Naam,
Mwezi januari umekuwa mbaya kwa wasema hovyo. Alinza Zitto na Fatma Karume sasa ni Tundu Lissu.
Ushauri tu kwa ndugu Lissu unapoenda kwenye mahojiano mahsusi hususani kwenye media za kimataifa jiandae achana na propaganda zisizo na uthibitisho. Ni dhahiri, Lissu amezoea mahojiano ya upande mmoja kupitia VOA au DW ambapo mara nyingi watangazaji humuacha azungumze anayotaka.
Tundu Lissu ulipwaya kwenye mahojiano sasa umethibitisha ya kwamba umepona rudi bungeni badala ya kupiga porojo.
Tundu Lissu umeongea uongo kuhusu makusanyo ya kodi,utawala wa sheria na zaidi kuongopea dunia ya kwamba mauaji au vifo vya watu havijawahi kutokea Tanzania.Kwa taarifa yako hapo London wapo wapemba kibao waliojitweka 'ukimbizi' baada ya uchaguzi wa mwaka 2000.
Umeongopa mengi hadi mtangazaji anamwambia ''allegetions being made are infamatory'' kamtuhumu kutumia blogs na social media. Ni kama amejifunua na kukiri kuwa ameamua kuwaunga mkono wawekezaji kwenye madini sababu 'hakuungwa mkono miaka ya 90''
Ameshindwa kuthibitisha madai ya wapinzani kununuliwa hadi mtangazaji kamuonya kwa kumwambia yeye (Tundu) kama mwanasheria hapaswi kueneza uzushi kwa mambo asiyokuwa na uthibitisho nayo.
Muandishi kaenda mbali kwa kumwambia ''mbona Masha alikuwa waziri wa Kikwete akahamia upinzani na sasa amerudi CCM huku akimuunga mkono Magufuli kabaki kutoa macho huku akishindwa kutoa uthibitisho wa kununuliwa wapinzani.
Alichosema ukweli ni idadi ya risasi alizopigwa mwilini ni 16 na sio 38 kama wafuasi wake wanavyosema, pia amekiri wazi kuwa kama akiwa rais ataweka sheria ya kuunga mkono ushoga. Pathetic!
Mwisho, Tanzania haiwezi kuwa nchi ya kishoga kama ambavyo unatamani.