Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo September 22, 2025

Tunaendelea na

Part 37

Mahakama imejaa.

Watu wapo katika ari ya kusikiliza kinachojiri siku ya leo.

Viongozi wa Chama wapo wakiongozwa na Mhe. John Heche, Makamu Mwenyekiti wa Chama.

Mhe. Lissu tayari ameingia

Na Sauti ya High Court imepigwaa hapa kwa ukali sana watu wote wamesimama.

Majaji wameingia tayari wakiwa na bashasha.

Wanaandika kidogo.

Leo watu wamekunja ngumi kwa vibe sana wakati wa kumsalimia Mhe. Lissu.

Anasimama Karani wa Mahakama kijana mmoja hivi amevaa miwani mfupi kwa kimo.

Anaita kesi hapa anataja namba yake. (Criminal Case 16905/2025)

Jaji Nduguru anamuita Wakili wa Serikali.

Anasimama Katuga anaanza kujitambulisha na kuwatambulisha wenzake sita waliopo hapa.

Majaji wanateta kidogo na kumuuliza Mh. Lissu kama yuko tayari.

Anajibu kuwa yuko tayari.

Hawa Mawakili wa Serikali wamevaa majoho yana nembo ya Bibi na Bwana nafikiri hizi ni kodi zetu kabisa.

Katuga anasema shauri linakuja kwa uamuzi mdogo lakini tuna ombi dogo tunaomba tulitoe kabla ya maamuzi kwasababu tukisubiri maamuzi ombi hilo linaweza kukosa maana kabisa.

Majaji wanateta kidogo.

Je wamruhusu Katuga au wasimruhusu kwenye ombi lake hilo?

Wanajadiliana namna ya kwenda mbele hapa.

Ngoja tuone.

Wametumia muda kidogo kama dakika tano hivi kujadiliana ni kama kila mmoja anamaoni tofauti.

Jaji Ndunguru anasema kwa vile kesi ilikuja kwa ajili ya uamuzi acha tusome uamuzi na hayo mambo mengine yatakuja baadae.

Kwasasa ni uamuzi kwanza hivyo usubiri kwahiyo Jaji anajiandaa kuanza kusoma uamuzi.

Mnakumbuka Tarehe 08/09 shauri lilipokuja kwa ajili ya hoja za awali, mshitakiwa alikuja na mapingamizi ikiwemo hili linalohusiana na hati ya mashitaka.

Tulishamaliza na lile la kwanza la mamlaka ya mahakama.

Sasa tuko na hili la hati ya mashitaka na hoja ya pili alisema viambatanisho vya hati ya mashitaka navyo viko kinyume na sheria vifungu vya 11 na vifungu vingine vya CPA.

Hivyo hizo hoja mbili ndio tutazitolea uamuzi siku ya leo na mshitakiwa alisema kwanini hati ya mashitaka ina makosa yasiyoweza kurekebishika.

Mahakama inaangalia kama mapingamizi hayo mawili yana mashiko.

Mahakama inaangalia sehemu kuu tatu.

1. Kama kweli hati ya mashitaka ina makosa yasiyorekebishika?

2. Je hiyo hati ya mashitaka ilikuwa na marekebisho?

3. Maelezo ya mashahidi yalikuwa na mapungufu ya kisheria ambayo yanaweza kuifanya ikose nguvu?

Mahakama itazingatia hayo.

Hoja ya kwanza ni uhalali wa hati ya mashitaka na hoja hiyo ilijengwa katika kurejea mashauri mbalimbali ikiwemo shauri la Grey na Khatibu Gandi.

Mashauri hayo yanataka hati ya mashitaka iandaliwe kwa mujibu wa English Procedure.

Sasa katika kujibu hilo tutarejea mashauri na sheria.

Kifungu cha 135 cha CPA kimeeleza namna hati ya mashitaka inapaswa kuwa ili iwe sahihi.

Anakinukuu hapa hicho kifungu cha 135.

Kwa mujibu wa kifungu hicho cha 135 kinasema lazima hati iwe na maelezo ya kosa maalumu ambayo mshitakiwa anakabiliwa pia maelezo ya shitaka lenyewe yawepo.

Sasa namna gani hivyo vitu viwili vinaweza kuonekana.

Soma kif. 138 cha CPA kimeelezea statement of the offence and particulars of the offence.

Anakisoma hapa hicho kifungu hapa…

Kumbuka CPA ni Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Sasa hicho kifungu cha 138 kinasema pia maelezo ya kosa yawe yanaeleweka na kwa kifupi ili kumuelezea kosa mtuhumiwa. (Ordinary language)

Anaendelea kukisoma kwa urefu hicho kifungu cha 138.

Sasa kutoka na vifungu nilivyotaja hapo juu. Statement ya offence inapaswa kueleza kosa maalumu ambalo mshitakiwa anakabiliwa nalo na pia kama kosa limerejewa kwa kifungu maalumu hasi na shitaka lizingatie hicho kifungu maalumu.

Vifungu vya 135 na 138 vya CPA ndio vinasema hati ya mashitaka inapaswa kuweje?

Part 38 itaendelea kwenye post inayofuata
 
Part 38

Anaendelea Jaji Nduguru

Sasa turejeee kwenye hati ya mashitaka tuliyonayo hapa mahakamani.

Anasoma statement of the offence na particulars of the offence kwenye hati ya mashitaka kama vipo au havipo?

Anaisoma hati ya mashitaka yote kuhusu maneno ya kukinukisha ya TUNDU LISSU.

Jaji anaendelea...

Sasa tukishasoma hiyo hati tunapaswa kurudi kwenye sheria.

