NI KWA MASLAHI MAPANA YA UMMA SHAURI LA TUNDU A.M.LISSU KURUSHWA MUBASHARA.
Jopo la Majaji Watatu wa Mahakama Kuu likijumuisha Waheshimiwa Jaji Ndunguru, Kiwonde na Karayemaha wamepangwa kusikiliza na kuamua Kesi ya Uhaini baina ya Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu, Shauri la Jinai Na. 19605 ya 2025 .
Mahakama ilianza vizuri kurusha mubashara katika hatua za awali ni rai yetu kwamba isirudi tena gizani na kuzuia kuoneshwa Mubashara kwa kesi hii muhimu.
Mahakama ijitahidi kuwa na consistency pale inapofanya mambo mazuri hasa ya kuhakikisha uwazi katika uendeshaji wa shauri labda iwe kwa matukio machache yenye uhitaji wa usiri kiusalama kwa mashahidi wale wanaozungumzianmambo ya ndani kuhusu taasisi zetu za usalama na siyo ushahidi wa kawaida.
NI VEMA KUHAKIKISHA KUWA SIYO TU HAKI ITENDEKE BALI IONEKANA BAYANA IKITENDEKA.
BAK Mwabukusi.
View attachment 3468686