Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Breaking newzzzzzzzzzzzzzzzzz.

M/kiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Mhe Tundu Lissu amegoma kuendelea na kesi inayomkabili mpaka watu waliozuiliwa kuingia Mahakamani kusikiliza kesi hiyo watakaporuhusiwa.

Asema hii siyo Mahakama ya Kijeshi bali ni Mahakama ya Umma.
FB_IMG_1758043011053.jpg
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 24

Anaendelea Mhe. Lissu

Ukiangalia maelezo ya mashahidi ambao ni raia wa kawaida yanatofautiana na maelezo ya mapolisi wenzao.

Maelezo ya AMANI MICHAEL kwenye orodha ni No. 20.

Huyu ni Detective Kopro ukisoma maelezo yake kuna askari amemuandika Kopro Robert, amemuandika maelezo Kopro Amani.

ASP Masalanga No. 21 na huyo vilevile ameandikiwa maelezo yake na another officer, nathibitisha kwa uaminifu nimemuandika na nimempa asome.

ASP. Charles Makunja kutoka kule Songea uthibitisho mimi D.cp ... nathibitisha nimemuandika maelezo na nimempa asome ameridhika yako sawa.

Sasa waheshimiwa mtapata muda kuangalia hayo niliyosema hapo juu.

Maelezo ya mashahidi yanapaswa kuandikwa kwa mujibu wa sheria kabisa na yakiandikwa yapelekwe kwa DPP na baadae yawe committed na tunafika Mahakama kuu.

Maelezo hayo yote yalisomwa Mahakama ya Kisutu kama yalivyo na yapo kinyume na sheria.

Hao waliojiandikia sio maelezo na yapo cha Sheria.

Sasa naomba nihamie kwenye maelezo ya akina P kuanzia P1 hadi P11 yalisomwa hadharani kama yalivyo na yameletwa mahakamani kama yalivyo. Yenye majina ya akina P.

Yanakiuka kifungu cha 194(4) cha CPA na rule 7 za kanuni ya ulinzi wa mashahidi.

S. 194 cha CPA inasema AMRI ya kuficha mashahidi hupaswi kuwatoa kabisa.

Sheria inasema maelezo hayo mtuhumiwa hapaswi kupewa pale ambapo mahakama imetoa amri ya maeneo fulani yasipewa kwa accused person.

Ndio sheria inasema hata kama sipendi.

Kanuni ya 7(3) ya ulinzi wa mashahidi inasema pia hivyo hivyo.

Kesi inapaswa kusikilizwa kwa amri husika.

Amri ya mahakama kuu katika kesi hii kwamba majina ya mashahidi yasiwepo na utanbulisho wao wote na mashahidi wote ambao mahakaama ilitoa amri ya kuwalinda haijawalinda.

Tunafahamu makazi yao, mitaa yao, kazi wanazofanya hadi namba zao za simu tumepewa.

Sasa kwa mazingira hayo maana yake mashahidi wameandaliwa bila kufuata utaratibu kabisa.

Ni wasilisho langu kuwa Waheshimiwa Majaji mna maelezo ya mashahidi ambayo yamekiuka sheria kwa mujibu wa Sheria zetu.

Maelezo yote hayo yanapaswa kuwa expunged from the record.

Sasa hatuhitahi kwenda huko maana tunaweza kulimaliza hapa.

Naomba sasa niwape authority waheshimiwa majaji.

Kesi ya Benga Said Kasamwa Abuu Rajabu abou Masoud Criminal session Case.

Kwenye hiyo kesi wakati wa Commital proceedings kwa ajili ya kesi ya mauaji taarifa iliyokuwa committed high court maelezo yalikuwa na maelezo ya juu tu.

Hiyo statement ilisomwa kwenye committal na ikapelekwa Mahakama kuu na Mahakama kuu ikasema kwasababu hakujaonekana ukurasa wa pili basi taarifa yote ikawa quashed. Iliondolewa information yote.

Jaji alisema hayo masharti ni masharti ya lazima ni lazima yafuatwe.

Hizo witness statement zote na mashahidi wote waliopaswa kulindwa na hawajalindwa ukizifuta maana yake hakuna kesi ita collapse kabisa.

Out of 30 witness statement zinaondoka 23.

Nini kinabaki hapo?

Zifutiliwe mbali.

Sasa Waheshimiwa majaji naomba naomba kumalizia.

Naomba nimalize kwa swali lifuatalo.

Kifungu cha 295(1) cha CPA kinasema the information inayotakiwa kufutiliwa mbali ni ile ambayo s.294 haijazingatiwa.

Is this information capable to sustain?

Hapana haina miguu ya kusimamia hii.

Ni wasilisho langu kwamba haiwezi kurekebishika.

Nimesema tangu jana, haioneshi kosa lolote la jinai, haioneshi kosa la uhaini nililoshtakiwa nalo.

Sasa unarekebishaje kitu ambacho hata sio kosa kabisa hayo maelezo ambayo wanasema niliyasema hayajafafanuliwa.

Hawakusema walielewaje nikisema kukinukisha maana yake ni nini?

Haya mambo hayawezi kurekebishika kwa hatua ya sasa huwezi rekebisha ambacho hakipo..

Hawawezi kuleta pleading mpya ya overt act.

Part 25 itaendelea kwenye post inayofuata

Naomba repost yako kwenye tweet hii.
 
Tundu A. Lissu ameleta hoja nzito sana aisee mawakili wa serikali ni kama wamechanganyikiwa hivi, hoja yake ni Askari polisi ambao ni mashahidi walijiapisha wenyewe wakajiandikia maelezo wenyewe na kujisainia wenyewe. Lissu ni Genius huyu jamaa

IMG_20250917_202205_353.jpg
 
Haya si mapenzi ni mahaba. Feedback kutoka uongozi wa Chadema ni kwamba kwa muda mfupi wale vijana waliopigwa mahakamani wamechangiwa kiasi cha TZS 8M kati ya 10M zilizokusudiwa. Kwahiyo bado 2M kukamilisha gharama zao za matibabu. Endelea kutuma mchango wako kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Chadema Bi.Brenda Jonas Rupia kupitia Airtel 0789160733 au Vodacom 0769180733. Wao wanapiga, sisi tunatibu, Mungu anaponya.!
FB_IMG_1758169663229.jpg
 
Leo Tarehe 18/09/2025

Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es salaam.

Tayari tupo Mahakamani na tunasubiri muda wowote majaji wataingia Makarani na wafanyakazi wengine wa Mahakama tayari wameingia.

Viongozi wa Chama na Mawakili pia wamefika.

Leo tunachotegemea kufanyika ni kupokea mawasilisho (Reply Submission) kutoka kwa Mawakili wa Serikali mara baada ya mawasilisho ya mheshimiwa Lissu kuhusu mapingamizi yake ya awali aliyowasilisha (submission in chief)

Mapingamizi ya Mh. Lissu yalikuwa yanahusiana na ubovu wa hati ya mashitaka na la pili ni kwamba maelezo ya mashahidi (witness statement) yamechukuliwa kinyume cha sheria na pia yapo maelezo ya mashahidi ambao mahakama ilisema utambulisho wao ufichwe wameshindwa kufanya hivyo.

Sasa mara baada ya wasilisho la Mh. Lissu Tarehe 16/09/2025 na Jamhuri waliomba wapewe muda wa kwenda kujiandaa kujibu hoja za Mh. Lissu.

Leo imefika na tunasubiri majibu yao mawakili saba (7) wa Serikali ambao wanaiwakilisha Jamhuri.

Tunasubiri Wamjibu Wakili Tundu Antipass Lissu ambae ni mtuhumiwa na anajiwakilisha mwenyewe.

Tuendeleee kusubiri na tutawaletea moja kwa moja yatakayojiri hapa Mahakamani leo hii.

Mapolisi Leo pale nje ni kama wamechanganyikiwa au wanataka kutusahaulisha wamenywea sana.

Wako kama wamemwagiwa maji. Wanachadema wanawambia kwa vitendo kuwa sisi Hatupoi na wako vibrant sana.

Acha tuupe muda nafasi.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Leo September 18, 2025

Tunaendelea tulipoishia juzi

Part 26

Sauti ya Askari inasikika na watu wote wanasimama.

Inapigwa High Court!……….

Majaji wanaingia hapa wapo watatu.

Mhe. Lissu ameingia kama kawaida ana style yake ya kukunja ngumi na kuizungusha juu kwa nguvu sana na wananchi wanaitikia kwa kuzungusha pia ngumi.

Majaji sasa wamekaa na kuanza kuandika kidogo.

Wameinama chini.

Jaji Ndunguru anasema tuko tayari tuendelee.

Anasimama Katuga anaanza kuongea kumbe kesi haijaitwa.😂

Anakaa haraka.

Amesimama Karani ameita kesi.

Jaji anaita Upande wa Jamhuri.

Katuga anajitambulisha anasema yupo na Job Mrema, Thawabu Issa, Mossie Kaima, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringe na Winiwa Kasala wote ni Mawakili saba wa Jamhuri katika shauri lililopo mbele yenu.

Na mshitakiwa yupo anajiwakilisha mwenyewe waheshimiwa majaji.

Shauri lipo kuendelea na usikilizwaji wa upande wa Jamhuri kujibu yaliyosemwa na mshitakiwa tuna afya na tuko tayari kuendelea.

Anakaaa chini Katuga na majaji wanaandika kidogo hapa.

Mhe. Lissu leo ametupia T-shirt nyekundu ya No Reforms, No Election.

Majaji wanauliza mshitakiwa uko tayari?

Lissu: Naomba nizungumze mambo mawili.

1. Wakili wa serikali kila siku anasema mwenzetu anajiwakilisha mwenyewe. Amekuwa ananiita sana Mwenzetu mwenzetu sasa Mimi sio mwenzao.

Naomba wasinitambue kama mwenzao na Mimi sio mwenzao ieleweke hivyo.

2. Jambo la pili niliomba wiki mbili zilizopita kuwa kesi hii iwe live na watu wanapigwa sana hapo nje, niko Gerezani lakini najua yanayoendelea hapo nje ya Mahakama na nje kwa ujumla.

Sasa nilifikiri hili lingepewa uzito mkubwa sana maana wananchi wanapigwa sana na jambo hili halina afya kwa mahakama hii na kwa nchi hii.

Mlisema mtalitolea ufafanuzi lakini mmekaa kimya kuhusu jambo hili hamjalitolea ufafanuzi licha ya kwamba niliwaandikia barua na kusema hapa mahakamani.

Nahitaji majibu kutoka kwenu. Nimemaliza.

Amemaliza kusema hivyo Mheshimiwa Lissu

Majaji wanaandika kidogo hapa.

Wanateta wote watatu pale.

Tunasubiri mwongozo.

Jaji Nduguru : Sasa Wakili wa Serikali mshitakiwa hataki kuitwa Mwenzetu kwahiyo usifanye hivyo umtambue kama Mshitakiwa.

Katuga: Sasa Mheshimiwa unajua ni Wakili mwenzetu ndio maana tunamuita Mwenzetu.

Jaji anasema tusivutane, muite mshitakiwa na sio mwenzetu pia kuhusu hilo la kurusha matangazo haya ya mwenendo wa kesi hii tunalikumbuka na tutalitolea ufafanuzi kwahiyo hatujasahau wala kulipotezea.

Ameanza Katuga

Anasema katika kujibu hoja za Mshitakiwa nitaanza mimi Nassoro Katuga na baadae wenzangu wataongezea chochote na katika kujibu naomba nianze na utangulizi ufuatao.

Nilikuwa naiomba Mahakama hii tukufu i note kwamba jamhuri tunakubaliana na hoja ya mshitakiwa wakati ana lay foundation wakati wa utangulizi akirejea kifungu cha 135 cha CPA kwamba hati ya mashitaka lazima iwe na statement of the offence na particulars of the offence na hayo maelezo ya kosa ni lazima yajitosheleze kumpa mshitakiwa kutokana na mashitaka anayoshitakiwa nayo.

Tunakubaliana kwenye hilo na Mshitakiwa.

Lakini pia waheshimiwa Majaji tunakubaliana ya kwamba mashauri yaliyorejewa na Mshitakiwa ya Mulokozi dhidi ya Jamhuri Criminal Appeal No. 321 Mahakama ya Rufaa.

Lakini pia Isdory Patrice dhidi ya Jamhuri Rufaa ya Jinai No. 224/2007 Mahakama ya Rufani ya Tanzania tunakubaliana na kesi hizi zilipotumika kuunga mkono kwamba taarifa ya mashitaka ni lazima yaweze kutamka kosa kwa uwazi kwa kutaja visifa au viini muhimu vya shitaka ambalo mshitakiwa anashitakiwa nalo.

Mbali na kukubaliana na mambo haya. Tunasema kwamba kesi hizi ni tofauti (distinguishable) nitaeleza mbeleni nikijibu hoja za mshitakiwa.

Part 27, itaendelea kwenye post inayofuata

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
0 #UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 27

Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga

Wahesimiwa Majaji mbali na kukubaliana nae lakini tunapinga pingamizi lake la hati yetu ya mashitaka kwamba ina mapungufu yasiyotibika. Kwamba defective incurable na tunaleta chini ya kifungu cha 238 cha CPA ambacho kinaeleza.......

Kama hati ya mashitaka itaandaliwa kwa mujibu wa kifungu cha 138 cha CPA bila kuathiri rule of law hayawezi kuwa wazi kwenye mapingamizi kama yatakuwa yametengenezwa kwa kifungu hiki.

Haruhusiwi kuleta mapingamizi kama mashitaka yetu yametengenezwa kwa mujibu wa kifungu hiki.

