Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tupia mkuu inayofuata!
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 134

Anaambiwa hapa Mh. Lissu kuwa GN. iliyomteua ilikuwa inasema anapaswa kuteuliwa na AG na sio DPP.

Mhe. Lissu anawaomba hapa Vijana wake wamfanyie research kama kipindi hicho sheria ilikuwa inasema hivyo.

Anaambiwa ni sahihi.

Anasema sasa nakubali hata kama Sheria inasema AG ndio alipaswa kumteua swali la msingi linabaki kuwa AG alimteua shahidi huyu kama mtaalamu wa picha na sio mtaalamu wa video.

Lakini pia shahidi ameandaa taarifa badala ya Certificate wakati CPA imetoa kwenye third schedule format ya hiyo certificate.

Pia GN. No. 823 na GN. No. 825 zimewataja wataalamu wa cyber forensic na huyu shahidi hayumo.

Kwahiyo nasisitiza vielelezo hivi visipokelewe kwa maana ya ripoti ya mtaalamu.

Naomba kuishia hapo.

Majaji wanateta kidogo pale na wanawaita upande wa Mashitaka.

Anasimama Renatus Mkude na anasema mara baada ya kupokea ile ruling ya kwanza na Mshitakiwa ameirejea sana ile ruling ya kwanza tunaomba nusu saa ya kwenda kutafakari halafu tukirudi tutakuja na msimamo wa namna ya kwenda mbele.

Majaji wanateta kidogo.

Jaji Nduguru anasema Mahakama imehairishwa mpaka saa sita mchana ili upande wa Jamhuri waende kutafakari.

Watoto wa mjini wanasema Hii Kesi ishakuwa ngumu, aliyetumwa kumpelekea chakula mtuhumiwa na yeye kakamatwa kawekwa lock.😀😀😀

Tukutane baada ya nusu saa.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 135

Mahakama imerejea.

Amesimama Renatus Mkude kusema Uwakilishi uko kama asubuhi na tunaomba Job Mrema atoe majibu.

Amesimama Job Mrema sasa kujibu.

Upande wa Jamhuri tumesikia pingamizi lililowasilishwa na mshitakiwa kuhusiana na upokelewaji wa taarifa ya mtaalamu ambae ni PW 3.

Ni msimamo na hoja yetu kwamba tunapinga pingamizi la Mshitakiwa kuhusiana na kielelezo tunataka kukitoa.

Job Mrema huwa anaongea kama anarap anaanza kwa sauti ndogo baadae anaongeza sauti.

Sisi tutajibu kwa kifupi sana ingawa yeye amesema kwa urefu sana.

Anaendelea Job Mrema hapa.

Waheshimiwa Majaji muda mfupi Mahakama ilitoa uamuzi wa kutopokea kielelezo cha flash na memory card.

Ni dhahiri kuwa uamuzi kuhusiana na flash disk na memory card ni tofauti na kielelezo ambacho Mahakama hii imeombwa na Shahidi kukipokea.

Pia Mshitakiwa alikuwa anajaribu kusema wino haujakauka.

Alikuwa anajaribu kuhusianisha hivi vielelezo viwili.

Suala la wino umekauka au haujakauka sio subject matter kwenye hii kesi katika mazingira kama haya Mahakama hii ione hivi vitu ni tofauti.

Ni hoja yetu kwamba katika mazingira ya sasa hoja muhimu ni suala la upokelewaji wa kielelezo.

Mshitakiwa ameanza kusoma maudhui ya kielelezo.

Huko kwenye maudhui hatujafika bado hapa tulipaswa kujadili upokelewaji wa kielelezo tu.

Waheshimiwa Majaji kwenye kueleza hilo Mahakama hii ya Tanzania imedevelop principle zinaisadia Mahakama kufikia kwenye maamuzi yaliyo sahihi.

Katika mazingira tuliyonayo tunaialika Mahakama hii kutizama principle ya admissibility of an exhibit before the Court of law.

The exhibit must be cleared before admission hicho ndio Mahakama inapaswa kuanza nacho.

Utaratibu haujafuatwa, kielelezo kingesomwa na shahidi baada ya hiyo hatua ya kwanza sasa Mshitakiwa ameanza kukisoma yeye mwenyewe.

Labda nichomekee, hivi mnamuelewa kweli hapa Job Mrema anapiga akapela, hasemi kifungu cha Sheria wala hajatoa zile kesi zake nyingi anazotoa, ngoja tumsubiri.

Sasa amekumbuka kutaja kesi anasemaa Kesi ya Robison Mwanjisi Criminal Appeal No. 154/1994. Ukurasa wa 18 unasema katika kufafanua principle ambayo Jamhuri imeisema kwamba before you read out the documentary evidence, it must be cleared first and after admission the witness will read the same.

Pia Mshitakiwa alirejea kifungu cha 216 cha CPA na mtaalamu anayezungumziwa kwenye kifungu hicho ni huyu mtaalamu ambae yuko Mahakamani.

Pia amerejea GN. No. 799/2020 kuwa PW 3 ametangazwa kwenye gazeti la Serikali na sisi tunasema ni kweli ametangazwa na hili ndio jukumu alilokuwa nalo.

Swala la substance ya taarifa hii ni mtego ambao sisi tunautegua upande wa Jamhuri. Tunaialika Mahakama isifike huko.

Anaendelea Job Mrema hapa anasema Kesi ya Sharif Mohamed Mahakama itabaini kuwa wakati wa upokelewaji wa kielelezo mahakama inazingatia vitu vitatu ambavyo ni competence, materiality and relevance.

Katika kipindi hiki Mahakama inazingatia hivyo vitu vitatu.

Mtaona pia vinakuja kuwa qualified kwenye shauri la Robison.

Je vielelezo vinavyopaswa kutolewa na shahidi ni relevant? Jibu ni NDIO ni relevant kabisa.

Pia issue ya materiality na sisi tunasema ile nyaraka ina ushahidi ambao ni material kabisa.

Pia vifungu alivyocite vyote hatuoni kama ni relevant.

Hoja ya msingi hapa ni kwamba baada ya shahidi kufanya kazi vielelezo alivyoletewa nini kilipatikana? Ndio hiki kielelezo.

Halafu kutokuandikwa kuwa hii ni certificate je inafuta content iliyopo ndani ya hiyo taarifa?

Haiwezi kabisa kufuta content ya hiyo nyaraka.

Kwa taarifa yenu tu leo kivuruge wao KATUGA hayupo kabisa Mahakamani. pengine aliona kuna aibu itatokea akaamua kula nyoya so leo ameachiwa msala Job Mrema.

Part 136 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Kama video ya ushahidi imekataliwa kuna ushahidi gani tena?au ndio kupoteza muda ili mama apite kwa mbeleko?
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 136

Anatoa kesi nyingine ya Maghimbi Mzini Criminal appeal No. 304/2023 Mahakama ya Rufani

Ukurasa wa 21 unasema admissibility of documentary evidence huo ni mtego na Mahakama isiingie hapo.

Kwa kumalizia Mahakama hii naomba isiyazingatie mapingamizi ya Mshitakiwa.

Jaji anasema Mshitakiwa karibu kwa ajili ya Rejoinder.

Mhe. Lissu anaanza.

Waheshimiwa Majaji msishawishiwe na uamuzi wa awali kuhusu admissibility ya flash disk na memory card kwasababu hivi vitu viwili ni tofauti kabisa.

Hivyo msishawishike kusimama na msimamo wenu wa flash disk na memory card.

Wakili wa serikali Mkuu hajaelezea kwanini hizo nyaraka ni tofauti.

Sasa Majaji ni kweli hivi vitu ni tofauti kimoja ni karatasi na kingine ni memory card huo utofauti ni wa kweli hata kama hajaelezea.

Lakini swali la msingi hapa ni hii ripoti ambayo iko tofauti na flash na memory card inahusu nini? Content yake ni nini? Inahusu flash disk na memory card pamoja na kwamba they are different but they are related.

Bila flashdick na memory hakuna report na hayo ndio mahusiano yake kimoja kikianguka kingine hakiwezi kusimama.

Hii report Waheshimiwa Majaji kwasababu ni report ya Vitu vilivyokataliwa na Mahakama haiwezi kusimama yenyewe, kusimama kwake kunategemeana na kile ilichokichunguza.

Waheshimiwa Majaji kama taarifa ikipokelewa haitakuja kuprove chochote Mahakamani.

Wakili wa Serikali Mkuu Mrema amewaalika msiangalie content za hiyo report na anasema mimi nimeenda kwenye content za report.

Wakili wa Serikali Job Mrema anasema the fact kwamba hiki kielelezo hakijaitwa CERTIFICATE kuitwa kwake taarifa hakubadilishi Content.

Hii sio kesi ya kukosewa jina. This is not the case of misnaming this is a case of something being tendered which have never been tendered.

