PROFESA: SUALA LA LISSU LINAFEDHEHESHA NCHI YETU DUNIANI.
Aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye kwa sasa ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu, Olaf cha Marekani Prof. Joseph Mbele ametoa kauli nzito juu ya serikali ya Tanzania inavyofanya kwa Tundu Lissu. Prof. Mbele amesema kuwa:
"Dunia nzima inashuhudia uvunjifu wa haki za binadamu unaofanyika Tanzania. Mambo yako wazi mitandaoni. Kinachonishangaza ni pale viongozi wa Tanzania wanapokuja ughaibuni na kutuhimiza wanadiaspora tuitangaze nchi yetu vizuri. Mbele ya hayo yanayofanywa na polisi, askari magereza, na kadhalika, yakishuhudiwa na dunia yote, Tanzania ipi ya kuitangaza vizuri?"
Prof. Mbele ametoa kauli hiyo kupitia maoni yake katika ukurasa wa Facebook wa Askofu Mwamakula baada ya Askofu kutoa kauli juu ya kitendo cha askari magereza kumfedhehesha Mhe. Lissu aliokuwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kesi yake tarehe 11 Julai 2025.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 12 Julai 2025; saa 5:00 asubuhi