Tundu Lissu: Kufuta kesi ya Mbowe sio kuingilia Uhuru wa Mahakama

Mahakama ikikuhukumu miaka 10 na ukakata rufaa,je kipindi unasubiri rufaa ianze kusikilizwa utakuwa nje kama raia huru au utaendelea kutumikia hukumu yako ya miaka 10 mpaka hapo rufaa yako itakapohitimishwa?Same na wale wabunge 19 maadamu wamefukuzwa uanachama hawapaswi kuwepo bungeni mpaka pale rufaa zao zitakapowarejeshea uanachama na chama kuridhia wakawe wawakilishi wake.
Kuhusu suala la Mbowe kuiachia na kuamini mahakama itafanya Haki,Unataka kutuambia mahakama hizi hazijawahi kuhukumu watu kwa kuonea?Rejea hukumu ya Sugu na Mwasonga mpaka mahakama ya rufaa iliposema walionewa
Bunge halina taarifa ya kufukuzwa kwao. Zimgatieni utaratibu wa kushughulika na wanachama wenu
 
Huyo Zitto mnayemtetea kiasi hicho ni nani katika nchi hii?Kati ya Zitto na Lissu nani kiongozi wa CDM?Je,baada ya Zitto kudaiwa kumwombea msamaha Mh.Mbowe,nini kilibadilika kuhusu kesi ya Mbowe?
Utetezi wa ccm kuhusu CDM kumpinga Zitto msingi wake nini?
CCM waliishazoea na kunogewa na ushetani wa kubambikia watu mashitaka ili kuwanyamazisha, kama walivyorithishwa na Babeli mkuu.
Zito alijaribu bila mafanikio, kulitumia hilo kwa faida yake.
 
Sasa wale pingapinga FC mliompinga zitto kuomba kwa rais gaidi amsamehewe njooni mpige makofi kwa tundu tafadhali.
Shida hapa ni uelewa wako kuwa "very low" kiasi kwamba huwezi kutofautisha kinachozungumzwa na Lissu na kinachozungumzwa na Zitto!
 
Kama kuna kitu kinasikitisha kama mtanzania/mtanganyika ni hii hali ya kuacha hii "brain" ya Lissu ipotelee hewani badala ya kutumika kuijenga nchi yetu. Watu aina ya Lissu wanazaliwa mara chache sana. Hii ni "asset" kwa nchi.

Angekuwa kwenye nchi za wenzetu zisizo na ubaguzi wa kijinga wa kiitikadi zingemtumia vizuri pamoja na kuwa na itikadi tofauti na watawala. Ndio maana kila siku huwa napingana na watu wanaomsema vibaya spika wa zamani mama Makinda kwa sababu licha ya mapungufu yake kidogo kama spika lakini alikuwa anatumia watu wenye akili kutanzua mambo tata bungeni.

Makinda alikuwa anawatumia akili za akina Lisu, Chenge (pamoja na makando kando yake), na wengineo. Sasa hivi kukiwa na mambo tata bungeni watu wanotumika kutatua naona hata aibu kuwataja hapa.
Msukuma na Kibajaj ndio watu mashuhuri kwenye vikao vya CCM.
 
Sasa wale pingapinga FC mliompinga zitto kuomba kwa rais gaidi amsamehewe njooni mpige makofi kwa tundu tafadhali.
Lissu hakuomba hurum ya rais. hoja yake hii kesi haina maslahi kwa taifa au yeyote. Hoja ya Zitto ilikuwa huruma, yaani Mbowe ahurumiwe japo mkosajii. Mbona vichwa vigumu ahh
 
Lissu hakuomba hurum ya rais. hoja yake hii kesi haina maslahi kwa taifa au yeyote. Hoja ya Zitto ilikuwa huruma, yaani Mbowe ahurumiwe japo mkosajii. Mbona vichwa vigumu ahh
kuombqa kesi ifutwe ni kuomba huruma kwa nini asiombe hukumu itolewe kama hana kosa si atatoka tu?
 
Bunge halina taarifa ya kufukuzwa kwao. Zimgatieni utaratibu wa kushughulika na wanachama wenu
Ndugu sio kweli,
Ndugai ndie 'kwa maslahi yao' aliyeanza kwa kukataa kutambua ofisi ya bunge kupokea barua/mawasiliano ya kutowatambua COVID 19, kutoka CHADEMA hata baada ya kuonyeshwa nakala ya hati ya makabidhiano.
Spika wa sasa anajitoa fahamu tu ili kujisafisha kwa kuwa 'yule' Babeli Mkuu aliyekuwa anawapa vichwa kwenda zake. Lakini ni wazi kuwa alikuwa pamoja na Ndugai katika maujinga hayo hadi kufikia hatua ya kumuwahisha ili kumwapisha 'mmoja' aliyetolewa rumande usiku usiku.
Mahera nae alifanya hivyohivyo zaidi ya kuwa nae mpaka sasa kila akiulizwa hataki kuonyesha form ya makadhiano ya uteuzi wa majina yanayodaiwa yalitumwa na CHADEMA.
 
Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA nchini Tanzania Tundu Lissu anayeishi uhamishoni Ubelgiji ameeleza azma yake ya kurudi nchini Tanzania wakati wowote.

Lissu alisema hayo katika mahojiano maalum na VOA baada ya kukutana na rais wa Tanzania Samia suluhu mjini Brussels Jumanne.

