#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 172
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P6.
Mhe. Lissu: Mhe. Jaji naomba shahidi ajibu maswali yangu.
Jaji: Hebu muulize tena.
Mhe. Lissu: Hayo maneno ya simu infinix smart 8 yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: sifahamu.
Jaji: Nafikiri lengo lako mshitakiwa ni ku empeach credibility ya shahidi kwahiyo akisema hafahamu wakati kielelezo kipo na sisi Mahakama tutakipitia. Basi acha aendelee kusema hafahamu.
Mhe. Lissu: Maneno kwamba ulikuwa na bando la kuingia youtube hebu tuoneshe kwenye maelezo yako hapo?
Shahidi wa kificho P6: Yapo.
Mhe. Lissu: Tuonyeshe.
Shahidi wa kificho P6: Majira ya saa nne niliona mtandao wa youtube hotuba ya Tundu Lissu.
Mhe. Lissu: Swali langu ni ulikuwa na bando la internet.
P6: Hayo hayapo.
Lissu: Kumbe una akili unaelewa. Tukienda hivi itakuwa vizuri. Haya tuendeleee.
Ulisema uliingia katika mtandao ya Jambo TV?
P6: Nilisema niliingia kwenye account.
Lissu: Hivyo hivyo account eheee yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe. Lissu: Umeeleza kwamba wakati nahutubia huo Mkutano nilisema maneno kwamba yeyote atakayekuwa nasi tutaenda nae na asiyetaka tutamuacha, yapo kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe.Lissu: Ulisema nilisema kuwa kama kuna anayetaka kugombea udiwani asahau na anayetaka kugombea ubunge asahau, hayo nayo yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Polisi nilitoa ila hapa kwenye maandishi sioni.
Mhe. Lissu: Ahsante, Polisi ni waongo wamekuibia maneno yako, tuendelee.
Haya umesema nilisema maneno No Reforms, No Election, haya ni maneno yangu kweli nimeyasema sana.
Shahidi wa kificho P6: hayo sikusema. nilisema bila mabadiliko hakuna uchaguzi.
Mhe. Lissu: Basi twende na hayo hayo, yapo kwenye maelezo au hayapo?
Shahidi wa kificho P6: Hayo maneno siyaoni kwenye maelezo.
Mhe. Lissu: Turudi kwenye simu kwenye maelezo yako yote Polisi nataka uniambie ulisema kama ulikuwa na simu popote pale? Nataka unioneshe humo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: nilisema nimejiunga na magroup ya whatsapp kwahiyo maana yake ni simu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama maneno ya bendera za taifa na Chadema yapo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe.Lissu: Kwamba nilivaa kombati za Kaki nayo pia yapo humo kwenye maelezo?
Shahidi wa kificho P6: Maelezo siyaoni.
Mhe. Lissu: Umemuelezea mtu anaitwa Essau Chiza pia anaitwa Mwamba wa Kigoma sasa tuoneshe Mwamba wa Kigoma kama yapo?
Shahidi wa kificho P6: Hayapo.
Mhe. Lissu: Ulisema Essau ni Katibu sehemu nyingine ni Mwenyekiti kipi ni kipi?
Shahidi wa kificho P6: Mimi sijasema hivyo.
Mhe. Lissu: Sasa wewe leta hayo maelezo nikuoneshe, anamsomea aliposema Mwenyekiti na aliposema ni Katibu.
Shahidi wa kificho P6: Mimi sikusema hivyo watakuwa mapolisi ndio walikosea.
Mhe. Lissu: Pole kwa kuingizwa chaka na mapolisi.
Shahidi wa kificho P6: Ahsante sana.
Watu wanacheka.😂😂😂
Mhe. Lissu: Ulisema ulivyohamasika kufanya vurugu tuoneshe hizo habari nazo kwenye maelezo yako?
Shahidi wa kificho P6: anasoma mambo tofauti kabisa.
Mhe. Lissu: Wewe ulihamasika kwamba utazuia uchaguzi kwa kukinukisha ndio nayataka yapo?
Shahidi wa kificho P6: Mimi binafsi maneno ya Mwenyekiti wa Chama yalinihamasisha na kupata moyo wa kijasiri na kunipa hamasa ya kuvuruga uchaguzi mkuu 2025 kwa kukinukisha.
Mhe. Lissu: Ohoo Hongera sana kumbe wewe na mimi letu lilikuwa moja ila Mwenzangu uko kizimba cha shahidi nashangaaa. Haya tuendelee lakini.
Part 173 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba repost yako.