Statement of the offence tunaona iko clear kabisa imeelezwa kwenye hati ya mashitaka.

Kingine ni Particulars of the offence na sheria pamoja na mashauri ukisoma shauri la Mwaikunda linasema lazima maelezo ya kosa yawe yakutosha ana kueleweka vizuri.

Shauri la Isdory lilisema pia ni muhimu sana kuwepo na reasonable information in relation to the charge.

Anasoma kilichosemwa na Jaji katika hukumu ya hiyo kesi ya Isdory aliyoitaja hapa.

Na hivi basi baada ya kurudi kwenye hati ya mashitaka. Information imeeleza suala la nia ya kushawishi kuzuia uchaguzi mkuu na kutishia utawala.

Nia hiyo imethibitika kwa matendo ya kutamka hayo maneno.

Hoja ya kwamba maneno yanamanifest matendo ni suala la ushahidi.

Tunakubaliana na mshitakiwa kuwa pande zote mbili zinabanwa na pleadings. Hatupaswi kutoka nje.

Tunaungana na mshitakiwa katika kulitatua hilo tusubiri ushahidi huo.

Kifungu cha 138 cha CPA tulikisoma na mshitakiwa alisema hati ya mashitaka kwenye kesi kubwa hivi yanapaswa kutengenezwa kwa mujibu wa kesi hizo tajwa za Grey likungu na Khatibu Gandi.

Mshitakiwa alisema lazima kuwepo na particulars of the offence lazima upande wa mashitaka waonyeshe manifestation na lazima iwe pleaded na ielezwe kama alipublish au vipi na pia lazima overt act ionekane.

Hayo yote yanapaswa kuwa pleaded separately ndio alisema hivyo Mshitakiwa akiwa anaegemea kwenye hayo mashauri mawili ambayo ndio muundo qa kiingereza wenyewe.

Shauri la Grey Likungu kuhusu adoption ya English Procedure (English Mode za kuendesha mashitaka) mahakama ilisema nchi ya Tanzania haibanwi kufuata English Procedure and Practice sio lazima kuifuata inaweza kutafuta utaratibu wake bora zaidi.

Tumeyasema hivi ili kuonesha kuwa mahakama hii haibanwi wala kulazimishwa kutumia mfumo wa kiingereza.

Kwahiyo kifungu cha 135 na 138 vya CPA ndio vitatumika katika kuamua jambo hili na tusiende kwa KHATIBU GANDI na Kwa GREY LIKUNGU.

Tunabanwa na sheria yetu wenyewe.

Hoja ya pili kuhusiana na endapo Hati ya Mashitaka ilifanyiwa amendment. Kimsingi ukisoma kosa la treason linaangukia sehemu ya pili ya Penal Code. (Kanuni ya Adhabu)

Mahakama hii imeyapa uzito mwasilisho ya pande zote mbili. Ambapo kif. Cha 262(1) cha CPA kinazungumza kuhusu mshitakiwa anavyopaswa kupelekwa mahakamani mara baada ya kukamatwa. Apelekwe na Charge.

Ukisoma kifungu hiki ni dhahiri hati ya mashitaka katika makosa ambayo mahakama kuu inasikiliza basi hati ya mashitaka inakuwa ni proposed charge au holding Charge na ita exist hadi siku anapelekwa mahakamani na DPP akiona kuna ushahidi basi atatengeneza hati ya mashitaka nyingine na kuisubmit akiwa na nakala tatu pamoja na viambatanisho.

Kifungu hiki kinasema DPP asome kwanza maelezo ya mashahidi akijiridhisha ndio anaandaa hati ya mashitaka na kuiwasilisha mahakamani.

Kwahiyo hati inayopelekwa mahakama kuu ndio hati halisi ndio mshitakiwa anasomewa wakati shauri lake linapoanza kusikilizwa. Na ndio hati ambayo ilitumwa Kisutu.

Hati ambayo imeletwa hapa mahakama kuu haijawahi kubadilishwa na haina marekebisho yoyote.

Kwahiyo hoja ya kwamba imefanyiwa marekebisho haiko sahihi tunakubaliana na mawakili wa serikali.

Part 39 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
“Waheshimiwa majaji wa Mahakama Tukufu, mimi Tundu Antipas Lissu ni Mtanzania Mtiifu kwa Nchi yangu. Maneno yaliyosomwa hapo ni yangu, niliyasema mimi mwenyewe kwa kinywa changu. Lakini,hakuna hata neno moja ambalo ni kosa la jinai. Mimi ni mpinzani, ninapinga Serikali"

Tundu Antipas Lissu
22 Septemba 2025
20250923_060502.jpg
 
KIVUMBI MAHAKAMANI.

Mhe. Lissu : sasa waeleze kama umewahi kufanya uchunguzi wa kesi ya aina hii.

George : publication ya false information ya Dr. Slaa.

Mhe. Lissu : Iliishia wapi?

George Hiyo sikumbuki iliishia wapi,Kesi nyingine ya Lembeli, alikuwa Mbunge

Mhe. Lissu: iliishia wapi?

George : kimya

Mhe. Lissu : waeleze majaji katika miaka yako 22 umewahi kufanya kesi ngapi mtu muhimu kisiasa ni mshitakiwa. Mfano Kama Tundu Lissu? Nataka kujua kama una uzoefu.

George : Kesi ya nne nae iliondolewa ya John Heche Tarime iliondolewa kule Tarime akimuita Rais wa Nchi ana akili ya Tope.

Swali: Je iliishia wapi?

George: Nayo baadae iliondolewa.

Mhe. Lissu : kwahiyo miaka 22 yako ya Upolisi hujachunguza kesi yoyote ya makosa ya aina hii hajapatikana na hatia?

George : ni kweli hakuna ambae aliwahi kukutwa na hatia.

Mhe. Lissu : Kuna yeyote ukiachana na hii ambayo mahakama ilifikia mwisho mahakama ikatoa hukumu?

George: zote hazikufika hatua ya judgement.
 
Wana JF kuna mahali tulipitiwa na kujisahau.. Tulipaswa kuwa na mada maalum ya Tundu Antipas Lissu.

Mwanasheria nguli, mwanaharakati wa haki za binadamu na sasa mfungwa wa kisiasa wa kesi ya uhaini na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanganyika

Ana historia yake maalum .. Ana mengi mazuri ya kiwango kaifanyia Tanganyika.. TUMUENZI SASA. NI WAKATI WAKEView attachment 3381742
(7,029) Historia fupi ya maisha ya shule ya Tundu Lissu | JamiiForums Historia fupi ya maisha ya shule ya Tundu Lissu
Mkuu kama yale majibizano ya mahakamani ( cross examination), tunaweza kupata itakua farajra. # free Humphrey Polepole
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo Oktoba 7, 2025

Jana tuliishia part 53 so leo tunaendelea na

Part 54

Imepigwa High Courrrrrttttttttttt ni sauti ya Askari inatoka kizembe kabisa.

Watu wote wanasimama kwa utii mkubwa sana.

Majaji wanaingia na kutoa heshima ya kuinama mahakama yote inafanya bowing.

Mh. Lissu ameingia anawaambia watu changanyachanganya ile style ya kukunja ngumi na kuizungusha.

Muda huu anatoa makabrasha yake ni mengi sana.

Anayafungua fungua kwa vibe.

Shahidi hajaingia bado Mahakamani.

Namuona anaingia amevaa kaunda na kanyoa kipara.

Huyu Afande George ni mfupi wa kimo.

Leo amepanda kizimbani anacheka cheka.

Majaji wanaandika hapa.

Kesi haijaanza.

Kimya kidogo kimetanda hakuna kinachoendelea kama dakika 5 hivi.

Anasimama karani Criminal session No. 19605/2025.

Anasimama Renatus Mkude, Wakili Mkuu wa serikali, Johari, Katuga, Mrema, Cathbert Mbiringe na Winniwa Kasawa.

Amemaliza kuwatambulisha mawakili wake.

Mhe. Lissu anaulizwa kama yuko tayari.

Nasikitika kusema Dr. Stephen amezuiliwa kuja mahakamani na amezuiliwa na afisa wa uhamiaji.

Idara ya Uhamiaji wanazuiaje mtu kuingia mtu mahakamani.?

Lakini pia mgeni aliyeingia ndani ya nchi na ana Visa hawezi kukatazwa kuingia mahakamani.

Sasa hawa Uhamiaji wanahusika nini na hawa watu wanaozuia watu kuja mahakamani.?

Mimi jukumu langu ni kusema tu hata ikija kutokea mkaamua kunipeleka kokote mtakapoamua baada ya uamuzi wetu nitaenda huko nikiwa na amani (happily) lakini siwezi kunyamaza.

Niko tayari kuendelea.

Majaji wanaandika hapa.

Majaji wameteta kidogo hapa. Kuhusu swala alilolizungumza Mh. Lissu.

Jaji anawasha kipaza sauti muda huu, tumekusikia mshitakiwa tutafuatilia na tutawasiliana na Msajili.

Mhe. Lissu anadakia kuwa huyo yupo na hataondoka nimemwambia asiondoke kabisa.

Jaji anasema ni sawa.

Jaji anamkumbusha shahidi kuwa yuko chini ya kiapo. Lissu anaanza.

Mhe. Lissu . Jina lako ni George

George : ni jina langu.

Sasa nakuuliza maswali nataka ndio au hapana.

Nikisema toa maelezo toa.

Sitaki rongorongo.

George : sawa.

Mhe Lissu. Wambie majaji kama uliandika maelezo huko nyuma.

George . Ndio niliandika.

Mhe Lissu : ni kweli au si kweli uliandika maelezo mara mbili. Tar. 08 na 10 April 2025.

George : Niliandika mara moja aaaaaa ni kweli niliandika mara mbili.😂

Mhe. Lissu : waeleze kama ukionyeshwe hayo maelezo yako utayatambua?

George :Nikionyeshwa nitayatambua.

Mhe. Lissu : Na mimi ninayo. Sasa niliyo nayo ni copy. Waheshimiwa majaji naomba shahidi aonyeshwe maelezo ya maandishi ya mkono wake nisitumie haya copy ya kwangu.

Mawakili wa Serikali: wanatafuta hayo maelezo, wanafungua makabrasha yao hapa.

Part 55 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 55

Anaendelea Mhe. Lissu

Mhe Lissu : umeyapata eee?

George : nimeyapata.

Mhe Lissu. Sasa waeleze majaji hivyo ni vitu gani? anza na ya kwanza tafadhali.

George : Ya kwanza ni karatasi ya maelezo yak wangu SSP George.

Mhe. Lissu . Hati ya maelezo yako? Sahihi ni yangu.

George : ya pili pia ni maelezo yangu ya Nyongeza ya tarehe 10.

Mhe.Lissu : je hayo maelezo yana sahihi na wamabie ni za kwako?

George : ni za kwangu sahihi zote.

Mhe. Lissu : Wambie majaji kama ni za kwako kama uko tayari ziingie kama ushahidi wa vielelezo vya utetezi?

George : Hii ya kwanza niliandika

Mhe.Lissu : umeelewa swali langu kweli?

George : niko tayari ziingie mahakamani kama sehemu ya ushahidi.

Mhe. Lissu : Waheshimiwa Majaji naomba hizo nyaraka ziingie kama kielelezo E01.

Anasimama Wakili wa Serikali: Renatus Mkude sijui anataka kusema nini.

Anasema Wah. Majaji naomba Igans semboka aseme. Anasimama Ignas hapa. Waheshimiwa Majaji sisi upande wa Jamhuri mshitakiwa hajazingatia taratibu kwasababu misingi ya kisheria ya maelezo ya shahidi ni kwa ajili ya impeachment purpose na waheshimiwa majaji utaratibu wa kuzingatiwa wa namna ya kuwasilisha maelezo umefafanuliwa na maamuzi lukuki wa mahakama ya rufani ni kifungu cha 154 ambacho kwa sasa ni kifungu cha 163 kwenye R.E 2023. Kinasomwa kwa pamoja na 164 na 173 vya EVIDENCE ACT.

Kimsingi katika vifungu hivi anaweza kuempeach kwa kumuonesha maelezo yake na akitaka kumuonesha lazima afuate utaratibu.

Naomba niwarejeshe katika mashauri matatu.

Shadrack Sospter Mkaruka Mangangari vs Jamhuri Rufaa No. 233/2022 Tanzlii 14/03/2025.

Lilian Jesus vs Jamhuri shauri la rufaa no. 151/2018 Mahakama ya Rufaa.

Shauri la Mahakama ya rufaa ambalo la Ruchere Mwita vs Jamhuri shauri la rufaa no. 348/2013.

Waheshimiwa Majaji mashauri haya yote yalieleza utaratibu wa kuzingatia na naomba ninukuu.

Mhe. Lissu: wanaaongea hizo kesi hawanipatii, wanasema ziko tanzlii mfungwa anafikaje huko.

Jaji: mpatieni tafadhali.

Kumbe hawana. Wameambiwa wakatafute.

Sasa anaendelea.

Mh. Jaji kwenye kesi zote tatu Mahakama ya rufaa ilisema

Jaji huwezi kusema kesi zote tatu, tuambie unasoma kesi gani muda huu.

Wakili: samahani Jaji ni ukurasa wa 26 kesi ya Jesus hii Mahakama ilisema kuhusu hatua za ku impeach shahidi.

Shauri la Jamhuri vs Mnawara hamis Nyanda na wenzake 9 la mwaka 2022. Tanzlii. Jaji Manyanda alisema zipo taratibu 8 za kuzingatia maamuzi ya maelekezo ya mahakama ya rufani.

Hivyo Mh. Jaji tunaona mshitakiwa hajazingatia vigezo.

Anasimama Ajuaye Wakili wa Serikali, Waheshimiwa Majaji lengo la kutumia maelezo ni msimamo wa sheria kwamba yanatumika kwa impeachment peke yake.

Test credibility ya shahidi na yale aliyoyaandika kabla ya kuja mahakamani na ndio maana S.
163 Cap.6 R.E 2023 anakisoma na kukifafanua anavyojua yeye.

Kwahiyo tunaona procedure hazijafuatwa na ombi lake lisikubaliwe.

Anasimama Katuga anasema Waheshimiwa Majaji naunga mkono kilichosemwa na mawakili wenzangu ni msimamo wa sheria kwamba kielelezo kabla hakijapokelewa ni msimamo wa sheria lazima kifuate utaratibu wa kisheria.

Kesi ya Mwanjilisi and 3 others Criminal Appeal no. 154/1994 imesema pia kuhusu utaratibu.

Kifungu cha 163 Cap. 6 kinatoa njia mbili. Kwa kumuonyesha au kutokumuonyesha.

Mashauri waliyosema wenzangu ndio sasa yanaelezea taratibu za kufuatwa.

Naomba maelezo hayo yasipokelewe.

Part 56 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 56

Wamemaliza amesimama Lissu kujibu hilo pingamizi.

Kwa vile ni sheria.

Shahidi amesema yeye hana shida maelezo ni yake na yapokelewe.

Mawakili wake hawataki kabisa yapokelewe wanasema kama lengo ni kufanya impeachment sasa kama hana lengo hilo wamejuaje mapema hivi kwamba yasipokelewe kabisa.😂 Ngoja tuone lakini.

Mhe. Lissu anasema Waheshimiwa Majaji nimewasikiliza mawakili wa serikali na jibu langu ni fupi, nakubaliana nao, nakubali kuwa nilikosea kuanzia hatua ya tatu ili nisipoteze muda niko tayari nianze upya kwa utaratibu ambao mahakama ya rufani imemuelekeza.

Anasema siwezi kufanya ilivyo sahihi kwasababu ya Estoppel. Kwasababu I'm estooped.

Kifungu cha 131 cha Evidence Act kinasema ukifanya jambo na upande mwingine ukachukua hatua, Mawakili wa serikali wamepinga wakati nyaraka bado haijapokelewa na mimi nimewakubalia.

Estopel haihusiki hapa hili jambo wao linawaathiri nini kama shahidi ni wakwao na maelezo ni ya kwao.

Hakuna wanachoathirika.

Majaji wanaandika hapa

Anaitwa Katuga kwa ajili ya rejoinder anasema kifungu cha 131 cha Evidence Act kinatuzuia kurudi nyuma anapokuwa amekosea.

Intentionally kinatuzuia, tunamalizia kuwa pingamizi letu liko kishseria na limeletwa kwa ajili ya kulinda integrity.

