Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

UPDATES KUTOKA MAHAKAMA KUU DAR ES SALAAM.

Leo Tarehe 20/07/2026 Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es salaam. Kesi Na. 7300/2026 iliyofunguliwa na Mawakili watatu, Paul Kisabo, Nashon Nkungu na Maduhu William baada ya kukumbana na vikwazo wakati wanaenda kumtembelea Mh. Tundu Lissu.

Vikwazo hivyo ni ikiwemo mazungumzo yao kuwa yanasikilizwa na magereza.

Kesi hii imefunguliwa mwezi March, 2026 dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Kamishna Mkuu wa Magereza na Mkuu wa Gereza la Ukonga.

Mh. Tundu Lissu ni sehemu ya wajibu maombi kwenye hii kesi ambapo yeye ni mjibu maombi wa nne katika maombi haya.

Baada ya pande zote kubadilishana nyaraka. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kiliomba kuunganishwa kwenye kesi hii kama interested party kwasababu waliofungua maombi haya ni wanachama wa TLS. Mahakama iliwakubalia.

Mara baada ya wajibu maombi kuwasilisha kiapo kinzani. Mheshimiwa Lissu aliomba kuwauliza maswali ya Dodoso mawakili waliofungua kesi pamoja na Mkuu wa Gereza la Ukonga.

Mahakama ilimkubalia ombi hilo na leo linaanza zoezi la kuulizwa maswali ya Dodoso kwa Mkuu wa Gereza la Ukonga anaitwa Andrew Shabani Ntamamiro.

Hapa maswali kwa Mkuu wa Gereza la Ukonga tutegemee ataulizwa maswali ya namna anavyotekeleza majukumu yake ikiwemo utaratibu wa mawakili kuingia na kutoka magerezaa na namna ya kuzungumza na wateja wao.

Tutapata nafasi ya kujua kama Wakuu wa Magereza nchini wanajua wajibu wao au hawajui? Wanajua sheria au hawajui sheria. Je nao akili zao zinafanana na maafisa wa jeshi la Polisi katika usimamizi wa sheria.

Muda huu saa tano na dakika 40 maombi haya yataanza kusikilizwa kwa mjibu maombi kuanza kuulizwa hayo maswali ya Dodoso.
 
Namuonea huruma sana huyu Mkuu wa Gereza 😂😂😂
 
Saa nane kamili,Lete update!
 
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA

Part 2.

Anaendelea Mhe. Lissu

Mhe. Lissu: Nenda ukurasa wa 27 angalia defence counsels angalia jina la Kulwa Maduhu na Paul Kisabo kama hayapo?

Wakili Maduhu: Yapo majina ya hao mawakili.

Mhe. Lissu: Ukurasa wa 40 kwenye huo mwenendo wa Kisutu angalia upande wa corum useme kama Paul Kisabo na Kulwa Maduhu.

Wakili Maduhu: Wapo wote wawili.

Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama kuna utaratibu wowote wa kisheria wa unaopaswa kuufuata kumuona mteja?

Wakili Maduhu: Hakuna utaratibu wowote wa kisheria zaidi ya kuonesha kitambulisho tu cha uwakili.

Mhe. Lissu: Haya Maneno ya Bwana jela kuwa sijakutambulisha ni maneno ya bure tu?

Wakili Maduhu: Kabisa maneno ya bure kabisa.

Mhe. Lissu: Unazifahamu kanuni za maadili za mawakili?

Wakili Maduhu: Nazijua ndio.

Mhe. Lissu: Je kwa kanuni hizi wakili anaruhusiwa kumuonesha makubaliano yake na mteja mtu anayeitwa Bwana Jela?

Wakili Maduhu: Duty to confidentiality hairuhusu. Kwahiyo siruhusiwi kabisa kutoa siri za mteja wangu.

Mhe. Lissu: Sasa unasemaje kuhusu hizi habari za Bwana Jela kuwa sijakutambulisha kwake?

Wakili Maduhu: Hizo ni kauli za bure kabisa. Mimi silazimiki kufanya hivyo. Nina miaka 6 ya uwakili kwa sasa huo utaratibu haupo kabisa.

Mhe. Lissu: Nenda Ukurasa wa 41 hadi 43 wa proceedings za Kisutu. Soma Tar. 16/06 sema kama mahakama ya Kisutu haikuandika malalamiko yangu kuhusu mawakili wangu kunyimwa kuniona.

Wakili Maduhu: Ni kweli malalamiko yapo.

Mhe. Lissu: Ni kwamba nilikuwa nazuiwa kuonana na mawakili wangu?

Wakili Maduhu: Kweli yapo hapa

Mhe.Lissu: Kwamba ni kinyume na kanuni za uendeshaji wa magereza?

Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa yapo yote kwenye hizi kurasa za mambo ya Kisutu.

Mhe. Lissu: Pia kuna malalamiko specific kuwa kitendo hicho cha mimi kuninyima nisionane na mawakili wangu ni kinyume na sheria na kanuni za kimataifa?

Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu: Nikalalamika kuwa naishi na wafungwa waliohukumiwa kifo? Na natendewa sawa na watu hao?

Wakili Maduhu: Kweli kabisa ulisema.

Mhe. Lissu: Baada ya hayo nilisema nitajiwakilisha mwenyewe kwasababu sitaki mawakili wangu waje kulaumiwa bure?

Wakili Maduhu: Ni kweli ulisema hivyo na ikawa hivyo.

Mhe. Lissu: Ulipoamua kujiwakilisha mwenyewe nilisema waendelee kunisahuri na kunipa nyaraka wakati kesi inaendelea. Nilisema hivyo?

Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.

Mhe. Lissu: Sasa waeleze toka siku hiyo tar. 16/05/2026 hadi leo mmeendelea kunipa ushauri wa kisheria na kunipa nyaraka Gerezani?

Wakili Maduhu: Ni kweli tumeendelea kufanya kazi hiyo.

Mhe. Lissu: Je una kumbukumbu za kilichotokea Mahakama Kuu kuhusu shauri hilo lilipofika Mahakama kuu niliwaeleza waheshimiwa majaji kuwa nina mawakili wanaonisaidia kwa research na ushauri.

Wakili Maduhu: Ni sahihi ulisema.

Mhe. Lissu: Naomba nimuonyeshe proceedings za Mahakama Kuu. Tuambie from page 4 to 6 wambie majaji kama huo mwenendo unaonesha niliwaambia Majaji wa Mahakama kuu nina mawakili ambao wananisaidia na nikaomba waingizwe kwenye corum.

Wakili Maduhu: Nimeona ndio.

Mhe. Lissu: Na Katuga alipinga ombi langu hilo.

Wakili Maduhu: Ni sahihi naona hapa.

Mhe. Lissu: Mahakama ikasema hatutawaingiza kwenye corum lakini mawakili wako waendelee kukusaidia?

Wakili Maduhu: Naona iko hapa.

Mhe. Lissu: Kwahiyo ni kweli sio tu Kisutu hata Mahakama kuu hii inakutambua wewe na wenzako kama mawakili wangu?

Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.

Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA

Part 3

Anaendelea Mhe. Lissu

Mhe.Lissu: Nenda kwenye supplementary affidavit ya wajibu maombi wa 3 ya Tarehe 12/05 anasema kuwa wewe na Paul Kisabo hampo kwemye orodha ya mawakili niliyowasilisha kwake?

Wakili Maduhu: Ni sahihi.

Mhe. Lissu: Amewasilisha SUPP 1 kwenye supplimentary affidavit na anasema hakuna jina la Kulwa maduhu na Paul Kisabo. Sasa angalia hiyo annexure SUPP 1 na uwaeleze majaji kama maneno yake haya ni ya kweli?

Wakili Maduhu: Kwenye SUPP 1 hayapo.

Mhe. Lissu: Je pamoja na wewe na Paul Kisabo kutokuwepo kwenye orodha hii mmewahi kuja kuniona gerezani na kuongea na mimi?

Wakili Maduhu: Ni sahihi tumewahi kuja na kama mara tatu nimewahi kuingia na kuja kukuona.

Mhe.Lissu: Katika hizo mara tatu zote je ulijiandikisha pale magereza kabla ya kuniona na ukaonesha kitambulisho chako?

Wakili Maduhu: Sahihi nilifanya hivyo.