Hii taarifa sio tu taarifa jina ni taarifa kwa content kungekuwa na umaana wa hii taarifa yao wangeambatabisha na kurasa moja ya Certificate kwa mujibu wa sheria.

Sasa wametuletea kurasa 11 za maandishi hiyo tunaita nini kama sio taarifa?

You should not be persuaded kuwa hili jina halina shida, hilo jina linaelezea kilichopo ndani.

Maghimbi Mzini dhidi ya Jamhuri ni kesi nyingine imeletwa na wenzetu pia hii kesi haiwasaidii hata kidogo naomba nisome paragraph mbili kwenye ukurasa wa 21.

Amesoma hiyo kesi.

Anasema hoja hapa hatujajadili uzito wa ushahidi wa hiyo taarifa, My only contention has been hii taarifa is not admissible.

Haijakidhi matakwa ya sheria ya kupokelewa kama kielelezo, sijasema ripoti hii ni ya uongo na ina mambo yasiyo ya ukweli.

Mimi sijafika huko nimeishia kwenye suala la kwamba hayakidhi vigezo.

Kwahiyo with all due respect hii kesi ya Maghimbi Mzini haiwasaidiii kwasababu inasema tusichanganye uzito wa ushahidi na kupokelewa kwa kielelezo.

Ni hayo tu Mhe. Jaji, Mhe. Lissu amemaliza kufanya Rejoinder

Majaji wanaandika kidogo.

Mawakili wa Serikali kwa mara ya kwanza leo wapo na kahali fulani ambako ni kama hawaitaki kesi kabisa.😂

Ukiwaangalia unaona moja haikai na mbili haikai, wapo wapo kama wamerogwa.

Majaji wanamaliza kuteta hapa.

Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti.

Anasema Mahakaman itatoa uamuzi kesho saa tatu asubuhi.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo Oktoba 23, 2025

Jana tuliishia part 136 so leo tunaendelea na-;

Part 137.

Mh. Lissu ameingia ila leo amekuja na ujumbe anasema kuwa yatakwisha tu.

Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.

Karani anasoma namba ya shauri

Wakili wa Serikali Renatus Mkude anatambulisha jopo la Mawakili wa Serikali na anasema yuko tayari kwa ruling kwa upande wao wa Jamhuri.

Mshitakiwa nae anasema yuko tayari.

Anaanza kusoma Jaji Kiwonde kwa niaba ya Majaji watatu.

Mshitakiwa alipinga shahidi Na. 3 kutoa report kwani ilipaswa kuwa ni certificate lakini pia mshitakiwa alisisitiza kuwa shahidi huyu ni mtaalamu wa picha na sio video.

Lakini pia Mr. Job Mrema yeye alijibu pingamizi hilo na kusema pingamizi halina mashiko.

Alisema Mahakama hii haibanwi na maamuzi yake aliyoyatoa siku ya jana kuhusu flash na memory card.

Na mshitakiwa alienda mbali kuingia kwenye content za report wakati Mahakama ya Rufani ilishazuia jambo hilo.

Mr. Mrema anasema kwa mujibu wa kifungu cha 216 cha CPA shahidi anaruhusiwa kutoa hiyo report.

Kwasababu ina uhusiano mkubwa na kesi na hata yeye ndio aliandaa basi ni yeye ndio anaweza kuitoa.

Na katika rejoinder mshitakiwa anasema taarifa hii au report vina uhusiano mkubwa kama hizo device zimekataliwa hivyo hata report haina miguu ya kusimama.

Mahakama inapaswa kuamua kama shahidi Na. 3 yuko competent kutoa hicho kielelezo.

Sisi tunaona shahidi Na. 3 ni mtaalamu na kwa mujibu wa kifungu 216 kimeeleza majukumu ya mtaalamu na GN Na. 799/2020 inasema kinagaubaga wajibu na kazi ya shahidi.

Hakuna ubishi aliteuliwa na DPP na Attorney General na hicho kilichopo hapa Mahakamani ndio kipo kwenye kifungu hicho.

Kwetu sisi tunaona kazi yake ni kuzichunguza zile picha na baada ya kufanya huo uchunguzi yeye analo jukumu la kuandaa certificate.

Hizo ndizo kazi aliteuliwa kufanya.

Tunakubaliana na Mshitakiwa kuwa shahidi alipaswa kuandaa Certificate badala ya kuandaa Report.

Angekuwa ameteuliwa kama Forensic expert basi tungekubaliana na nyaraka yake.

Kwenye kesi hii shahidi Na. 3 aliteuliwa kushughulikia picha mnato ambazo zinapelekwa kwake na hilo tulisema jana pia na mwishoni anaandaa certificate.

Kwa maana hiyo hatukubaliani na Mr. Mrema kuwa kuna mtego na sisi hatuko tayari kuingia kwenye mtego alitupatia Mrema na kumuamini.

Hii taarifa inalenga kwenda kuelezea nini kama tutaipokea?

Hicho kinachoelezewa kwenye taarifa kama hakipo tukiipokea tunaopokea ili kije kutusaidia nini kama Mahakama.

Huyu Shahidi hana uwezo wa kutoa hiyo taarifa bali alipaswa kutoa CERTIFICATE.

Tunaona pingamizi lina Mashiko. Na tunakubaliana na Mshitakiwa na tumeamua hivyo.

Leo tena wamepigwa na kitu kizito hawa ndugu zetu wa Jamhuri. Wamechanganyikiwa tena kwa mara nyingine. 😂😂

Jaji amesema haya sasa muendeleee.

Anasimama Thawabu Issa Wakili wa Serikali anasema Mhe Jaji.

Jaji anamwambia subiri kwanza Wakili,
Shahidi nakuonya upo chini ya kiapo.

Ukiwa unaendelea kutoa ushahidi wako.

Shahidi sawa Mhe. Jaji.

Thawabu Issa anasema Mhe. Jaji hatuna kingine cha zaidi kwa Shahidi huyu.

Tunaomba kuishia hapa

Watu wanacheka.😂😂😂

Anaitwa Lissu kwa ajili ya Maswali ya Dodoso.

Mhe. Lissu: Shahidi uliandika maelezo yako Polisi tarehe 08/04/2025 kwenye ofisi za Polisi Forensic Bureau?

Samweli Kaaya: Ni kweli.

Mhe. Lissu ; Je ukiyaona hayo maelezo yako utayatambua.

Samweli Kaaya: Ndio nitayatambua. Ni maelezo yangu.

Anasomewa hapa Maelezo yake na anapatiwa.

Mhe. Lissu ananendelea kumsomea Maelezo yake Polisi huyu shahidi ambae ni Samweli Elibariki Kaaya.

Part 138 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 138

Mhe. Tundu Antipas Lissu akiwa anaendelea kumsomea Shahidi maelezo yake.

Anasema naomba tuelezane yafuatayo.

Majaji watatu ambao ni Dunstan Ndunguru-Mwenyekiti wa jopo.

James Karayemaha – Jaji mjumbe wa jopo.

Ferdinand Kiwonde – Jaji mwingine wa jopo.

Wameingia kwenye rekodi ya kusikiliza shauri hili la Uhaini linalomkabili Mhe.Tundu Lissu na kwakweli kwa hatua ya sasa ya wao kukataa kupokea hivi vielelezo viwili kwa maana video pamoja na report ya mtaalamu nafikiri hata kama wamefanya kwa mujibu wa sheria na kweli.

Mungu atawabariki kwa hilo kwasababu kwa Mahakama zetu na namna tulivyowazoea hawa Majaji wangeweza kuamua vinginevyo na tusingekuwa na la kusema.

Nafikiri katika hili na sisemi wamefanya kwa nguvu zao ila ninachokisema lolote walilolifanya angalau rekodi zitawatambua kuwa kuna maamuzi ya msingi waliyafanya katikati ya kesi hii.

Kazi kwao huko mbele kama hawatajidharirisha.

Kwa hatua ya sasa nafikiri WATANZANIA hawawadai chochote hawa Majaji.

Wamejitahidi kutenda haki na Mimi binafsi nawaombea kwa Mungu kila la kheri kwasababu tunafahamu wanaafanya kazi kwenye utawala ambao professionalism hakuna kabisa pongezi sana kwao kwa hatua ya sasa.

Mara baada ya pongezi hizo, Mheshimiwa Lissu anamueleza shahidi maeneo ambayo anataka kum contradict shahidi kutokana na kilichopo kwenye maelezo yake Polisi na alichosoma hapa Mahakamani.

Ameshafika eneo la 30 kwa sasa ambayo yanatofautiana na maelezo yake hapa Mahakamani. Ikiwa ni pamoja na Elimu yake ya Upolisi, Masomo aliyosoma nyakati tofauti tofauti, vyuo na course mbalimbali za kipolisi alizosoma South Africa, India na maeneo nengine.

Mhe. Lissu alikuwa anasoma maeneo ambayo amefikisha maeneo 75 anayotaka kwenda kumcontradict shahidi.

Mhe. Lissu amemuuliza Shahidi je ungependa maelezo yako sasa yapokelewe kama ushahidi Mahakamani?

Shahidi: Waheshimiwa Majaji naomba yapokelewe kama ushahidi.

Jaji Ndunguru anasema maelezo hayo yamepokelewa kama kielelezo cha Mshitakiwa na nitayapa alama Exhibit D2 ya upande wa Mshitakiwa.

Kwa kifupi kwa msio elewa hadi sasa Jamhuri hawana kielelezo chochote kilichopokelewa kuunga mkono kesi yao.

Ila upande wa Mshitakiwa Tundu Lissu hadi sasa amefanikiwa kuingiza vielelezo viwili yani Exhibit D1 na Exhibit D2 ambavyo vyote lengo lake ni kuonesha mashahidi wa Jamhuri ni waongo na wanatunga mambo.

Waliyosema hapa Mahakamani ni tofauti na walichokiandika kule Polisi nako ni tofauti kabisa.

Kwahiyo kwenye vielelezo hadi sasa ni mbili bila. 😂

Mhe. Lissu anaanza sasa kuendelea na maswali yake.

Kwenye ushahidi wako ulisema wewe ni mtaalamu wa picha na uliteuliwa kwa kazi hiyo naomba angalia maelezo yako uliyotoa polisi kama ulisema kuwa wewe ni mtaalamu wa picha kwa mujibu wa GN NO. 725/2020.

Samuel Kaaya : Hayapo.

Mhe. Lissu: ulisema hapa Mahakamani Kati ya 2003 na 2004 ulihudhuria mafunzo ya Polisi Moshi CCP sasa angalia kwenye maelezo yako kama mambo hayo yapo?

Samuel Kaaya : Hayapo.

Mhe. Lissu: Hapa Mahakamani ulisema ulisomea Criminal Law, Singe, Judo na Karate na masomo mengine sasa waeleze majaji kama yapo kwenye maelezo yako Polisi?

Samuel Kaaya : Hayapo.

Mhe. Lissu: je kuhusu ulipandishwa cheo na kupata cheti cha umahiri nayo yapo kwenye maelezo yako Polisi?

Samuel Kaaya : Hayapo.

Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuwa ulifanya mafunzo ya upigaji picha je yapo hayo kwenye maelezo yako Polisi?

Samuel Kaaya : Hayapo.

Part 139 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 139

Mhe. Lissu: Kati ya Mwaka 2021 na 2022 ulihudhuria mafunzo ya Assistant Inspector of Police kule Moshi, sasa kwenye maelezo yako Polisi mambo hayo yapo?

Samuel Kaaya : Sikuyasema.

Mhe. Lissu: Ulisema umesomea medani za kivita na masomo mengine mengi hayo nayo umesema kwenye maelezo yako Polisi?

Samuel Kaaya : Sikusema.

Kwa kifupi huyu shahidi amesema mambo mengi sana hapa Mahakamani ambayo siku anaandika maelezo yake Polisi kuhusu kesi hii hakuyaandika ila hapa Mahakamani ameyasema.

Ndio yale maeneo 75 ambayo Mhe. Lissu ameyasema hapo awali na anaendelea kumuuliza.

Kila kitu anachomuuliza shahidi kwamba ulisema hivi hapa Mahakamani je kwenye maelezo yako yapo? JIBU LA SHAHIDI NI HAPANA, HAYAPO NA SIKUANDIKA.

Yataulizwa maswali mengine ya utofauti wa statement mfano alisema hapa Mahakamani hivi na kwenye maelezo alisema tofauti tutafikia pia hatua hiyo.

Lengo la zoezi hili ni kuonesha shahidi ni muongo na hapaswi kuaminika.

Mhe. Lissu: Je ulisema sana hapa Mahakamani kuhusu mafunzo uliyopata South Africa, Je kwenye maelezo yako yapo?

Samuel Kaaya: Sikuandika kwenye maelezo yangu.

Mhe. Lissu : Ulisoma miezi sita chuoni hapo?

Samuel Kaaya : Sikuandika na hilo pia.

Mhe. Lissu: Anauliza kuhusu chuo cha IFM na Masomo aliyosoma ya kuhusu Uhasibu na Data Management anayosema alisomea na kuzawadiwa shahada ya Sayansi ya Tehama kwenye vyuo mbalimbali je yako wapi kwenye maelezo yake?

