TUNDU LISSU 'AITEKA MIOYO' YA WATUMISHI WA UMMA NCHINI TANZANIA!
Idara yetu ya 'wapiga doria mitandaoni' yabaini kuwa Watumishi wa Umma ndio wanaoongoza kufuatilia kesi ya Lissu. Aidha, Lissu anaungwa mkono zaidi na watumishi wa umma, idadi hiyo imepanda zaidi tangu Lissu aieleze Mahakama ya Kisutu kuwa ananyanyaswa!
Maelezo ya Lissu mahakamani yaliwafumbua watu wengi ambao sasa wanajua kuwa Lissu anaonewa kwa sababu hoja zake na misimamo yake vinakubalika kwa wananchi walio wengi! Kundi hili la watumishi wa umma linamuunga mkono kwa siri kutokana na mazingira yao ya kazi lakini hupitia kurasa za watu ambao wote mitandaoni ambao linajua kuwa hutoa taarifa za uhakika na haraka kuhusu Lissu.
Watumishi wa umma wanaomuunga mkono zaidi Lissu ni walimu, Polisi, Idara ya Usalama (hawa ndio wengi zaidi), wahadhiri, wanajeshi, uhamiaji na madereva wa viongozi! Hata hivyo, idara yetu imebaini kuwa 'kundi la watu ambao hulipwa pesa miongoni mwa watu wa idara, sio watu wa Idara yenyewe kwani wamepenyezwa maalumu kushughulikia wakosoaji, wanasiasa na wanaharakati! Na hili ndio kundi la watekaji!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 27 Juni 2025; saa 4:17 asubuhi