Mhe. Lissu: Je wewe ni mtunzaji wa hizo kumbukumbu za watu wanaoingia na kutoka Gereza la Ukonga?

Wakili Maduhu: Sio mimi kabisa. Ni Bwana Jela huyo hapo amekaa kwenye kiti ndio kazi yake. Anamuonesha kwa kidole chake.

Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kama jina lako lipo kwa watu waliotembelea gereza?

Wakili Maduhu: Ndio tar. 28/10 jina langu lipo lakini hii siku sikumuona niliambiwa sitaweza kumuona. Na mara tatu zote nilizowahi kumuona hizo nyaraka hazijaletwa na Bwana Jela. Mkuu wa Gereza yani.

Mhe. Lissu: Nenda SUPP 2 angalia hiyo nyaraka halafu useme item no. 10 aliyekuja ambae ni Paul Kisabo ameoneshwa jina lake na shida yake wameandika shida za kisheria.

Wakili Maduhu: Namuona hapa ndio yupo.

Mhe. Lissu: Tarehe 30/09 angalia jina la kwanza hapo la watu waliotembelea Gerezani ni akina nani?

Wakili Maduhu: Jina ni la Paul Kisabo.

Mhe. Lissu: Je yupo kwenye ile orodha ya kwanza ya watu niliowatambulisha kwa mujibu wa Bwana Jela?

Wakili Maduhu: Kule hayupo.

Mhe. Lissu: Kumbe hayupo kule na magereza walimruhusu aingie?

Wakili Maduhu: Ndio kabisa

Mhe. Lissu: Nenda sasa SUPP 3 na yenyewe. Majina ya mawakili unaowaona na wataje.

Wakili Maduhu: Andrew Mathew Chima na Nashon Nkungu.

Mhe. Lissu: Hao mawakili walikuja kuniona mimi?

Wakili Maduhu: Ndio

Mhe.Lissu: Huyo Andrew aliyekuja kuniona ni mmoja wao au sio mmoja wao kwenye ile orodha aliyosema Bwana Jela?

Wakili Maduhu: Hayumo kabisa.

Mhe. Lissu: Nenda SUPP 5 sasa kwenye hicho kielelezo ni register book ya Gereza la Ukonga. Pembeni imeandikwa SUPP 5 ukurasa unaofuata unaonesha entry ya Tar. 07/05 mwaka jana kuna mtu wa kwanza kabisa anaitwa Nashon Nkungu kazi yake ni wakili amekuja kumuona Mahabusu Tundu Lissu. Shida za kisheria.

Wakili Maduhu: Ni kweli kabisa.

Mhe. Lissu: Sasa waeleze majaji kwanini aliruhusiwa kuja kuniona huyo Nashon.

Wakili Maduhu: kwasababu ni wakili wako.

Mhe. Lissu: Tarehe inayofuata aliruhusiwa tena kuingia?

Wakili Maduhu: Ndio anaonekana hapa kwenye ukurasa unaofuata. Kwenye kurasa kadhaaa. Ukurasa wa 9 na tarehe 28/07 alikuwa mtu wa kwanza kuja kukuona.

MheLissu: Tar. 24/12 jina namba 2 ni Nashon Nkungu tena?

Wakili Maduhu: kweli kabisa.

Mhe. Lissu: Kisabo je yupo au hayupo?

Wakili Maduhu: Na Kisabo nae yupo kabisa.

Mhe. Lissu: 04/03/2026 mtu wa pili Nashon Nkungu aliruhusiwa kuja kuniona?

Maduhu: Sahihi kabisa.

Part 4 itaendelea kwenye post inayofuata.

1784549363213.jpg
 
Kesi imeahirishwa hadi kesho saa 3:00 asubuhi. Mwenyekiti Tundu Lissu ameomba usikilizwaji wa kesi uanze mapema tofauti na ilivyokuwa leo, kutokana na utaratibu wa kumuweka katika chumba cha mahabusu (lock up) hadi muda wa kuanza kesi unapofika.

Katika hatua hiyo, Mheshimiwa Jaji ametoa amri kwamba Mwenyekiti Lissu asipelekwe lock up, kwa kuwa yeye si mshtakiwa katika kesi hii.

Tunawaalika wanachama, wapenda demokrasia na watetezi wa haki wote kufika mahakamani kushuhudia mwenendo wa kesi hii muhimu, ambapo kwa mara ya kwanza kiongozi wa upinzani atamhoji Mkuu wa Magereza kuhusu utaratibu wa Gereza la Ukonga kuzuia au kuweka vikwazo kwa mawakili kukutana na mteja wao.

Tunaendelea kusimamia misingi ya haki, uwazi na utawala wa sheria.
 
Shauri la Kikatiba Na. 7300/2026 lililofunguliwa na Mawakili Kulwa William Maduhu, Nashon Nkung, na Paul Kisabo dhidi ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP) na wenzake, limeendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Amir Mruma.

Katika shauri hilo lililofunguliwa rasmi Masjala Kuu Dodoma, mawakili hao wa Tundu Lissu wanalalamikia kuzuiliwa pamoja na kunyimwa haki ya faragha wanapokwenda kumtembelea na kuzungumza na mteja wao katika Gereza la Kuu la Ukonga.

Akihoji maswali ya dodoso kwa shahidi wa pili wa waleta maombi, Wakili Nashon Nkung, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu (ambaye ni mjibu maombi wa nne), ameunga mkono hoja za mawakili wake huku akiibua madai mazito dhidi ya Jeshi la Magereza.

Lissu ameeleza kuwa maafisa wa magereza wamekataa kumpatia nakala ya hotuba iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya Oktoba 29, 2025, Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman.

Lissu amebainisha kuwa aliahidiwa na kuagiza mawakili wake wamletee nyaraka hiyo ili kumwezesha kujiandaa na utetezi katika kesi ya uhaini inayomkabili, baada ya Jamhuri kuwasilisha maombi ya kumuongeza shahidi anayelenga kumhusisha na vurugu za Uchaguzi Mkuu—matukio yaliyotokea akiwa tayari yupo gerezani kwa miezi sita. Hata hivyo, licha ya mawakili wake kuifikisha nyaraka hiyo gerezani, maafisa wa magereza wameizuia hadi leo.

Katika hatua nyingine, Lissu amegusia namna viongozi waandamizi wa CHADEMA wakiwemo John Heche, John Mnyika, Amani Golugwa na mawakili wake akiwemo Dickson Matata, Deogratias Mahinyila na Gaston Garubindi walivyopigwa marufuku kumtembelea gerezani, jambo linalokwaza maandalizi ya utetezi wake kwani baadhi yao ni mashahidi wake kwenye kesi ya uhaini.

Kwa upande wake, Wakili Nashon Nkung, aliyehojiwa kama shahidi leo Jumanne, Julai 21, 2026, ameieleza Mahakama namna maafisa wa Magereza Ukonga wanavyompekua, kumpa onyo, na kumnyima faragha ya kuzungumza na mteja wake—kitendo alichokosoa kuwa ni kinyume cha miongozo, sheria, na kanuni zinazosimamia mawakili na magereza.

#TunduLissu #MahakamaKuu #ShauriLaKikatiba
1784647743131.jpg
 
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA

Leo July 22, 2026

Jana tuliishia part 10 so leo tunaendelea na

Part 11.

Leo tunaendelea na Andrew Shabani Ntamamiro ambae ni Mkuu wa Gereza yaani Bwana Jela.

Mhe. Lissu: Wewe ndio Mkuu wa Gereza?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio

Mhe. Lissu : una cheo cha ACP?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni Kweli

Mhe. Lissu: Unawajibika kufuata sheria?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio

Mhe. Lissu: Ni jukumu lako wewe na maafisa wengine mnatekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sheria ya magereza na kanuni zake?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Kweli

Mhe. Lissu: Unaifahamu vizuri sheria ya Magereza?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Unaifahamu.

Mhe. Lissu: Yote niliyokuuliza ni maswala ambayo yapo katika sheria?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Kweli

Mhe. Lissu: Yote niliyokuuliza yapo kwenye kifungu cha nane cha sheria ya magereza?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Anaguna

Mhe. Lissu: Sikutegei jibu swali au omba sheria usome kifungu cha 8.

Ntamamiro (Bwana Jela) : kweli

Mhe. Lissu: kuna kanuni za mwaka 1968 na pia kuna PSO yaani Prison Standing Orders?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Naifahamu.

Mhe. Lissu: Ni ya mwaka gani? Tumeitafuta hatuipati sisi. Unaweza kuniazima?

Watu wanacheka 😂😂😂

Ntamamiro (Bwana Jela) : Hapa sina ila naifahamu.

Jaji: Ofisini unayo hiyo PSO?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ninayo ndio.

Jaji: Itasaidia sana ukituletea na ukamletea Lissu pia aitumie.

Mhe. Lissu: Nawashukuru sana majaji nataka kushughulika nae kupitia hiyo sheria.

Mhe. Lissu: Sasa hizo PSO zimetungwa na kamishna wa magereza na kanuni za usimamizi wa magereza zimetungwa na waziri?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio

Mhe. Lissu: Na PSO zinatungwa na kamishna wa magereza baada ya ruhusa ya waziri?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Sijui

Mhe. Lissu: Sasa shika sheria soma section 5(2) Prison Service

Ntamamiro (Bwana Jela) : Kumbe kweli. Inasema hivyo ndio.

Mhe. Lissu: Angalia kifungu cha 105 cha Sheria hiyo ya magereza na kinasema waziri amepewa mamlaka hayo kwa mujibu wa sheria?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli nimeona.

Mhe. Lissu: Yapi ni mamlaka ya kamishna mkuu wa magereza kwa mujibu wa sheria hiyo? Soma ile 5(2)

Ntamamiro (Bwana Jela) : Nimeona.

Mhe. Lissu: Hayo mamlaka ya Kamishna mkuu ya kutunga PSO na Circulars. Je yanahusu maafisa wa magereza peke yake?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Yuko kimya.

Mhe.Lissu: jibu swali sasa.

Ntamamiro (Bwana Jela) : Sio kweli

Mhe. Lissu: Soma sasa hicho kifungu

Ntamamiro (Bwana Jela) : anakisoma kwa sauti.

Mhe. Lissu: Hiyo ni 5(2) kweli?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Hii ni 5(1)

Mhe. Lissu: Sasa nimesema ni 5(2) afande wangu.

Ntamamiro (Bwana Jela) : Naomba tuanze na 5(1)

Mhe. Lissu: Kinahusu nani na nani?

Ntamamiro (Bwana Jela) : wafungwa na maaskari.

Mhe. Lissu: Wambie majaji kuwa neno Prisons linajumuisha na wafungwa?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio

Mhe. Lissu: Kifungu kinasema taratibu zinaongoza Prison and officers?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio

Mhe. Lissu: Kama ni hivyo kwanini Prisons inajumuisha hadi Prisoners na officers kwanini kifungu kitaje sasa hao Prison Officers?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sio mtaalamu wa sheria.

Mhe. Lissu: Mtu pekee mwenye mamlaka ya kutunga kanuni ni waziri peke yake?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Mimi sio mtaalamu wa sheria ni mtekelezaji tu.

Jaji: Shahidi umeelewa lengo la swali unaulizwa ili atake kujua unatekeleza sheria ambazo unajua zimetungwa na nani?

Ntamamiro (Bwana Jela): Aniulize tena.

Mhe. Lissu: Ni kweli kanuni zinazohusu wafungwa mwenye mamlaka ya kuzitunga ni Waziri peke yake?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Sifahamu.

Mhe. Lissu: Soma kifungu 105(1)(j) kuhusu kusearch wafungwa, askari ni waziri ndio anayetunga.

Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli.

Mhe. Lissu: Soma.

Ntamamiro (Bwana Jela) : Basi ni kweli.

Part 12 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Bwana Jela ameshaanza kupelekewa moto 😂😂😂
Ajira za hapa Tanzania ni za kubebana yaani hajui kabisa hata sheria za magereza
 
Yaani mijitu imebebwa na kuwekwa tu haina hata hiyo taaluma. Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi inatakiwa ifanye kazi kubwa sana ya kuangalia uhalali wa nafasi za ajira walizo nazo hawa Watumishi wa Umma.
 
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA

Part 12

Mhe. Lissu anaendelea kumdodosa Ntamamiro (Bwana Jela)

Ntamamiro (Bwana Jela) : Lakini suala la searching zipo sheria zingine.

Mhe. Lissu: Sasa huko tutafika. Mashahidi wengine nilikuwa nawambia waache kiherehere sasa unataka na wewe nikwambie hivyo halafu tutaendaje Ukonga baadae, sitaki kukwambia hivyo Afande wangu.

Watu wanacheka. Majaji pia wanacheka sana. 😂😂

Mhe.Lissu: Sasa soma kifungu cha 105(1)(l) kama hakisemi kuwa Waziri ndio mwenye mamlaka ya kutunga kanuni za management na treatment za prisoners. Ndio au hapana?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Naomba nielezee kidogo.

Mhe. Lissu: Nimesema mimi na wewe kwetu ni ukonga tukitoka hapa. Tukitoboa mtumbwi tutafika? Haya jibu swali tusigombane?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Kweli

Mhe. Lissu: Kamishna Mkuu ana mamlaka ya kutunga hizo kanuni za kutunga mambo haya ambayo nimesema hapo juu?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Waziri ndio amempa mamlaka kamishna wa magereza.

Mhe. Lissu: kwa kifungu?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Kile nilichosema cha 5(2)

Mhe. Lissu: Kile hakijataja Prisoners sasa.

Ntamamiro (Bwana Jela) : Kimetaja Prison ndio Prisoners wapo.

Mhe. Lissu: Kasome Definition section kwenye hiyo sheria kuna tofauti kati ya Prison na Prisoners. Havitumiki interchangebly. Gereza na wafungwa ni vitu tofauti.

Ntamamiro (Bwana Jela): Sijui.

Mhe. Lissu: Kanuni ya 8 ya kanuni za usimamizi magereza. (Prison Management regulation) je inaeleza utaratibu wa ku search wafungwa.

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ndio lakini zipo na sheria zingine.

Mhe. Lissu: Tutaenda kila mahali. Tutafika kwa hizo sheria zote.

Ntamamiro (Bwana Jela) : Sawa. Nakubali.

Mhe. Lissu: Haki za wafungwa tunaenda kanuni ya 9 hadi ya 11?

Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli

Mhe. Lissu: Kanuni ya 12 na Kanuni ya 17 je kanuni hizo zinahusu haki ya wafungwa kutembelewa gerezani?

Ntamamiro (Bwana Jela): Kweli.

Mhe. Lissu: Soma kanuni ya 13 na useme inahusu nini? Ni kweli inahusu haki ya wafungwa kutembelewa na mawakili au washauri wao wa kisheria?

Ntamamiro (Bwana Jela) : Ni kweli.

Mhe. Lissu: Kanuni hizo pia zimeeleza hata namna ya adhabu ya kifo ifanyike kwa maana ya kunyonga wafungwa na masuala yote yanayohusu wafungwa wa adhabu ya kifo? Soma kanuni ya 33.

Ntamamiro (Bwana Jela): haeleweki amesoma nini?

Mhe. Lissu: Ngoja nikusomeee. Anamsomea hapa.

Ntamamiro (Bwana Jela): Nilikuwa sijaiona nimeiona.

Mhe. Lissu: Namna ya kunyoa wafungwa si imeandikwa kwenye kanuni?

Ntamamiro (Bwana Jela): Naam

Mhe. Lissu: Mimi huoni nimefuga rasta sio mfungwa ndio hamuwezi niambia chochote unaelewa hilo?

Ntamamiro (Bwana Jela): uko sahihi.

Mhe. Lissu: Kwa kanuni hizo mahabusu kama mimi napaswa kusimamiwa na askari magereza wawili usiku na mchana.

Ntamamiro (Bwana Jela): Kuna kipengele cha segregation kwenye sheia zetu.

Mhe . Lissu: Jibu kwa kanuni hizo?

Jaji: Kamishna hakuna mtu atakuadhibu maana kanuni hujatunga wewe. Kwahiyo kama kanuni hazisemi sema hazisemi. Usijipe presha kabisa mzee wangu.

Kumbukeni ana miaka 57 huyu Ntamamiro (Bwana Jela).

Ntamamiro (Bwana Jela): Hakuna hiyo kanuni.

Mhe. Lissu: Ni wafungwa wa adhabu ya kifo tu ndio wanatakiwa kulindwa na askari wawili na wasikilizwa mazungumzo yao ni wa adhabu ya kifo pekee? Kweli au sio kweli.

Ntamamiro (Bwana Jela): Sio kweli

Mhe. Lissu: Inasemaje Baba yangu? Kwanza wewe sio Baba yangu mimekuzidi umri. Si umesema una miaka 57.

Ntamamiro (Bwana Jela): Kwa mujibu wa hiki kifungu ni sahihi wafungwa wa kifo ndio wanapaswa kulindwa.

Mhe. Lissu: Safi tukienda hapa tutafanya vizuri. Kwa hayo ambayo umeyasoma na kwa kanuni hizo. Mahabusu, mfungwa hatakiwi kulindwa muda wote kwa masaa 24 isipokuwa wa kifo kwa mujibu wa kanuni hizo? Kanuni ipi?

Ntamamiro (Bwana Jela): Nimesema Jeshi la magereza linaendeshwa na kanuni, sheria na miongozo.

Part 13 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Yaani mijitu imebebwa na kuwekwa tu haina hata hiyo taaluma. Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi inatakiwa ifanye kazi kubwa sana ya kuangalia uhalali wa nafasi za ajira walizo nazo hawa Watumishi wa Umma.
Ndio Maana kesi nyingi serikali inaangukia pua!
 
KITUKO KILICHOTOKEA MAHAKAMANI.

Wakati Mkuu wa Gereza yaani BWANA JELA ambae ni Andrew Shabani Ntamamilo alipohojiwa na Mhe. Tundu Lissu kuhusu Kuwazuia kabisa Mawakili kama Vile Deogratias Mahinyila, Dickson Matata lakini pia viongozi wakuu wa Chama akiwemo John Heche, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika na Amani Golugwa ambao ni mashahidi katika kesi ya Uhaini wamekataliwa kuingia Gerezani Ukonga.

Majibu ya Mkuu wa Gereza amesema yeye hajawazuia. Mhe. Lissu akasema basi watakuja kuanzia kesho. Akasema SITAWARUHUSU waingie kwasababu kesi bado iko mahakamani.

Jaji Amir Mruma ndio akaanza kumuhoji kuna amri yoyote ya Mahakama kuwa watu hawa hawapaswi kuja kumtembelea Tundu Lissu? Akasema kwa kiburi tena kuwa SITAWARUHUSU.

Jaji akavua miwani na kumuuliza unataka tufike huko. Uko serious kweli? Akiwa amekasirika sana. Maaskari Magereza walioko nyuma niliokaa nao karibu wamekimbilia nje kucheka.

Baada ya Jaji kukasirika Bwana Jela akaanza kuomba radhi kwa Jaji. Majaji wote watatu wametikisa vichwa vyao na kuonesha wanashangaa mambo haya yanawezekanaje kwenye Taifa lenye sheria na taratibu.

Kesi hii imeendelea tena kutuonesha watawala wa nchi hii wakoje. Ukisikia majibu ya Mkuu wa Gereza unajiuliza kiburi anakitoa wapi?

Ngoja tusubiri maamuzi ya Majaji mwisho wa kesi hii utakuwaje lakini naamini kila mtu anashuhudia uhalisia wa mambo ulivyo katika Taifa letu.

Tuendelee kusubiri lisaa likamilike turudi kuendelea.

Wanachama leo ni wengi mno. Mahakama imetapika. Yupo Makamu Mwenyekiti John Heche, Yupo Katibu Mkuu, Mnyika. Mama Suzan Lyimo, Mwenyekiti BAZECHA, Yupo Boniface Jacob Mwenyekiti Kanda ya Pwani, Dua Lyamzito, Katibu Mkuu BAVICHA, Pamela Massey, Katibu Mkuu Bawacha. Mzee Azaveli Lwaitama, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na wanachama wengine mbalimbali.

Tutaendelea kuwaleteeni live moja kwa moja mwenendo wa kesi hii kutokea Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam.
1784724915843.jpg
 
Back
Top Bottom