Samuel Kaaya : Sikusema.

Mhe. Lissu: Mwaka 2024 ulipata mafunzo katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Sayansi ya Jinai. Kule India, Je yako wapi hayo kwenye maelezo yako?

Samuel Kaaya : sikuandika kwenye maelezo yangu, hayapo.

Mhe. Lissu: Ulisema mambo mengi ikiwemo utaratibu wa kuchunguza vielelezo ikiwemo ile kanuni yenu ya first inn first out kama umeuelezea kwenye maelezo yako ya pale Polisi?

Samuel Kaaya : Sikuelezea kabisa.

Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuhusu kuwepo na Police Notebook muda wote ili kila unaloliona unarekodi kwenye Polisi Notebook, je hayo yapo kwenye maelezo yako?

Samuel Kaaya : Hayapo

Mhe. Lissu: Hivi nyie Mapolisi nani huwa anawafundisha kuandika maelezo yenu?

Samuel Kaaya : Tunafundishana wenyewe.

Mhe. Lissu: Neno Confimatory test ulifanya, sasa nionyeshe hapo kwenye maelezo yako hiyo confirmatory test ulipoandika.

Samuel Kaaya : Kiukweli Sijaandika hilo neno, halipo.

Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuwa unafanya Chron analysis ili kugundua kama kuna Deep Fake yaani teknolojia ya AI imetumika katika video husika je hayo yapo kwenye maelezo yako uliyoandika Polisi?

Samuel Kaaya : Hayapo Sikuandika.

Mhe. Lissu: ulisema habari za kuangalia video kama iko compressed or decompressed nao upo kwenye maelezo yako?

Samuel Kaaya : Haupo.

Mhe. Lissu: Ulisema kuhusu censor pattern analysis na non Uniformity je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?

Samuel Kaaya : Hayapo.

Mhe. Lissu: Ulisema habari za kufanya noise analysis kwenye hiyo video sasa tueleze hayo mambo mengi na utaratibu wa kufanya noise analysis na unaweza kuona vichengachenga kwenye video kama yapo kwenye maelezo yako ya Polisi?

Samuel Kaaya : Hayapo

Mhe. Lissu: Nitakuwa sahihi nikisema huu ushahidi wa maeneo niliyokupitisha ulikuwa ni wa muhimu kwenye kesi hii?

Samuel Kaaya : Ni kweli.

Mhe. Lissu: Na ni kweli ni muhimu kwasababu unaonesha maabara yenu inavyofanya kazi kitaalamu?

Samuel Kaaya : Ni kweli

Mhe. Lissu: kuhusu notebook ni muhimu askari awe nayo muda wote wa uchunguzi hilo nalo ni muhimu?

Samuel Kaaya : Ni muhimu.

Part 140 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Tunaendelea

kilichoonekana kama uchunguzi wa kawaida kimegeuka kuwa cross examination ambush.

Lissu ameanza kumvua shahidi wake, Kaaya, silaha moja baada ya nyingine, akitumia maelezo yake mwenyewe kama counterintelligence weapon.

Anapouliza, haulizi kama wakili anauliza kama operative anayefanya interrogation ya field asset aliyekosa consistency kwenye mission report zake.

Mtaalamu aliyetarajiwa kuwa nguzo ya Jmt, amegeuka kuwa compromised source.

Kila jibu lake "Hayapo" limekuwa trigger point ya kudhoofisha credibility ya ushahidi wote wa upande wa serikali.

Kila "Hayapo" ni bomu dogo la kimyakimya, likilipua kwa taratibu imani ya Mahakama kwa ushahidi wa Jamhuri.

Majaji Ndunguru, Karayemaha na Kiwonde, wameonyesha rare operational integrity.

Kukataa kupokea vielelezo vilivyotengenezwa kwa makosa ni ishara ya kwamba ndani ya mfumo bado kuna operatives wachache waaminifu, wanaofanya kazi kwa misingi ya sheria, si amri.

Kwa macho ya intel, hii ni hatua ya restoration of judicial signal ndani ya mfumo uliokuwa unakaribia kufungwa na kelele za mamlaka.

Kwa sasa, Jmt iko kwenye blackout zone hakuna kielelezo, hakuna traction, hakuna narrative.

Wakati huo huo, Lissu amepata nafasi ya kipekee ya kuendesha information warfare kwa kutumia vielelezo vyake mwenyewe kama firewall dhidi ya propaganda ya upande wa mashtaka.

