Tundu Lissu kwenye spotlight: Unaikumbuka kesi ya Rais Magufuli? Clip yake haitaji "Rais Samia". Inataja "Rais" na "mama" tu

Uzima Tele

JF-Expert Member
Jan 20, 2023
1,101
2,344
Ukisikiliza ile clip inayodaiwa na Nape kuwa Tundu Lissu kamtukana Rais na ghafla kwa kufikiri ni kosa, DCI Kingai kamwita Tundu Lissu ili amhoji na bila shaka ikiwezekana afungulie mashitaka, basi utagundua mambo kadhaa kuonesha kuwa walioindaa wana akili sana na kina Nape na Kingai bila kutumia akili wanataka kuingia mkenge ili kulipa milage suala la mkataba wa bandari kusikika zaidi na zaidi.

Na bila shaka unaweza kuona tu kuwa, kesi hiyo itakuwa aidha kosa la uchochezi au defamation of character au yote mawili.

HERE ARE THE SOME FACT CHECKS ZA HIYO CLIP

1. Ukisikiliza ile clip vizuri, utagundua kuwa mazungumzo hayo yalikuwa katika mtindo wa mahojiano yaani maswali na majibu. Kuna aliyekuwa anauliza swali/maswali na kisha Tundu Lissu kutoa majibu ya maswali hayo.

2. Producer wa clip ya mazungumzo hayo ame - mute sauti ya muuliza maswali kiasi cha msikilizaji asijue swali lilikuwaje. Sauti inayosikika ni ya mjibu maswali tu - Tundu Lissu. Bila shaka ni walikubaliano hivyo.

3. Kwenye clip hiyo, Tundu Lissu hamtaji Rais kwa jina. Kinachosika ni maneno mawili "Rais" na "mama". Na ofcoz hataji ni Rais wa wapi au wa taasisi gani. Na hataji mama fulani kwa jina specific. Maana tuna Marais wengi kama Rais wa TFF, TLS nk nk. Na tuna kina mama wengi akiwemo mama yake mwenyewe Tundu Lissu..

Kilichomwibua Nape na Kisha DCI Kingai bila shaka ni kuoanisha kilichozungumzwa na Tundu Lissu na kutamkwa kwa maneno "Rais" na "mama" na mjadala mkali unaoendelea sasa hapa nchini wa mkataba wa kuuza au kugawa bure kwa bandari zote za Tanganyika kwa waarabu wa Dubai kulikofanywa moja kwa moja na Rais Samia Suluhu Hassan (ambaye ni mama pia) na Waziri wake Prof Mbarawa - hawa wote ni Wazanzibari na wamesaini mkataba wa kugawa bure mali za Tanganyika kwa waarabu..!!

4. Hii itukumbushe huko nyuma wakati wa utawala wa hayati Rais Magufuli ambapo TL aliwahi kufunguliwa kesi tata ya dizaini hii hii akidaiwa kumtukana au kumkashifu mtu anayeitwa JPM.

Kesi hii iliishiaga hewani kwa sababu mshitakiwa alimtaka huyo mtu anayeitwa JPM aje mahakamani aseme ni kwa namna gani ameathiriwa na maneno yake. Hakutokea ama walioshitaki walishindwa kumleta maana haikujulikana wamlete JPM yupi!!

Na sasa Je, ikitokea Kingai kapeleka kesi mahakamani, atampeleka Rais au mama yupi mahakamani ili aeleze namna alivyoathiriwa na kauli ya TL..??

Haaa haa haa😂😂😂😂. Patamu sana hapo...!!!

5. Naona na utawala huu wa Rais Samia Suluhu Hassan unafuata njia ileile ya hayati Rais Magufuli na kwa mtu yule yule.

Je safari hii watashinda? Tusubiri huyu mwamba (Tundu Lissu) arudi toka safari yake huko ughaibuni ili akabiliane na Kingai kwanza....
 
Nchi yangu Tanzania ni ya ajabu Sana yaani mabingwa na wataalamu walo bobea kwenye sekta mbalimbali za kitaaluma wanashambuliwa na hata kumalizwa kabisa.

Ila mbumbumbu wengi ndo washauri wa viongozi wetu na baadhi wanatumwa hadi abroad kuisemea Nchi.

Ndiyo maana Donald Trump aliamua kutueleza ukweli !!
 
Lissu ni akili kubwa huwezi kumlinganisha na hawa wajinga

Angekuwa akili kubwa asingekubali kuongozwa na Freeman Mbowe miaka yoote hiyo wewe.

Tokea chama kiangukie mikonon mwa yule mchaga amegoma moja kwa moja kukuiachia na anashangaza sana anavyoota ndoto za mchana kuwa anaweza shika dola ya nchi hiii na watu vichaa kama tundu lisu.
 
Nchi yangu Tanzania ni ya ajabu Sana yaani mabingwa na wataalamu walo bobea kwenye sekta mbalimbali za kitaaluma wanashambuliwa na hata k !!

Sasa lisu zaid ya kazi ya siasa tueleze amebobea kwenye kitu gani hasa, hiyo sheria wabobezi wapo wengi nchi hii kuliko hata yeye.

Ubobezi wa kupiga kelele kwenye majukwaa ya siasa na bungeni huku akipigania tumbo ndiyo tuite ubobezi?
 
Huwenda Nchi yangu, watu wake wameathiriwa saana na ugonjwa wa kusahau, si vijana wala wazee

Labda tumuombe mheshimiwa Nape, asahihishe kauli yake kusema, Akitukanwa baba, wametukanwa mababa wote, hasa inapokuwa anatukanwa Rais

Yapo matusi yaliyokuwa akitukanwa hayati JPM, yaliwaumiza watanzania wengi na mimi nikiwemo, matusi yale yalienda mbaali sana hata kutaka kuitenga jamii ya wasukuma kwamba, ni watu wa hovyo na washamba washamba, ni kwa sababu tu Rais aliyekuwa akiongoza nchi alikuwa ni wa jamii hiyo!

Huko ni kupanda mbegu ya hovyo sana katika jamii yetu, na huwenda hata haya yanayotokea leo, chanzo chake ni hiyo mbegu iliyopandwa na wana ccm wenyewe!

Ifike wakati, kama taifa, tuseme kuna mahali tulikosea, kunyamazia dhihaka matusi na kejeli kubwa kabisa zilizokuwa zikimlenga Magufuli na jamii yake

Na kiongozi yeyote anaposimama kukemea udhalilishaji wa viongozi wetu, kwa kuwa kumbe ccm wameona ubaya wakutukanwa kwa viongozi, basi asisemee hili la leo peke yake, bali aanze kukemea yote yaliyokuwa yakiwadhalilisha viongozi wote wa kipindi cha nyuma miongoni mwao akiwapo hayati JPM

Niulize,

Wakati Hayati JPM akidhalilishwa, Nape hakuwepo? Aliwahi kukemea?

Ccm, hiyo dhambi itawatafuna kwa kushindwa kuikemea

Mtasweka watu rumande na magereza yatajaa msijue chanzo ni ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom