Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,294
- 9,726
Ndugu zangu watanzania,
Wafanyabiashara wengi sana wameendelea kuonyesha msimamo wao wa kuendelea kuiunga mkono serikali ya Rais Samia kutokana na usikivu wake katika kutatua kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uendeshaji wa biashara zao. Wanasema kuwa serikali wakati na muda wote imetoa nafasi ya majadiliano na mazungumzo kufanyika pale panapojitokeza changamoto na wakati wote wamekuwa wakisikilizwa na kupata ufumbuzi.
Wanasema Tundu lissu na chadema yake wakati wote wamekuwa Ni watu wa kupandikiza chuki na migogoro kwa wafanyabiashara ili wafanye migomo, wametolea mfano kauli ya Tundu lissu aliyoitoa Mkoani kigoma miezi michache iliyopita akiwahamasisha wafanyabiashara kufanya migomo Jambo ambalo hata hivyo halikufanikiwa kutokana na wafanyabiashara kumdharau na kumpuuza hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa watu wanafahamu kuwa lissu na chadema yake ni matapeli, wababaishaji,wasio na misimamo, wanafiki, watu wa ndimi mbili na wasio na uzalendo wa Aina yoyote Ile kwa Taifa letu.
Wafanyabiashara wanasema kuwa kwa Sasa serikali ya Rais Samia imeweka mazingira mazuri ya kibiashara na wanafanya biashara kwa amani na utulivu pasipo bughudha Wala kero, wanasema kuwa kwa Sasa wanajiona fahari na huru sana kufanyia biashara Tanzania na kulipa Kodi kwa hiyari, wanasema wanakadiriwa Kodi kwa haki kabisa na penye shida wanasikilizwa kupitia meza ya mazungumzo.
Wanasema hawawezi kukubali kwa Sasa kutumika hovyo Kama walivyokuwa wanatumiwa miaka kadhaa iliyopita ,wanasema wapo bega kwa bega na mh Rais na wanaendelea kumuunga mkono katika juhudi zake za kuinua uchumi wa Taifa letu.
Wanasema kwa Sasa Hakuna mwenye Akili Timamu atakayeweza kuiunga mkono chadema chama ambacho kimefirisika kisera na kiajenda, lchama kilicho kosa Dira na muelekeo, chama ambacho hakina Safu ya uongozi yenye kuleta matumaini kwa watu na chenye kutanguliza mbele maslahi yao binafsi.
Rai yangu kwa akina lissu na chadema yao ni kuwa wakati Ni ukuta, kwa Sasa wapo nje ya wakati, Hakuna wa kuwaunga mkono , watanzania wa leo hawadanganyiki Wala kupotoshwa, kwa Sasa chadema wakae kwa kutulia kuangalia nchi inavyo paa kiuchumi chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia.
Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
0742-676627.
Pia soma
- Tundu Lissu aonekana Kariakoo, atangaza opereshani rejesha Bandari za Tanganyika kutoka kwa Sultan wa Dubai imeanza