Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Anaandika Wakili Paul Kisabo

Leo, Julai 27, 2026, nimemtembelea Mhe. Tundu Lissu Tundu Antiphas Lissu Gereza la Ukonga. Mbali na kunipa maelekezo kuhusu maandalizi ya nyaraka za submissions katika kesi yetu, kufuatia kukamilika kwa maswali ya dodoso Julai 23, 2026, Mhe. Lissu amesisitiza kwamba watu wote waliokamatwa na kufunguliwa mashitaka ya ugaidi wanapaswa kupata uwakilishi wa kisheria na kutembelewa mara kwa mara magerezani ili kuwafariji, kufuatilia ustawi wao na kujua maendeleo ya kesi zao.

Amenieleza pia kwamba hakuna hata mmoja anayepaswa kusahaulika, wote wanapaswa kutetewa na mawakili.

Nilienda na Wakili Deogratias Mahinyila Deogratius Mahinyila lakini hakuruhusiwa kuingia baada ya maafisa wa Magereza kudai kuwa jina lake halipo kwenye orodha ya mawakili wanaoruhusiwa kumwona Mhe. Lissu.

Mhe. Tundu Lissu anawasalimieni sana Watanzania. Pokeeni salamu zake.
1785200352634.jpg
 
Leo majira ya mchana maamuzi ya maombi ya marejeo ( Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu Antipas Lissu, katika mahakama ya rufaa yamesoma na Lissu ameshinda.

Sasa ni mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia kwenye kesi ya uhaini, au waifute na kumwachia huru Tundu Antipas Lissu.

Kumbuka hata tukirudi na kuendelea na kesi hii ya uhaini mahakam kuu lakini ushahidi wake muhimu ulishakataliwa na mahakama.
 
MAHAKAMA YA RUFANI YATUPILIA MBALI MAOMBI YA MAREJEO YA DPP KATIKA KESI YA TUNDU LISSU

Mnamo tarehe 18 Februari 2026, Jamhuri iliwasilisha Notisi ya Nyongeza ya Ushahidi (Notice of Additional Substance of Evidence) chini ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), ikikusudia kuwasilisha ushahidi wa ziada kupitia shahidi ACP Amini Mahamba.

Hata hivyo, tarehe 24 Februari 2026, Mahakama Kuu ilitupilia mbali notisi hiyo baada ya kubaini kuwa kifungu hicho hakiruhusu shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi kurejeshwa ili kuwasilisha ushahidi wa ziada. Kufuatia uamuzi huo, tarehe 3 Machi 2026, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu. Maombi hayo yalisikilizwa tarehe 3 Julai 2026.

Leo, tarehe 30 Julai 2026, Mahakama ya Rufani ya Tanzania imetupilia mbali maombi hayo ya marejeo na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu. Mahakama imeeleza kuwa Mahakama Kuu ilitafsiri kwa usahihi kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho hakiruhusu upande wa mashtaka kumrejesha shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi ili kuwasilisha ushahidi wa ziada.

Uamuzi huu unaweka mwongozo muhimu kuhusu tafsiri na matumizi ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na unasisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu za kisheria katika uwasilishaji wa ushahidi wakati wa mwenendo wa kesi za jinai.

Paul Kisabo (Wakili)
Julai 30, 2026
 
Wana JF kuna mahali tulipitiwa na kujisahau.. Tulipaswa kuwa na mada maalum ya Tundu Antipas Lissu.

Mwanasheria nguli, mwanaharakati wa haki za binadamu na sasa mfungwa wa kisiasa wa kesi ya uhaini na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanganyika

Ana historia yake maalum .. Ana mengi mazuri ya kiwango kaifanyia Tanganyika.. TUMUENZI SASA. NI WAKATI WAKEView attachment 3381742
(7,029) Historia fupi ya maisha ya shule ya Tundu Lissu | JamiiForums Historia fupi ya maisha ya shule ya Tundu Lissu
Mwamba anaendelea kutafakari
 
MAHAKAMA YA RUFANI YATUPILIA MBALI MAOMBI YA MAREJEO YA DPP KATIKA KESI YA TUNDU LISSU

Mnamo tarehe 18 Februari 2026, Jamhuri iliwasilisha Notisi ya Nyongeza ya Ushahidi (Notice of Additional Substance of Evidence) chini ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), ikikusudia kuwasilisha ushahidi wa ziada kupitia shahidi ACP Amini Mahamba.

Hata hivyo, tarehe 24 Februari 2026, Mahakama Kuu ilitupilia mbali notisi hiyo baada ya kubaini kuwa kifungu hicho hakiruhusu shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi kurejeshwa ili kuwasilisha ushahidi wa ziada. Kufuatia uamuzi huo, tarehe 3 Machi 2026, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliwasilisha maombi ya marejeo katika Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu. Maombi hayo yalisikilizwa tarehe 3 Julai 2026.

Leo, tarehe 30 Julai 2026, Mahakama ya Rufani ya Tanzania imetupilia mbali maombi hayo ya marejeo na kuthibitisha uamuzi wa Mahakama Kuu. Mahakama imeeleza kuwa Mahakama Kuu ilitafsiri kwa usahihi kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, ambacho hakiruhusu upande wa mashtaka kumrejesha shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi ili kuwasilisha ushahidi wa ziada.

Uamuzi huu unaweka mwongozo muhimu kuhusu tafsiri na matumizi ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na unasisitiza umuhimu wa kuzingatia taratibu za kisheria katika uwasilishaji wa ushahidi wakati wa mwenendo wa kesi za jinai.

Paul Kisabo (Wakili)
Julai 30, 2026
Nakumbuka hii siku LIssu alibishana Sana na Jopo la Mawakili
 
Hivi hii kesi kuu imefikia wapi? Hukumu au mashahidi bado hawajamaliza? Na ile kesi yake dhidi ya bwana jela nayo inaingilia muendelezo wa kesi kuu?
Leo majira ya mchana maamuzi ya maombi ya marejeo ( Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu Antipas Lissu, katika mahakama ya rufaa yamesoma na Lissu ameshinda.

Sasa ni mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia kwenye kesi ya uhaini, au waifute na kumwachia huru Tundu Antipas Lissu.

Kumbuka hata tukirudi na kuendelea na kesi hii ya uhaini mahakam kuu lakini ushahidi wake muhimu ulishakataliwa na mahakama.
 
‼️🚨BREAKING NEWS - TUNDU LISSU FAKE TREASON TRIAL TO RESUME‼️

The High Court in Dar es Salaam has scheduled the hearing of the case of treason no. 19605/2025 facing Tundu Lissu from 10/08/2026 to 07/09/2026.
Note: the Commonwealth deadline of 30 days to resolve Tundu Lissu’s politically motivated trumped up trial expires on August 10,2026 👊🏽

‼️WAMEBANWA‼️
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imepanga kufanya kikao cha kusikiliza
Shauri la Uhaini Na. 19605/2025 linalomkabili Tundu Lissu kuanzia tarehe 10/08/2026 hadi tarehe 07/09/2026.
Zingatia: Siku ya mwisho wameambiwa na Jumuiya ya Madola wapate suluhu ya kumwachia Lissu ni Agosti 10 😁 yaani tunafinya hadi mwisho!
Sasa msitupotezee muda
Mwachieni Lissu #FreeTunduLissuNOW
 
Back
Top Bottom