Operesheni ya leo inaacha alama mfumo wa Jmt umevurugika, shahidi wao mkuu amejichafua kwa ushahidi wake mwenyewe, na Mahakama imeanza kusimama kwenye mhimili wa haki.

Kwa lugha rahisi tuseme, Target Neutralized. Enemy Credibility Collapsed. Judicial Optics Secured.
 
#BREAKINGNEWS

Kutoka kwenye chumba namba moja (cha Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu inaendelea tena leo, Alhamisi Oktoba 23, 2025, chini ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru

Mapema kabisa, Mahakama imeanza kutoa 'uamuzi mdogo' kufuatia pingamizi lililokuwa limewekwa na mshtakiwa Tundu Lissu ambaye anajitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo, ambapo pingamizi hilo limelenga kupinga kuwasilishwa Mahakamani kama kielelezo taarifa ya uchunguzi ya picha jongefu (video), kutoka kwa shahidi wa tatu (3) wa Jamhuri Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Samwel Elibariki Kaaya

Katika kujenga hoja ya pingamizi hilo, sambamba na kufanya marejeo ya hoja mbalimbali za kisheria na kesi mbalimbali, Lissu aliieleza Mahakama kuwa shahidi huyo ana uwezo wa kutoa 'certificate' na sio 'report', na kwamba shahidi alipaswa kuandaa picha mnato (still picture) alizopelekewa kufanyiwa uchunguzi na kuzikuza, baada ya kuteuliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) na au Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kwa mujibu wa tangazo la serikali

Wakili wa Serikali Mkuu Job Mrema alipinga vikali hoja hiyo, akieleza Mahakama kuwa Mahakama hiyo haibanwi na maamuzi yake iliyotoa mapema jana, Oktoba 22, 2025 ya kukataa kupokelewa Mahakamani hapo kwa 'Memory Card' na 'Flash Disk' kama kielelezo kutoka kwa shahidi huyo

Mrema alienda mbali zaidi na kuieleza Mahakama kuwa, mshtakiwa ameingilia 'content' ya hizo 'report' kwa kuzisoma jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya Mahakama Kuu, yanayoelekeza kwamba nyaraka yoyote haitakiwi kusomwa kabla haijawasilishwa na kupokelewa Mahakamani, hivyo kuiomba Mahakama kutupilia mbali pingamizi hilo

Akijibu hoja za kutetea pingamizi lake alilokuwa ameliweka hapo jana, Lissu alisisitiza kuwa Mahakama hiyo imekataa kupokea 'Memoy Card' na 'Flash Disk' kama kielelezo, hivyo kwenye mazingira ya kisheria taarifa hiyo ya uchunguzi haiwezi kusimama yenyewe

Akitoa uamuzi huo, Jaji Ndunguru amesema Mahakama imekubaliana na hoja za mshtakiwa hivyo kielelezo hicho kimekataliwa...



View: https://x.com/Royal_Tv_Tz/status/1981267744231194891?t=QaijFP1RacshVLjYhxpavQ&s=08
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 140

Anaendelea Mhe. Lissu na maswali ya Dodoso

Ulisema Wakati wa kuandaa taarifa yako ya Uchunguzi ni lazima ufanye reference kwenye Police Notebook na huku ukiangalia yale uliyokuwa umeandika kwenye Polisi Notebook, ni sahihi ulisema hivi?

Samuel Kaaya : Nilisema.

Mhe. Lissu: Yako wapi sasa kwenye maelezo?

Samuel Kaaya : Hayapo.

Mhe. Lissu: Ulisema hapa Mahakamani kuhusu covering letter na ukaiambatabisha na taarifa ya Uchunguzi, Je hayo nayo yapo kwenye maelezo yako?

Samuel Kaaya : Ni kweli nilisema lakini hayapo kwenye maelezo yangu yale ya Polisi.

Mhe. Lissu: Hiyo covering letter umeleta?

Samuel Kaaya : sijaleta kwasababu ni internal communication.

Mhe. Lissu: Kwahiyo haiwahusu Majaji?

Samuel Kaaya : Ni kweli haiwahusu.

Mhe. Lissu: Sasa kama haiwahusu uliisema hapa Mahakamani ili iweje?

Samuel Kaaya : Mimi Sijui.

Shahidi hapa amepiga ile tunaita CHAKUFIA NINI?😀😀😀

Mhe. Lissu: Je barua uliyoandikiwa ya kukuomba ufanye uchunguzi umeiwasilisha kwenye kesi hii?

Samuel Kaaya : Hii haina uhusiano na kesi hii.

Mhe. Lissu: Je barua ya pili umewasilisha?

Samuel Kaaya : Sijui wanayo Mawakili wa Serikali.

Mhe. Lissu: Unasema ulifungua mafile mawili ya Uchunguzi baada ya kupata hizo barua kutoka requesting authority. Je hayo mafile umewasilisha mahakamani kama kielelezo?

Samuel Kaaya : Sijawasilisha.

Mhe. Lissu: Mahakama sasa itajuaje kama wewe ndio uliombwa kufanya uchunguzi kama hujaleta barua uliyoombwa kufanya uchunguzi na pia hujaleta ripoti wala video itakuaminije?

Samuel Kaaya : Itaniamini kwa maneno yangu hapa Mahakamani na hayo maelezo ya Polisi.

Mhe. Lissu: Umewahi kusikia msemo wa Kiswahili kuwa maneno matupu hayavunji mfupa?

Samuel Kaaya : Sijawahi kuusikia.

Mhe. Lissu ; Je mkono mtupu haulambwi?

Samuel Kaaya : Sijawahi sikia.

Mhe. Lissu: Je Mali bila daftari hupotea bila habari?

Samuel Kaaya : Huo nao sijawahi kuusikia.

Mhe. Lissu: Sasa maneno yako na wewe hapa Mahakamani yamepotea bila habari.

Watu wanacheka 😂

Mhe. Lissu: Ulisema habari ya kitabu cha Laboratory Boom Register, Je nayo umeileta hapa Mahakamani?

Samuel Kaaya: Sijaleta pia.

Mhe. Lissu: Hivi ili uwe assigned kufanya uchaguzi utararatibu ukoje?

Samuel Kaaya : Zipo minutes pale kwenye file la Ofisi ndio anaandika huko.

Mhe.Lissu: Hiyo ndio tunaita kwa lugha za ofisi ni Dokezo 70 kwamba inaandikwa kazi fulani aifanye fulani?

Samuel Kaaya : Ni sahihi.

Mhe. Lissu: Sasa umeleta hiyo dokezo 70 hapa Mahakamani?

Samuel Kaaya : Sijaleta.

Mhe. Lissu: Nisaidie ulisema kulikuwa na majalada mawili la kwanza ni taarifa za uongo na la pili ni uhaini. Hayo maneno yako wapi kwenye maelezo yako?

Samuel Kaaya : Hayapo sikuandika.

Mhe. Lissu: Katika uchunguzi wako ulisema hiyo video ilikuwa uploaded kwenye channel ya youtube ya JAMBO Tv ni sahihi?

Samuel Kaaya : sio sahih, mimi nilisema video imepatikana kwenye youtube kupitia account ya Jambo Tv.

Mhe. Lissu: Kwahiyo hiyo video ilipatikana kwenye account ya Jambo TV?

Samuel Kaaya : sahihi.

Mhe. Lissu: Sasa waeleze kama uliweza kubaini mtu aliyeiweka video clip kwenye hiyo account ya Jambo Tv?

Samuel Kaaya : Mimi experts sijibu facts najibu kama mtaalamu.

Mhe. Lissu: Sasa mimi ndio nashitakiwa kuwa nimeiweka huko Jambo TV na wewe ni mtaalamu umekuja leo nataka utusaidie, nani aliweka?

Samuel Kaaya : Account ya Jambo Tv ndio iliweka hiyo account.

Jaji Kalyamaahe: Kwahiyo ulibaini mtu au hukubaini mtu aliyeweka hiko youtube?

Samuel Kaaya : Mimi sikubaini mtu.

Mhe. Lissu: Mimi nashitakiwa kwa kuweka hiyo video huko Jambo Tv basi na mimi nitumie fursa kusema Mwenyezi MUNGU akurehemu na kukubariki sana maana kama mtaalamu umesema mimi sijaweka huko hiyo video nani mwingine atakuja kusema mimi niliweka hiyo video. Ahsante sana.

Part 141 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Mhe. Lissu: Mimi nashitakiwa kwa kuweka hiyo video huko Jambo Tv basi na mimi nitumie fursa kusema Mwenyezi MUNGU akurehemu na kukubariki sana maana kama mtaalamu umesema mimi sijaweka huko hiyo video nani mwingine atakuja kusema mimi niliweka hiyo video. Ahsante sana.😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom