Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 371,732
- 861,113
- Thread starter
- #661
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 182
Mhe. Lissu anaendelea na maswali ya Dodoso
Mhe. Lissu: haya hayo ndio maelezo yako?
Shahidi wa kificho P8: Haya ndio maelezo yangu nayatambua. Yana sahihi yangu.
Mhe. Lissu: Amemsomea maelezo yake yote. Anamuuliza hayo ndio maelezo yako kama nilivyosoma?
Shahidi wa kificho P8: Bila shaka.
Mhe. Lissu: Bila shaka nini?
Shahidi wa kificho P8: umesoma sahihi.
Mhe. Lissu: Anamsomea maeneo ambayo atamuhoji kumkanusha.
Anamuorodheshea hapa.
Mh. Lissu amemaliza kumsomea hayo maeneo anamuuliza je ungependa maelezo yako yapokelewe Mahakamani kama ushahidi?
Shahidi wa kificho P8: Sina Pingamizi.
Jaji: Mawakili mnasemaje wa Serikali?
Renatus Mkude: Hatuna pingamizi kabisa.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa naomba apewe D7.
Mhe. Lissu: Sasa swali langu la kwanza kuhusu simu yako nioneshe uliposema kwenye maelezo
Shahidi wa kificho P8: Hakuna
Mhe. Lissu: Kuna mahali umesema chochote kuhusu simu?
Shahidi wa kificho P8: Hakuna.
Mhe. Lissu: ni kweli umesema ulikuwa na account ya youtube?
Shahidi wa kificho P8: Ni kweli
Mhe. Lissu: Na onyesha sasa wapi kwenye maelezo kua uliona hiyo video.
Shahidi wa kificho P8 : Kimya
Mhe. Lissu: Unasema Lissu alisema tunapaswa kufanya uasi dhidi ya Serikali?
Shahidi wa kificho P8: nilisema.
Mhe. Lissu: Tuonyeshe kwenye maelezo yako
Shahidi wa kificho P8: Huko hakuna.
Mhe. Lissu: Umetuambia habari za kupelekwa kwa Rashid kutoa maelezo.
Tuambie zipo wapi kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P8: Hakuna.
Mhe. Lissu: Je ulipelekwa kwa RCO na kuwekwa mahabusu kama ulivyosema?
Shahidi wa kificho P8: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Tuoneshe hayo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P8: Hakuna.
Mhe. Lissu: Haya uliyosema leo Mahakamani unaamini ni muhimu ndio maana umeyasema leo?
Shahidi wa kificho P8: Sahihi.
Mhe. Lissu: Nitakosea nikisema haukuyasema Polisi kwasababu hukuamini ni muhimu wao kuyajua?
Shahidi wa kificho P8: utakosea.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama wakati unatoa ushahidi ulitoa sababu.
Shahidi wa kificho P8: Naweza kuzitoa sasa hivi.
Mhe. Lissu: Huu sio muda wake we kaa nazo hizo sababu zako.
Mhe. Lissu: umesema kukinukisha hivi nilisema maana yake?
Shahidi wa kificho P8: Ndio ulisema maana yake ni kufanya uasi
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama umewasilisha hiyo video mahakamani.
Shahidi wa kificho P8: Sijawasilisha.
Mhe. Lissu: Soma kwa sauti kilichosababisha mimi kukuhamasisha
Shahidi wa kificho P8: Nisomeeee.
Mhe. Lissu: P8 amesema nilichukia wizi wa uchaguzi wa CCM kwenye uchaguzi na sisi wanachama hatukubaliani na mambo ya hovyo na ndio maana tunapinga.
Mhe. Lissu: Haya ni yako?
Shahidi wa kificho P8: We uliza swali hayo mengine ni siri yangu.
Watu wanacheka.😂😂😂
Mhe. Lissu: Jibu swali sasa.
Shahidi wa kificho P8: ndio hivyo yakwangu.
Mhe. Lissu: Umesema ulikuwa unasubiri kauli yangu baada ya ile hotuba.
Shahidi wa kificho P8: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Sasa baada ya kuona hiyo video hadi leo kama umewahi kuiona hiyo kauli ya Lissu?
Shahidi wa kificho P8: Hajatoa hadi leo maana ni muhalifu.
Watu wanacheka tena.😂😂
Mhe. Lissu: umesema ulivyosikia kauli yangu ukapata hamasa ukaanza kutekeleza uasi?
Shahidi wa kificho P8: Ndio
Mhe. Lissu: Kwahiyo ulijiongeza hata kabla sijatoa kauli.
Shahidi wa kificho P8: sikujiongeza lakini ndio hivyo.
Mhe. Lissu: Sasa wewe ni mwanachama wangu inabidi nisikutese hapa ngoja nimalizie uondoke.
Shahidi wa kificho P8: Mimi sio mwanachama wako kwani wewe unaona haya ni mazuri, Mimi sikuwahi kutegemea kama siku moja nitafika hapa.
Watu wanacheka sana.😂😂😂
Mhe. Lissu: Je umewahi kuwasiliana tena na Polisi kuanzia tarehe 22/04 hadi sasa?
Shahidi wa kificho P8: Sijawasiliana na Polisi hadi leo labda walivyoniambia tu nije kutoa ushahidi.
Part 183 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.