Huyu sio kibaka, sio muhalifu, sio mwizi, sio jambazi, sio mbakaji bali ni Katibu wa CHADEMA Kanda ya Pwani. Tukio hili halijatokea enzi za mkoloni mweupe wa Kijerumani na Kingerezahii miaka ile ya 1947 au 1920 au 1960 wakati wa kupigania Uhuru kutoka kwa wakoloni wazungu..
Tukio hili ni leo mahakama ya hakimu mkazi Kisutu..
Kosa la Mtanzania huyu ni kwenda kusikiliza kesi ya Kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu A. M. Lissu aliyepewa kesi ya uhaini na uchochezi.
Ni katika nchi hii hii club ya mpira imechangia fedha ili kufanikisha utawala huu huu unaofanya maovu haya dhidi ya raia upate pesa na nguvu ya kubaki madarakani..... wafanyabiashara na wengine waliochangia maana wanaunga mkono dhulma hizi dhidi ya raia, utekaji, mauaji, uzembe na maovu mengine yote..
Kumbuka kauli ya Mwalimu, lazima wanyonge waungane kukabili wenye nguvu. Haki haiombwi haki imadaiwa na kupiganiwa na hata kuporwa kwa nguvu mikononi mwa anayeikandamiza. Kwanza unamuomba nani yani umuombe anayenufaika na uporaji wa haki yako?
✍️𝗝𝗼𝗵𝗻 𝗛𝗲𝗰𝗵𝗲
#NoReformsNoElection