Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Lissu apinga ushahidi anaodai kutaka kutolewa kwa mlango wa nyuma
1786365798046.jpg
 
MATUKIO KATIKA PICHA | Baadhi ya matukio yaliyojiri leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, wakati kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Tundu Lissu, ikiendelea.
1786365867736.jpg
1786365864395.jpg
1786365859197.jpg
 
[8/10, 22:00] Kurwa 2: Shahidi: Baada ya kutazama ile video tulibaini kulikuwa na kulikuwa na kosa kutokana na maneno mengi aliyotamka ila kwa kesi hii naomba nirejee machache “Wanasema kitu kimoja sahihi hapa, msimamo huu unaashiria uasi… akaendelea kusema ni kweli kwa sababu tutazuia uchaguzi tutahamasisha uasi hiyo ndio namna ya kupata mabadiliko kwa sababu tunaenda kukinukisha sana huu uchaguzi tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya sana” Mwisho wa kunukuu
Wakili: "Sasa shahidi embu iambie Mahakama haya maneno baada ya kuyasikia ilipata tafsiri gani?
Shahidi: "Kwa mujibu wa yale maneno aliyoyasema mimi pamoja na timu yangu ndipo tuliona mshitakiwa Tundu Antipass Lissu alikuwa na nia ya kuitisha serikali ili ifanye anayotaka, kitendo cha kuitisha serikali kwa kuzuia uchaguzi na kuhamasisha uasi ndio uhaini wenyewe huo
Wakili: "Unasema uhaini kwa mujibu wa kifungu gani Shahidi Hilo kosa lipo kwa mujibu wa kifungu ….. Kwa mujibu wa uchunguzi wetu tuliofanya tulibaini Tundu Lissu alikuwa akihutubia raia na kwa kuwa ni Raia wa Tanzania anawajibu wa utii kwa Jamhuri ya Muungano, serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Wakili: "Hayo maneno yalikuaje ya kitisho kwa serikali embu waambie majaji
Shahidi: "Mshitakiwa alipotamka yale maneno yanaviashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani na kutamka yale maneno ni kuitishia serikali kwa uwazi"
Wakali: "Alafu'
Shahidi: "Aliidhirishia serikali nia yake kwa kuchapisha maneno hayo kwemye mtandao wa youtube wa Jambo TV"
Wakili: "Kingine mlichokiona cha kuigusa serikali ambayo ni wajibu wake kulinda amani'
Shahidi: "Uchaguzi ulizungumziwa ni uchaguzi wa wabunge madiwani na Rais na uchaguzi upo kwa mujibu wa katiba"
Wakili: "Waambie majaji ni nani mwenye jukumu la kulinda nchi"
Shahidi: "Ni wajibu wa serikali"
Wakili: "Na nini ambaye anachukua hatua sheria pale inapokuwa imevunjwa"
Shahidi: "Ni serikali"
Wakili: "Unapotishia kuvunja amani nani anaathirika"
Shahidi: "Anayeathirika unapotishia kuvuruga uchaguzi ni ule muhimili mmoja wa serikali ambao ndio unajukumu la kusimamia na kutekeleza sheria ndani ya nchi"
Wakili: "Tuambia kama uliwahi kufanya uchunguzi juu ya haya maneno ulifahamu uchaguzi ungevurugwa vipi"
Shahidi: Katika upelelezi wetu tulioufanya hayo maneno ya kukinukisha yalilenga kufanyika kwa matendo ambayo yangezuia uchaguzi usifanyike
Lissu anazungumza: "Waheshimiwa majaji ninapinga aina hii ya uhojigi wa shahidi mimi ni mshaitakiwa wa uhaini sikuwaambia watu wachome na kuchana kura haya maneno wanaokoteza na wanayaleta kwa mlango wa nyuma na sikubaliani nao"
Majaji wanajalili kidogo…….. Minong'ono Mahakamani…….
Wakili: "Waheshimiwa Majaji ushahidi unapimwa na Mahakama, na hazuiwi kusema huyu ni mpelelezi sasa anazuiwa vipi asiseme walichokibaini na huu sio ushahidi mpya mashahdi wengine walisema pia uchaguzi ungezuiwa vipi kumzuia kusema sio sawa na Mahakama hii nina amini inatenda haki
Majaji wanajadili kidogo......
[8/10, 22:00] Kurwa 2: Shahidi kesi ya Lissu - 1: "Tulizama video (ya Lissu) kwa masaa mawili"
Shahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA, Amini Mahamba Kamishna Msaidizi wa Polisi anatoa ushahidi wake akiongozwa na wakili wa Serikali.
"Nilipokea taarifa na nikaanza safari kuelekea ofisi za mkuu wa upelelezi kanda maalumu ya DSM ZCO baada ya kufika nilikutana na maofisa wengine kisha nikakaribishwa ofisini na kupewa mrejesho juu ya walipofikia yeye na timu yake ya upelelezi"
"Na kwemye Jalada niliona jina la mshitakiwa ambayae yuko mbele yetu ambaye ni Tundu Antipas Lissu. Baada ya hatua hizo niliwapangia majukumu, kupeleleza, kukusanya taarifa kuhoji"
Wakili wa Serikali: "Wewe unasema ndio ulisimamia upelelezi kwenye hizo timu kama unakumbuka kulikuwa na nani na nani"
Shahidi Mahamba: "Timu ya ukamataji, Mkaguzi wa polisi msaidizi Michael ndio alikuwa kiongozi wao ……. Inspekta Nunu na wengine. Shahidi anaendelea kuwataja kwa majina
"Baada ya kupanga majukumu mimi na ile timu tulitazama ile video picha mjongeo toka akaunti ya youtube ya Jambo TV".
Wakili Mahamba: "Waambie majaji ni video gani hiyo"
Shahidi: "Ilikua ni video ya Tundu Lissu akihutubia"
Wakili: "Mliweza vipi kuiangalia".
Shahidi: "Tukiwa pale ofisini kuna kompyuta maalumu ambayo anaitumia iInspecta Michael ndio tuliitumia kuangalizia hiyo video"
Wakali: "Mahakama inataka kujua mliitazama kwa kiwango gani?
Shahidi: "Tuliitazama kuanzia mwanzo mpaka mwisho, hiyo video ilikua ndefu na tulitazama kwa masaa mawili na zaidi"
Wakali: "Katika hiyo video ulimwona nani"
Shahidi: "Nilimuona Tundu Lissu na alikua amevaa vazi rasmi la chama la rangi ya kaki akiwa amesimama kwemye mimbari akitoa hotuba na kulikuwa na bendera ya chama na nyuma bendera kama ya taifa"
Wakili: Iambie Mahakama rangi za bendera ya taifa ni zipi"
Shahidi: "Rangi za bendera ya taifa ni bluu, njano kijani na nyeusi"
Wakili: Haya rangi za bendera ya chadema ni zipi"
Shahidi: "Kuna nyeupe, blue bahari nyekundu na nyeusi"
Wakili: "Tuambie kipi kingine uliona
Shahidi: "Pia alikuwa amevaa miwani na alikua akihutubia umma
Wakili: "Unaweza ukaimbia Mahakama lugha aliyokua akitumia mshitakiwa
Shahidi: "Lugha iliyokua ikitumika ni lugha yetu ya taifa kiswahili"
Wakili: "Wewe ulikua ukiratibu zoezi zima la upeleleze ulipata nini kwemye hiyo video kilichoonesha hapa kinafungamana na jalada lilokuwa mbele yenu".
 
Shahidi kesi ya Lissu - 1: "Tulizama video (ya Lissu) kwa masaa mawili"

Lissu: Kwa Miaka 25 Nimeonewa na Jeshi la Polisi

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeendelea leo Agosti 11, 2026, Mahakamani ambapo aliendelea kumhoji shahidi wa Jamhuri, aliyekuwa mpelelezi mkuu wa kesi hiyo, Amin Mahamba.

Lissu alidai kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likimuonea kwa takribani robo karne, akitaja kukamatwa mara kadhaa tangu 2002 hadi 2017, ikiwemo mara nane kati ya 2016-2017, kabla ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Katika roba karne hiyo ya kesi mbalimbali, kesi zote zimekuwa zikiondolewa na polisi wenyewe kabla ya kumalizika.

Lissu alimhoji pia shahidi kuhusu jinsi alivyojiandikia maelezo yake ya ushahidi bila mamlaka ya wazi kisheria.
Alizama zaidi kwenye tafsiri ya neno "uasi" kwenye sheria, akimtaka shahidi kusoma kamusi na Sheria ya Kanuni za Adhabu (kifungu 63), akisisitiza kuwa kukemea maovu ya serikali au vifo vya wapinzani wakati wa uchaguzi si kosa.

Lissu pia alihoji uhalali wa PGO 402 inayolazimu vyama vya siasa kupata kibali cha Polisi kufanya vikao vya ndani, akisema: "Kama kufanya kikao cha kamati kuu kunahitaji kibali cha Polisi, basi sisi ni nchi ya kidikteta."
 
ya Lissu imeanza lakini upande wa mashataka, wanasheria wanaiomba Mahakama ihairishe kwa sababu shahidi wao amepata dharura. Wanaomba Jumatatu wataleta mashahidi wao wote.

Lissu amesimama na kupinga hoja hiyo.

Lissu: "Kulikua na amri mliyoitoa mwaka jana siwezi kukumbuka tarehe, kwamba upande wa mashitaka ulete mashahdi wawili kila kesi inaposikilizwa, na hii amri mmeirudia tena juzi jumatano mmeirudia jana, kwamba upande wa mashitaka walete mashahidi wengi.

Lissu: Sasa waheshimiwa Majaji upande wa Mashitaka hautekelezi amri za Mahakama kwa sababu hamuwachukulii hatua, wanajua mtawakubalia. Lissu: Waheshimiwa majaji kusema maneno haya sio kitu chepesi kwangu ila mmeachia amri zenu kupuuzwa.

Lissu: Sasa kwa vile mlisema jana na hawajaleta mashahidi naomba msikubali Mahakama kuu ya Tanzania ikageuzwa kama ile iliyomuhukumu Jomo Kenyatta, ikiwakubalia waleta mashitaka kila kitu na kuukatalia upande wa utetezi kila kitu.

Lissu: Kwanini hawapo tayari kuheshimu amri ya Mahakama. Kama pumzi imekata wafunge ushahidi twende hatua inayofuata. Kama hawako tayari kuendelea wafunge kesi. Msikubali kugeuzwa kama hiyo mahakama niliyoisema.

Lissu: Again for the record (kwa kumbukumbu) hii ndio kesi kubwa zaidi kwa Jamuhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba, lazima Mahakama ioneshe umuhimu kwa namna inavyosimamia amri zake na maamuzi inayofanya. Hatutembelei njia ambayo haijafagiliwa, kesi ya uhaini ya kwanza ilichukua miezi sita na siku 17 miaka ya 1970. Na ikasafishwa tena miaka ya 1982 na 1983 kesi ilichukua mwaka mmoja na siku 17 chumba hiki hiki.

Lissu: Leo ni siku ya 495, mwaka mmoja na zaidi ya miezi minne hatujamaliza mashahidi wa upande wa mashitaka nikija kusema aitwe Samia si itachukua miaka mitano, na Philip Mpango na IGP Wambura mtakuwa mmestaafu hawajaitwa. Naomba msiwakubalie walete mashahidi tuendelee na kesi.

Mshirikishe mwenzako, "Nikija kusema aitwe Samia si itachukua miaka mitano?" - Lissu
1786696654234.jpg
 
Back
Top Bottom