Lissu anasema hii ya integrity nayo kaitoa wapi? Katuga anasimama anasema basi naomba niitoe.

Watu wanacheka 😂😂😂😂

Wanaandika majaji kwa muda sasa kama dakika 15 hivi

Wamemaliza na kuanza kujadili kidogo.

Majaji wanasema ni endapo una concede PO mahakama inapaswa kufanya nini?

Mahakama ya rufani imeshatoa maelekezo kwahiyo PO kama itakuwa sustained basi itakuwa sustained na kuidismiss kwasababu upande wa Pili na inareject hiyo nyaraka. Nyaraka haijapokelewa.

Maswali yanaendelea sasa.

Mhe : Elimu yako ulisema jana. Ulisoma kozi ya kwanza Moshi mieizi 6?

George : Ni kweli.

Mhe.Lissu : na baada ya hiyo course ukafuzu na kupata cheti? Jibu: Ni sahihi kabisa.

George : ukaajiliwa kama Polisi Constable?

George : ni sahihi kabisa.

Mhe.Lissu : Baada ya hapo ulienda kusomea Course ya Mkaguzi Msaidizi wa Polisi hapa Dar es Salaam.

George : Ni kweli.

Mhe.Lissu : hayo mafunzo ya mkaguzi msaidizi wa polisi yalichukua miezi mingapi?

George : Miezi 9.

Mhe. Lissu : na baada ya hiyo miezi 9 ulipata cheti?

George: Kweli nilipata cheti.

Mhe. Lissu : Ukapandishwa cheo pia?

George : Kweli nilipandishwa cheo kuwa Assistant Insp. of Police.

Mhe. Lissu : Sasa shahidi baada ya mafunzo hayo ulienda kusoma course ya tatu, Gazette officers course

George : ni sahihi kabisa, nilienda chuo cha Polisi Dar ni kweli.

Mhe. Lissu : na ulisoma kwa miezi 9.

George : kweli kabisa,

Anasema kweli kwa nguvu sana huyu shahidi.😂

Mhe. Lissu : Baada ya hapo hujawahi kusoma tena na kupata cheti hadi leo? Kwa mujibu wa ushahidi wako?

George : nimesoma course nyingine ndogondogo.

Mhe. Lissu : Sijakuuliza ndogo ndogo.

George: Nimesoma refresher course kwa mwezi mmoja.

Mhe. Lissu Chuo gani?

George: Mwezi mmoja pale Kidatu. Nikapata cheti.

Mhe. Lissu : na Chuo gani kingine?

George: Mubarak Police Academy kule Egypt miezi miwil kipo Cairo.

Mhe. Lissu : Ukapata shahada gani?

George: Nikapata vyeti viwili pale.

Mhe Lissu: Sasa naomba uwaeleze majaji kama kuna mafunzo mengine uliyohudhuria yaliyokupa kitu kingine zaidi ya Cheti? Nataka kujua mafunzo mengine uliyowahi kupata.

George : nina advance diploma ya uhasibu nilimaliza 2001, Post Graduate Diploma in finance Chuo cha Sauti.

Part 57 itaendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 57

George: Pia nimesoma masters of Bussiness administration nilimalizia Kisii University nchini Kenya.

Nikasoma Masters of Human Resource Management Chuo Kikuu huria cha Tanzania. Nikapata pia cheti. Na sasa nimeanza PHD.

Mhe. Lissu : ni sahihi nikisema kwamba kwa mujibu wa PGO za 2021 wewe ni Professionally qualified member of the Police Officer?

George: NI SAHIHI KABISA ANAJIBU.

Mhe. Lissu : Unatambulika kama ni professionally officer?

George; Ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu : Sasa naomba waeleze kama maelezo haya ya hiki kisomo umeyaweka kwenye hati yako ya maelezo ya mashahidi?

George: Nimeweka elimu yangu ya Kipolisi tu.

Mhe. Lissu: Naomba nikusomee maelezo yako ya Tar. 08/04 umesema hivi kuhusiana na elimu yako. Mimi mtajwa nimeajiriwa na kufanya kazi mikoa mbalimbali...... Anaendelea hapa.

Anamsomea maelezo yake.

Sasa katika niliyosoma kama kuna chochote kinahusiana na vyuo vya Polisi ulivyotaja jana?

George : hakuna kabisa hayo mambo niliyosema jana kuhusu vyuo vya Kipolisi na vyeti nilivyopata.

Mhe. Lissu : ieleze mahakama kama mafunzo yako mengine nje ya upolisi hayo madiploma ya uhasibu na mengine ya sauti kama yapo kwenye hati yako ya maelezo wambie kama yapo?

George : kwenye hiyo hati haipo ila jana nikiwa naulizwa nilisema.

Mhe. Lissu ; Ulitaja au hukutaja jana?

George: Sikutaja haikuwa na umuhimu na jana sikuulizwa ndio maana sikutaja.

Mhe.Lissu : na hizo masters hukutaja pia?

George: Ndio sikutaja kwasababu sikuulizwa ila leo umeniuliza ndio maana nimetaja.

Mhe. Lissu : twende kwenye ushahidi wako wa siku ya tar. 04/04/2025 uliiambia mahakama kwamba uliletewa taarifa za video clip yenye uhaini na ASP John Kaaya.

George : Ni kweli.

Mhe. Lissu : Ulisema pia ASP John kaaya alikwambia aliona video clip kwenye mtandao wa YouTube wa Jambo TV yenye kichwa cha habari uso kwa uso na watanzani ni sahihi?

George : ni kweli heading ilikuwa inasomeka hivyo.

