Tundu Lissu: Samia ni Malkia mwenye kauli tamu

Huyu malkia uchwara na ushungi wake kaingia ofisini kwa mbwembwe kumbe sifuri tupu!

Anawalaghai watanzania kwa maneno matupu bila utekelezaji!

Mara ooh ati kodi ni za dhulma!

Kama anajua kuwa kodi ni za dhulma mbona hatuoni michakato ya kufuta sheria mbaya za kodi?

Huyu bibi kizee hakuna kitu! Ni tapeli mzoefu.
Kaaazi kwelikweli
 
Lissu hajawahi kukosea anapombatiza mtu jina! Alifanya hivyo kwa Dikteta Uchwara, na sasa anafanya hivyo hivyo kwa Malkia mwenye kauli tamu.
Mimi sitakaa nimuamini kwa sababu mpaka leo anataka nini na mwendazake keshakwenda
bora hata Padri Slaa na Mch Mtikila RIP waieleweka na tukawasukuma kwenye magari
ni hicho kiti cha Malkia bado anakitaka?
 
Lissu hajielewi anajilazimisha kumkosoa Mama Samia ili aendelee kukaa ubelgiji
Hafai, Lisu hafai! Amwache mama yetu atuongoze kwa amani!! Yeye anakula vya kunyonga alivyovilipia kwa gharama ya kuuza uhuru wake kwa mabeberu!!
Hata ikitokea viongozi wetu wakakosea, Lisu hana moral authority ya kuwakosoa!! Kama Lisu ana ubavu awakosoe mabeberu tuone!
 
Mbeligiji...?? Simpendi
Umpeñde, usimpende, Lissu tayari ameingia kwenye historia. Sisahaugi alichokifanya tarime miaka ya nyuma. Bila ajenda za kisiasa, bila malipo, aliwatoa magerezani zaidi ya watu 400 waliobambikizwa kesi mpaka za mauaji, kisa wanapinga vitendo vya unyanyasaji wa kampuni ya uchimbaji dhahabu. Haya madhambi yalifanyika kwa msaada wa viongozi wa serikali ya ccm, enzi za Mkapa, Magufuli akiwa waziri.

Katika siasa zake, ni mtu anayejitoa tena kwa hamasa kubwa, bila kuangalia mafao binafsi.

Wakati wa uchaguzi uliovurugwa mwaka 2020, alipata sapoti ya Malaki kwa Malaki ya watanzania
 
unprecedented intelligent, convincing, charistmatic politician. unaweza kuona anavyotengeneza hoj. Siyo ile hotuba ya Mbowe ya kujisahahu kuwa yeye ni opposition.
Tunayo haba ya watu kama Lisu.

don‘t be mistaken, a good politician doesn’t mean he can be an implementer,
JPM alikuwa mfanyakazi lakini alikuwa hana Lisuism. Mama angejua angejaza hilo shimo, we don’t want cheap talk, it is about lives
Ni kweli Lissu ana uwezo mkubwa kiakili na kitaaluma. Pia ni mzungumzaji mzuri sana. Lakini unapomlinganisha na Mbowe, kumbuka hawa ni watu wawili wenye haiba tofauti. Lissu naweza kumuita hardliner, radical, wakati Mbowe ni Dove. Wote wana manufaa yao na mapungufu yao.

Enzi za Kikwete, Mbowe aliexcel zaidi na mikakati ya m4c na opereseheni kadhaa. Hapa, Lissu aliwahi kutoa kauli, kwenye kipindi cha Mkasi, kwamba wala hana interest na urais, kwamba anapendelea zaidi minyukano ya Bungeni.

Come Magufuli, Mbowe akarudi chini, Lissu akang'ara. Alikuwa mtanzania pekee nchi nzima aliyethubutu kumchana live Rais Magufuli.

It will be interesting kuona Lissu na Mbowe watakavyo play out kipindi hiki cha Malkia mwenye sauti tamu.
 
Hafai, Lisu hafai! Amwache mama yetu atuongoze kwa amani!! Yeye anakula vya kunyonga alivyovilipia kwa gharama ya kuuza uhuru wake kwa mabeberu!!
Hata ikitokea viongozi wetu wakakosea, Lisu hana moral authority ya kuwakosoa!! Kama Lisu ana ubavu awakosoe mabeberu tuone!
Hii lugha ya Mabeberu ilizikwa Chato pamoja na hayati Magufuli. Malkia wetu wala hana hizo vibes.

Rais anahitaji zaidi criticism kuliko sifa. Magu enzi zake mlimsifu na kumwabudu. Leo walewale, bila aibu, mnamkejeli.
 
Nimefuata ushauri wako nimeweka pembeni hisia.

Kwa maelezo yake ya mwisho kwenye clip hii, Lissu si muumini tena wa utawala wa sheria. Anahimiza watu wadai haki zao mitaani kwa nguvu. Kwa kuonyesha msisitizo wa hoja yake hiyo ya hatari ametumia mfano wa mwanaharakati Martin Luther Jr wa Marekani aliyewaandikia wenzake barua akiwa gerezani kuwa watafute haki yao wenyewe wasisubiri busara za Mahakama ya nchi hiyo.

Kwa maelezo hayo, ni kweli Lissu hajawa stable kisiasa hivyo bado nadhani itakuwa hujuma kwa nchi kumuamini "mtanzania" mwenzetu huyu!
Umemuelewa vizuri kabsa,halafu aje kujifanya ni muumini wa demokrasia, kiufupi hatufuati upuuzi huo.
 
Back
Top Bottom