangu....Roho iliniuma sana. Nanukuu "huyu kafiri leo ndio anakumbuka kurejesha haki yetu...makafiri waliotudhurumu tangu enzi za Nyerere".............Iliniuma sana. RIP Mwl. Nyerere..............................Jamani tukumbuke huenda MUNGU hayuko kama tunavyomfikiria, inawezekana YEYE...si MKRISTU wala MUISLAM...bali dini yake ni WEMA na UPENDO. Hakuna haja ya kuanzisha chuki...ni lazima tupendane kama wanadamu....na pia tufanye kazi kwa bidiii...tuache imani potofu.
 
Wakristo ni kweli wanapendelewa. Nashukuru kuona kuna Redio ambayo inatetea maslahi ya Waislamu. Good Job Redio Imaan
 
wana jf kwa hl cjawaunga mkono.aliecklsha redio iman hkfwatlia mjadala wote.mashee walitoa hoja nyng kthbtsha ukwl huo,great thnkers hawakurupuki
 
mimi naomba tume ya vyombo vya habari iifungie hii radio,leo nimeisikiliza ni hatari sana wanachochea chuki kwa maksudi na wanasema jihad ndo haki yao muuislam akifa akitetea uislam anaenda peponi,jamani serikali ipo wapi?
 
Sasa wewe unataka Waislamu wasitetee maslahi yao? mbona redio za injili zinahubiri mambo ya chuki dhidi ya Uislamu hupigi kelele? Ebu ondoa upuuzi wako hapa.
 
Jamani hawa wenzetu wenye mawazo hayo, haijulikani ni wa dini gani lakini ni dhahiri ni wachochezi wasiopenda amani, kwanza wapuuzeni. Siyo kwamba wana mawazo finyu naamini wanajua uwongo wa matamshi yao ila iwe hivyo kwa kutekeleza lengo lao na pengine ufinyu wao ni katika kutumia mbinu hii. Tatizo langu wao hutoa tu 'statements' ambazo hata wanapoulizwa hawajibu kwa hoja kutusaidia kuwaelewa ili tuwe pamoja. Enzi za zamani watu waliamini hakuna uwongo katika kila kilichosikilizwa redioni au kusomwa gazetini lakini leo hii sivyo pengine kwa wachache sana vijijini. Leo hii ukitangaza uwongo hadharani ni kujiaibisha hadharani tu na kwahiyo inahitaji asiye na akili timamu kufanya hivyo bila kuwa na hofu ya aibu. Kwahiyo, kwanza Waislamu na Wakristu wote na wa dini zingine tuwapuuze ile tuelekeze akili na nguvu yetu kwenye kumtukuza Mungu na Maendeleo yetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom