Tundu Lissu: Samia ni Malkia mwenye kauli tamu

Umpeñde, usimpende, Lissu tayari ameingia kwenye historia. Sisahaugi alichokifanya tarime miaka ya nyuma. Bila ajenda za kisiasa, bila malipo, aliwatoa magerezani zaidi ya watu 400 waliobambikizwa kesi mpaka za mauaji, kisa wanapinga vitendo vya unyanyasaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu. Haya madhambi yalifanyika kwa msaada wa viongozi wa serikali ya ccm, enzi za Mkapa, Magufuli akiwa waziri.

Katika siasa zake, ni mtu anayejitoa tena kwa hamasa kubwa, bila kuangalia mafao binafsi.

Wakati wa uchaguzi uliovurugwa mwaka 2020, alipata sapoti ya Malaki kwa Malaki ya watanzania
Unauwezo mdogo Sana wa kufikiri, aliyekwambia huyo uliyemtaja ndiye mbeligiji ni Nani??
 
Hafai, Lisu hafai! Amwache mama yetu atuongoze kwa amani!! Yeye anakula vya kunyonga alivyovilipia kwa gharama ya kuuza uhuru wake kwa mabeberu!!
Hata ikitokea viongozi wetu wakakosea, Lisu hana moral authority ya kuwakosoa!! Kama Lisu ana ubavu awakosoe mabeberu tuone!
Mabeberu ni nani hao? Wanaishi nchi gani?
 
Imani niliyokuwa nayo kwa huyo Malikia imeshatoweka. Hana jipya zaidi ya kudemka demka. Bila kumuendesha puta huyu siioni Katiba mpya wala Tume huru ya uchaguzi.
Leo anasema hakuna hela tufunge mikanda kesho anagawa mibenzi. Malikia apunguze spidi hii sio 1987.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Unauwezo mdogo Sana wa kufikiri, aliyekwambia huyo uliyemtaja ndiye mbeligiji ni Nani??
Sawa mimi nina uwezo mdogo wa kufikiri. Hapa tunamuongelea Lissu aliyeko Ubelgiji. Kwa hiyo mbelgiji usiyempenda ni nani?
 
Lissu in a way ni nembo ya Chadema, ukizingatia aliwakilisha chama hicho Kwenye uchaguzi uliopita. Na alipata kuungwa mkono na baadhi ya wapiga kura, bahati haikuwa yake kwani kura zilipelea.

Pia ni mwanasheria kwa 'usomi' wake. Binafsi naamini mwanasheria mzuri na msomi hupima kauli zake hasa anapokuwa kwenye maeneo anapotarajiwa kauli zake kutumika kama kumbukumbu rejea kwa umma.

Kwa kuzingatia hoja mbili hapo juu. Binafsi nadhani hajajitendea haki yeye kama mwanasheria na muhimiza matumizi ya utawala wa sheria na hajawatendea haki Chadema kwa kuhimiza matumizi ya nguvu bila kutumia taratibu tulizojiwekea za kisheria katika clip iliyowekwa na mleta mada.

Hii ndiyo imenifanya nihitimishe kwa kusema, Lissu bado hajawa stable Kisiasa hivyo itakuwa ni hujuma kwa nchi ya Tanzania kumuamini "mtanzania" mwenzetu.

Kwa hiyo, Mkuu, pima upya uungaji mkono wako kwa "mtanzania" mwenzetu huyu.
Mkuu Ujamuelewa au Umemuelewa Lisu au pia utakuwa unafanya kusudi kupotosha japo unaonekana Kama unaimiza sheria ifuatwe. Alichomaanisha Lisu Ni kuwa mahakama na mwakili pekee hawawezi kufanya haki ikapatikana bila watu wenyewe kuwa na nia ya kutaka haki itendeke. Nikupe mfano mdogo tu.mtu anaweza kufungwa kwa kuonewa tu. Utosikia mahakama Wala wakili kupinga huo uonezi kwa kukata rufaa na mtu anaendelea kusota gerezani.sasa hawa walio nje pamoja na mfungwa mwenyewe ndiyo wapinge kuonewa kwa mtu na kuhamasisha kukatwa kwa rufaa ili yule aliyefungwa apate haki yake.Ndicho Alishomaanisha Lisu ni wananchi kuwa na ile kiu ya kukaa kuonea na kutaka kutendeka kwa haki ili kusukuma wanaosimamia haki kuona umuhimu wa kutenda Haki. Maana hata hakuna wakili atakuruluka kukutetea wakati wewe mwenyewe hauna kiu ya kupinga uonezi uliofanyiwa na hiyo mahakama iliyokufunga kwa uonezi
 
Mheshimiwa Lissu ana hoja za msingi sana,nafikiri vyama vya siasa na asasi za kiraia zina wajibu mkubwa kupigania mapungufu yote katika katiba yetu.
Sio vyama vya siasa na asasi za kiraia pekee, hata sisi raia wa kawaida tuna wajibu. Kwa kutumia mitandao na kila aina ya fursa ya kuwasilisha maoni na taarifa ndipo kelele itakuwa kubwa zaidi
Mf. bila watu kuvamia maduka na kuvunja na kufanya fujo kubwa kule Minnesota ishu ya black lives matter ingekuwa ni ndoto za abunuwasi
 
Hana jipya kama mwendazake nchi imeshamshinda hata kabla ya miezi miwili tangu aapishwe.
Leo anasema hakuna hela tufunge mikanda kesho anagawa mibenzi. Malikia apunguze spidi hii sio 1987.
 
Tatizo la watanzania wanafikiri jukumu la kupigania haki za kikatiba na sheria kandamizi ni wa Mh. Mbowe na Lissu pamoja na CDM yao.
 
Back
Top Bottom