Mhe. Lissu : Sasa wambie majaji kama maneno yako hayo yapo kwenye maelezo yako ya mashahidi?

Mhe. Lissu : Hayo maneno hayapo kwenye maelezo yangu.

Mhe. Lissu : ulisema kwamba baada ya kuambiwa hivyo ulimwambia ASP John Kaaya. Akuonyeshe hiyo video clip?

George: Ni kweli ilikuwa hivyo.

Mhe. Lissu : pia jana ulisema kwamba ASP kaaya alikuonyesha sehemu sehemu?

George: Ni kweli alifanya hivyo kwa siku ya tar. 04.

Mhe. Lissu : Waeleze kama haya maneno ya alikuonyesha sehemu sehemu hakukuonyesha yote kama yapo kwenye hati yako ya maelezo.

Yapo au hayapo?

George : Sidhani kama ipo nadhani haitakuwepo. Haipo sawa.

Mhe. Lissu anamsomea na kumuuliza ni kweli au sio kweli.

George : uwa ni kweli.

Mhe. Lissu : Mtu anayetoa maudhui ya uchochezi ni kosa la uhaini. Kweli au si kweli?

George : naomba nitoe maelezo.

Mhe.Lissu : Sitaki maelezo we jibu maudhui ni kosa la uhaini au sio kosa la uhaini.

George : ni kweli ni kosa la uhaini.

Mhe. Lissu : sasa jana ulitaja kifungu cha uhaini ni 39?

George: Ni kweli we anza kusoma kwenye execution..

Mhe. Liissu : unasema??????

George: Samahani ni EXECUTIVE.

Mhe. Lissu ningeshangaa na kisomo chako chote usijue kingereza?

George: Nimekosea hapo.

Anamsomea hicho kifungu cha 39(d).

Mhe. Lissu : Je video uliyoisoma hayo maudhui ya uchochezi yanaingia kwenye 39(2)d?

George: Ndio yanaingia.

George: Naona kama vingine unaruka kwenye hicho kifungu.

Mhe. Lissu : twende taratibu tutamaliza vyote.

Mhe. Lissu : naomba nikusomee maneno nikiyoshitakiwa nayo. Maneno ya uhaini yanasema hivi WANASEMA KITU KIMOJA HAPA WANASEMA HIVI MSIMAMO HUU UNAASHIRIA UASI NI KWELI NI KWELI KWASABBAU TUNASEMA TUNAENDA KUZUIA UCHAGUZI NA TUTAUVURUGA NA TUTAENDA KUKINUKISHA.

Swali langu Je haya niliyosoma yapo kwenye hati ya mashitaka?

George: Hayo uliyosoma hayapo.

Part 58 itaendele kwenye post inayofuata

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 58

Mhe. Lissu : ukaelezea sababu za kumwambia kufungua jalada kwamba ulitaka kujua kama ni halisi au laa?

George: Ni kweli kabisa ilikuwa hivyo.

Mhe. Lissu : hayo maelekezo kwa Michael Gyumi ulitoa tarehe ngapi?

George: Ilikuwa Tar. 04/04/2025.

Mhe. Lissu : waeleze majaji kama hayo maneno kwamba ulimuelekeza Michael Gyumi afungue hilo jalada tar. 04/04.

George : yapo hayo maelezo.

Mhe. Lissu amempa maelezo asome ili kuonesha hayo maelezo. Anayasoma hapa.

Mhe. Lissu: Tafuta sehemu ambayo tar. 04 ulimuelekeza Michael Gyumi afungue hilo jalada. Naona unasoma tu hueleweki hata unasoma nini?

Shahidi anatafuta hapa.

Kimya kidogo.

George: Niliamuru jalada kufunguliwa ila Jina la Insp. Gyumi halipo kiukweli.

Mhe. Lissu : Je nilitaka kujua kama hiyo video halisi au laa?

George: Hayo maneno hayapo kwenye maelezo yangu

Mhe. Lissu : wakati unaangalia sehemu sehemu za video clip ulisema ulikuwa na police notebook na kuandika aliyokuwa anakwambia Kaaya.

George: Ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu : Je hayo maneno kwamba ulikuwa na Police notebook yapo kwenye maelezo yako au hayapo?

George : maneno hayo hayapo kabisa, ningeandika kurasa 200.

Mhe. Lissu: Kweli au si kweli kwamba ASP Gyumi linajitokeza Tar. 08/04 kwa mara ya kwanza?

Anamsomea alichoandika tarehe 08.

George : si kweli alishaonekana nilitaja timu mimi.

Mhe. Lissu : wambie majaji kama umewahi kutaja majina ya hiyo team yako?

George: Hiyo timu sikuwahi kutaja kabisa.

Mhe Lissu : Je ASP Kaaya alikuwa ni mmoja wa hiyo timu?

George : Yeye hakuwepo kwenye hiyo timu alikuwa anapeleleza kivyake.

Mhe. Lissu : Je Andrew Churu alikuwepo au hakuwepo?

George: Huyo nae hakuwepo.

Mhe. Lissu : Je ASP malugala nae alikuwepo kwenye timu uliyounda wewe?

George: Hakuwepo pia.

Mhe. Lissu : Je Elibariki Kaaya?

George: Hakuwepo.

Mhe. Lissu : Katika hati yako ya ushahidi kuna jina la Polisi yeyote ambae uliyeunda wewe lipo kwenye orodha ya hiyo timu yako.?

George : kuna timu mbili hapo,
Alikuwepo ASP Michael Gyumi, ASP Ibrahim, Senior Superitendent Reuben Mwakabonga, ASP Nunu, Detective Koplo Ibrahim, Mimi Mwenyewe, Detective Copro Ramadhani.

Mhe. Lissu : wote uliowataja na hao wengine saba kuna mahali umewataja kama timu ya upelelezi?

George : Kwenye maelezo yangu sijawataja.

Nafikiri hawa ndio wasiojulikana leo tumetajiwa pia.😂😂😂😂

Mhe. Lissu : Tar. 07/04/2025 ulisema majira ya mchana nilimuelekeza kupakua na kuitunza kwenye flash disk?

George: Ni kweli kabisa nilimwambia hivyo.

Mhe.Lissu : Naomba uwasomee Majaji maneno yanayoanzia siku ya tar. 07/04/2025 mpaka yanapoanza tarehe 08/04/2025.

Kwenye hayo maelezo hakuna mahali kokote kuwa ulimuagiza apakue hiyo clip, ni kweli au si kweli.

George : hayo yapo.

Mhe. Lissu: haya soma tuone.

George anasoma hapa ila Sauti imekauka anatetemeka.😂Kumbe na wao kuna mahali huwa wanakuwa wadogo.

Mhe. Lissu : Sasa yote uliyosoma kuna mahali nilimuelekeza Kaaya kuipakua.

George : Kwa haya niliyosoma sasa hivi hayupo huyo mtu anayeitwa Kaaya.

Mhe. Lissu : umemtaja hapa DCP Ramadhani Ng'anzi?

George: Ni kweli nilimtaja

Mhe. Lissu : Na kwenye ushahidi wako jana ulisema kwamba baada ya kufungua jalada ulimpigia DCI Ramadhani Kingai?

George: Ni kweli anaitwa Kingai.

Mhe. Lissu : na ulisema ulimpa taarifa kuhusu jalada hilo la uchunguzi?

George: Ni kweli nilifanya hivyo.

Mhe. Lissu : na alikwambia mawasiliano nae uwe unapitia kwa Ramadhani Ng'anzi ndo alivyokwambia Kingai?

George : ni kweli aliniambia hivyo kwenye jalada hili.

Mhe. Lissu : hata mimi nakuuliza kuhusu jalada hili.

Mhe. Lissu : je unafahamu kuhusu Chain of command?

George: Nafahamu vizuri.

Mhe. Lissu : ni kweli au sio kweli Boss wako ni ZCO wewe kama Deputy wake?

George : Ni kweli.

Mhe. Lissu : ZCO Boss wake ni ZPC?

George: Yes ni kweli Boss wake ni ZPC.

Mhe. Lissu : Nataka unisomee 6(16) PGO.

George Anapewa hapa kitabu cha PGO

Part 59 inaendelea post inayofuata,

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali
 
Updates kesi ya uhaini
Part 59

Naona George kapewa PGO

Anaisoma hapa kuhusu duties of regional and division crime officers.

Inasema investigators watakuwa responsible kwa maboss wao.

Mhe Lissu : Ni kweli wewe kama kaimu ZCO ulikuwa unawajibika kwa Murilo kama Boss wako?

George: aaah! eeeh unajua

Mhe Lissu : ni kweli au si kweli kama acting ZCO ulikuwa unawajibika maelekezo kutoka kwa ZPC.

George: Ni sahihi nina channel mbili.

Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa PGO hii ulikuwa unawajibika kumpa taarifa ZPC ni sahihi?

George: Ni sahihi na alikuwa anapata taarifa na kila hatua alikuwa anapata.

Mhe. Lissu : turudi kwenye maelezo yako ya shahidi yote kuna mahali kokote umemtaja ZPC

George: Kwa maelezo haya hakuna nilipomwandika.

Mhe. Lissu : Je kuna mahali ulisema ulikuwa unampa taarifa, kuna mahali umesema?

George : Kwenye maelezo hakuna hilo jambo, sijasema kwenye hayo maelezo.

Mhe. Lissu :Je kuna mahali ulisema Muliro amekupa maelekezo yoyote hapo?

George: Hakuna mahali nimesema hilo kwenye maelezo yangu.

Mhe. Lissu : wambie majaji Mafwele alirudi kazini lini?

George : kama sikosei kati ya tar. 01 au 02 mwezi wa 5 kwahiyo nisingeweza kumtaja. Unajua upelelezi uliendelea

Mhe. lissu anamdakia kwa juu Kaka unajibu maswali yangu acha rongorongo.

Mhe. Lissu : ni kwelI Dcp Ng'anzi alikuletea Boss mpya anayeitwa Amin Mahamba?

George: ni kweli alifanya hivyo.

Amin kama ile ya Idd Amin lissu anasema hivyo 😂

George : Tar. 08/04 ndio alimleta ACP Amin Mahamba.

Mhe Lissu : Ni sahihi nikisema kuanzia tar. 04 hadi 08 ni sahihi wewe ndio uliongoza hiyo timu? na alipokuja Amin akaanza.

George ni sahihi Mahamba ndio akawa kiongozi.

Mhe. Lissu : Je Amin alilichukua jalada likiwa la uhaini au la uchunguzi?

George ; lilishakuwa la uhaini tayari.

Mhe. Lissu : wewe ndie uliyefanya maamuzi ya kulifanya liwe jalada la uhaini na sio Mahamba Amin.

George : Ni mimi ndie niliyeamua.

Mhe. Lissu nimefurahi sana. Mimi napenda kukamata waongo. Ngoja tumsubiri Amin Mahamba.

Mhe. Lissu : wambie majaji kwamba aliyekwambia kwamba ufungue uhaini ni Kingai?

George: si kweli, nilivyoona element zimekamilika nikaelekeza mimi mwenyewe.

Mhe. Lissu : hizo siku nne ulizochunguza kama ulitoa taarifa ya ofisi ya DPP au hukutoa? Nina maelezo yako kumbuka.

George : Kwamba?

Mimi kama mimi sikutoa hiyo taarifa na sikumwambia ofisi ya DPP.

Mhe. Lissu : Miaka yako 22 ya Upolisi umewahi kufanya uchunguzi wa appendix C makosa ambayo yanashughulikiwa na watu wa ngazi yako.

George: hizo za appendix C.

Mhe. Lissu: usiwe na kimbelembele

Mhe. Lissu : sasa waeleze kama umewahi kufanya uchunguzi wa kesi ya aina hii.

George : publication ya false information ya Dr. Slaa.

Mhe. Lissu : Iliishia wapi?

George Hiyo sikumbuki iliishia wapi,Kesi nyingine ya Lembeli, alikuwa Mbunge

Mhe. Lissu: iliishia wapi?

George : kimya

Mhe. Lissu : waeleze majaji katika miaka yako 22 umewahi kufanya kesi ngapi mtu muhimu kisiasa ni mshitakiwa. Mfano Kama Tundu Lissu? Nataka kujua kama una uzoefu.

George : Kesi ya nne nae iliondolewa ya John Heche Tarime iliondolewa kule Tarime akimuita Rais wa Nchi ana akili ya Tope.

Swali: Je iliishia wapi?

George: Nayo baadae iliondolewa.

Mhe. Lissu : kwahiyo miaka 22 yako ya Upolisi hujachunguza kesi yoyote ya makosa ya aina hii hajapatikana na hatia?

George : ni kweli hakuna ambae aliwahi kukutwa na hatia.

Mhe. Lissu : Kuna yeyote ukiachana na hii ambayo mahakama ilifikia mwisho mahakama ikatoa hukumu?

George: zote hazikufika hatua ya judgement.

Part 59 itaendelea kwenye post inayofuata,

Naomba repost yako.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 60

Mhe. Lissu : wakati unaongoza hiyo timu ulisema, Tar. 06/04 ulimtafuta Mkurugenzi wa Jambo TV John Marwa?

George : siwezi kukutajia ila nilipata namba ya kiongozi wa Jambo TV sikujua jina lake kama ndio Marwa.

Mhe. Lissu : Huyu Kiongozi wa Jambo TV uliyemtafuta ulimuomba akupatie hiyo video clip halisi iliyochukuliwa kwenye mkutano?

George: Ni kweli.

Mhe. Lissu : ni kweli huyo kiongozi alikwambia mfanyakazi yupo Dodoma?

George: Ni kweli, alinipa namba ya simu pia ni kweli ya huyo mfanyakazi wake.

Mhe. Lissu : ni kweli namba hiyo ulimpa DCP Ng'anzi?

George: Ni kweli nilifanya hivyo.

Mhe. Lissu : ni kweli Ng'anzi alimpatia Andrew Churu yule Polisi mwingine?

George: Hilo sijui kwakweli.

Mhe. Lissu : ni kweli tar. 07/04 DCP Ng'anzi alisema amempata huyo aliyerekodi?

George: Ndio ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu : Na memory card nayo alikwambia imepatikana?

George: Ni kweli aliniambia hivyo.

Mhe. Lissu : Ni kweli DCP Ng'anzi alikwambia kwamba memory card na card reader yake vitaletwa siku hiyo hiyo na Andrew churu ofisini kwako?

George: Ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu : Ni kweli au si kweli kwamba siku ya tar. 07/04 Andrew Churu alisafiri kutoka Dodoma hadi ofisini kwako na kufika usiku?

George: Ni sahihi kabisa.

Mhe. Lissu : Je alikuja na hizo card, na vitu vingine?

George: Ni sahihi alikuja navyo na alikuja pia na hati ya makabidhiano.

Mhe. Lissu : acha kiherehere hiyo hati sijakuuliza.

Mhe. Lissu : je ulisoma maelezo ya P hiyo tarehe 07 ulivyoletewa.

George : ni kweli nilisoma.

Mhe. Lissu : Kwa vile ulisoma, kweli au si kweli huyo P alisema ni yeye ndie alirekodi mkutano na ni yeye alirusha kwenye Jambo TV akaunti?

Anamtafutia maelezo ya huyo P na anamwambia ayasome.

Anasoma George "kuwa mimi nakumbuka mkutano ...”

anasimama Katuga anasema haya maelezo sio yakwake shahidi kwahiyo asiulizwe.

Mhe. Lissu anajibu shahidi mwenyewe ndio kasema kuwa alipelekewa maelezo na huyo P akasoma, na maelezo hayo ndio yanasema nani alichapisha?

Majaji wanasema msomee wewe tafadhali.

Mhe. Lissu anasoma kuwa P anasema ni wao Jambo TV ndio walikuwa wanarusha. Na wao ndio walirekodi.

Mhe. Lissu : Je mimi ndie niliesambaza na kuchapisha?

George : ndio ni wewe uliyechapisha.

Amesimama Katuga Mh. Tunaomba twende kwenye health break tutaendelea.

Mhe. Lissu anasema sawa twende maana huyu shahidi ili nimalizane nae nahitaji siku zingine kama mbili au tatu. Kwahiyo bado tuko nae sana. Siwezi kumuacha haraka.

Majaji wanaandika hapa kidogo.

Sasa twende break tutarudi saa tisa mchana.

Part 61 itaendelea tukitoka break

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali
 
Back
Top Bottom