Ukisoma kifungu hicho (a) namna hati ya mashitaka inavyotakiwa kuwa. (i) maelezo ya kosa.(ii) iandikwe kwa kufuata ordinary language yaani lugha ya kawaida avoid technical terms.(iii) particulars of the offence yaani maelezo ya ufafanuzi wa shitaka jinsi lilivyotendwa na mshitakiwa.

Na maelezo hayo ya ufafanuzi unatakiwa kutumia lugha ya kawaida hutakiwi kutumia technical terms.

Busara hapa ni ili mshitakiwa aweze kuelewa shitaka na hapa ndio tunapata nani, wapi, lini na kipi tunapata zile W4.

KABLA sijaenda kwenye kila alichosema Mshitakiwa ameeleza nisije muita mwenzangu tena.

Naomba kuialika mahakama hii kwenye kifungu kilichotumika kumshitaki mshitakiwa kifungu hicho pia naomba mahakama iangalie taarifa ya mashitaka ambayo tumeifile.

Kifungu ni cha 39(d) cha Sheria ya Kanuni ya adhabu urekebu wa 2022.

Bila kukirudia kifungu hiki nitaomba kuchambua viini ambavyo vinatambulisha kosa kwenye kifungu hiki katika kutambua viini hivyo naomba nirejeee shauri la MATAKA & others vs R EALR 1971 EA 495.

Shauri hili lilivitaja main essentials yaani visifa vya kosa la uhaini kama ifuatavyo.

1. Allegiance to the Republic
2. Formation of necessary intent
3. Kudhihirisha hiyo nia kwa kuchapisha maandishi au michoro au kwa vitendo au kwa matendo.

Nimeirejea kesi hii ambayo ilizungumza main essential elemeents tatu ina maana kuna viini vingine mbali na hivi.

Sasa kupitia kifungu hiki cha 39 cha Penal Code mtaaona viini mbali na hivyo viini vingine ni kwamba;

Mtu huyo aliye chini ya utii yupo ndani ya United Republic au else where sasa ndio ana form hiyo intention kuweza kufanyika au kusababisha kuweza kufanyika. Au anatengeneza nia kuchochea, kuhamasisha, kushawishi, yaani kanso yani kushawishi 😂 kushauri au kundi la watu kuweza kutendaa.

Hiki ndio kifungu kimetengeneza kosa ambalo mshitakiwa ameshitakiwa nalo.

Ukisoma hiki kifungu kuna maneno yametumika hapo ambayo ni or na tafsiri ya maneno hayo kwamba hayaendi kwa pamoja.

Ni lazima itafsiriwe tofauti tofauti kwa bahati mbaya hii tafsiri ya neno Or, sio tafsiri yangu mimi wakili wa serikali mkuu ni tafsiri inayotokana na kifungu cha 13 cha Sheria ya Tafsiri Sura ya 1, 2023.

Kwa tafsiri nyepesi haya maneno ukiona kuna mahali ipo "or" ujue linaweza tumika lile likaachwa hili au likatumika hili likaachwa lile huwezi tumia yote kuepuka mkanganyo.

Hii ndio tafsiri ya sheria.

Nabuy maneno ya mshitakiwa kwamba kifungu kidogo kinataja makosa mengi yeye aliyataja kumi na mimi nasema yapo zaidi kweli ya hayo kumi na hii inatokana na maneno "or" sasa naomba kuwaalika kwenye hati ya mashitaka

Part 28 itaend kwenye post inayofuata.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 28

Anaendelea Wakili wa Serikali Katuga

Anasema kama kuna mahali mshitakiwa hajaelewa hapa ataelewa.

Hati ya Mashitaka inamuita kwa jina na kumwambia inasema akiwa mwenye utii... hapo ni kiini cha kwanza halafu kinasema akiwa ndani ya Tanzania hapo ni kiini cha pili tumetaja halafu hati inasema kuchochea.. hicho ni kiini kingine.

Pia yapo maneno kwa nia ya kuitishia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hicho ni kiini kingine kwahiyo wakati wa ushahidi tutaeleza kama serikali imetishika au haijatishika, pia hati inataka nia ielezwe dhahiri.

Kwa mujibu wa kifungu kudhihirisha nia kuna njia mbili ambazo ni kwa kuchapisha maandishi au michoro na njia ya pili inasema by any overt act or deeds

Sasa hati yetu ya mashitaka iliacha publication ikasema habari ya overt act

Sasa tukisoma blacks law dictionary 10th edition chapisho la 2014.

Page 501 imetafsiri neno deed kuwa ni kitu fulani kilichotendwa au kinachotegemea kutendwa.

Sasa jamhuri ambayo iliambiwa haijui kutengeneza mashitaka iliamua kuchagua by his deed ambayo ni by uttering and publishing the following words.

Sasa hapa tatizo tulipoligundua ni neno publishing lilipotumika, Waheshimiwa majaji neno publishing lilikuwa na maana ya kutoa maneno na kuchapisha

Publishing ya hapa sio ya s. 39 sio hii ya hapa maana ile imesema writing au printing lakini haijatoa chapisho la maneno.

Chapisho lililotumika kwenye hati ya mashitaka ni lile tendo na imetumika ili mshitakiwa aelewe kwa maana ya kuchapisha kwenye mitandao na maneno yake ni deed.

Naomba nichomekee hapa jamani kidogo. Anachokisema Katuga kinachanganya sana, anasema kuna mambo hawajatumia sheria inalolitambua kosa husika ila kuna sheria zingine wamezitumia.

Ngoja tuendelee. 😂😂😂😂

Katuga anasema baada ya maneno haya mshitakiwa atakuwa ameeelewa baada ya kutoa ufafanuzi huo.

Naomba nianze kujibu hatua kwa hatua yale aliyokuwa anayasema mshitakiwa.

Nimefafanua hati ya mashitaka hatua kwa hatua. Kosa lake tumesema ni kuitishia serikali.

Kusema kwamba kuzuia Uchaguzi sio kosa la uhaini na sisi hakuna mahali tuliposema ameshitakiwa kwa kosa la kuzuia uchaguzi.

Angetulia angeelewa hati ya mashitaka na kwamba alitengeneza nia na kutoa maneno hayo kwa nia ya kuitisha serikali.

Sasa sijui hili la kuzuia uchaguzi limetoka wapi?

Nimemsikia pia mshitakiwa anasema kuzuia uchaguzi hakuwezi kuwa uhaini. Vifungu vya 42 hadi 49 na kusema hakuna kosa lililotengenezwa kwenye vifungu hivyo.

Nafikiri hakuelewa hati ya mashitaka.

Kwahiyo tuelewane nia yake ni kutishia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mshitakiwa alisema hayo maneno hayacreate kosa la uhaini na akawareejesha kwenye kesi ya Khatibu Gandi.

Naona Mhe. Lissu anacheka tu pale kizimbani anaangaliana na Mawakili wake wanafurahi ni kama Katuga anaongea utoporo tu.

Mimi pia naandika ila kiukweli simuelewi hata anazungumza nini? Halafu ana vimaneno fulani vimejaa ulimbukeni mwingi huko serikalini sijui huwa wanapewa nini hawa watu.😤

Anasema turejee ukurasa wa 67 wa Khatibu Gandi inasema kwamba maneno hayatengenezi overt act lakini huu msimamo unaenda kwa mtu mmoja akishitakiwa as individual.

Treason ya mtu mmoja anaweza kushitakiwa kwa maneno tu kwasababu yanatolewa na mtu mmoja.

Yote ambayo mshitakiwa ameeleza maneno na maana yake amesema akiwa hajaelewa kosa limetengenezwa na kiini kipi? Hati ya mashitaka haijasema kukinukisha ni UHAINI hati ya mashitaka inazungumzia nia ya maneno hayo.

Tafsiri hizi zote na hata mliporejeshwa kwenye vifungu vya 55 na vifungu vingine vyote.

Sasa tafsiri ya haya yote ni pale ambapo mahakama itaamua kesi hii tusubiri hadi huko mwisho.

Tusubiri mwisho.

Part 29, itaendelea kwenye post inayofuata

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali
 
Wana JF kuna mahali tulipitiwa na kujisahau.. Tulipaswa kuwa na mada maalum ya Tundu Antipas Lissu.

Mwanasheria nguli, mwanaharakati wa haki za binadamu na sasa mfungwa wa kisiasa wa kesi ya uhaini na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanganyika

Ana historia yake maalum .. Ana mengi mazuri ya kiwango kaifanyia Tanganyika.. TUMUENZI SASA. NI WAKATI WAKEView attachment 3381742
(7,029) Historia fupi ya maisha ya shule ya Tundu Lissu | JamiiForums Historia fupi ya maisha ya shule ya Tundu Lissu
Screenshot_20250918-130434.jpg

Hivi hii timu ya akina Mafwele na masks zao bado wako beneti nae kila akienda mahakamani? Hawaliamini jeshi la Magereza? Wanaogopa asiwasiliane na nani anapokuwa akienda na kutoka mahakamani?
Obviously wanajua hawezi kutoroka hata akiachwa nje peke yake, wanaogopa asiwasiliane na nani?
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 29

Katuga anaendelea hapa.

Tumemsikia kwenye hati ya mashitaka anasema amemtaja Rais au Serikali au Makam au Waziri Mkuu. Anawataja katuga kama waheshimiwa kwa unyenyekevu sana.😂😂😂

Sasa akisema kuwa hatujawataja hao watu ndio hati ya mashitaka haijaeleweka kwa mashitakiwa. Kuwataja au kutowataja ni suala la ushahidi.

Mahakama itakaposikiliza ushahidi ndio itajua hayo mengine yote.

Waheshimiwa mlikuwa mnaambiwa msema kuna uhaini hapa. Katika hatua hii mahakama haiwezi kujibu kuna uhaini au hakuna.

Haya maneno yanaleta uhaini au hayaleti ni suala la ushahidi.

Taarifa ya mashitaka inaweza kuwa na dosari either kwa muundo au kwa maudhui.

Sasa kuhusu hati ya mashitaka kutokuwataja watu sisi tumesema ali instigate public kwahiyo hapo public ilikuwepo na yeye alikuwepo mtoa maneno.

Hatuwezi kutaja public huyu na yule kwa sasa.

Nimewaona Wazee akina Nshala na Mpoki ni kama wamekasirika hivi wanaona kuna ujinga mkubwa sana unazungumzwa na huyu Bwana Katuga.

Katuga aninipa uvivu mpaka kuandika.😤

Anaendelea Katuga

Naomba tuijibie hoja nyingine alisema kwenye kesi ya Mataka mahakama ilisema kwa kuwa hakuna sheria iliyowekwa ya namna ya kuandaa mashitaka ya uhaini na ilishauri kufuata English Procedure.

Kwenye hili tunasema kifungu cha 138 cha CPA sura ya 20. Kinazungumzia jinsi ya kuandaa hati ya mashitaka kwenye makosa ya jinai.

Ingawa ukisoma kifungu hiki kinasema jinsi ya kuandaa hati ya mashitaka na pia kinashauri waandaaji wa hati za mashitaka kuandaa hati zinazoendana na second schedule ya sheria hii.

Hakuna mfano wa hati ya mashitaka ya kosa la treason na kutokuwepo na hati ya mfano haipekekei mtu atoke alipotoka aseme kwamba hakuna sheria mahsusi inayoeleza hati ya mashitaka inavyopaswa kuandaliwa.

Kifungu 138 ni kifungu mahsusi kinachoelezea kosa hili la uhaini.

Pia kuhusu Hati aliyosomewa tar. 10/05 na hii aliyosomewa juzi kuna maneno yameongezwa.

Ametumia maneno kuwa imekuwa amended na akasema kuwa hawa jamaa hawa hawajaonesha mamlaka ya kurekebisha hati ya mashitaka.

Hawajasema mahakama iliyowapa hayo mamlaka.

Hati ya mashitaka iliyopelekwa mahakama kabidhi ni hati inayopelekwa chini ya kifungu cha 262 cha CPA.

Kifungu kinasema mshitakiwa anapokuwa amekamatwa apelekwe mahakama ya chini akiwa na hati ya mashitaka inayopendekeza kosa lake.

Kwa tafsiri halisi hii sio actual hati ya mashitaka hii ni holding charge.

Hii sio hati halisi ni proposed charge. Kule chini ilikuwa ni uhaini na mbele yenu anashitakiwa na uhaini.

Anaendelea Katuga:

DPP atakapojirishisha ushahidi upo wa kutosha ataandaa au atalazimisha kuandaliwa hati ya mashitaka na ataiwasilisha Mahakama kuu pamoja na mashahidi.

Hajasema huruhusiwi kubadilisha hati ya mashitaka kwa mujibu wa kifungu gani na ingawa nikikumbuka alisema yeye ni Wakili wa miaka 23.

Pingamizi la pili alisema hati ya mashitaka haiwezi kutibika kwasababu viambata vyake havijachukuliwa kwa mujibu wa sheria.

Hati ya mashitaka inampa taarifa ya kosa lake na kuwapa jukumu upande wa mashitaka kuthibitisha pasipo kuacha shaka hiyo hati waliyomsomea mshitakiwa.

Kwenye hoja hiyo mshitakiwa hakuiambia mahakama kuwa hati ya mashitaka ili iwe valid lazima iambatane na orodha ya mashahidi.

Kwa vile hakusema ni wasilisho letu kuwa alikuwa sahihi kabisa kutokusema.

Upande wa jamhuri tunasema kuwa hati ya mashitaka ni nyaraka inayojitegemea na imetengenezwa kwa mujibu wa kifungu cha 138 cha CPA na hakuna mahali inaposema hati ya mashitaka itakuwa pamoja na hayo maelezo ya mashahidi. Hili ni jambo jipya.

Waheshimiwa majaji suala la maelezo ya mashahidi kuambatana na hati ya amshitaja ya mahakama kuu imeanza kuonekana kwenye kifungu cha 262(6), 263(2).

Part 30 itanendelea kwenye post inayofuata.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 30

Anaendelea Katuga,

Mshitakiwa anapaswa kupewa nyaraka hizo lakini sio kwamba nyaraka hizo unaweza kutumia moja dhidi ya nyingine.

Maelezo ya mashahidi hayawezi kutumia hati ya mashitaka kuondoa uhalali wa hati ya mashitaka.

Kutafsiri vifungu vya sheria unaweza kwenda kwenye vifungu vingine kupata maana.

Maombi yoyote chini ya sheria hii ni lazima kuwepo na Chamber summons na affidavit sasa hakuna kifungu kinasema mashitaka haya yanafunguliwa kwa hatinya mashitaka yakiwa yamesupportiwa na maelezo ya mashahidi.

Natamani siku moja binti yangu Kylie aje kuwa Wakili lakini sitaki awe kama Katuga 😂 kiukweli napata wakati mgumu hata kumsikiliza anachosema.

Anaendelea Katuga.

Hii hoja tunaona ilitakiwa kuja mwanzoni na sio muda huu.

Sasa hivi ni afterthought kwamba witness statement ilipaswa kupingwa wakati ule wa awali na sio pingamizi la leo.

Tunaomba jambo hilo lisiruhusiwe muda huu.

Kifungu cha 11 cha CPA kinasema Police officer afanye nini anapomuhoji nani? Kinachosema hicho kifungu ni kumtenganisha police officer na shahidi mwingine wa kawaida.

Na hayo yote yanahitaji ushahidi kwahiyo tunapaswa kusubiri wakati wa ushahidi.

Sasa kesi ya Jamhuri vs Mbenga Seif Kasanwa, Abdu Masibu, Abdu Rajab.

Sasa stare decis hii ni persuasive kwenu ni kesi ya mahakama kuu hii. Haiwafungi mikono.

Ni kesi pia inayozungumziwa mazingira tofauti kabisa.

Sasa kuna kesi ya Silius Mlokozi vs Jamhuri nayo haiungi mkono chochote kuhusu madai ya mshitakiwa hapa mahakamani.

Katuga anasema hata mshitakiwa alikubali kusema haya maneno.

Amesimama Lissu anasema mheshimiwa huko hatujafika bado kwamba nimekubali kuwa nilisema au sijasema.

Nilichokuwa nakiongea mimi ni kuwa hayo maneno kwa mujibu wa katiba ibara ya 18 na kifungu cha 52 cha Penal Code na sheria ya vyombo vya habari ni maoni tu na sio kwamba nilikubali.

Jaji Ndunguru anasema sasa mjielekeze msiseme vitu ambavyo havipo hakusema hivyo labda useme maneno yanayoonekana kwenye hati ya shitaka ni haya hapa.

Imeita simu ya Polisi mara mbili inapiga kelele.

Mahakama imesimama lakini hawajachukuliwa hatua yoyote.

Angekuwa mwanaChadema hapa sijui Kama hili jambo lingepita kimya kimya maana huyu askari sijui anashida gani mara ya nne simu yake inatusumbua hapa.

Anaendelea Katuga na kusema Mheshimiwa Jaji hati ya mashitaka haina shida yoyote kwasababu imejengwa kwenye kifungu cha 138 cha CPA hivyo huwezi kuweka pingamizi.

Tunaomba kumalizia kuwa tunaomba mapingamizi hayo yatupiliwe mbali na upande wetu ni hayo tu hatuna kingine..

Majaji wanaandika kidogo na kuulizana mawili matatu.

Tunasubiri sasa Rejoinder ya Mh. Lissu sijui ataifanya Leo au na yeye atahitaji muda arudi geto huko Magereza akaandae nondo za kuwajibu hawa jamaaa.

Binafsi sijaelewa Katuga alikuwa anasema nini kwa kiwango kikubwa sana.

Ngoja tuone ngoma bado ni mbichi.

Mahakama imemuuliza Mhe. Lissu amesema anaomba health break kidogo na azungumze na mawakili pia.

Mahakama imesema turudi saa saba na nusu kwa ajili ya rejoinder kutoka kwa Mh. Lissu.

Askari Magereza wameamuriwa wasije kumzuia Lissu kuonana na Mawakili kwasababu Lissu amelalamika kuwa Mawakili wanazuiwa kule lockup.

Tunatoka muda huu kwa ajili ya Break.

Tukutane saa saba na nusu mchana.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI

Part 30

Anaendelea Katuga,

Mshitakiwa anapaswa kupewa nyaraka hizo lakini sio kwamba nyaraka hizo unaweza kutumia moja dhidi ya nyingine.

Maelezo ya mashahidi hayawezi kutumia hati ya mashitaka kuondoa uhalali wa hati ya mashitaka.

Kutafsiri vifungu vya sheria unaweza kwenda kwenye vifungu vingine kupata maana.

Maombi yoyote chini ya sheria hii ni lazima kuwepo na Chamber summons na affidavit sasa hakuna kifungu kinasema mashitaka haya yanafunguliwa kwa hatinya mashitaka yakiwa yamesupportiwa na maelezo ya mashahidi.

Natamani siku moja binti yangu Kylie aje kuwa Wakili lakini sitaki awe kama Katuga 😂 kiukweli napata wakati mgumu hata kumsikiliza anachosema.

Anaendelea Katuga.

Hii hoja tunaona ilitakiwa kuja mwanzoni na sio muda huu.

Sasa hivi ni afterthought kwamba witness statement ilipaswa kupingwa wakati ule wa awali na sio pingamizi la leo.

Tunaomba jambo hilo lisiruhusiwe muda huu.

Kifungu cha 11 cha CPA kinasema Police officer afanye nini anapomuhoji nani? Kinachosema hicho kifungu ni kumtenganisha police officer na shahidi mwingine wa kawaida.

Na hayo yote yanahitaji ushahidi kwahiyo tunapaswa kusubiri wakati wa ushahidi.

Sasa kesi ya Jamhuri vs Mbenga Seif Kasanwa, Abdu Masibu, Abdu Rajab.

Sasa stare decis hii ni persuasive kwenu ni kesi ya mahakama kuu hii. Haiwafungi mikono.

Ni kesi pia inayozungumziwa mazingira tofauti kabisa.

Sasa kuna kesi ya Silius Mlokozi vs Jamhuri nayo haiungi mkono chochote kuhusu madai ya mshitakiwa hapa mahakamani.

Katuga anasema hata mshitakiwa alikubali kusema haya maneno.

Amesimama Lissu anasema mheshimiwa huko hatujafika bado kwamba nimekubali kuwa nilisema au sijasema.

Nilichokuwa nakiongea mimi ni kuwa hayo maneno kwa mujibu wa katiba ibara ya 18 na kifungu cha 52 cha Penal Code na sheria ya vyombo vya habari ni maoni tu na sio kwamba nilikubali.

Jaji Ndunguru anasema sasa mjielekeze msiseme vitu ambavyo havipo hakusema hivyo labda useme maneno yanayoonekana kwenye hati ya shitaka ni haya hapa.

Imeita simu ya Polisi mara mbili inapiga kelele.

Mahakama imesimama lakini hawajachukuliwa hatua yoyote.

Angekuwa mwanaChadema hapa sijui Kama hili jambo lingepita kimya kimya maana huyu askari sijui anashida gani mara ya nne simu yake inatusumbua hapa.

Anaendelea Katuga na kusema Mheshimiwa Jaji hati ya mashitaka haina shida yoyote kwasababu imejengwa kwenye kifungu cha 138 cha CPA hivyo huwezi kuweka pingamizi.

Tunaomba kumalizia kuwa tunaomba mapingamizi hayo yatupiliwe mbali na upande wetu ni hayo tu hatuna kingine..

Majaji wanaandika kidogo na kuulizana mawili matatu.

Tunasubiri sasa Rejoinder ya Mh. Lissu sijui ataifanya Leo au na yeye atahitaji muda arudi geto huko Magereza akaandae nondo za kuwajibu hawa jamaaa.

Binafsi sijaelewa Katuga alikuwa anasema nini kwa kiwango kikubwa sana.

Ngoja tuone ngoma bado ni mbichi.

Mahakama imemuuliza Mhe. Lissu amesema anaomba health break kidogo na azungumze na mawakili pia.

Mahakama imesema turudi saa saba na nusu kwa ajili ya rejoinder kutoka kwa Mh. Lissu.

Askari Magereza wameamuriwa wasije kumzuia Lissu kuonana na Mawakili kwasababu Lissu amelalamika kuwa Mawakili wanazuiwa kule lockup.

Tunatoka muda huu kwa ajili ya Break.

Tukutane saa saba na nusu mchana.

Naomba nisaidie kushare ujumbe uende mbali.
 
Polisi akipiga watu picha hapa mahakamani leo.
1758192139104.jpg
 
Tundu A. M. Lissu aitishia serkali naomba tafisili ya maneno hayo wajamaniii

Nukuu toka Kwa Katuga

"Nimefafanua hati ya mashitaka hatua kwa hatua. Kosa lake tumesema ni kuitishia serika
1758198268196.jpg
li".
 
Back
Top Bottom