Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

Tundu Antipas Lissu special thread (CHADEMA CHAIRMAN)

 
 

Attachments

  • 6133511-68a3fb5fe884f800336fabbed577375.mp4
    1.1 MB
 
1753739451782.jpg
 
Kuna watu hasa ndani ya CCM na vikaragosi vyao pia katika upinzani waliomwita @TunduALissu eti ni kichaa 😁
Sasa hivi wanamwelewa wamejikaza kisabuni tu 🤣🤣
Alipowaambia #NoReformsNoElection ni ya kila mtanzania mkafikiri mko salama

Kesho Simba ananguruma mahakamani! Hii fighting spirit 🔥 hamtakaa kuelewa ila ni kubwa kuliko chochote walicho nacho madhulmat
#FreeTunduLissu
FB_IMG_1753848977665.jpg
 
Baadhi ya Askari Magereza waliopungukiwa akili, wakimsukuma kizimbami Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu ambapo alikaribia kuanguka kabla ya kuzuiwa na Askari wengine waliokua mbele yake. Ikumbukwe Lissu ni mlemavu wa mguu kutokana na shambulio la kikatili la kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake mwaka 2017. Mpaka leo anatembea kwa kuchechemea. Ni ujinga wa hali ya juu kumsukuma mtu ambaye unajua ni mlemavu na mguu wake mmoja umejaa vyuma.

Lissu angeweza kuanguka na kupata madhara makubwa akiwa mahakamani. Angeweza kuvunjika mguu, mbavu, au kupasuka kichwa kutegemea na alipoangukia. Hawa askari wamefanya jambo ambalo ni kinyume na maadili ya kazi zao, kinyume na taaluma zao na kinyume na ustaarabu. Natumaini Kamishna Jenerali MagerezaTanzania hatafumbia macho ujinga huu, ili usijirudie tena. Mahakamani ni mahali salama. Hakuna anayestahili kuumizwa, kudhalilishwa au kutwezwa utu wake akiwa kizimbami.!
 
Leo nimetazama video
Yenye msisimko mbaya Sana
Majonzi inayoashiria Taswira mbaya na ya kusikitisha Sana aliyofanyiwa mh lissu na Askari magereza kizimbani !

#Lissu amesukumwa kwenye kizimba kama mbwa na Askari magereza nimetazama mara nyingi tukio lile la unyanyasaji mwingine unaoongeza hisia hasi nimejiuliza
Kuna mtanzania hajui Hali aliyo nayo lissu kiafya hasa mwili wake uliojeruhiwa vibaya kabisa Kwa Risasi nyingi 2017

Nimeendelea kujiuliza mwenyewe
Je nini lengo la wale Askari Wetu wa magereza kufanya harassment kwenye macho ya Dunia kwa chuki kiasi kile ?
Vipi wakiwa naye mwenyewe Hali ikoje ?

Je Wana baraka za Nani kufanya Yale ?

Je Ile NI mbegu njema ya nchi inapandwa mioyoni mwa watu ?

wenye madaraka hasa mnaowatuma hawa wanaofanya haya
Mkiliona huko mtakakokuwa kama mnasali na mnajua Mungu yupo
Mjiulize vipi tabia hii itadumishwa kwa vizazi vyetu Tu? ! Hiyo ahadi mnayo toka kwa Mungu ? Ili tusishangae tena

NI swala la muda mlioko kwenye madaraka oneni umuhimu WA kuondoa mambo mengine yasiyokuwa na sababu ya kuzidisha vilio kwenye mioyo ya Watanzania kama Mungu aishivyo
Haya yatasimamishwa siku Moja Ten kwa aibu kubwa na sio mbali

Mwisho niseme Tu nimeumia Sana kwa kitendo kile
Nimeogopa kurudia kuangalia Tena Ile video isiyokuwa na tofauti kabisa na uovu mwingine wowote
Kama Mungu aishivyo kisasi NI chake yeye
FB_IMG_1753891226735.jpg
 
Back
Top Bottom