Akizungumzia dai lake la kutaka kesi ya mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe ifutwe, Lissu amesema jambo hilo sio kuingilia uhuru wa Mahakama na kwamba kesi hiyo “haina maslahi yoyote na afanye kama alivyofanya kuhusiana na kesi ya mashekhe wa Uamsho wa Zanzibar ambao walifutiwa mashitaka baada ya kukaa gerezani miaka 9 hakuna cha kuingilia mhimili wowote hapa”

Akisisitiza kwamba hajamwambia Rais aongee na Jaji bali mwendesha mashitaka ambaye ni mteule wa Rais na anafanya kazi kama sehemu ya utawala sio sehemu ya Mahakama.

Pia kiongozi huyo wa upinzani na mgombea Urais mwaka 2020 amemwambia Rais kuhusu suala la Serikali kutaka kuwafukuza kwa nguvu wananchi wa wilaya ya Ngorongoro kutoka eneo la mamlaka ya hifadhi kuwa ni jambo la hatari na linaweza kuchafua nchi na akasema Rais amemwambia amelizuia.

Lissu pia amegusia Uhuru wa vyama vya siasa kufanya kazi akisema amemweleza Rais Samia kuhusu zuio aliloliita haramu la vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na maandamano na madai ya hitaji la katiba mpya nchini humo na mfumo mpya wa uchaguzi.

Itakumbukuwa mbunge huyo wa zamani na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema mwaka 2020 alinusurika katika shambulizi baya la risasi na watu wasiojulikana mwaka 2017 na amemtaka rais ahakikishe anatendewa haki kwa mambo ambayo alinyimwa baada ya shambulizi hilo, mwaka 2019 alivuliwa ubunge na mpaka sasa gari yake iko mikononi mwa Polisi.

Akizungumzia kuhusu sakata la Spika wa bunge Dr.Tulia Ackson juu ya wabunge wa CHADEMA amemwambia Rais kwamba spika Ackson asiwafundishe CHADEMA namna ya kuendesha chama chao yeye anatakiwa afanyie kazi maamuzi ya chama kama wanavyompa taarifa na walishamwambia hao si wabunge wa CHADEMA na yeye kuwaambia mpaka mchakato ukamilike “hayo hayamhusu kabisa Spika huyo na hata kama haujakamilika hawa sio wanachama wa Chadema na kwa maana hiyo kama sio wanachama wa Chadema hawatakiwi kuwa bungeni hata kwa siku moja zaidi” alisisitiza Lissu.

Lissu amesema Rais Samia amewamwambia amemsikia na atayafanyia kazi hayo madai yake.

Lissu pia amesema kuna mazuri yananayofanywa na utawala wa Rais Samia, akisema hasa kurejesha uhusiano na mataifa ya nje na kurejesha mapambano dhidi ya Covid lakini angependa kuona mengi zaidi kama kubadilisha sheria na taratibu ambazo zimeumiza watu wengi nchini humo.

Lakini anasema kwa ujumla hali ya jumla imebadilika tangu aingie madarakani lakini hali hiyo peke haitoshi. Lakini atamuuunga mkono ikiwa atakubali kwamba nchi inahitaji uponyaji aiongoze kuiponya nchi hiyo aliongeza.

VOA Swahili
Vipi kuhusu watuhumiwa wengine ? Je, kuna usawa kisheria baina ya mwanasiasa na mwananchi wa kawaida?
 
Mimi naona tofauti kati ya Zito na Lissu:
Zito alimwomba rais amsamehe Mbowe, Lissu amemtaka rais (kupitia dpp) amfutie Mbowe mashtaka (ambayo hayana faida kwa ccm, Chadema Wala taifa).
Anamtaka yeye Kama Nani, nadhani ni busara kuomba kuliko kutaka, zito was right, sema kwa Kua alikua wa Kwanza kuliwasilisha kwa raisi, mliona aibu kawazidi kete.
Yani chadema tangu mbowe awekwe ndani chama kimepoteza uelekeo. Hakuna kinachofanyika Hadi mbowe atoke
 
CCM waliishazoea na kunogewa na ushetani wa kubambikia watu mashitaka ili kuwanyamazisha, kama walivyorithishwa na Babeli mkuu.
Zito alijaribu bila mafanikio, kulitumia hilo kwa faida yake.
Siyo kwa faida yake bali ya CCM ili waonekane wana huruma.Zitto ni daraja tu,alitumwa.
 
Itakumbukuwa mbunge huyo wa zamani na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema mwaka 2020 alinusurika katika shambulizi baya la risasi na watu wasiojulikana mwaka 2017 na amemtaka rais ahakikishe anatendewa haki kwa mambo ambayo alinyimwa baada ya shambulizi hilo, mwaka 2019 alivuliwa ubunge na mpaka sasa gari yake iko mikononi mwa Polisi.
Walikuwa hawajulikani lakini kwa sasa wanajulikana mkuu, wengine wanaonekana LIVE ktk kesi ya Mbowe na mwingine 'keshanasa' huko Mtwara!
 
Mimi naona tofauti kati ya Zito na Lissu:
Zito alimwomba rais amsamehe Mbowe, Lissu amemtaka rais (kupitia dpp) amfutie Mbowe mashtaka (ambayo hayana faida kwa ccm, Chadema Wala taifa).
Lissu hana mamlaka ya kumwambia rais nini cha kufanya kwahiyo tafsiri sahihi hapo ni kumuomba rais amfutie kesi Mbowe.
 
Matokeo ya wanachopigania ni sawa Mbowe atakua huru. Ila zitto anaomwombea msamaha while Lissu anataka kesi ifutwe. Maana yake kwa mujibu wa Zitto Mbowe ana hatia, while Lissu anaona Mbowe Hana hatia.
Samia halazimiki kufuata alichoambiwa na Lissu hivyo maamuzi ni yake amuachie Mbowe au asimuachie. Na wakimuachia itakuwa na maana ya kumsamehe na si kwamba rais kafuata alichoambiwa na rais.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom