#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Oktoba 15, 2025.
Last time tuliishia part 101 so leo tunaendelea na
Part 102
Leo Tarehe 15/10/2025.
Mheshimiwa Tundu Lissu ameingia Mahakamani.
Amesimama Kizimbani anauliza Polepole amepatikana na Mama anasemaje si Balozi wake?
Majaji wameingia na Shahidi nae kama kawaida ameingia yupo hapa. Inspector wa Polisi John Kaaya.
Karani anasimama Criminal Session No. 19605 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Iwapendeze naitwa Renatus Mkude Wakili wa Serikali niko na Job Mrema, Ignas Mwinuka, Harrison Lukosi, Winiwa Kasawa tunaiwakilisha Jamhuri. Na Mshitakiwa yupo. Lakini pia tuna jambo tunaomba kuiambia Mahakama.
Mhe. Lissu anasema na mimi niko tayari na pia nitakuwa na jambo la kuieleza Mahakama.
Renatus Mkude, tulipokea taarifa ya Msiba wa Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya Shinyanga.
Tumekuwa na utaratibu wa kwenda kushiriki matukio kama haya na tulipanga kuhudhuria kwenye msiba huo kwa vile ni jambo la kibinadamu ilikuwa na rai yetu itakapofika saa tano twende tukamuage huyu ndugu yetu ili tuendelee kesho tena. Ni hayo tu.
Mhe. Lissu anasimama kwenye hilo mimi sina pingamizi lolote na ikiwapendeza wakienda kwenye huo msiba wanipelekee salamu zangu za rambirambi kwa wafiwa.
Lakini pia niwaeleze kuhusu watu waliokuwa wanazuiwa kuingia Mahakaman, nimesema sana jambo hili.
Kasoro juzi Jumatatu sikulizungumzia kwasababu niliambiwa wangeruhusiwa siku hiyo lakini walikuja wakazuiliwa hapo getini.
Kwa taarifa nilizonazo walichukuliwa na maafisa wa uhamiaji na baadae wakafukuzwa nchini ili wasiweze kuingia Mahakamani kushuhudia kesi hii.
Sasa waheshimiwa majaji hii ni mara ya tatu kwa watu wanaotaka kuja kuhudhuria mahakama hii kufukuzwa nchini.
Walianza na Ujumbe uliotoka Kenya ukiongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Kenya, Willy Munyoki Mutunga.
Wakafuata Boniface Mwangi na Agatha Atuhire walikamatwa na kuteswa na kupelekwa mipakani na kutupwa.
Na sasa hili limetokea kwa raia wa Ujerumani na Marekani walioingia nchini kihalali kuja kutaka kuona kinaendelea nini.
Hii ni kesi kubwa kuliko zote ndivyo inasema Katiba yetu ni kesi inayo draw Regional and International attention.
Haya yaliyofanyika Kisutu tayari yapo kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa yapo katika mahakama za haki za binadamu na watu Afrika.
Kwahiyo haya sio mambo madogo kabisa. Mahakama inapoingiliwa inasababisha sintofahamu kwenye mfumo wetu wote wa haki jinai ndani ya Taifa letu.
Mwaka 1958 kulikuwa na kesi kubwa sana katika Mahakama ya Wilaya Dar es salaam Kivukoni ambayo ni Regina Vs Julius Nyerere na wenzake wawili mmoja wapo Robert na mwingine Rashid baldell.
Wakoloni wa kingereza did not dare kuzuia watu kwenda kushuhudia kesi ya kiongozi wao na wanaofahamu historia ya nchi hii Mwalimu alitetewa na Wakili kutoka Wingereza.
Wakoloni hawakukataza pia hawakupiga watu wasiingie Mahakamani.
Kesi ya Jommo Kenyata pia ilikuwa kubwa sana ambayo ilifanyika katikati ya Vita vya Maumau, Waingereza did not dare kuzuia watu kwenda kusikiliza the trial of Jomo Kenyata ilifuatiliwa.
Mwaka 1956 mpaka 1961 tulikuwa na kesi ya Uhaini Afrika Kusini imeelezwa kwenye Long Walk to Freedom, Kesi ya Nelson Mandela hakuna mtu aliyepigwa wala kuzuiwa kwenda Mahakamani, hakuna watu walioteswa ili wasiingie Mahakamani.
Sasa nchi hii baada ya miaka 64 ya Uhuru Serikali yetu na vyombo vya Ulinzi na Usalama inazuia watu wasiingie Mahakamani kwenye nchi ambayo sheria zinasema mahakama ni ya wazi.
Tunafanya mambo ya hovyo kuliko wazungu waliotutawala sisi hapa Tanganyika, walioitawala Kenya na wale wa Afrika Kusini sasa mimi niko Gerezani na Mahakama imeshindwa kufanya lolote.
Sasa ili isije kuja kusemwa baada ya mimi na nyie majaji kutoweka hapa Duniani kuwa nilikuwa kwenye dhambi ya watu ambao walinyamaza kimya mambo haya kutokea. Nimesema kutimiza wajibu wangu na sitaki dhambi ya kunyamazia uovu au maovu, naomba kumalizia hapo.
Part 103 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako.